Nilimdaka tapeli Mbeya baada ya kutapeli simu Dar

EvilSpirit

JF-Expert Member
Jun 15, 2017
8,558
12,684
Nikiwa Mbeya 2022 nilifahamiana na bwana mmoja tuliyekuwa tunamuita ngosha lakini baadae nilitambua anaitwa Katemi. Huyu mtu nilifahamiana naye baada ya kuwa tunaonana mara kwa mara sehemu ambayo nilikuwa napenda kushinda ni mtu ambaye tulikuwa tunaheshimiana na ni mtu mzima.

Kwa muonekano wake huwezi fikiria anaweza kuwa tapeli. Mwezi wa 10 2022 nilipoenda Dar nikiwa City Center kwa fundi viatu nikamuona anapita hiyo ni baada ya kutomuona kitambo kidogo kule Mbeya. Baada ya kuonana tukapiga stori mbili tatu tukapeana namba za simu. Nilimuuliza anafanya mishe gani akasema yuko kwenye ofisi inayojishughulisha na utoaji wa mizigo ya wateja bandarini

Kwa uelewa wangu shughuli hizi hufanywa na ofisi za Clearing and Forwarding japo yeye hakuitambulisha kwa jina hili na hata hii siku niliyokutana naye alidai anaenda bandarini. Tukiwa tunapiga story hapo kwa fundi viatu kuna mda aliniomba buku 2 kitu kilichonitia mashaka.

Baada ya kumpa namba yangu kuna siku alinipigia simu akidai ofisini kwao wanahitaji mfanyakazi akidai aliyekuwepo amehamishiwa Zenji ambako wamefungua ofisi, nilipomuuliza kazi gani akadai mtu wa kupokea wageni na kuingiza data kwenye computer akishindwa kubainisha title ya huyu mtu anayehitajika kufanya hiyo kazi..

Alikuwa anaulizia iwapo kama kuna ndugu yangu yoyote amuunganishe na hiyo kazi, ilinibidi niwashirikishe wenyeji wangu ambao waliniambia kuna binti waliwahi kuishi nae hapo nyumbani alimaliza form 4 pengine anaweza fanya hiyo kazi. Basi binti akatafutwa kwenye simu wakamjulisha kuhusu hiyo kazi binti akaonyesha ari ya kuitaka hiyo kazi nami nikaona nimwambie yule tapeli kuwa kuna binti anahitaji hiyo kazi ila yuko safarini kuja Dar akifika nitakuja nae umueleweshe vizuri kuhusu hiyo kazi, tapeli akasema sawa na akasisitiza binti awahi kwa kuwa ofisi haina mtu wa mapokezi.

Baada ya binti kufika Dar siku inayofuata nikampeleka posta ili aonane na huyu tapeli ambaye alidai wakionana atampeleka hadi kwa boss.Tulipofika Posta tukaonana na huyu tapeli tukaenda kukaa sehemu tukiwa watatu binti, tapeli na mimi kuzungumzia masuala ya kazi. Tapeli alidai boss yupo kwenye kikao hivyo anamuwakilisha hivyo tutamalizana naye yeye haina shida. Tukiwa hapo alidai kazi mshahara ni laki 4 chakula na nauli ni juu ya ofisi aliongea mengi ya kutuaminisha kuhusu hiyo kazi hewa aliongea pia juu ya uaminifu wake unaomfanya afanye kazi na watu mbalimbali

Baada ya maongezi tukaachana naye mda wa saa 8 mchana binti akijua siku inayofuata anaenda kuanza kazi wakati tunaachana akatuonyesha ghorofa moja refu sana kuwa ndio ofisini kwao ila nikashangaa kwanini hatupeleki ofisini.

Siku iliyofuata huyu binti alitakiwa akaonane na yule tapeli kisha ampeleke ofisini siku hiyo binti kadamka zake asubuhi kwenda Posta akaonana na tapeli badala ya kumpeleka ofisini akawa anamzungusha mitaani binti akaanza kuingiwa na wasiwasi mwishowe akamdanganya binti amuazime simu sijui afanya nini binti akampa simu kwa kuwa ilikuwa ina pattern akaomba atajiwe pia pattern za simu akamuazima binti na sh 5000 kisha akapotea. Simu ya binti na hela vikawa vimepotea kwa style hiyo, binti alisubiri toka saa 2 asubuhi mpaka saa 6 mchana mtu hakutokea na mpaka leo hatatokea.

Baada ya hiyo ishu nikawashirikisha jamaa zangu wa Mbeya ambao tulikuwa tunashinda nao sehemu fulani ambapo ndipo nilifahamiana na huyu tapeli. Wiki 2 zilizopita huku Mbeya kuna jamaa alimuona huyu tapeli akanijulisha hivyo siku moja saa 1 jioni nikawa eneo lile. Nikiwa naongea na jamaa nikamuona mtu kama yule tapeli mita kama 30 hivi akija tulipo, kilichonifanya nimtambue ni shati lake ambalo alilivaa hata ile siku tuliyokutana naye Posta tukiwa na yule binti alivyoniona akasimama akageuza kurudi alipopotoka
huku akijifanya anaongea na simu nilimwambia jamaa mmoja amkimbilie amuongeleshe kumzuga ili mimi nifike, mpango ulifanikiwa tapeli akawa chini ya ulinzi tukamshughulikia kufupisha kisa hiki kwenye wallet alikuwa na ID kadhaa za watu huku kukiwa hamna hata ID yake.
 
ungeweka picha yake ingekuwa vyema zaidi, pia hujasema kama mlifanikiwa kuvipata vitu alivyomtapeli huyo ndugu yako.
Alitapeli simu na hela buku 5 ilikuwa Oct 2022 nimemshika tarehe 10/6/2023 isingekuwa rahisi nimkute na simu aliyoiba ni lazima aliiuza
 
NILIMDAKA TAPELI MBEYA BAADA YA KUTAPELI SIMU DAR

Nikiwa Mbeya 2022 nilifahamiana na bwana mmoja anayejulikana kama ngosha
huyu mtu nilifahamiana naye baada ya kuwa tunaonana mara kwa mara sehemu ambayo nilikuwa napenda kushinda ni mtu ambaye tulikuwa tunaheshimiana na ni mtu mzima.

