Nilichosikia kongamano la kiisilamu arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nilichosikia kongamano la kiisilamu arusha

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Kisendi, Mar 29, 2011.

 1. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Wakati habari juu ya babu huko Loliondo zinapumzika kidogo, naomba
  > niwape na haya niliyoyasikia kwa masikio yangu kutoka redio Imani. Hii
  > ni redio ya Waislamu ambayo inatangaza kutokea mkoa wa Morogoro. Sijui
  > kama husikika nchi nzima au la. Hapa kwetu Arusha kulikuwa na
  > kongamano kubwa la Waislamu wa madhehebu yote, jana Jpili na lilianza
  > tangu asubuhi hadi jioni. Walikuwepo watoa mada mbalimbali, lakini
  > mimi nilifanikiwa kumsikia mmoja, pamoja na immamu wa mkoa aliyetoa
  > maazimio ya kongamano.Bila shaka magazeti yataripoti vizuri.
  >
  >
  >
  > Nimesukumwa kuandika tena kwa urefu kwani nilisikitika sana kusikia
  > maneno ambayo sikuwahi kuyasikia tangu nizaliwe yakiongelewa hadharani
  > ndani ya nchi yangu. Nakumbuka nilisoma maazimio ya Mwanza, lakini hii
  > imenistua sana. Kama tunamwomba Mungu basi tuongeze nguvu, kama
  > hatuombi basi tuanze. Kwa mtindo huu, ninawasiwasi na amani ya
  > Tanzania ambayo tumejivunia miaka hamsini sasa. Mliopata neema ya
  > kupata nafasi za juu serikalini, sijui serikali inayaonaje mambo haya.
  > Hayajaanza leo, ila imeyaachia yaendelee. Makanisa yanazidi kuchomwa,
  > hakuna msikiti uliwahi kuchomwa kama sijakosea. Wakristo wanavamiwa na
  > kupigwa, hakuna mhadhara wa Waislamu uliwahi kuvamiwa. Redio Imani na
  > magazeti ya Kiislamu (mfano Al-alnuur) yanazidi kumwaga sumu ya udini,
  > na ubaguzi, na chuki, lakini sijawahi kusikia vyombo hivi vikikemewa.
  > Huu, ukimya wa serikali na vyombo vyake, sijui maana yake ni nini?
  > Sumu hii ikiishapandwa kuing’oa ni kazi. Jamaa hawa walifanya mambo
  > yao sirini tangu enzi za Mwinyi, na sasa, wameamua kuyaweka wazi na
  > kuhamasisha Watanzania waziwazi tuuane. Haiingii akilini mwangu. Je,
  > viongozi wetu wa dini wanazo taaarifa za kutosha kuhusu mambo haya?
  > Wanachukua hatua gani? Je, sisi tuchukue hatua gani?
  >
  >
  >
  > Shehe Ilunga Hassan ndiye niliyeweza kumsikia. Ameongea mambo mengi,
  > lakini yote ni ya kupandikiza chuki ndani ya Watanzania. Ameanza kwa
  > kutoa pongezi kwa kile Waislamu walichokifanya huko Mto wa mbu
  > (Arusha) kwa kuwapiga wachungaji, na kuwajeruhi, nk. Amesisitiza kuwa
  > Tanzania inaongozwa na mfumo Kristo. Na sasa umefika wakati mfumo huo
  > uondolewe na hiyo ndiyo itakuwa pona ya Waislamu. Serikali inaongozwa
  > na maaskofu. Wao ndiyo wanaweza kumwambia rais tunataka hiki au la.
  > Amesisitiza kuwa amani tunayoiona TZ ipo kwa gharama ya Waislamu.
  > Umefika wakati Waislamu waseme basi kwa mfumo Kristo ili na Wakristo
  > wabebe gharama ya amani hii.
  >
  >
  >
  > Ametoa takwimu kuwa mwaka 1992 Serikali iliingia mkataba na Wakristo,
  > na tangu hapo imekuwa ikitoa fedha za kuwaendeleza wao huko Waislamu
  > wakibaki nyuma. Kwa mfano, mwaka 2009, serikali imetoa bilioni 45,
  > mwaka 2010 bilioni 54, na mwaka huu kwa miezi miwili hii na siku
  > imekwisha toa bilioni 611, zote hizi zikiwa ni kuwaendeleza Wakristo.
  >
  >
  >
  > Wakati serikali ikifanya hayo yote, Waislamu wameachwa nyuma na watoto
  > wao wamezidi kuwa wamachinga huku watoto wa Wakristo wakiendesha
  > baiskeli za kizungu na kufurahia beach. Amesema ifike mahali Waislamu
  > waamue kama walivyofanya Wahutu dhidi ya Watutsi.
  >
  > Ati Kikwete hawezi kuongoza nchi bila maaskofu, maana kila analotaka
  > kufanya lazima awaone.
  >
  >
  >
  > Amesema kuwa Chama cha kususa na maandamano kipo tu kwa ajili ya
  > maslahi ya Wakristo. Waislamu wanadanganywa wakidhani hicho chama kipo
  > kuwatetea WaTz kumbe kipo kwa ajili ya Wakristo. Makafiri wanasaidiana
  > wao kwa wao hivyo waislamu waamke, waungane hili kuuondoa mfumo
  > Kristo. Amesema mfumo huu ulianza zamani,kwani hata 1964, Nyerere
  > aliwafunga kina Chief Fundikira na wenzake kwakuwa walikuwa Waislamu.
  > Akaendelea kuwa hata Azimio la Arusha lilikuwa kiini macho kwani
  > liliwalenga Waislamu hata mali zilizotaifishwa zilikuwa za Waislamu
