Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

sio lazima tuteseke aisee



ww ulienda ukala bata lako ukageuka bongo....sio lazima tuteseke aisee

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Nashangaa watu kunivamia jamani! nimeeleza tu ka experience changu cha mdada kunisemesha mwenyewe halafu baada ya hapo kunikaushia kama sio yeye 😀. Labda nilitakiwa niseme kwa maneno machache tu kuwa kuna mdada alinitaka stori baada ya hapo hakutaka tena stori, sasa sijui ningeeleweka?
 
Hili tunaweza kusaidiana kujibu,barabara Tanzania bado sana tena sana,hii T1 yetu ni bado sana,Zambia wanajitahidi sana hasa barabara ya Lusaka to Livingstone,ya kwenda Chilindu sio mbaya sana ILA kuna tatizo kubwa mno btn Nakonde na Mpika ni shida sana(hii kwangu ni sabotage wanayotufanyia wazambia maana wameelekeza nguvu nyingi kusini but pure kibiashara)Chilundu hadi Beitbrige wanaifanyia ukarabati na nzuri in general,na N1 ya kutoka Beitbrige hadi cape town ni first class road ni super,na ukija Botswana nao ni super kuanzia ile A3 hadi A1,border ya zambia na Namibia sio safi hasa Zambia side ila upande wa pili ni super.Tanzania tuache siasa ni vema hii T1 yetu tuitengeneze ili tuchukue even 40%ya mizigo ya DRC(hii ndio future ya kibiashara Africa)
Naomba ufafanuzi huwa naona hizo T1, A1, N2, kwenye vibao barabarani, huwa na maana gani!?
 
SEHEMU YA KUMI

Kwa Kifupi ndo nikawa South Africa nimeshaingia ivo bila ya kuwa na Ndugu wala Rafiki wakunipokea. Mambo ya kusubiria kuwa na Ndugu au Rafiki yangenichelewesha sana.

Basi Nilikaa pale nje mpaka saa saba usiku ndo Jamaa akaja kunichukua. Alisema kuna sehemu alikuwepo kuna Harakati alikuwa anafanya. Jamaa akanipokea Begi hao mdogo mdogo mpaka KFC tukapata chakula kisha tukaenda Magetoni kwake. Ilikuwa ni ghorofa. Yeye alikuwa amepanga Ghorofa kama ya tatu hivi. Tulifika na kuingia ndani kwake. Kilikuwa ni chumba kimoja, sebure kubwa, Choo na Jiko. TV Kubwa, Makochi ya Kisasa. Kwa kifupi jamaa alikuwa anaishi vizuri.

Tukawa tunapiga piga story pale, Jamaa alikuwa ananichukua Maelezo ili awe na uhakika kama kweli Mimi ni Mtanzania na Kama kweli natokea Temeke. Wabongo wengi wanafanya hivyo ili kujiridhisha kama kweli wewe ni Mbongo wasije kupokea Mburundi, Mkenya au Mkongoman. Baada ya story kidogo jamaa akaniambia panda kitandani upumzike.

Hapa nitasema kama ilivyokuwa, Juu ya Kile Kitandani jamaa alikuwa ametandaza Dawa za Kulevya Kibao. Ilikuwa ndo Mara yangu ya kwanza kuziona dawa za kulevya vile. Zilikuwa nyingi sana halafu Jamaa haogopi wala nini. Alikuwa anazifunga funga. Nikahisi pengine jamaa alichelewa kuja kunifata labda alikuwa busy kufunga hizi Kete zake. Yan jamaa anafunga bila woga, tena mbele ya Mgeni. Nikajiuliza jamaa anajiamini nini.

Mimi sasa, Usingizi wote wa Safari ulikata. Maana nakumbuka nililala pembeni ya hicho kitanda halafu pembeni yangu ndo kulikuwa na hizo Dawa. Huku tunaendelea kupiga story.

Katika Maisha yangu, Dawa za Kulevya nilikuwa nazisikia tu kwenye Vyombo vya Habari na kuwaona Mateja Mtaani. Lakini ile nafika tu South Afrika ndo kama hivi nilikutana nazo tena ile ile siku ya kwanza. Mara pale ghetto tukasikia Hodi, Kisha Jamaa wawili wakaingia ndani. Nao ni wabongo. Tukasalimiana pale kisha wakaendelea na Mishe zao. Wakafungua mabegi yao na kuanza kutoa Kete zao za Dawa za Kulevya na Pesa, ni kama vile walikuwa wanamkabidhi jamaa mahesabu ya siku hiyo. Kwa haraka haraka nilisikia pale, kila mmoja alimkabidhi jamaa kama Laki Nane za Kitanzania. Moyoni nikasema duh jamaa anatengeneza hela. Laki Nane kila mmoja, Je Jamaa ana vijana wangapi ambao kwa Siku kila mmoja anamletea Laki Nane?

