Nilichokishuhudia mume wangu akifanya siamini

Nilichokishuhudia mume wangu akifanya siamini

ukiondoka ndio umempa nafasi nzuri kabisa vumilia tu hayo ndio majaribu katika ndoa kaa nae vizuri uongee nae atajirekebisha pia sala ni muhimu sana
 
Dada please fuata ushauri wa Gfson.Akirudi kwenye mstari maisha yaendelee.Sahau na samehe kuanzia sasa.Ila formula ya Gf muhimu sana.
 
Jaribu kuongea na ndugu zake wa karibu hasa mama yake mzazi! Labda itasaidia kidogo! Aharggg ndoa ngumu!! WALIOMO WANATAMANI KUTOKA!NA WALIOKO NJE WANATAMANI KUINGIA!
 
Mtegemee huyo hapo kwenye rangi nyekundu pamoja na kuwa umemwandika kwa herufi ndogo. Nina uhakika yeye ni kila kitu kwenye ndoa yako
naamini kwa uwezo wa mungu mko wazima!

napenda kuwashukuru sana kwa michango yenu ambayo huwa mnatoa humu mm n mdau japo huwa siyo mchangiaji sana lakini siyo mara ya kwanza kuleta matatizo yangu hapa na mkanisaidia,

kama utaweza kupitia topic zangu za nyuma utanielewa vizuri ila leo nimekuja na lingine
nimeolewa nina mtoto mmoja ana miaka 5 nimeolewa miaka 7 iliyopita, kipindi chote cha maisha yangu ya ndoa nimepitia mambo magumu sana kutokana na tabia ya ufataki aliyonayo mume wangu lakini mungu amenisaidia mpaka hapa nilipo,
, kama wiki 3 zilizopita kuna mtoto wa kike wa shangazi yake na mume wangu alikuja nyumbani kama kawaida huwa anakuja kutusalimia then anaondoka ila safari hii akawa amekaa sana nkamuuliza vpi unarudi au umekuja mjini kwa lengo gani akaniambia amechoka kukaa kijijini bora akae nyumbani anisaidie kazi za nyumbani nikamwambia sawa, tumekaa nikaona tuna shida ya mfanyakazi katika biashara yetu na yeye kwa elimu yake ndogo hiyo kazi anaiweza, basi nikamweleza mume nae akakubali tukaona kuliko akae nyumbani na kuna msichana wa kazi haina sababu, basi jana kaanza kazi na hiyo kazi anafanya hadi saa nne usiku then wanarudi na mjombaake ( yaani mume wangu)

jana usiku saa nne nikiwa ndo nataka nijilaze kitandani nilisikia gari la mume wang akiwa anarudi coz najua mlio wake, basi nikakaa kama dk 10 gari ipo nje nikajiuliza mbona hafungui geti aingize gar akili ikanijia labda anaongea na simu, nikalala zangu kama dk 20 mbele bado gari ipo silent nje, nikaamka nikatoka nje nikafungua geti taratibu nilishuhudia mume wangu akikisiana na huyo mtoto wa shangazi yake,niliishiwa nguvu nikamsogelea kuwaangalia vizuri bint akashtuka sana akataka kukimbia akashuka kwenye gari, nikamuuliza mnafanya nini hapa akaniambia wanafanya mahesabu nikamwambia mbona giza ebu leta hilo daftari la mahesabu mnalofanyia, akababaika akamuita yule bint akamwambia leta daftari akakimbia ndani chumbani kwake akajifungia akalala, nilistaajabu sana sikuamini nilichokina, mume wangu akaingiza gari ndani akaja chumbani jasho linamtoka sikumsemesha wala kumuuliza chochote nikalala,

leo asubuhi nilipoamka nikamwamsha yule binti nikamwambia ajiandae arudi kwao kajiandaa nikampa nauli nikamwambia asije tena nyumbani kwangu.
wapendwa kichwa kinaniuma na kinachoniuma siyo kuwakuta katika hali ile ila roho inaniuma mume wangu alipofikia ukiangalia yule binti ni ndugu yake wa damu kabisa ana miaka 17 tu, mume wangu ana miaka 47 mtu mzima, nimefikiria cha kufanya nakosa sina wa kumueleza naogopa mume wangu ni kiongozi nikisema kwa watu ni aibu natamani nifungashe niende kwanza nyumbani kwetu kwani naishi mbali na wazazi labda huyu mume atabadilika nikiondoka au nifanye nini msaada wenu jamani
 
Naomba tu nikuulize maswali kadhaa, labda nitakurudisha nyuma sana;

Mume wako kabla hamjaoana ulimchunguza vizuri tabia yake?