  > Wahindi kwani wakati huo wakristo wengi walikuwa makarani na hawakuwa
  > na chochote. Kwa hiyo Azimio lililenga kuwakandamiza Waislamu.
  > Wakristo na mfumo wao wamekanyaga nyoka mkia, au wanamkamata ng’e
  > mkia.
  >
  >
  >
  > Aliendelea kusema kuwa imefika sasa Waislamu kuongea lugha wanayoilewa
  > makafiri kwani wao hawataelewa kama waislamu wataendelea kuongea kwa
  > njia ya makongamano kama haya. Kuendelea kudai haki kwa njia hii ya
  > mikutano na makaongamano ni kama mtu anayemwambia mbuzi lugha ya
  > kibinadamu wakati hailewi. Mbuzi lugha yake ni kupigwa ndipo huelewa.
  > Ndivyo walivyo makafiri. Ifike wakati waislamu waseme basi.
  >
  > Usilamu hauna historia ya kushindwa. Allah alikwisha wahaidi
  > waisalamu ahela, hivyo wao wana kazi mbili tu, KUUA au KUUAWA, na
  > ndipo watapata zawadi ya ahela. Hivyo ndivyo wanaweza kuuondoa mfumo
  > Kristo.
  >
  >
  >
  > Akasisitiza kuwa huko Rwanda ilifika ambapo ilipotakiwa kuubadili
  > mfumo, Mtusi na Mhutu hakuna aliyelala ndani, sasa Waislamu waseme
  > basi. Akasema kuwa hata kama kunasemwa mabadiliko ya katiba, nayo
  > hayatakuwa na maana kama bado kuna mfumo Kristo. Akasema kwa mfano
  > waislamu wanabaguliwa hata kama katiba inakataza ubaguzi, hivyo, shida
  > si katiba bali ni mfumo Kristo.
  >
  >
  >
  > Amesisitiza kuwa Waislamu hawana historia ya kushindwa hivyo hata sasa
  > watashinda tu. Amekiponda sana chama cha kususa na maandamano
  > akiwasihi Waislamu wasikiunge mkono.
  >
  >
  >
  > Jamani yamesemwa mengi, laiti ningekuwa mwanahabari ningeadika mengi.
  > Kwa ufupi yule bwana amehamasisha chuki, uuaji, kuchukia CHADEMA, nk.
  >
  > Muda wote wafuasi walikuwa wakishangilia kwa TAKBIR! TAKBIR! Yaani
  > kama angesema sasa tunaaza kazi nakwambia kungekuwa na balaa hasa.
  >
  >
  >
  > Ndugu zangu, inaonyesha hawa jamaa wamefanya mikutano,
  >
  > Dar es Salaam, Kigoma, Tabora, Mwanza, Shinyanga, Morogoro, Singida,
  > na sasa Arusha. Wanaendelea hadi nchi nzima wakihamasisha haya na
  > Waislamu kuungana na kuondoa tofauti za madhehebu yao kwani mfumo huu,
  > unawaathiri wote.
  >
  >
  >
  > Baada ya hapo alikaribishwa Imamu wa mkoa wa Arusha naye akatoa
  > maazimio ambayo yaligawanyika katika makundi mawili.
  >
  >
  >
  > 1. MAAZIMIO YA KITAIFA
  >
  > i) Wanaunga mkono maazimio yote yaliyotangulia kutolewa katika mikoa
  > mingine
  >
  > ii) Wanaunga mkono tamko la Immam mkuu (Shehe Issa Bin Simba)- sasa
  > dhuluma basi
  >
  > iii) Wanaitaka serikali kuangalia uwiano wa kimadaraka katika ngazi
  > zote za serikali
  >
  > iv) Wanaiagiza Wizara ya Elimu ifuatilie na kuhakikisha waraka wa
  > mavazi (hijabu,nk), na ibada kwa Waislamu wanafunzi inatekelezwa.
  >
  > v) Wanamtaka waziri wa fedha kuthibitisha uhalali wa mkataba kati ya
  > Wakristo na Serikali wa mwaka 1992.
  >
  > vi) Wanasema suala la mahakama ya kadhi si ombi ila ni lazima
  > litekelezwe na pia TZ ijiunge na OIC
  >
  >
  > vii) Wanaagiza ubalozi wa Vatican uondolewe nchini
  >
  >
  >
  > 2. MAAZIMIO YA KIMKOA
  >
  > i) Halmashauri ya Arusha imepewa mwezi mmoja irudishe mali za Waislamu
  >
  > ii) Waislamu wapewe kibali kujenga msikiti katika kiwanja cha NHC
  > kilicho karibu na Mahali pa Kumbukumbu ya Azimio la Arusha.
  >
  > iii) Mahali ilipo stendi ya daladala ni mali ya Waislamu, irudishwe
  > mara moja
  >
  > iv) Kwa kuwa serikali ya JK ni halali kwa mujibu wa sheria, wanaoleta
  > chokochoko waache mara moja.
  >
  > v) Waislamu wanamuunga mkono Meya wa jiji la Arusha kuwa alichaguliwa
  > kihalali, na wanamtambua kwa nguvu zote. Aachwe afanye kazi. Wao
  > hawatakuwa tayari kuona upuuzi huo wa kumpinga.
  >
  > vi) Kama Chadema itaandamana kama ilivyotoa taarifa ya siku 21, basi
  > nao watatoka ili wapambane nao ili kujihami kwani maandamano
  > yaliyopita yaliwaathiri
  >
  > vii) Wanamwagiza IGP amrudishe kazini yule askari aliyesimamishwa kazi
  > kwa kuwakamata wachungaji huko mto wa mbu. Pia mkuu wa kituo
  > aliyehusika kumsimamisha kazi achunguzwe na kushughulikiwa.
  >
  >
  >
  > viii) Waislamu wanasema sasa dhuluma basi.
  >
  >
  >
  > Ni hayo kwa ufupi jamani.

