Niko Njia Panda.... Ushauri wenu ni muhimu

Niko Njia Panda.... Ushauri wenu ni muhimu

pole kwa mkasa huu dada.Kwa bahati nzurh umeligundua mapema kuwa hafai.Huyu mwanaume ana nia ovu ambayo hataki uigundue..inawezekana anataka mali zako kupitia ndoa.Please kumbuka umetumia miaka mingi kujenga maisha...angalia usiyaharibu ndani ya dakika...kama hufahamu kwake wala ndugu zake hashindwi hata kukuua mkishafunga ndoa. Nashauri kama mumeo wa zamani yupo na hajaoa mrudiane muombane msamaha mmalizia maisha kwa baraka. Otherwise hakikisha unawapa taarifa watu wako wa karibu au hata polisi ili ajue kuwa kama atafanya kitendo kibaya atajulikana.

Mimi ni mdada above 40 niliolewa nikaachana na mwenzangu some years ago. Kwa vile nilikua busy kusomesha watoto zangu watatu ambao sasa wameweza kujitegemea, sikutaka kua na uhusiano wa kimapenzi na mtu yoyote maana elimu ya watoto wangu na kuwasimamia was my priority.
The time has now come that I need a companion wa kumalizia nae hii n’ngwe ya maisha niliyobakiza kuliko kua mwenyewe. Watoto pia wameshasambaratika kuhangaika na maisha. Wawili wako nje ya nchi wanafanya masters na mmoja ambaye ndio mkubwa ameshaolewa ana degree ya BSc electronics aliyopata UDSM.

Nimekutana na kaka mmoja above 40 nae japo nimemzidi 3 years, hii hainipi tatizo kwani umri kwangu sio shida, most important kwangu is how we feel for each other. Nae aliwahi kuoa akazaa watoto wanne lakini pia akaachana na mkewe. Mtoto mmoja katika hao wanne alizaa wakati wa ujana na mwanamke mwingine ambaye hawakubahatika kuoana. Aliyemuoa ndio walizaa watoto watatu.
Ni miezi kama 5 – 6 hivi tangu nifahimiane na huyu kaka. Sote ni waajiriwa japo mimi kipato changu kinamzidi mwenzangu. Hili pia si tatizo kwangu, kama nilivyosema mwanzo najali tunavyojisikia tukiwa pamoja.

Tatizo kubwa ni kwamba, huyu bwana amekua kama limbukeni wa mapenzi tangu tufahamiane. Kama ni kupendwa kwa style hii mwenzenu nahisi nashindwa. Amekua king’ang’anizi kupita maelezo na wakati mwingine kulazimisha yasioyowezekana.

Analazimisha anataka kuhamia kwangu na atanioa. Sio tatizo kwangu lakini kwa maisha niliyoishi for years nikiwa mwenyewe sio kitu naweza kuamua in a night. Hataki kuelewa kwa namna yoyote ile. Juzi juzi hapa tulikwaruzana, actually niliamua kuachana nae kabisa! Lakini alinipa vitisho sana, kwamba siwezi kumuacha na hayuko tayari kuniacha hata iweje. Mpaka alitaka kuja kuleta fujo nyumbani baada ya kumwambia sitafungua gate akija.

Naomba mfahamu kwamba huyu anayejifanya ananipenda kupita kiasi, hana msaada hata mmoja katika maisha yangu. Nahangaika na maisha yangu mwenyewe kama nilivyozoea, ninachokula au ninachovaa nakijua mimi. Yeye kutwa ni kujitetea kua kipato chake ni kidogo kuliko cha kwangu japo sioni kama ni kigezo cha kutotoa msaada kama baba mtarajiwa. Sihitaji msaada 100%, hata 20% kwangu nitashukuru maana sijashindwa kuendesha maisha yangu. Ila msaada wake kidogo kwangu will mean so much ili kudumisha uhusiano wetu. Sasa hivi nina wasiwasi maana ananisumbua kupita kiasi kua lazima tuishi pamoja. Siwezi kuamua hili mara moja hasa kutokana na maisha niliyoishi ya muda mrefu nikiwa mwenyewe na pia nina watoto, I have to make them understand, na siwezi kuwafanya waelewe kwa mara moja. Watoto ni wakubwa na wana akili hivyo ni lazima niwapeleke polepole waelewe kua nili sacrifice my love life kwa sababu yao na sasa nahitaji mwenza. Sijui watalielewaje hili maana ni process. Hapa napo mkinishauri jinsi ya kulileta kwa watoto nitashukuru, maana naamini hapa jamvini wapo waliopitia mtihani kama huu.

