Frank Wanjiru
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 25,423
- 46,140
Kutoka kwa dada Mariam Mbano
______
Kumekuwepo na wimbi kubwa la watu ambao wanatumia matatizo ya wengine kuwadhalilisha, kuwatapeli ama kuwafanyia unyanyasaji. Huyu binti anaitwa Josephine David, picha yake imetumwa kwenye mitandao mbalimbali akidaiwa kuwa ni mwizi na tapeli.
Ukweli ni kwamba Joseph alituma taarifa zake mitandaoni, ikiwemo picha na namba za simu akiomba kwa yeyote mwenye nafasi ya kazi amsaidie. Alieleza elimu yake, uzoefu wake na umri wake. Alisema yupo tayari kufanya kazi yoyote isipokuwa kazi ya bar na kazi za ndani.
Kijana mmoja aitwaye Baraka Haonga mwenye namba za simu 0629260222 alidai kuwa anafanya kazi shirika la reli nchini (TRC) akamtafuta na kumuahidi kumpatia kazi. Akampa namba za simu na wakaanza mawasiliano. Wakakubaliana kuonana ili amuunganishe na boss wa TRC. Siku ya kukutana ilipowadia Baraka akatuma location. Binti akapanda gari na kufika eneo aliloambiwa.
Wakaonana na Baraka. Lakini katika hali ya kushangaza Baraka akawa tayari amelipia lodge na kumtaka waingie chumbani. Josephine akahamaki na kuuliza kwanini amemuita lodge wakati alimuahidi anaenda kumkutanisha na boss wa TRC?
Baraka akawa anasisitiza waende ndani kuzungumza na kila kitu kitakuwa sawa. Josephine akakataa, akaondoka. Baada ya kuondoka ndipo Baraka alipochukua picha yake na kuanza kuisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii akimtuhumu kuwa ni tapeli.
Taarifa imetolewa kituo cha polisi Mbagala na kufunguliwa jalada nambari MBA/RB/5643 na tayari Baraka amekamatwa na yupo rumande kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria. Hili ni onyo kwa wote wanaotumia mitandao ya kijamii kudhalilisha, kutweza au kuchafua wengine kwa maslahi binafsi. Tujifunze matumizi sahihi ya mitandao. If you cant help them atleast dont hurt them.!