  ALIYE ARUSHA ATUJUZE NI KWELI AU UONGO, TUZIDI KUSALI JAMANI
   
 2. bmx

  bmx Member

  #2
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tumeshawazoea hao ucpende kuumiza kichwa kuwafikiria,,
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Looo poleni sana, sasa mkishatoa haya matamko mnalia? Pole sana.:hug:
   
 4. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2011
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Kuwazoe sawa, lakini mdharau mwiba...! Kama kuna ukweli basi serikali na intelijensia yake ifanye kazi.
   
 5. Gosheni

  Gosheni Senior Member

  #5
  Mar 29, 2011
  Joined: Oct 28, 2008
  Messages: 188
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 60
  hawa ndg zetu waislamu mm siwaelewi,wao siku zote ni watu wa kuonewa tu.wasizani kama wakianza fujo,wao watapona.kwa nini pawepo na uhasama,sisi wengine tunandugu zetu wa damu tukiwa dini tofauti.

  Hii zambi yote ya udini ipo juu ya kikwete,kwani yeye ndie muhasisi wa haya yote.
   
 6. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nilijiunga uislamu kwa kumpenda bint ambaye kwa sasa ni mama mtoto wangu.ktk miaka 6 niliyokaa kwenye dini hii najuta,kwa haya wanayofanya HAKUNA DINI HAPA!NAJUTA KUWA MWISLAMU
   
 7. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nimesoma kwa masikitiko makubwa sana habari hii huku machozi yakinilenga. Kama ni kweli viongozi hao wa dini wameyatamka hayo hadharani basi basi nchi inaelekea kubaya. Natumaini serikali itachukua hatua za haraka kuwakamata hao watu na kuwafungulia mashaka ya uchochezi na kuvuruga amani ya nchi. Natumaini pia steven wassira akipata habari hii atoe matamko ya kukemea kauli hizo za uchochezi kupitia vituo mbalimbali vya tv kama alivyofanya kwa chadema. Serikali ikikaa kimya juu ya haya basi tutaamini kwamba imebariki kauli hizo.
   
 8. m

  matawi JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huu mziki mzito. NO comment-kwaheri
   
 9. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Lo! hayo Stephen Wasira anayasikia, au kwake mahusiano ya kijamii yanahusu tu vyama vya siasa? Wakati mwingine mtu unashindwa kuelewa namna hawa waheshimiwa tuliowakabidhi mustakabali wa nchi yetu, wanavyopanga vipau mbele vyao; wakati kundi moja la jamii linajitokeza wazi wazi kupandikiza mbengu ya uhasama miongoni mwa watanzania, mh. Wasira anaona hilo siyo jambo muimu kwake bali maandamano ya CDM!
   