Ni kitu gani kilichokushawishi hadi ulikubali kufunga naye ndoa?

swali la ili unataka akujibu ni MAHELA
 
Hao wanajua mbinu zote za kuwa hivyo, ndio maana hawaupati

Yaani kuna Boss wangu, ni mchafu wa kupindukia; ila humuoni hata na kakikohozi. Life is not fair kwa kweli, the way ninavyomuhate!!!!!!!!!!!
 
ni mbishi huwezi kuongea nae atakana tu!
Dada kama hadi umri huu mumewo anapambana katika huo uwanja ujue yuko ukingoni na usikimbie just mpe miaka mingine 5 atatengamaa ila uwe mvumilivu.

Kisa cha kweli mimi ni mfano kwani mume wa mama yangu alimpa mimba na kumzalisha mtoto wa dada yake ila mama yangu alivumilia ili atututnze and here we are!!!!.

Epuka kuwapa watoto adhabu kwa kosa la baba; kukimbia hakuta solve chochote inabidi uvumilie mithili ya mwanamke aliyetarajia kujifungua mtoto mzima lakini akajifungua mtoto asiye na miguu na mikono; whata are you going to do; je utakimbia hospitali umwache au itabidi tu umtunze mtoto wako? Hii ya mume kuwa fuska kiasi hicho ni mambo ya kupita kwa hiyo usiache ndoa yako kwa mambo kama hayo kwani hapao ndo unatakiwa kuonyesha ukomavu. Asikudanganye mtu yeyote ukakimbia kwani ushujaa wako utapotea utakaporudi; nakueleza hivi kwa sababu kwetu waTZ ni mara chache mke anaondoka moja kwa moja kwani nijuavyo hata ukikaa 10 years lazima ipo siku utarudi
 
kwa hiyo age ya huyo mume,hahitaji vikao tena.huo uzinzi wake,kuacha ni aamue mwenyewe tu na sio kwa kuambiwa.inauma ukiangalia ya kuwa unalala nae kila siku na unamuona ndani mtu ambae amekuumiza.kama kusema umeshasema.na huyo bwana kama ulivyosema alikurubuni wakati ulikuwa mdogo,ni kuwa anapenda watoto wadogo.huyo bwana haogopi ukimwi jamani.kuna watu wanajuta baada ya kupata hilo gonjwa kwa uzinzi wao.fanya maamuzi ambayo unayaona yanafaa kwako na kwa mtoto wako.maana sometimes mambo ya ndoa ni magumu kutoa ushauri
 
:msela😛ole sana dada yetu,kila ndoa na matatizo yake,unaweza kudhani lako ni kubwa kuliko yote.kuna wengine wengi tu wanawafuma bwana zao wakiliwa tigo na wanaume wenzao sembuse la kwako hilo dogo,hauitaji kuwa na haraka ya kufanya maamuzi,jifikirie sana pia tafuta ushauri kwa wale wenye uzoefu kwenye ndoa kuliko kwa watu ambao hawajawahi kuoa/kuolewa
 
Yaani akisikia unamtakia kikohozi anakufukuza kazi

wa hivyo huwa hawaugui hata vipele, mzima January hadi Dec

Yaani kuna Boss wangu, ni mchafu wa kupindukia; ila humuoni hata na kakikohozi. Life is not fair kwa kweli, the way ninavyomuhate!!!!!!!!!!!
 
MI NAOGOPA KUKUSHAURI HUYO BABA ANA AKILI ZAKE TIMAMU DAI TALAKA YAKO KISHA MPELEKE MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MTOTO wa WATU MARA KWA MARA NDO WAZEE WANAOTUHALIBIA WATOTO WETU HAO KWANZA HAKUFAI KABISA ZEE ZIMA LINAKAVULIA CHUPI KATOTO KADOGO KAMA AKO FANYA MAAMUZI MAGUMU ILI IWE FUNDISHO KWA WENGINE WANAOCHEAT NA VITOTO VIDOGO , AMEAMUA ALE KUKU NA VIFARANGA VYAKE MWAACHE AKANYEE DEBE ASIJE AKAMTIA MIMBA MTOTO WA WATU.
 
Back
Top Bottom