Niko Njia Panda.... Ushauri wenu ni muhimu

Da Asia, mimi nakupa lawama wewe moja kwa moja!
Umekuwa na uhusiano na mwanaume kwa miezi mitano;
...Huwajui watoto wake?
...Hujui hata anapokaa?
Mko katika uhusiano wa aina gani;
...Anakuja kwako tu siku zote na wewe huulizi wapi anaishi, ama anaishi na nani?
...Kwa nini asikutambulishe angalau kwa ndugu yake mmoja?

Je, akifia kwako usiku(siombi/sisemi hivo) utampeleka kwa nani?

Au jamaa Yahaya?
 
Mtafute/m PM Lara 1 nahisi kwa hii tatizo lako kwake atakupa bonge la wazo na nahisi

litakuwa muafaka.
 
Dada Pole sana kwa maelezo haya huyo mwanaume hafai sababu inawezekana yote aliyokwambia ni ya uongo. Inakuwaje hataki ufahamu anakoishi je huoni kama ni hatari kwako kukaribisha mjitu wa aina hiyo nyumbani kwako. Ni kweli unahitaji mwenza lkn si wa mashaka namna hii. Anajifanya anakupenda sana kitu ambacho si kweli , mwenzako amekuja kwako akiwa na business plan yake na hiyo ndiyo anayoitazama zaidi.

Kuwa makini na watu wa dizaini hii watakuliza bure. Kuna wengine hawapendi kujulikana kwani wana mambo ya kutisha huko nyuma ya pazia.Kabla hujaendelea na huyu tafuta kwanza kujua anaishi wapi na nani na kwanini yuko peke yake. Nasema hivi kwa sababu wengine wamekimbiwa na wake zao kwa tabia chafu au waliwatishia kuwaua. Hebu fikiria umehamia kwenye nyumba yako na huyu jamaa akaamua kufanya lake wanao utawaachaje. Wengine wanaongoza kwa dhuluma hata uwe umeweka mambo sawa namna gani.

Dada yangu sikutishi bali napenda kuyaangalia mambo kwa namna zaidi ya 1. Wewe ni mtu mzima unajua anaekupenda na asiyekupenda so kuwa mwangalifu na watu wa aina hii kamwe usikaribishe mtu nyumbani mpaka uwe umejiridhisha na mambo mengi juu ya mtu huyo. Kwa huyu shemeji sisemi kitu bali akili mkichwa my sister. Afadhali amani kuliko kuishi kwa mashaka. Jiulize ni mwanaume gani mwelevu anayeweza kung'ang'ania akaishi kwa mwanamke tena analalamika kila mara kipato chake kidogo hii kali aisee.
 
Da Asia,

Nimekupm. In short this is very red alert , the most dangerous. A very close person in the family alipata mtu wa dizaini hii baada ya kuwa single (mjane) for 6 yrs .... what happened ni alitapeliwa kila kitu na mwishowe watoto wake (kama wako wamesoma nje) walimsema mama yao mbaya hadi akacommit suicide ..goodluck she was rescued.

Umefanya makosa sana kumwonyesha mali zako kabla yeye hajawa open.

Dada huyu mtu mkimbie sana na kama unaweza fanya inteligensia ya kutosha (talk to Police investogators hawa walipe pesa nzuri upate full data ) la sivyo huyo huyo unayemdhania ni life patner ndio atakuwa wa kwanza kukuletea majambazi nyumbani (im saying with experience)

Please Please Run away and take all safety precautions . huko site make sure haendi ng'o na home asije katu katu. Pia very important katika kuachana usimpe nafasi ya kujieleza , this is where he will take the chance to murder /destroy u. Please love life ,Love ur kids and family .Huyu ni Jambazi sugu
 
aisee nkupe hongera dada,ur a super woman,watu wengi wanapenda kulalamika sana,ts good u'handle ur life..jamaa hapo juu kasema vzur,tumia ht polisi wakusaidie kumjua ni nan,anavojistukia tht hana hela all th tym kashaona we unazoo,u deserve a better and wealthier man aisee,stress za kukuza watt on ur own zishatosha ,u need settlement,Mungu akutangulie
 
Da Asia,

Nimekupm. In short this is very red alert , the most dangerous. A very close person in the family alipata mtu wa dizaini hii baada ya kuwa single (mjane) for 6 yrs .... what happened ni alitapeliwa kila kitu na mwishowe watoto wake (kama wako wamesoma nje) walimsema mama yao mbaya hadi akacommit suicide ..goodluck she was rescued.

