Nilichosikia kongamano la kiisilamu arusha

nimefuatilia JF kwa mda mrefu sasa, nimekuwa nikiipenda kwa kuwa nimekuwa nikipata taaria za kina. Pia namna gani tutaweza kuleta mageuzi na mwanzo mpya wa nchi yetu iliyoharibiwa. Lakini kwa staili hii ciamini kama hayo tunayoyataka tutaweza kuyafikia kwa haya niyaonayo humu.
Kwanza, wachangiaji wengi wa JF linapokuja suala kama hili linalohusu imani, kunatokea mgawanyiko, wana jf ambao wengi ndio chadema tunajiita sisi, na ndio tunaegemea katika hoja ya kupinga yale ambayo yanahusu imani waislam. Ninachokiona hapa ni kwamba, hawa waislamu ambao na wao wanapigika na hali ngumu ya maisha watapata na wasi wasi juu ya michango yetu humu. Pia na wale waislam waliokuwa wana tusupport tutawapoteza.
Kama ni kweli chadema tunajua na tunataka support ya waislamu, tuungane nao na kuwapa support kwa yale wanayodai kwamba ni haki zao.
Mfano, kama ni kweli wameporwa eneo, chadema isaidie kujua kama kuna ukweli na kusaidia waliodhurumiwa kama raia na c imani, kupata haki yao. Kama kweli wakristu wamewepa hayo mabilioni, cha dema inatakiwa kuhoji kama kweli haisupport upande wowote wa imani
tupunguze jazba katika kuzungumza haya mambo. Kama kila mtu akichangia kwa kusema waislamu hawana shule, mambumbumbu, maana yake ni kwamba wakristu ni waelevu na ndio wanafaa kwa kila kitu, tutakuwa tujenga ama tunarudi pale pale waislamu wanapoholi kwamba wamenyimwa haki ya kupewa elimu? Kwani jukumu la kutoa elimu ni la serikali.
 
Katika zama hizi elimu ni muhimu sana. Dini ambayo haikazanii elimu kwa waumini wake na watu wengine ni hatari. Mambo kama haya yanatokea kwa sababu ya kukosa elimu ya kawaida na ya dini yenyewe. Masheikh wengi hawafahamu kiundani historia, chimbuko na maandiko ya dini yao, ndiyo maana wanafanya upuuzi mwingi, wanaishia; kukariri aya za kiarabu za msaafu, kuona wasio wa dini yao makafir(ushetani mtupu), kuhamasisha waumini wao kuhujumu mali za wa dini tofauti nayo kama Z'bar(ushetani na kukosa elimu), kutetea viongozi wa serikali kwa sababu rais ni wa dini yao hata kama wao pia wanaathirika na hali mbaya ya kiuchumi iliyoletwa na huu uongozi(ujuha mtupu). Narudia tena katika muda huu ni vyema sana kutafuta elimu ya darasani na dini unayoabudu.
 
Mhh,,tulisema matamko ya maskofu yangeleta hisia za udini watu mkabisha.HAYA SASA MNAKUBALI KUNA UDINI?
Hizo bilion 600 wamepewa za nini?maelezo yanatakiwa hapa
 
Jamani hii si UISLAMU! SIO UISLAMU! Waislamu ni tofuati kabisa. Hao waliyosema haya kama alivyoleta mwenye mada ni WAHUNI, NI WAHAINI, ambao wameamua kutumia dini ya kiislamu kutolea upupu wao. Ningependa sana kuona waislamu wanakemea na serikali inawatia hatiani. HII NI HATARI KWELIKWELI. Vijana wasio na shughuli ni rahisi kurubuniwa na hao na kuanza vurugu ambazo hazitasitishwa, kwani kutakuwepo na kulipizana kisasi. Hivi JK atapataje taaarifa hizi!
 
Nadhani hii ni strategy iliyopangwa na jk+ccm kwa nia ya kuiua cdm kisiasa lakini hawajui au hawajali consequences zake. Kwa lolote baya litakalotokea jk ndo atabeba lawama kwa kuwa ndiye aliyeanzisha 'udini siasa' wakati wa kampeni na sasa mbegu inamea kuelekea kwenye 'udini jamii' na ukimya wake kwa haya yanayoendelea ni aidha amepigwa na bumbuwazi hakujua hali ingefikia hivi au anajifariji kuwa lengo lake limeanza kutimia!
 