Baada ya mahesabu yao, jamaa aliwapatia tena mzigo mwengine wa kuuza siku inayofuata yaani asubuhi yake. Kisha jamaa akaniambia "Sasa Homeboy utafatana na hawa jamaa utakwenda kuishi wanapoishi wao"

Basi pale nikaamka chap, Nikatoka pale Ghetto na wale jamaa wawili. Hao mtaa kwa Mtaa na Begi langu Mgongoni. Hiyo ni Kama saa Tisa au Kumi hivi usiku. Uchovu wote umekata. Natembea na jamaa ambao najua kabisa kwenye Mabegi yao kuna Dawa za Kulevya kibao.

Yan Mwili wangu ni kama vile ulichanganyikiwa kiasi, kutokana na uchovu wa safari, Mambo ya Dawa za Kulevya na Macho nayo yalikuwa yanashangaa tu uzuri wa ile Mitaa. Mitaa mizuri sana. Basi ilikuwa shida tu. Mchanganyiko wa Hofu na Furaha kwa pamoja.

Hao Hao mpaka kama mtaa wa Saba huko. Tulisimama mbele ya Ghorofa kubwa kama Kama Ghorofa 12 hivi. Pale getini mmoja wao alitoa Kadi ya kufungulia Mlango kisha Mlango ulifunguka wenyewe. Hao mpaka ndani, Tulipanda kwenye Lift mpaka Ghorofa ya 8 au 9 hivi. Walifungua Mlango tukaingia ndani. Kilikuwa chumba kimoja kikubwa, Chini walilaza magodoro kama manne hivi. Kulikuwa na Sebure, Choo na Jiko. Jamaa wakanikaribisha pale, tukapanda kwenye Magodoro tukalala. Kwa jinsi chumba kilivyokuwa nilihisi hawa jamaa humu ndani hawana muda wa kupika, vyombo vilikuwa shagalabagala, Kilikuwa ni chumba cha wao kulala tu.

Basi haikuchukua muda jamaa wengine kama Watatu wakaingia ndani. Ndo walikuwa wametoka kwenye mizunguko yao. Tukasalimiana kidogo kisha wote tukalala.

Baadae nilikuja kuelewa kuwa hawa jamaa wote wanafanya kazi ya kuuza na kusambaza Dawa za Kulevya za yule jamaa wa kwanza niliyekuta ametandaza Dawa Kitandani. Wote ni wabongo. Yule Jamaa Bosi wao, tumpe Jina Y, anawatumia nauli hawa Vijana huku Bongo halafu anakwenda kuwafanyisha hizo Kazi. Wengine ni Rafiki zake, Wengine ni ndugu zake. Wakifika hapo South ndo kama ivo anawapangia jamaa chumba na kuwalipia kodi na mambo mengine. Kwa hiyo hiki nacho ni chumba cha yule jamaa Y. Niliwaza kama hawa jamaa wote humu ndani kila mmoja anapewa mzigo wa Laki nane akauze kwa Siku, Jamaa Y atakuwa na pesa kiasi gani? Kwa hiyo Mimi kujileta mwenyewe kwenye huu mtandao wake jamaa alifurahi sana kuwa amepata mtu wa kumuuzia Dawa zake bila shida. Yaan Mbuzi Kafia kwa Muuza Bucha.
Haha haha piga kazi wew acha uoga
 
mimi bado naandaa kitabu cha harakati zangu..kutokea Dsm-Mogadishu-Yemen-Iran-Dsm-kahama-Geita-Mwanza-kakola-tarime-Dsm-Mafia- Dsm-kampala-Nairobi-kigali-Namibia-Lusaka-Nampula-Pemba-Beira-Maputo- Durban-Pretoria-Joberg- Iran-Kandahar-Peshawar-Kabul-Khost-Uzbegistan-Chechniya-Yemen-Moscow-Madagascar-Capeverde-France-Gabon-Burkinafaso-Namibia - capeverde-grenada-france-Swiss - Namibia -Dsm..

Hakikisha kila unapofika unaacha mbegu sio mnakuwa wavivu wavivu...
Mzee wa fursa, utauza au utavigawa bure!?
 
Nashangaa watu kunivamia jamani! nimeeleza tu ka experience changu cha mdada kunisemesha mwenyewe halafu baada ya hapo kunikaushia kama sio yeye . Labda nilitakiwa niseme kwa maneno machache tu kuwa kuna mdada alinitaka stori baada ya hapo hakutaka tena stori, sasa sijui ningeeleweka?
nimecheka sana wana walivyomaindi......et pandisha hilo pajama



watz tuko na stress sana

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Hapa niko class nakula hii course. Ukimaliza kuhadithia nisha graduate... Mtoa mada wewe ni mkweli nimeunganisha dot sana nimeona ni ukweli mtupu. Kilichobaki ni kutafuta jitu nilitapeli nipate 1.5m na mimi niingie uko.... Mpaka kieleweke. Uzuri mimi nina washkaji wa mtaani wananitambia tu na mapicha yao Facebook. Naenda kule buzaman nakuwa shoeshine muuza ngada.
Duh, mkuu ushajipanga kabisa? Huogopi sembe mkuu?
 
Back
Top Bottom