Umefanya makosa sana kumwonyesha mali zako kabla yeye hajawa open.

Dada huyu mtu mkimbie sana na kama unaweza fanya inteligensia ya kutosha (talk to Police investogators hawa walipe pesa nzuri upate full data ) la sivyo huyo huyo unayemdhania ni life patner ndio atakuwa wa kwanza kukuletea majambazi nyumbani (im saying with experience)

Please Please Run away and take all safety precautions . huko site make sure haendi ng'o na home asije katu katu. Pia very important katika kuachana usimpe nafasi ya kujieleza , this is where he will take the chance to murder /destroy u. Please love life ,Love ur kids and family .Huyu ni Jambazi sugu

are you a counsellor? May i be you client? Nimekuelewa vilivyo i wish nikutafute kwenye matatizo yangu chungu kizima nilonayo u have all we called counselling skills uknow! May GOD be with u. Amen
 
Mimi ni mdada above 40 niliolewa nikaachana na mwenzangu some years ago. Kwa vile nilikua busy kusomesha watoto zangu watatu ambao sasa wameweza kujitegemea, sikutaka kua na uhusiano wa kimapenzi na mtu yoyote maana elimu ya watoto wangu na kuwasimamia was my priority.
The time has now come that I need a companion wa kumalizia nae hii n’ngwe ya maisha niliyobakiza kuliko kua mwenyewe. Watoto pia wameshasambaratika kuhangaika na maisha. Wawili wako nje ya nchi wanafanya masters na mmoja ambaye ndio mkubwa ameshaolewa ana degree ya BSc electronics aliyopata UDSM.

Nimekutana na kaka mmoja above 40 nae japo nimemzidi 3 years, hii hainipi tatizo kwani umri kwangu sio shida, most important kwangu is how we feel for each other. Nae aliwahi kuoa akazaa watoto wanne lakini pia akaachana na mkewe. Mtoto mmoja katika hao wanne alizaa wakati wa ujana na mwanamke mwingine ambaye hawakubahatika kuoana. Aliyemuoa ndio walizaa watoto watatu.
Ni miezi kama 5 – 6 hivi tangu nifahimiane na huyu kaka. Sote ni waajiriwa japo mimi kipato changu kinamzidi mwenzangu. Hili pia si tatizo kwangu, kama nilivyosema mwanzo najali tunavyojisikia tukiwa pamoja.

Tatizo kubwa ni kwamba, huyu bwana amekua kama limbukeni wa mapenzi tangu tufahamiane. Kama ni kupendwa kwa style hii mwenzenu nahisi nashindwa. Amekua king’ang’anizi kupita maelezo na wakati mwingine kulazimisha yasioyowezekana.

Analazimisha anataka kuhamia kwangu na atanioa. Sio tatizo kwangu lakini kwa maisha niliyoishi for years nikiwa mwenyewe sio kitu naweza kuamua in a night. Hataki kuelewa kwa namna yoyote ile. Juzi juzi hapa tulikwaruzana, actually niliamua kuachana nae kabisa! Lakini alinipa vitisho sana, kwamba siwezi kumuacha na hayuko tayari kuniacha hata iweje. Mpaka alitaka kuja kuleta fujo nyumbani baada ya kumwambia sitafungua gate akija.

Naomba mfahamu kwamba huyu anayejifanya ananipenda kupita kiasi, hana msaada hata mmoja katika maisha yangu. Nahangaika na maisha yangu mwenyewe kama nilivyozoea, ninachokula au ninachovaa nakijua mimi. Yeye kutwa ni kujitetea kua kipato chake ni kidogo kuliko cha kwangu japo sioni kama ni kigezo cha kutotoa msaada kama baba mtarajiwa. Sihitaji msaada 100%, hata 20% kwangu nitashukuru maana sijashindwa kuendesha maisha yangu. Ila msaada wake kidogo kwangu will mean so much ili kudumisha uhusiano wetu. Sasa hivi nina wasiwasi maana ananisumbua kupita kiasi kua lazima tuishi pamoja. Siwezi kuamua hili mara moja hasa kutokana na maisha niliyoishi ya muda mrefu nikiwa mwenyewe na pia nina watoto, I have to make them understand, na siwezi kuwafanya waelewe kwa mara moja. Watoto ni wakubwa na wana akili hivyo ni lazima niwapeleke polepole waelewe kua nili sacrifice my love life kwa sababu yao na sasa nahitaji mwenza. Sijui watalielewaje hili maana ni process. Hapa napo mkinishauri jinsi ya kulileta kwa watoto nitashukuru, maana naamini hapa jamvini wapo waliopitia mtihani kama huu.

