Nilianza kuagiza mizigo midogomidogo (small parcel ) miaka mitatu iliyopita na sijawahi kulipa kodi zaidi ya ile tsh 2350 ila mwaka huu nikapata shauku ya kuagiza mzigo kwa ajili ya biashara niliagiza saa pieces kama 20 pamoja na airpod
Mzigo wangu ulichukua takribani siku 12 tu toka china hadi TZ ulipofika nikatumiwa sms na posta inayoanza na RDP baada ya kwenda posta nikaambiwa nilipe 5900 kisha nikapelekwa kwa maafisa wa TRA aisee jamaa wakaufungua mzigo na kuanza kuukagua wakafanya mahesabu yao kisha nikaambiwa nilipekodi nusu ya gharama niliyonunulia bidhaa
Hiki kitu kwangu kilikua kigeni ndo mara ya kwanza kukutana nacho.
SWALI, je kipi ni nafuu kati ya kuagiza mzigo pc 50 za airphone aliexpress na sehemu nyingine kama alibaba maana sijawahi agiza sehemu nyingine tofauti na aliexpress
Wakati mwingine ukiwa unaagiza angalia shipping method. Nzuri ni ile Aliexpress standard shipping, ambayo mizigo wanasafirisha kwa Speedaf, haipiti posta.
Utaona tracking namba inaanzia na TZR……
Mizigo inafika haraka sana, na wala hawakucharge kodi.
Last week nmetoka kupokea simu 3, na sijawa charged hata one cent!