Niliroga sana

Muda mwingine ni harakati za kimaisha ndio zinapelekea mtu kuroga, fungua biashara uswahilini afu ndio utajua umuhimu wa waganga.
Phone book yako taratibu itaanza kujaa namba waganga, ili wasijulikane utawaita majina kama ostadh.
 
Muda mwingine ni harakati za kimaisha ndio zinapelekea mtu kuroga, fungua biashara uswahilini afu ndio utajua umuhimu wa waganga.
Phone book yako taratibu itaanza kujaa namba waganga, ili wasijulikane utawaita majina kama ostadh.
ili wasijulikane utawaita majina kama ostadh. πŸ˜€
 
Hongera kwa kuwa mkweli sana, Katika maisha yangu moja ya vitu ambavyo sikuwahi kuamini toka nikiwa mtoto ni uchawi! Nilikuwa naamini na ndivyo ninavyoamini hata sasa siwezi kurogwa! Wakati fulani kazini kwangu kulikuwa na jopo la watu wabadhirifu, niliwasimamisha kazi, lilikuwa kundi la watu wanaogopeka liliongozwa na Mzee mmoja wa kindengereko al maarufu kwa jina la Matimbwa, wakachanga mapesa kwenda kwa mganga hakuna kitu niliona, japo kuna kijana alikuwa rafiki yangu babu yake ni mganga hatari visiwani na wakuu huruka kumfuata, akaniambia niende kwa babu yake anigange, nilimkatalia. Sijawahi kuogopa uchawi .
 
Unajua dini nao ni uchawi?
Hapana, dini si uchawi

Kidini, kihistoria na kisosholojia, mambo haya mawili yana misingi, malengo na taratibu tofauti kabisa.

Angalia tofauti kubwa kati ya dini na uchawi:
1. Chanzo cha Nguvu na Mamlaka
Dini:
Huamini uwepo wa Mungu mmoja au miungu, ambaye ndiye muumba wa vyote na mwenye mamlaka ya mwisho. Waumini humwomba Mungu na kukubali mapenzi yake.

Uchawi:
Hutegemea mbinu za siri, nguvu za kishirikina, au majini/mizimu ili kulazimisha matokeo fulani kutokea. Mchawi anajaribu kudhibiti asili au watu kwa kutumia maarifa yake ya siri.
 
Uchawi upo na unafanya kazi lakini si kila anayerogwa anarogeka na sababu nyingi mojawapo ikiwa ni ulinzi wa kiroho, usafi wa kiroho.. Imani juu ya Mungu nknk
 
Mtu anayekataa au kusema vibaya Ulozi na ushirikina, ni hayajamkutaa.

Mie na Mambo ya ushirikina ni ulalo ulalooo tuu.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…