Kikubwa ambacho ndio mtachoka, mtu huyu mwenye mapenzi mazito kwangu, sijui anaishi wapi..... japo yeye anajua kwangu na watoto wangu wawili anawafahamu. Huyo mmoja anayeishi nje ya nchi alikuja likizo wakaonana alipokuja nyumbani. Wanamjua as Mama’s friend, japo nahisi vile ni wakubwa they might have smelt something, japo hainipi shida maana mwisho wa siku its my happiness. Simfahamu mtoto wake hata mmoja maana anasema watoto wake hawawezi ku support yeye kua kwenye mahusiano, sina hakika na hili, sasa sijui akiamua kutelekeza watoto watatu ambao anaishi nao itakuaje, maana mmoja huyo mdogo anaishi na mama yao, nashindwa kupata hesabu inayojumlishika kwa hili. Niko katika harakati za kumalizia nyumba yangu nje ya mji ambayo nahamia soon, ana insist kua tuhamie pamoja, nisiende kuishi mwenyewe maana ni sehemu ya ugenini na nyumba ni kubwa. He’s got a point in a way, lakini haiwezi kua rahisi kiasi hiki anavyofikiria yeye. Kwangu mimi bado niko njia panda. Pia hatujawahi kujadili kua anakuja kuishi na mimi kwa namtiki gani na watoto wake atawaacha wapi. Vile ni kitu ambacho sijakiunga mkono 100% hata nguvu ya kuuliza haya sijawa nayo.

Naomba ushauri wenu wapendwa, hivi unaweza kweli kumpenda mtu kwa moyo wako wote, lakini mwenzio asijue unakoishi zaidi ya kazini kwako na usitoe msaada hata mmoja kwake, ilhali ukienda kwake unataka ukarimiwe kwa chakula na mapenzi? Hii mimi hainiingii akilini.

Tulipokwaruzana juzi niligundua nilifanya makosa kumfanya awe free nyumbani kwangu, as he used to come any time. Japo alikua anaingia chumbani kwangu only kama tuko wawili tu ndani ya nyumba, maana nina msichana wa kazi ambaye weekends mara nyingi anaenda kwao kusalimia na binti wa mdogo wangu ambaye namsomesha. Naye pia weekends anaenda kwa mama yake. Baada ya kugundua hilo kosa na mkwaruzano uliokuwepo, nilimwambia kuanzia sasa hatakuja tena nyumbani kwangu. Tutaonana nje ya nyumbani kwangu, in a hotel, for drinks, dinner etc... lakini kwangu sio sasa mpaka niweke mambo sawa na watoto. Hili tunalumbana nalo kwa karibu wiki mbili sasa hataki kunielewa. Anadai yuko more comfortable kama tutaonana nyumbani kwangu. Mimi nahisi anapenda kuja kwangu kwa vile he gets everything for free. Samahani kama nitawakwaza wanaume lakini ndivyo nidhaniavyo, maybe am wrong, mtaniambia. Tangu kumetokea kutoelewana hajaja tena nyumbani maana nimekataa kata kata ila tunaongea kwenye simu na kubishana ndio kwingi zaidi maana hataki kunielewa. Naomba mnijuze kama nina kosa hapa.

Niliamua kumueleza kua, kama yeye ameona haiwezekani mimi kujua kwake na kufahamu watoto wake vile anawaheshimu, kwanini mimi pia hataki ku consider hili? Kama ni makosa nilishayafanya, na nimegundua, sitaki kurudia tena! Hataki kuelewa, maana ameshikilia kwa vile mimi nina kipato namnyanyasa vile hana uwezo wa kulipia hotels, drinks and maybe meals if we decide to sit somewhere kuongea.

