Wana MMU hata cha kuwalipa sina ila mwenyezi mungu ndio atakayewalipa kwa nasaha zenu zilizokwenda shule. Hakuna hata mmoja ambaye amenishauri jambo likanikwaza, kwa kweli wote mmeongea kuonyesha wote ni wanafamilia ya MMU.
Nashukuru sana kwa hilo na muendelee hivyo.
Sasa basi kwa ufahamisho tu wapenzi, baada ya kumkalia kooni huyo shemeji yenu bandia kua uhusiano kwishnei na yeye hili neno hataki kulisikia, leo nina kikao nae joini, amekiomba yeye, eti atafunguka kunieleza background yake ambayo aliogopa kunieleza siku za nyuma kwa kudhani hatonipata.
Week end pia ameahidi kunitambulisha kwa wazazi wake ambao wote wako Dar.
Mtoto wake mmoja wa kiume ndio kasema ni simple atanitambulisha kwake kwanza kabla ya wale wakubwa wakike ambao anasema kitabia hawajakaa sawa, hivyo inabidi awaweke sawa kwanza kabla hajanikutanisha nao.
Lakini wapenzi naomba tu niwaambie, baada ya kusoma nasaha zenu wote zilizojaa busara, kuolewa na huyu mtu haipo tena, kwani nimeishi miaka yote hii bila mume, nimeharibikiwa na nini. Kama nitaridhika na maelezo yake tutaishi kama bf na gf that's all. Sitaki kesho nife halafu watoto wangu wapate tabu kwa sababu ya mtu ambaye mimi mwenyewe nimemleta kwenye familia ambaye kumekutana wakati umri umeshaenda awape tabu watoto wangu.
Kuna wengine wamesema labda hana kazi. Naomba niwahakikishie kua yuko kazini, na ofisi yake nimeshaenda mpaka boss wake na wafanyakazi wenzie baadhi nawafahamu kwani aliwahi kunialida kwenye function ya ofisini kwao. Hilo halina mjadala ila tatizo tu ni hizo jazba zake na kulazimisha ndoa ya kuishi kwangu, hapo ndio kuna utata.
Sijawahi kumpa msaada mkubwa sana wa kutisha zaidi ya mambo madogo madogo sana kwani nilishamuonyesha toka mwanzo kua mimi ni mwanamke na yeye ni mwanamme no matter what, hivyo a play roll zake kama baba anavyotakiwa.
hiyo kidogo ilimrudisha nyuma, hivyo kama alikua anategemea kupata chochote kwangu, alijua hakipo kwa sasa.
Naomba niwashukuru sana sana kwa ushauri wenu na sitasita kurudi tena kuwapa updates za kikao maana hili litakua fundisho si kwangu tu bali ni kwa wengine pia.
Asanteni na muwe na asubuhi njema....