Unajua ccm wanajifanya kujua sana.
Yani fikira zao ni mgando mi nadhani. Sasa mtu mzima kama Msekwa anawezaje kusema jamii forum ndio adui wa CCM? Je humu yanayojadiliwa ni ya uongo? Wao kama CCM then only way ya kujiweka salama ni ku-prove wrong yale yote yanasemwa lakini wanashindwa, sasa jamii ambayo inatumika na watu wasiozidi 40,000, wengi wakiwa mijini na nje ya nchi wanawezaje kukipaka CCM matope...chama kilicho na mizizi hadi huko ambapo barabara hakuna kama Loliondo?
Hapa badala ya kujenga ndio wameharibu sana, mana sasa ndio watanzania wengi, wenye access ya internet, ndio watataka kujua jamii forum, na watakapoingia watajua mambo mengi.... bora wangekaa kimya.
Kwa nini CCM wasianzishe forum yao? si wanatumia vyombo vya habari kama Uhuru, Daily News etc....je hivyo vimeshindwa kukijenga chama?