Kwa kweli sijui nielezeje maana mimi sio mwandishi mzuri but niko njia panda! Nawagetemea nyinyi mnipe ushauri maana huyu baba si muelewa. Kutwa anajitetea kua mimi namnyanyasa kwa vile hana kipato kizuri kama mimi. Ni mtu wa kulalamika kutwa hana pesa! Kwa kweli nachoka maana hata mimi nina shida zangu na majukumu ya ndugu lakini silalamiki kwa mtu yoyote kuhusu matatizo yangu, sana sana natafuta ufumbuzi mwenyewe. Mwanamme mzima kutwa kulalamika hana pesa kwa mwanamke, mimi sioni kama ni sawa.

Naomba msinihukumu kwa lolote, ninachotaka ni msaada wa ushauri maana nimekamatwa na huyu baba ambaye nashindwa kujua ananitafuta nini kusema kweli na nitamtoka vipi maana hataki kusikia kitu kinaitwa kuachana.

Samahani pia kwa kuwachosha, mimi sio mwandishi mzuri hivyo uandishi wangu ni wa kuzunguka zunguka ila naamini mtanielewa.

Miezi 5-6 ni mda mdogo sana kumjua mtu. Huyo nafikiri anataka kukutapeli pesa zako na kukutumia.
Wanaume matapeli ndio wapo hivo bi dada.
Atakuja kukuliza, nawafaham wanaume dizain hiyo, wengi walilizwa.
Bora umemgundua mapema. Hapo hamna mume, tapeli la pesa, na kukuletea matatizo yake uyatatue.

Huyo nafikiri anae mwanamke na watoto. Na vile vile anayo nyumba ndogo.
Na wewe utakua mwanamke namba 3.
Anataka aje kuishi kwako bure na akulaghai pesa zako. Au anataka umlele na umsomeshe watoto wake.

Mwanamme anae kupenda kweli hawi hivo.
Fuata msimamo wako, hasikuendeshe kama gari bovu. Kama una mnyanyasa sasa kwanini atake kuishi nawe? si akatafute mwema mwenzie. Huyo anataka ujione unamakosa na ujisikie vibaya, ili akukontroll na ufanye kama anavotaka yeye. Ukimfuata atakuchanganya changanya akili, na kukuaribia plan zako, na watoto wako pia.
Mchawi anaweza kukuroga, kua makini na matapeli bi dada.

Kama unampenda, na unataka kujitoa sadaka kwa upendo, basi jaribu kumpeleleza bila yeye mwenyewe kujua.
Mfuatilie fuatilia maisha yake alio ishi kabla yako, ju anapoishi, fanya utafiti kama kweli anafanya kazi hapo alipokuambia. Ili ujue ukweli.

Kwa vile una watoto jaribu kuwa na mwanamme miaka mingi ili umjue tabia yake kwanza kabla hauja mtambulisha kwa watoto wako, tumia si chini ya miaka 2-3.
Wewe ndio unapanga na kuamua sio yeye. Kama anakupenda inabidi akufuate na akubali, sababu unajitegemea na haumtegemei yeye. Kama atakuambia uamie kwake na atakulisha, sawa anaweza kukupangia, lakini kama unajilisha na kujitegemea na yeye pia anataka kuja kukutegemea basi inabidi akufuate na akuheshm.

Sio ufunge nae ndoa leo, kesho wanakuja polisi kumkamata, au anamadeni mengi anakuambia wewe ulipe, au alifungwa jela, nk. na kukuletea kesi za uongo ili ulipe pesa, au umlipie ili umtole aibu. wajanja hao.
 
Pole sana dada yangu kimbia kabisa bila kugeuka nyuma huyo mwanaume ni muongo na anataka kukufaidi tu ukizingatia hagharamii maisha. Tena atakuwa ana mke na watoto ndo maana hataki upafahamu kwake. Kujua tatizo ni nusu ya utatuzi tuliza akili yako dada ukivuke hicho kichaka kinachokuandama na utampata akupendaye kwa dhati.
 
