Nimepokea mzigo kutoka Ali Express kupitia Posta

SECRET AGENT

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
252
488
Habari wana Jamvi, nilikua nina mashaka sana na kuagiza mizigo Ali Express kwamba ntapokeaje mzigo wangu.

Nikafanya majaribio nilinunua bidhaa mbili Moja ni flash ambayo ipo kama kadi ya master card (GB16) na nyingine ni Case ya external hard disk.

Niliingia kwenye aliexpress nikatengeneza profile yangu na kwenye adress niliweka morogoro na nkaweka postal code ya morogoro ambyo ni 67000. Basi nkaenda kwenye kulipia bidhaa.

Malipo niliyafanya kwa kuingiza namba za Visa Card yangu ya CRDB then nkaweka security code (namba 3, zilizopo nyuma ya kadi yako) nilipomaliza basi wao wakakata kiasi cha pesa kinachohitajika moja kwa moja kutoka CRDB.

Bidhaa zangu zote nilizonunua zilikua hazizid elf 10 bei yake kwa pesa ya kitanzania na zote nilichagua za free shipping. Baada ya kuweka order ilikua mwez wa 12 mwishon nkatulia kusubiri na kila siku nlikua naingia kwenye shipped items naona progress mzigo umefika wapi.

Nmesubiria sana mpaka mwez wa kwanza ukaisha kwenye track ya mzigo wangu naona zmeshafika destination country, nikawa nasubiria.

Mpaka mwanzon mwa mwezi wa 2 kama tar 4 ivi nkapigiwa simu na Posta Mkoa Morogoro naambiwa kuna package zako 2 hapa, nkaenda pale nkapewa control number. Kila mzigo pale posta nmelipia 2350. Jumla nkalipa 4700. Nkapewa package zangu.

Bidhaa ni nzuri na hazina shida yoyote nmekua confident kuagiza mizigo kwa hawa jamaa.

Screenshot_20220212-091917.jpg
 
Inategemea na supplier uliponunua. Baadhi sio waaminifu. Ali Express ni kiunganishi tu kati yako na muuzaji. Eg. Mwaka jana August Nilinunua bidhaa mbili totauti kutoka wauzaji wawili tofauti kupitia Ali Express. Bidhaa moia ilifika Dec/2021, sababu aliyotoa supplier ni kuwa Logistic company aliyotumia kuutuma mzigo kwangu ilipoteza mzigo, hivyo nilipofuatilia sana ndio akatuma tena!!! (Ina maana nisingefuatilia ungepotea). Bidhaa ya pili mpaka leo Feb/2022 haijafika. Supplier hana jibu la kuridhisha. (Ina maana umepotea).
 
Mzee wajinga sana hawa bei zao bora ukatafte sim kariakoo
Inategemea..kariakoo redmi note 10 inauzwa hadi 650 uko wakat aliepress simu ilikua ni 450 tu,redmi note 11 imetoka inauzwa 392k,bongo wanapiga 700 uko... Bluetooth speakers ya anker soundcore motion plus bongo 450 wakat aliepress laki 2 na 10 tu,jbl charger 5 wanauza hadi 350 wakat bongo inapigwa 600+ ,hizo item zote hakuna hela utalipia,na incase ukikutana nayo ni 2300 ikizid 5900 kama sio bure kabisa..
 
Inategemea..kariakoo redmi note 10 inauzwa hadi 650 uko wakat aliepress simu ilikua ni 450 tu,redmi note 11 imetoka inauzwa 392k,bongo wanapiga 700 uko... Bluetooth speakers ya anker soundcore motion plus bongo 450 wakat aliepress laki 2 na 10 tu,jbl charger 5 wanauza hadi 350 wakat bongo inapigwa 600+ ,hizo item zote hakuna hela utalipia,na incase ukikutana nayo ni 2300 ikizid 5900 kama sio bure kabisa..
Duuh asante kwa kutoa mwanga mkuu
 
Back
Top Bottom