Leo wasira kawa mzuri tena,si mlimponda kipindi cha maandamano ya cdm THIS IS undumilakuwili bwana.ifike tu wakati tuheshimu imani za watu vinginevo ni matatizo na tuzo la serikali kwa kanisa bilion 600 lisitishwe ama misikiti nayo ipewe kiwango hicho,PERIOD
 
Mhh,,tulisema matamko ya maskofu yangeleta hisia za udini watu mkabisha.HAYA SASA MNAKUBALI KUNA UDINI?
Hizo bilion 600 wamepewa za nini?maelezo yanatakiwa hapa
Matamko ya maaskofu hayajawahi kuchochea watu kufanya maasi kama yenu.
Hata kama makanisa yanapewa hizo 600bil ndo mnataka kupigana na makanisa au serikali ya msilamu(******)? Sie tunapewa na ******! Poleni
Msifikiri kama mtatoka salama pindi mkianza hizo fujo zenu.
Anzeni stand ndogo ya vifodi kama mlivyo tishia muone moto
 
jamani eeh, tusisumbue vichwa kuwajadili hao jamaa, maana kula yao inategemea uchochezi na machafuko, wanatumia mwamvuli wa uislam ili kujinufaisha. Walishindwa wenyewe kwenda shule matokeo yake hata upeo wa kuchambua mambo umekuwa mdogo kiasi kwamba lugha anayoongea atashangiliwa na majuha wenzake Waislam waelewa hawawezi kushabikia na kushangilia ujinga huo. Urithi muhimu kwa watoto ni Elimu, mpeleke mtoto shule apate elimu ili ajikomboe na utumwa wa fikra hao jamaa kinacho wasumbua ni utumwa wafikra ndio maana anadoriki kusema AHERA hipo kwa ajili yao hivyo wao ni KUUWA AU KUUWAWA ndio njia ya kuifikia AHERA, kama kweli huyo ni SHEIKH basi taabu kweli kweli.Akumbuke vita haina macho na anatamka hivyo kwa sababu yeye kazoea kuua kwa MAJINI lakini vita haitumii MAJINI ni risasi na mabomu ingekuwa ni matumizi ya majini basi SADDAM HUSSEIN na MULLAR OMAR na swahiba wake SHEIKH OSAMA BIN LADEN kule AFGANISTAN wangekuwa washindi, lakini kwa sababu vita si majini leo SADDAM ni marehemu tena kanyongwa na WAISLAM wenzake na MULLAR OMAR na OSAMA wanaishi kama digidigi kama kweli wapo hai. SHEIKH huyo hayawani akumbuke kuwa ALIWAZALO MJINGA NDILO LITAKALO MTOKEA (si anatamani kufa vitani).

Waislam kibao tupo nao mitaani ni marafiki zetu jamaa zetu tumeoa na kuoleana nao hivyo huyo HAYAWANI AJUI ATENDALO, Kweli ukiwa na umaskini wa akili ni shida eti dunia ya sasa unatolea mfano mauaji ya RWANDA na kuona kilichofanyika kule ni USHUJAA na UJASIRI kiufupi huyo SHEIKH UCHWARA bado anaishi ktk dunia ya kijima anadhani dunia hii ni ya wajingajinga kama yeye hata haelewi wauaji kama yeye ni nini kinawapata huko RWANDA aende ktk FILES za mahakama ya ICC hapo ARUSHA atapata somo kidogo, AU ajifunze kwa GADDAFI kinachompata sasa. Dunia ya utemi wa kijinga imekwisha ukilianzisha unapata kibano hapo hapo kama GADDAFI. HITLER na MUSSOLINI wapo wapi AACHE ujinga. Kama yeye ni mkereketwa wa UISLAM akajiunge na ELQAIDA au TELIBAN wenzake hadi leo wapo ktk mapambano akapate somo jinsi vita inavyopiganwa yeye anaisema vita na kuisifia wakati anaishi TANZANIA aende AFGAINSTAN au IRAQ ndipo atajua vita ni nini?