aisee, huyo hafai dada
km inawezekana kuanzia mda utakaochukua maamuz ya kuwa mbali asijue ratiba zako, unakopita au unakoelekea

hongera, uko juu
 
mama yangu pole kwa huu mkasa najua wew ni mtu mzima unaejua zuri na baya kwa uelewa wangu umepitia changamoto nyingi hadi kufikia hpo ulipo.
Back to de point - naamini unaweza kupambana kupitia maelezo ya hapo juu yanajieleza kabisa wew sio tegemezi kama umelea watoto na kuwasomesha na saiv wanajitegemea mungu akubariki na akuzidishie mama angu. Sasa ktk kipindi hiki ni kipind cha wew kupumzika na kustarehe na mwenza as ulivyoeleza kuwa huwezi kuishi pekeako wew ni binadamu(hisia ni muhimu) hivyo mungu akujalie upate mtu anaeeleweka na sio tegemezi yan mtu mwanaume mzima uanze kumgharamia kwa kila kitu ooh sorr 4 dat an dont even try 2do such thing. Huu sio mda wa kuwa na stress za maisha kwa umri uliofikia unatakiwa urelax sasa kama analeta habar za kitoto uyahaya mwingi atoke zake hapo mama angu haiitaji roho ya huruma piga moyo konde aende zake asikufirisi wallah sio mwanaume wa kweli. Afu mwanaume mlalamishi hajawahi kuwa na maendeleo hata siku moja. Hapo nikutakie kila la kheri ktk kuachana naye na look foward mtu anayeeleweka as kuwa na mwanaume sio lazima bt ni muhimu.
 
Huyo mwanaume inawezekana
1. ana mke
2. Ni yahaya

Inawezekanaje hujui kwake wala wanae?
Akifa ghafla je?

Ndugu hakufai kimbiaaaaa bila kugeuka nyuma

mimi mwenyewe hilo la kuwa ana mke mwingine limenijia akilini..huyu bibie inafaa amchunguze huyu bwana kabla hajapiga hatua zaidi..
 
Dada Pole sana kwa maelezo haya huyo mwanaume hafai sababu inawezekana yote aliyokwambia ni ya uongo. Inakuwaje hataki ufahamu anakoishi je huoni kama ni hatari kwako kukaribisha mjitu wa aina hiyo nyumbani kwako. Ni kweli unahitaji mwenza lkn si wa mashaka namna hii. Anajifanya anakupenda sana kitu ambacho si kweli , mwenzako amekuja kwako akiwa na business plan yake na hiyo ndiyo anayoitazama zaidi.

Kuwa makini na watu wa dizaini hii watakuliza bure. Kuna wengine hawapendi kujulikana kwani wana mambo ya kutisha huko nyuma ya pazia.Kabla hujaendelea na huyu tafuta kwanza kujua anaishi wapi na nani na kwanini yuko peke yake. Nasema hivi kwa sababu wengine wamekimbiwa na wake zao kwa tabia chafu au waliwatishia kuwaua. Hebu fikiria umehamia kwenye nyumba yako na huyu jamaa akaamua kufanya lake wanao utawaachaje. Wengine wanaongoza kwa dhuluma hata uwe umeweka mambo sawa namna gani.

Dada yangu sikutishi bali napenda kuyaangalia mambo kwa namna zaidi ya 1. Wewe ni mtu mzima unajua anaekupenda na asiyekupenda so kuwa mwangalifu na watu wa aina hii kamwe usikaribishe mtu nyumbani mpaka uwe umejiridhisha na mambo mengi juu ya mtu huyo. Kwa huyu shemeji sisemi kitu bali akili mkichwa my sister. Afadhali amani kuliko kuishi kwa mashaka. Jiulize ni mwanaume gani mwelevu anayeweza kung'ang'ania akaishi kwa mwanamke tena analalamika kila mara kipato chake kidogo hii kali aisee.

i got u very very and very matapeli wawawezi kuisha washajua mioyo ya wanawake myepesi mamaaaa hawajakutana na mawe huhuhuuuu asijemletea matatizo makubwa mama etu bureeee
 
Miezi 5-6 ni mda mdogo sana kumjua mtu. Huyo nafikiri anataka kukutapeli pesa zako na kukutumia.
Wanaume matapeli ndio wapo hivo bi dada.
Atakuja kukuliza, nawafaham wanaume dizain hiyo, wengi walilizwa.
Bora umemgundua mapema. Hapo hamna mume, tapeli la pesa, na kukuletea matatizo yake uyatatue.

