Hata Mimi imenitokea Sana mpaka sasa siwezi kusema neno baya kwa mtu kwan lazma litokee. Wakati nipo darasa la tatu kuna dada nilipigana nae akanipiga watu wakanicheka sana, roho iliniuma Sana nkamtafuta baadae tukajibizana kwa maneno nikamwambia atakufa na usiku wa siku ile ile akafa, mwingine alinipiga darasa la tano akafariki wk hyo hyo japo sikumwambia kitu, nikiwa form 1 kuna rafk yangu alikua tuliondoka shule anasema anaumwa ila alikua kawaida. Baadae nkakutana na pacha wake nikamwambie msalimie KULWA mwambie mwaka wake huu hawez kupona, nilisema kiutani ila usiku wa siku hyo akafariki kweli. Mwingine nilisema tukiwa chuo kwenye stori tu mada ilikua watu marafiki kufiwa na wazazi wao ndani ya mwaka huo huo kwan washkaj wengi walifiwa mwaka huo, kuna jamaa akasema sababu wazaz washazeeka ndo maana rate ya wao kufa ni kubwa, mimi nikasema kifo anapanga Mungu.wakat natetea hoja yangu nikasema Mungu anapanga nikamtolea mfano jamaa kwamba hata yeye anaweza kufa siku yeyote wala sio mpaka azeeke. Yule jamaa aligongwa na gari wiki ile ile akafariki. Toka hapo sitaki kumsemea mtu mabaya kabisa
Sent using
Jamii Forums mobile app