Halafu nchi hii ni ya ajabu sana kuna WASIRA na Serikali nzima kimya, utadhani kilichosemwa hapo ni jambo la ujenzi wa Demokrasia na amani nchini, Watu wakitumia haki yao ya kikatiba kuandamana na kufanya mikutano wanasema ni uchochezi wakiamasisha mauaji ya kimbari viongozi kimya, kazi kweli kweli Ila tukumbuke HATA MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA, hivyo CHOKOCHOKO uanza kama utani zisipodhibitiwa zikikuwa tunatengeneza SOMALI nyingine

umemwaga cheche kamanda
 
Matamko ya maaskofu hayajawahi kuchochea watu kufanya maasi kama yenu.
Hata kama makanisa yanapewa hizo 600bil ndo mnataka kupigana na makanisa au serikali ya msilamu(******)? Sie tunapewa na ******! Poleni
Msifikiri kama mtatoka salama pindi mkianza hizo fujo zenu.
Anzeni stand ndogo ya vifodi kama mlivyo tishia muone moto

lakini kama hujajibu hoja zangu bana,hasa kuhusu hizo bilions NI Ufisadi ama halali.
Kuhusu kujaribu jamani hukusikia ya mto wa mbu mbona hakuna cha moto walichoona?WACHA KUONGEA KISHABIKI HAPA SAWA?
Hizo hela wadhani ni sawa kupewa pengo ?short and clear.
 
Mimi binafsi naskitika kama kweli haya waliyasema wanamkosea hata mungu. Mimi nafikiri wakae chini na serkali waongee wafikie muafuka vizuri kuliko kufanya makongamano ya kidini ya kukashfu, Sisi wanatuta makafiri lakini hatusemi chochote na nawaomba maskofu wala makanisa yasijibu yakae kimya watachoka.
 
Ndio maana ninaipenda Israel,maana wao kikitokea kitu kama hiki hawamcheleweshi mtu,huyo mpuuzi anayelalamika hajui kuwa Rais wetu ni muislamu?Afisa mnadhimu mkuu wa jeshi ni muislamu,makamanda watatu wa polisi waliopita wamekuwa ni waislamu na listi ni ndefu sasa yeye alitaka mpaka ateuliwe yeye ndio aone kuwa waislamu wanatendewa haki?
 
Mungu Ibariki Tanzania Tunawaombea na Viongozi wetu wawe na hekima na busara katika matamshi yao. Amina
 
Hiyo ya kusema CHADEMA wakiandamana na wao watatoka kupambana nao ni suicide kwao.
Simple logic, Wakristo ni wengi Arusha kuliko waislam. Unaweza count misiki yote ya Arusha lakini makanisa ni kila kona. Na waislam wengi tu wako CHADEMA. Nimejaribu ku picture itakavyokua kama watetekeleza hili, nikapata goose bumps. Hiyo wangeenda kuifanyia maala pengine na siyo Arusha.
 
hahaaaaaaa bongo bwana sasa wanalalamika na sisi wengine ambao mama zetu ni waislamu na baba mkristo tukamlalamikie nani?mambo mengine bwana mie nadhani hoja zibaki tu kwamba tanzania haina dini wala ukabila na wala ubaguzi wa aina yeyote ile!
Pumbavu kabisa wewe, unaingia dini kwa sababu ya mtu na siyo imani yake binafsi. Utajuta sana
 
Kiukweli matamko ni mengi na hoja ni nyingi pia.
Serikali inashutumiwa kwa mfumo kristo, kwa nini ipo kimya? kuna ukweli wowote? Kwa nini haiwakamati? inaogopa kushindwa kesi sababu madai yote ni ya kweli? Serikali ijitokeze kukanusha haya kama si ya kweli na iwafungulie mashtaka. Kama ni ya kweli pia ijitokeze kurekebisha haya ili nchi iendelee kuwa na amani.

Nawasilisha...
 
Leo wasira kawa mzuri tena,si mlimponda kipindi cha maandamano ya cdm THIS IS undumilakuwili bwana.ifike tu wakati tuheshimu imani za watu vinginevo ni matatizo na tuzo la serikali kwa kanisa bilion 600 lisitishwe ama misikiti nayo ipewe kiwango hicho,PERIOD


Nikiangalia mada nimeona kama serikali iliingia huu mkataba na serikali ya muislam Mwinyi, inachonishangaza kwa nini Mwinyi aliingia huu mkataba ambao mimi kama mkristo nisiye mkatoliki sijui faida yake ni nani hasa aliingia huu mkataba tusipinge bila kujua chanzo tukalalamikia matokeo kwa tutibu chanzo kisha matokeo yabadilike.
Hato siku moja one hawezi kuendelea kwa kulalama bila kutibu chanzo.
 