Huyo nafikiri anae mwanamke na watoto. Na vile vile anayo nyumba ndogo.
Na wewe utakua mwanamke namba 3.
Anataka aje kuishi kwako bure na akulaghai pesa zako. Au anataka umlele na umsomeshe watoto wake.

Mwanamme anae kupenda kweli hawi hivo.
Fuata msimamo wako, hasikuendeshe kama gari bovu. Kama una mnyanyasa sasa kwanini atake kuishi nawe? si akatafute mwema mwenzie. Huyo anataka ujione unamakosa na ujisikie vibaya, ili akukontroll na ufanye kama anavotaka yeye. Ukimfuata atakuchanganya changanya akili, na kukuaribia plan zako, na watoto wako pia.
Mchawi anaweza kukuroga, kua makini na matapeli bi dada.

Kama unampenda, na unataka kujitoa sadaka kwa upendo, basi jaribu kumpeleleza bila yeye mwenyewe kujua.
Mfuatilie fuatilia maisha yake alio ishi kabla yako, ju anapoishi, fanya utafiti kama kweli anafanya kazi hapo alipokuambia. Ili ujue ukweli.

Kwa vile una watoto jaribu kuwa na mwanamme miaka mingi ili umjue tabia yake kwanza kabla hauja mtambulisha kwa watoto wako, tumia si chini ya miaka 2-3.
Wewe ndio unapanga na kuamua sio yeye. Kama anakupenda inabidi akufuate na akubali, sababu unajitegemea na haumtegemei yeye. Kama atakuambia uamie kwake na atakulisha, sawa anaweza kukupangia, lakini kama unajilisha na kujitegemea na yeye pia anataka kuja kukutegemea basi inabidi akufuate na akuheshm.

Sio ufunge nae ndoa leo, kesho wanakuja polisi kumkamata, au anamadeni mengi anakuambia wewe ulipe, au alifungwa jela, nk. na kukuletea kesi za uongo ili ulipe pesa, au umlipie ili umtole aibu. wajanja hao.

kabisa asimtie hasara bure mama etu na kumpa pressure saiv wanaume wengne jaman ni pasua vichwa sasa anataka awe analelewa kama mtoto mdogo hapo ndevu zimekomaa na mvi usikute zimeanza aaggh!!!! Nimechukia hapa jaman loo!!!!!
 
Hakika.

Mtu unaoa unang'ang'ania kwenda kula jasho la mwanamke???

"Mwanaume atakula kwa jasho na mwanamke atazaa kwa uchungu''

Kweli ana haki ya kupenda, lakini kwa hali hiii, Anakaribisha majuto mengi sana nyumbani kwake.

May be nina tatizo na mimi, lakini akili hiyo ya kipumbavu ya huyu jamaa at least ningeisikia kutoka kwa under 18 ningejitahidi kumtetea hajakua bado, alkini over 40 bado akili ndio hiyo na kulalamika lalamika tu,,, kaaazi kweli kweli.

Dada /mama angu.... Mie ushauri wangu ni mdogo tu!

"Ingawa inauma, ruhusu moyo wako ukubali matokeo" Achana naye huyo baba, why??

1. Hufahamu anakoishi ingawa yuko tayari kukuoa

2. Anakung'ang'ania kwa faida, laiti yeye ndiye angekuwa wewe angeshakuacha kitambo.

3. Hana mpango wa kukuoa bali anafuata anachokitaka "pesa" akipata huyooo anatimua zake.

4. Sio muwazi / mkweli hata kidogo, na pia hana nia ta dhati. Angelikuwa navyo asingesita kukupeleka kwake.

CL
 
Huku mtaani maisha magumu hata wanaume siku hizi tunataka kulelewa.HUYO SIO MPENZI NI MTAMANI MALI ZAKO ila na wewe si ungeachana na maswala ya kuishi na mume sasa hivi umri umeenda sana( unakaribia meno pause) so kama vip kula nae mapenzi juu kwa juu ila hamna kukaa na mtu.
 
Wewe kipato unamzidi, unataka msaada wa 20percent wa nini? Sio kwamba wewe ndio umpe hiyo 20%? Ila dalili zinavyoonyesha huyo jamaa atakusumbua sana. Inaonekana ni mtata mbaya. Kwa ushauri wangu achana nae, umri uliofika sio wa kupeana stress!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom