Kwa kumpenda mumeo, mtoto wako na wewe mwenyewe nakushauri yafuatayo;
Achana nae na uendelee na maisha yako! Usipofanya hivyo yafuatayo yanaweza kukutokea;
1. Kuambukizwa magonjwa ya zinaa
2. Kuambukizwa UKIMWI na kufa kifo cha huzuni
3. Kama mtoto wako mdogo ni wa kike ipo siku mumeo atambaka
4. Kama mtoto wako mdogo ni wa kiume ipo siku mumeo atamlawiti
5. Atakuletea watoto wa nje wengi hivyo kuleta kero na bughudha kwenye familia.
6. Kuishi maisha ya huzuni na kukosa amani, hivyo utapungua, mng'ao na uzuri wako utapotea, roho ya ukatili na chuki itakuingia, pressure itakuwa juu, Stroke itakunyemelea
Huyo zinaa imemzidi. Kama ni mtu wa dini piga goti chini msamehe KISHA endelea na maisha yako!!!! Jitahidi mtoto asiwe affected na upuzi wake.
Pole sana
Kwa mtu kama huyo, ukiondoka si utakuwa umemsaidia sasa kuimport hata machangudoa ndani? Kama ameshindwa kumheshimu ndugu yake. Yaani mjomba wake, hivi kweli atamheshimu nani? Lakini mke pia ajiangalie labda hampi vema mmewe. Au kuna mapungufu fulani yapo ndani ya ndoa yenu. Si vizuri kuhukumu upande mmoja. Inawezekana kuna kitu huyo mme anakosa kwako. But hii ni extreme, ameshindwa hata kuchukua madada poa huko arudi kuchukua mwanae?
Mungu wangu moja.........hata siamini....hv akiingiza inaingia kweli......hata kusimama itasimama kweli kwa ndugu yako......pole sana davina........
Naogopa haya hapa
1.mwenendo wake na hiv
2.jinsi ya kutoa ushauri....mzee wa miaka 47.......tena kiongozi nina uhakika atakua ni ccm
davina
Kuondoka nyumbani SIO SULUHU, ni kuyakimbia matatizo.
Unachopaswa kufanya ni, kama wewe ni Mkristo, ninaamini ni hivyo, ni kwenda kwa Kiongozi wa Kanisa aliye karibu nawe. Mwite, aje nyumbani, awasikilize kila mmoja kwa wakati wake, kisha mkae kwa pamoja.
Mzungumzie matatizo yenu, muyakabili, mfanye maombi. Msameheane, muanze upya.
Kuna mambo ambayo mlipoanza maisha mlikuwa mnayafanya, lakini sasa hamyafanyi. Jiulize, kwa nini?
Mojawapo ya mambo ambayo hutokea kwenye familia nyingi - za Kikristo au Kiislam, au hata kwa wale walio katika imani tofauti - ni kuacha kumtumikia Mungu. Watu hawaendi kufanya Ibada, wanazembea, wanasema: Niko busy na maisha.
Kumbuka alivyoimba Bushoke: Hayo maisha yasije kukuchanganya, ukaabudu wengine ukamwacha Mola.
Nini maana yake? Kumwacha Mola ni nini?
Unapoacha kumtumikia Mungu, imani yako inashuka, Shetani anapata mwanya MKUBWA wa kukuingilia, kisha unapotoka. Unakosa woga mbele ya Mungu. Shetani anakupa imani ya uongo. Unajiona mwenye nguvu kumbe umeingia SHIMONI kwenye giza tororo! Hujijui. Unaanza kumdharau mumeo/mkeo. Unatamani wanawake/wanaume wasio wake/waume zako. Unazini. UMEKWISHA.
Lakini Mungu ni Mwema, kwani ni Mwingi wa Kusamehe. Kwa wale wote wenye imani au wasio na imani, wakiamua kutubu na kuungama kwa Mungu, husamehewa dhambi zao, ambazo hufutwa, nao huzaliwa upya.
Ukiondoka na kwenda nyumbani, Shetani ataukaza kabisa moyo wako. Huyo anayekuambia uondoke uende nyumbani HAMJUI MUNGU! Anakupotosha.
Kwani kuna binadam gani ASIYEKOSA? Jiulize: Unapokata tamaa kwa huyo mume wako, je, Mungu amekuvumilia wewe kwa makosa yako kwa muda gani?
Sikufahamu, lakini huu ndio naona kuwa ni ushauri bora kwako, kwani HAKUNA KINACHOSHINDIKANA kwa Mungu!
Ukae kwa amani, Mtumishi wa Mungu.
Nakutakia kila la heri kwenye ndoa yako. Mbarikiwe. Mumrejee Mungu na mdumu daima kwenye ndoa yenu takatifu.
Alichounganisha Mungu hapa duniani na mbinguni, asitengue binadamu!
Amina!
Kwenye kumchukua ndugu yake kwakweli hapo naona ni dalili ya laana. Though going home will not help either. Kama dada ni mfanyakazi, mnafikiri kwamba aache kazi ili akakae home mwezi mmoj angalau, au ahame nyumba akapange mahali pengine? Natafakari, sioni ushauri mzuri kwa huyu dada.Unaona hata kama mke hampi vizuri haiwezi kuwa sababu ya kumchukua ndugu yake!
Huyo dada aondeke kwa muda hapo home ili ali-fresh akili. Na option nzuri arudi kwao.
Akikaa ndani atakufa kwa kihoro
Well, naona umejibu vyema maswali yangu...nilikosea tangu mwanzo na sitaki kukumbuka, lakini jua alinirubuni nikiwa binti mdogo sana!
Ushauri wa maana huo. Like miaMh mimi nakushauri usiondoke zungumza naye na umkanye na sasa umwangalie kwa karibu zaidi.
Dawa ni kukaa kimya tu, wala usimuulize kitu, utakuwa unamuumiza kuliko maelezo
safi sana huyo mumewe kweli wakajanga....wee ameona umechoka wacha ale nyama fresh!!!
Na ukiondoka jua umemfungulia mwenzio ataendelea gegeda kwa raha zake
ni hivyo ndiyo jaribu ambalo ninalo
mwenzio ndio ataona my wife wake "du kinaa".
Shetani anakemewa, huwezi kumwona nyani anakula mahindi shambani kwako halafu ukae kimya.
ndo maana yake, tena atajiachiaje! Lakini mboo si yake bwana, angemuacha ajinafasi tu kwa raha zake. Na yeye akitaka akajinasi kwa raha zake. Ndoa pasu kichwa hizi, bora kuwa digital tu kama mie, naibiwa na mi naiba kama kawa, no wivu no love! Ni maelewano tu ndani ya nyumba.
naamini kwa uwezo wa mungu mko wazima!
Napenda kuwashukuru sana kwa michango yenu ambayo huwa mnatoa humu mm n mdau japo huwa siyo mchangiaji sana lakini siyo mara ya kwanza kuleta matatizo yangu hapa na mkanisaidia,
kama utaweza kupitia topic zangu za nyuma utanielewa vizuri ila leo nimekuja na lingine
nimeolewa nina mtoto mmoja ana miaka 5 nimeolewa miaka 7 iliyopita, kipindi chote cha maisha yangu ya ndoa nimepitia mambo magumu sana kutokana na tabia ya ufataki aliyonayo mume wangu lakini mungu amenisaidia mpaka hapa nilipo,
, kama wiki 3 zilizopita kuna mtoto wa kike wa shangazi yake na mume wangu alikuja nyumbani kama kawaida huwa anakuja kutusalimia then anaondoka ila safari hii akawa amekaa sana nkamuuliza vpi unarudi au umekuja mjini kwa lengo gani akaniambia amechoka kukaa kijijini bora akae nyumbani anisaidie kazi za nyumbani nikamwambia sawa, tumekaa nikaona tuna shida ya mfanyakazi katika biashara yetu na yeye kwa elimu yake ndogo hiyo kazi anaiweza, basi nikamweleza mume nae akakubali tukaona kuliko akae nyumbani na kuna msichana wa kazi haina sababu, basi jana kaanza kazi na hiyo kazi anafanya hadi saa nne usiku then wanarudi na mjombaake ( yaani mume wangu)
jana usiku saa nne nikiwa ndo nataka nijilaze kitandani nilisikia gari la mume wang akiwa anarudi coz najua mlio wake, basi nikakaa kama dk 10 gari ipo nje nikajiuliza mbona hafungui geti aingize gar akili ikanijia labda anaongea na simu, nikalala zangu kama dk 20 mbele bado gari ipo silent nje, nikaamka nikatoka nje nikafungua geti taratibu nilishuhudia mume wangu akikisiana na huyo mtoto wa shangazi yake,niliishiwa nguvu nikamsogelea kuwaangalia vizuri bint akashtuka sana akataka kukimbia akashuka kwenye gari, nikamuuliza mnafanya nini hapa akaniambia wanafanya mahesabu nikamwambia mbona giza ebu leta hilo daftari la mahesabu mnalofanyia, akababaika akamuita yule bint akamwambia leta daftari akakimbia ndani chumbani kwake akajifungia akalala, nilistaajabu sana sikuamini nilichokina, mume wangu akaingiza gari ndani akaja chumbani jasho linamtoka sikumsemesha wala kumuuliza chochote nikalala,
leo asubuhi nilipoamka nikamwamsha yule binti nikamwambia ajiandae arudi kwao kajiandaa nikampa nauli nikamwambia asije tena nyumbani kwangu.
Wapendwa kichwa kinaniuma na kinachoniuma siyo kuwakuta katika hali ile ila roho inaniuma mume wangu alipofikia ukiangalia yule binti ni ndugu yake wa damu kabisa ana miaka 17 tu, mume wangu ana miaka 47 mtu mzima, nimefikiria cha kufanya nakosa sina wa kumueleza naogopa mume wangu ni kiongozi nikisema kwa watu ni aibu natamani nifungashe niende kwanza nyumbani kwetu kwani naishi mbali na wazazi labda huyu mume atabadilika nikiondoka au nifanye nini msaada wenu jamani