Talk to your fanboy already.
chakii trust me sikutegemea kama hii post itakuwa kitishoMshana Jr mbona unatutisha mkuu?
Mmh OK sitaki ligi ila hata mimi dunia nimeisafiri halafu sio leoTalk to your fanboy already.
I am good from Copa Cabana, Havana, Ghanato Savanna.
To the center of the galaxy I slash fallacies.
Ambaye hajawahi kufariki awe wa kwanza kumuambia mwenzie atafariki
Hutaki ligi wakati unaianzisha?Mmh OK sitaki ligi ila hata mimi dunia nimeisafiri halafu sio leo
Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni malaika wa kifo na sio kosa lako kuna watu wako hivyo wakikutabiria jambo huwa kuna kitu so amazing!!! POWER TO CREATEHata Mimi imenitokea Sana mpaka sasa siwezi kusema neno baya kwa mtu kwan lazma litokee. Wakati nipo darasa la tatu kuna dada nilipigana nae akanipiga watu wakanicheka sana, roho iliniuma Sana nkamtafuta baadae tukajibizana kwa maneno nikamwambia atakufa na usiku wa siku ile ile akafa, mwingine alinipiga darasa la tano akafariki wk hyo hyo japo sikumwambia kitu, nikiwa form 1 kuna rafk yangu alikua tuliondoka shule anasema anaumwa ila alikua kawaida. Baadae nkakutana na pacha wake nikamwambie msalimie KULWA mwambie mwaka wake huu hawez kupona, nilisema kiutani ila usiku wa siku hyo akafariki kweli. Mwingine nilisema tukiwa chuo kwenye stori tu mada ilikua watu marafiki kufiwa na wazazi wao ndani ya mwaka huo huo kwan washkaj wengi walifiwa mwaka huo, kuna jamaa akasema sababu wazaz washazeeka ndo maana rate ya wao kufa ni kubwa, mimi nikasema kifo anapanga Mungu.wakat natetea hoja yangu nikasema Mungu anapanga nikamtolea mfano jamaa kwamba hata yeye anaweza kufa siku yeyote wala sio mpaka azeeke. Yule jamaa aligongwa na gari wiki ile ile akafariki. Toka hapo sitaki kumsemea mtu mabaya kabisa
Sent using Jamii Forums mobile app
Gerezani kuna simu?mshana jr upo gereza gani sasa ukiwa unasimulia haya?
Pls not that way.... BTW wale haters wangu leo hii siwaoni tena! Baadhi waliomba poonaogopa hapa kucomment manake ukisema neno moja tu Imoo
Mtu kutokwa UHAI inatia hofu mkuu
We jamaa una mikwala ya hatari...Nimekumbuka hili tukio kuna mtu kanikera leo nikataka kumwambia utakufa ila nikasita
Sent using Jamii Forums mobile app
Bora uamkie mapema kabla hujaambiwa utakufa...Hatarious...
Shikamoo kaka Mshana
Umeonaee... Bora niwe mpole tuu babuBora uamkie mapema kabla hujaambiwa utakufa...
Interesting....Sijui inakuwaje lakini. Nilikutana na kisanga hiki:
Mtoto wangu mchanga wa miezi 10 hivi nilikuwa nampa chakula huku analia, kikampalia kooni. Nilimkimbiza kituo cha afya na mpaka nifike saa zikawa zimeenda sana. Yapata saa 5 usiku. Nikapokelewa na mlinzi na akaenda kumwita mganga (Dakitari) wa kituo kwenye nyumba yake. Alichukua kama nusu saa kuja. Nikawa nimekasirika sana nikasema kwa sauti kubwa kuwa; Hata akija, huyu mama hastahili kumtibu mwanangu. Kumbe ndo alikuwa anataka kufungua mlango.
Kuingia tu, akaanza kunifokea kwamba ninajivunia nini?? Bila hata kumjibu, nikambeba mwanangu nikaishia kwenye hosp ya mission. Wakampokea na baada ya vipimo wakasema ana pneumonia. Akaanzishiwa tiba ya haraka na akalazwa.
Asubuhi nikaendelea na shughuli zangu. Mchana, nikakutana na mgambo wa kijiji akaniambia kuwa, Kwa kuwa nakuheshimu, nenda mwenyewe kituo cha polisi Kata unatakiwa haraka. Nilipofika tu, nikaamriwa kuvua viatu na nikatupwa sero.
Sikujua ni nini kosa wala nini sababu. Nikatii amri bila shuruti. Nikakaa humo tangu saa 7 mchana hadi 11 jioni. Nikapewa dhamana na kuambiwa kuwa nilimtukana dakitari wa kijiji hivyo kwa usalama wangu niende kumwomba msamaha.
Nikafanya hivyo ila naomba muelewe si kweli nilimtukana ila kumbe alikuwa hawara yake yule afwande na mzee ndo alikuwa kalala na mimi nilikuwa nimemsumbua afwande.
Yaliyotokea:
Ilikuwa ijumaa, Jumatatu yule afwande alikuwa Sajinti nikamkuta central ana mbavu moja zile 2 zimengofolewa tena nikakutana naye analia na aliponiona akaniomba msamaha kuwa alinionea tu. Jumanne, yule Bibi afya (dakitari) akafukuzwa kazi kwani walikuwa wanamhisi kuiba dawa.
Yote hayo yalitokea kwa sababu nilisema; Kama nilikutukana mabaya na yanikute ila kama sikukutukana Mungu aamue. Akasema, kimbia haraka nisikuone au leo utalala ndani hadi Jumatatu.
Nikajiuliza, aliyekimbia haraka ni mimi au yeye?? Samahani kwa habari ndefu