 10. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,960
  Likes Received: 20,299
  Trophy Points: 280
  Nitarudi tena, mh!
   
 11. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nimesoma kwa masikitiko makubwa sana habari hii huku machozi yakinilenga. Kama ni kweli viongozi hao wa dini wameyatamka hayo hadharani basi basi nchi inaelekea kubaya. Natumaini serikali itachukua hatua za haraka kuwakamata hao watu na kuwafungulia mashaka ya uchochezi na kuvuruga amani ya nchi. Natumaini pia steven wassira akipata habari hii atoe matamko ya kukemea kauli hizo za uchochezi kupitia vituo mbalimbali vya tv kama alivyofanya kwa chadema. Serikali ikikaa kimya juu ya haya basi tutaamini kwamba imebariki kauli hizo.
   
 12. Bigjahman

  Bigjahman JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 644
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  Co wote aisee,mm kama mwislam ukwel ilniuma mambo waliongea hawa viongoz we2 mtaan nina marafk wakirsto ambao wana shda kama mm au zaid hawa viongoz wana2miwa makafr halsi na wao ndo makafri usengeeeee,ndugu zangu akl kichwan kwako
   
 13. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Tz ina udini. Tatizo baya zaidi ni hao wenye kukanusha na kuspin. Hawataki kuona ukweli, hawataki kujifunza hivyo maangamizi, machafuko nk hayaepukiki kwa mwendo huo.

  Nakumbuka miaka ile ya tisini mwanzoni yalikuwapo mambo hayo....mzee wa ruksa hakushughulikia. Akaja Ben naye akayeyusha, huyu Kikwete ndio kabisa kamwagia majivu ya moto petrol. Inahitajika strong leadership among others to halt the momentum and arrest the situation.

  Ndio, nakubali kuomba, sala na dua ni muhimu hasa katika mambo kama haya.
   
 14. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Ndugu,
  serikali ndio chanzo, mhimili na mnufaikaji mkubwa wa haya mambo. Neno "tumaini" hapo sio mahali pake
   
 15. U

  Uswe JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  wapuuzi hawa
   
 16. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Natumaini waislamu wenye akili timamu na walioenda shule watachambua pumba na mchele katika hayo yaliyozungumzwa. Tatizo kubwa ni kwamba hata hao viongozi wa juu waliotoa matamko hayo shule yao ni ndogo wangekuwa wameenda vidato wasingekuwa na mawazo ya kubomoa kiasi hicho. Bahati nzuri ni kwamba siku hizi kuna waislamu wengi tu wameenda shule naamini wengi watapotezea huo uchochezi.
   
 17. l

  luhwege Member

  #17
  Mar 29, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Si hayo tu kaka wakristo tumefundishwa umpende jilani yako kama nafsi yako,
  wao wamefundishwa kama jilani si muislam huyo ni kafiri.
  Mifano ni mingi tu kuna hii ya kuchinja wanyama wewe mkristo ukichinja wao hawali sasa hapo tujiulize kwanini sisi tunakula walivyochinja? Tulikubali kuwa chini yao hivyo tutazidi kuwa hivyo ni lini tutabadilika kwa misingi yetu hii.
   
 18. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #18
  Mar 29, 2011
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Ni hatari sana hii. Kwa hiyo tuanze kuunda vikundi vya kujihami? Maana wakati fulani ujambazi ulipozidi tulianzisha sungusungu. Leo hii ikitokea vurugu ya kidini mimi pia nitapigana kufa na kupona. Sitapigania dini, maana naamini dini haipiganiwi, Mungu anayehitaji binadamu wampiganie nadhani hana sifa za kimungu. Nitapigania nafsi yangu, familia yangu, nitajihami dhidi ya anayetaka kunidhuru, huyo ndiye nitakayepigana naye. Hebu na sisi tuanze uhamasishaji maana inakoelekea hii nchi ni kubaya sana.
   
 19. m

  mtwevejoe Member

  #19
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kaka,umeenda mbali saaana! ebu pitapita pale mitaa ya Manzese Darajani mitaa ya jionijioni siku za wikiend,kunakuwa na mahubiri yanayotolewa na hawa ndugu zetu wa kiislam,matusi matupu kwa wakristo.wakati mwingine nashindwa kuelewa,kwa nini vyombo vya dola vimekaa kimya,hv na sisi wakrito tukianza kubwatuka kama wafanyavyo wao,kweliii patakalika.
   
 20. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #20
  Mar 29, 2011
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pumbavu kabisa wewe, unaingia dini kwa sababu ya mtu na siyo imani yake binafsi. Utajuta sana
   
Loading...