Viongozi wa waislamu wametekwa na CCM.......na sasa wanataka kuwabadilisha waislamu wenye nia njema ya kudai mabadiliko, Katika jina la Yesu Kristo hawatafanikiwa.........Mungu wetu yu HAI na Kusudio lake litasimama milele.
 
Jamani hii si UISLAMU! SIO UISLAMU! Waislamu ni tofuati kabisa. Hao waliyosema haya kama alivyoleta mwenye mada ni WAHUNI, NI WAHAINI, ambao wameamua kutumia dini ya kiislamu kutolea upupu wao. Ningependa sana kuona waislamu wanakemea na serikali inawatia hatiani. HII NI HATARI KWELIKWELI. Vijana wasio na shughuli ni rahisi kurubuniwa na hao na kuanza vurugu ambazo hazitasitishwa, kwani kutakuwepo na kulipizana kisasi. Hivi JK atapataje taaarifa hizi!


Nasikitika kama Tanzania tumefikia huku! Nasikitika kwa sababu maisha yangu yote nimeshuhudia udugu, urafiki na mshikamano baina ya wenye imani za kikristo na kiislam.Nasikitika kwa sababu hata siku moja sikuamwangalia mtu kwa misingi ya kidini bali Kitanzania.Nasikitika kwa sababu hali inavyoendelea tutatenganishwa na wapendwa wetu kwa sababu tu ya imani zetu za kidini. Hapo kwenye nyekundu ningependa nipaongelee kidogo:
  • Siamini kuwa wanaofanya haya mambo ni wahuni.Wangekuwa wahuni wasingepata ridhaa na mamlaka kusimama ndani ya sehemu za ibada na kuhutubu chuki na uongo
  • Siamini kwamba hawa watu wanaofanya haya, wamekosa uelewa wa mambo.Ingekuwa hivyo wasingeweza kutumia vyombo kama redio na machapisho ( magazeti, vitabu etc) kueneza chuki na propaganda za uongo wakati wanajua kabisa kuwa Serikali ina dola yenye vyombo vyake kama polisi vyenye kusimamia na kuzuia uvunjifu wa amani
  • Kwamba mpaka sasa hakuna jitihada zozote za kukemea au hata kuzuia basi inanifanya nishangae zaidi
  • Mauaji ya Rwanda yalianza hivi hivi kwa kutumia propaganda za chuki!Watu walikaa kimya na kudharau hadi balaa lilipotokea wakaacha ulimwengu mzima ukiwaangalia na kuwashangaa wanavyomalizana kama hayawani mwituni!
  • Nitaona ajabu sana kama serikali yangu ninayoiamini itajifanya haioni wala kusikia na kuchukua hatua muafaka dhidi ya wachochezi hawa
  • Kama kuna tatizo ambalo Waislam wanaona linahitaji kutatuliwa nadhani hata kikatiba wanayo haki kulipeleka mbele ya vyombo husika ili litatuliwe ndani ya sheria
  • Huwezi kudai haki yako kimabavu bila kuzingatia sheria.Ingekuwa hivyo basi wezi wanaotuibia au wanaotuhumiwa kuiba mali za umma tungekuwa tunawafuata majumbani mwao na kuwachoma moto. Hatufanyi hivyo kwa sababu kwanza imani zetu hazituruhusu, pili sheria inataka kuthibitisha pasipo shaka ukosaji ndipo adhabu itolewe.
  • Kutumia mabavu kupata haki hata kama unayo ni sawa na kurudi enzi za zama za mawe ambapo hakukuwepo na ustaarabu wa kuwa na vyombo vya kutatua migogoro. Maadam tunaishi karne ya Ishirini na moja, itakuwa aibu kujifanyia mambo kama vile bado ustaarabu haujatufikia.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mhh,,tulisema matamko ya maskofu yangeleta hisia za udini watu mkabisha.HAYA SASA MNAKUBALI KUNA UDINI?
Hizo bilion 600 wamepewa za nini?maelezo yanatakiwa hapa

Wana jf,
Mwenye datas kuwa wakristo wanapewa hayo mabilioni amwage hapa jamani! Elungata, una maana maaskofu ndo walisema wanapewa 600b?
 
Back
Top Bottom