Nilikua siijui jamii Forums

welcome to the internet where everyone has his/her own opinion.. "welcome to JF" where we dare to talk openly :A S-key:
 
Jana Makamu wetu Pius msekwa alituambia kuwa jamii forums inakipaka matope chama chetu.

Baada ya kuulizia kwa wafanyakazi wenzangu,jamiiforums ni kitu gani,,nimefanikiwa kuelezwa na kujiunga rasmi leo.

Nimesoma post zote, mbona sione uchochezi wowote?

hapo kwneye red sijakuelewa,.we kada au??nina wasiwasi utapata presha humu maana wakina january,tambwe hiza,beno,shegella sijui wamekimbia humu kwa pumba zao,kwa pumba ccm hakuna exceptional hivyo am watching you closely utaanza na pumba ipi...
 
Wenzio tayari tumekuwa mateja wa JF kutokana na sera yake ya uwazi na uhuru wa kujieleza karibu sana
 
Karibu saaana, ila jf yaleo si ile ya zamani. Siku hizi imevamiwa na watu wenye upeo mdogo hawaleti thread zenye kufanya watu wafikirie na kutumia akili.
 
Asanteni kwa kunikaribisha, sehemu gani nzuri za kujivinjari humu?

Jivinjari popote uwezapo(Area of Interest),ila chonde chonde jitahidi kuwa smart,humu kuna majukwaa! Sasa ukitaka uione JF chungu we kurupuka tu!
 
Kauli ya msekwa imetuongezea members wengi sana sio wewe tu maana watu wengi wametaka kujua jf ni nini na ni kwa nini inatajwa kuwa hatari kwa ccm na serikali yake.
 
Jana Makamu wetu Pius msekwa alituambia kuwa jamii forums inakipaka matope chama chetu.

Baada ya kuulizia kwa wafanyakazi wenzangu,jamiiforums ni kitu gani,,nimefanikiwa kuelezwa na kujiunga rasmi leo.

Nimesoma post zote, mbona sione uchochezi wowote?

.
Karibu Surprise.
Ila ni kwa nini umeficha jina lako?
Potelea mbali, tuachane na hayo. msekwa bana ni mwanachama wetu huku Jf kwa jina la Malaria sugu.
Alifanya vurugu za kukiuka maadili na kanuni za jamii forumu na amepigwa ban na uongozi wa jamvi.
Hata wewe chunga sana utamfuata kwa kupigwa ban kama hutazingatia kanuni. Hivyo chukua muda kuzisoma na kuzielewa. Kuna mdau mmoja amekuuliza ni kwa nini umetinga kwenye jukwaa la siasa ilhali kuna majukwaa mengi humu? Sidhani kama umetoa jibu.
Msekwa yupo kwenye foleni za wapiga chabo kwa sasa, ukitaka kujua hili, wewe angalia wafuatiliaji wa post inayotumwa huku utakuta kuna wageni wengi wakifuatilia kuliko members. Mmoja wao ni Pius.
.
 
SURPRISE naona km ugeni hana ila kajivua gamba, anajua kila kona humu ndani,kwa desturi mgeni ukiingia sehemu unashanga shanga kwanza lakini huyu kaanza na zote.
 
Karibu kwa wakomavu wa fikra,
Hapa hakuna chama,
Hapa ni kwa watetea maslahi ya taifa.
Cha muhimu unatakiwa uwe ulikukuwa unaelewa sera za vyama vyote, jukumu tulilo nalo watanzania kwa sasa katika kupigania ukombozi wa kiuchumi, basi hapo michango yako itakuwa ya maana, lakini ukileta uchambuzi usiokuwa na maslahi kwa taifa, JF utaiona chungu sana!!
 
Jana Makamu wetu Pius msekwa alituambia kuwa jamii forums inakipaka matope chama chetu.

Baada ya kuulizia kwa wafanyakazi wenzangu,jamiiforums ni kitu gani,,nimefanikiwa kuelezwa na kujiunga rasmi leo.

Nimesoma post zote, mbona sione uchochezi wowote?

Hakuna uchochezi hapa Mkuu bali hawapendi kuona Watanzania tukijadili matatizo mbali mbali ya nchi yetu ambayo kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na chama kilichopo madarakani. Kuyajadili matatizo ya nchi yetu na kuyahusisha na chama tawala basi kwa Viongozi wa CCM ni kukipaka matope CCM kitu ambacho hakina ukweli wowote na wewe mwenyewe umejionea hapa kwamba hakuna uchochezi wa aina yoyote ile. Karibu sana jamvini Mkuu.
 
Back
Top Bottom