Kwa muonekano wake huwezi fikiria anaweza kuwa tapeli.Mwezi wa 10 2022 nilipoenda Dar nikiwa City Center kwa fundi viatu nikamuona anapita hiyo ni baada ya kutomuona kitambo kidogo kule Mbeya.Baada ya kuonana tukapiga stori mbili tatu tukapeana namba za simu.

Nilimuuliza anafanya mishe gani akasema yuko kwenye ofisi inayojishughulisha na utoaji wa mizigo ya wateja bandarini
,kwa uelewa wangu shughuli hizi hufanywa na ofisi za Clearing and Forwarding japo yeye hakuitambulisha kwa jina hili na hata hii siku niliyokutana naye alidai anaenda bandarini.

Tukiwa tunapiga story hapo kwa fundi viatu kuna mda aliniomba buku 2 kitu kilichonitia mashaka.

Baada ya kumpa namba yangu kuna siku alinipigia simu akidai ofisini kwao wanahitaji mfanyakazi akidai aliyekuwepo amehamishiwa zenji ambako wamefungua ofisi, nilipomuuliza kazi gani akadai mtu wa kupokea wageni na kuingiza data kwenye computer akishindwa kubainisha title ya huyu mtu anayehitajika kufanya hiyo kazi.

Alikuwa anaulizia iwapo kama kuna ndugu yangu yoyote amuunganishe na hiyo kazi,ilinibidi niwashirikishe wenyeji wangu ambao waliniambia kuna binti waliwahi kuishi nae hapo nyumbani alimaliza form 4 pengine anaweza fanya hiyo kazi.

Basi binti akatafutwa kwenye simu wakamjulisha kuhusu hiyo kazi binti akaonyesha ari ya kuitaks hiyo kazi nami nikaona nimwambie yule tapeli kuwa kuna binti anahitaji hiyo kazi ila yuko safarini kuja dar akifika nitakuja nae umueleweshe vizuri kuhusu hiyo kazi tapeli akasema sawa na akasisitiza binti awahi kwa kuwa ofisi haina mtu wa mapokezi.

Baada ya binti kufika dar siku inayofuata nikampeleka posta ili aonane na huyu tapeli ambaye alidai wakionana atampeleka hadi kwa boss. Tulipofika Posta tukaonana na huyu tapeli tukaenda kukaa sehemu tukiwa watatu binti, tapeli na mimi kuzungumzia masuala ya kazi.

Tapeli alidai boss yupo kwenye kikao hivyo anamuwakilisha hivyo tutamalizana naye yeye haina shida.

Tukiwa hapo alidai kazi mshahara ni laki 4 chakula na nauli ni juu ya ofisi aliongea mengi yakutuaminisha kuhusu hiyo kazi hewa aliongea pia juu ya uaminifu wake unaomfanya afanye kazi na watu mbalimbali

Baada ya maongezi tukaachana naye mda wa saa 8 mchana binti akijua siku inayofuata anaenda kuanza kazi wakati tunaachana akatuonyesha ghorofa moja refu sana kuwa ndio ofisini kwao ila nikashangaa kwanini hatupeleki ofisini.

Siku iliyofuata huyu binti alitakiwa akaonane na yule tapeli kisha ampeleke ofisini siku hiyo binti kadamka zake ahsubuhi kwenda posta akaonana na tapeli badala ya kumpeleka ofisini akawa anamzungusha mitaani binti akaanza kuingiwa na wasiwasi mwishowe akamdanganya binti amuazime simu sijui afanya nini binti akampa simu kwa kuwa ilikuwa ina pattern akaomba atajiwe pia pattern za simu akamuazima binti na sh 5000 kisha akapotea.

Simu ya binti na hela vikawa vimepotea kwa style hiyo binti alisubiri toka saa 2 ahsubuhi mpaka saa 6 mchana mtu hakutokea na mpaka leo hatatokea.

Baada ya hiyo ishu nikawashirikisha jamaa zangu wa Mbeya ambao tulikuwa tunashinda nao sehemu fulani ambapo ndipo nilifahamiana na huyu tapeli.Wiki 2 zilizopita huku mbeya kuna jamaa alimuona huyu tapeli akanijulisha hivyo siku moja saa 1 jioni nikawa eneo lile.Nikiwa naongea na jamaa nikamuona mtu kama yule tapeli mita kama 30 hivi akija tulipo kilichonifanya nimtambue ni shati lake ambalo alilivaa hata ile siku tuliyokutana naye posta tukiwa na yule binti alivyoniona akasimama akageuza kurudi alipopotoka.

Huku akijifanya anaongea na simu nilimwambia jamaa mmoja amkimbilie amuongeleshe kumzuga ili mimi nifike mpango ulifanikiwa tapeli akawa chini ya ulinzi tukamshughulikia kufupisha kisa hiki kwenye wallet alikuwa na ID kadhaa za watu huku kukiwa hamna hata ID yake inawezekana ID hizi ni za watu aliowaibia
 
Dar kila mtu kawa tapeli. Trust nobody
 
Back
Top Bottom