Kikubwa ambacho ndio mtachoka, mtu huyu mwenye mapenzi mazito kwangu, sijui anaishi wapi..... japo yeye anajua kwangu na watoto wangu wawili anawafahamu. Huyo mmoja anayeishi nje ya nchi alikuja likizo wakaonana alipokuja nyumbani. Wanamjua as Mama’s friend, japo nahisi vile ni wakubwa they might have smelt something, japo hainipi shida maana mwisho wa siku its my happiness. Simfahamu mtoto wake hata mmoja maana anasema watoto wake hawawezi ku support yeye kua kwenye mahusiano, sina hakika na hili, sasa sijui akiamua kutelekeza watoto watatu ambao anaishi nao itakuaje, maana mmoja huyo mdogo anaishi na mama yao, nashindwa kupata hesabu inayojumlishika kwa hili. Niko katika harakati za kumalizia nyumba yangu nje ya mji ambayo nahamia soon, ana insist kua tuhamie pamoja, nisiende kuishi mwenyewe maana ni sehemu ya ugenini na nyumba ni kubwa. He’s got a point in a way, lakini haiwezi kua rahisi kiasi hiki anavyofikiria yeye. Kwangu mimi bado niko njia panda. Pia hatujawahi kujadili kua anakuja kuishi na mimi kwa namtiki gani na watoto wake atawaacha wapi. Vile ni kitu ambacho sijakiunga mkono 100% hata nguvu ya kuuliza haya sijawa nayo.

Naomba ushauri wenu wapendwa, hivi unaweza kweli kumpenda mtu kwa moyo wako wote, lakini mwenzio asijue unakoishi zaidi ya kazini kwako na usitoe msaada hata mmoja kwake, ilhali ukienda kwake unataka ukarimiwe kwa chakula na mapenzi? Hii mimi hainiingii akilini.

Tulipokwaruzana juzi niligundua nilifanya makosa kumfanya awe free nyumbani kwangu, as he used to come any time. Japo alikua anaingia chumbani kwangu only kama tuko wawili tu ndani ya nyumba, maana nina msichana wa kazi ambaye weekends mara nyingi anaenda kwao kusalimia na binti wa mdogo wangu ambaye namsomesha. Naye pia weekends anaenda kwa mama yake. Baada ya kugundua hilo kosa na mkwaruzano uliokuwepo, nilimwambia kuanzia sasa hatakuja tena nyumbani kwangu. Tutaonana nje ya nyumbani kwangu, in a hotel, for drinks, dinner etc... lakini kwangu sio sasa mpaka niweke mambo sawa na watoto. Hili tunalumbana nalo kwa karibu wiki mbili sasa hataki kunielewa. Anadai yuko more comfortable kama tutaonana nyumbani kwangu. Mimi nahisi anapenda kuja kwangu kwa vile he gets everything for free. Samahani kama nitawakwaza wanaume lakini ndivyo nidhaniavyo, maybe am wrong, mtaniambia. Tangu kumetokea kutoelewana hajaja tena nyumbani maana nimekataa kata kata ila tunaongea kwenye simu na kubishana ndio kwingi zaidi maana hataki kunielewa. Naomba mnijuze kama nina kosa hapa.

Niliamua kumueleza kua, kama yeye ameona haiwezekani mimi kujua kwake na kufahamu watoto wake vile anawaheshimu, kwanini mimi pia hataki ku consider hili? Kama ni makosa nilishayafanya, na nimegundua, sitaki kurudia tena! Hataki kuelewa, maana ameshikilia kwa vile mimi nina kipato namnyanyasa vile hana uwezo wa kulipia hotels, drinks and maybe meals if we decide to sit somewhere kuongea.

Kwa kweli sijui nielezeje maana mimi sio mwandishi mzuri but niko njia panda! Nawagetemea nyinyi mnipe ushauri maana huyu baba si muelewa. Kutwa anajitetea kua mimi namnyanyasa kwa vile hana kipato kizuri kama mimi. Ni mtu wa kulalamika kutwa hana pesa! Kwa kweli nachoka maana hata mimi nina shida zangu na majukumu ya ndugu lakini silalamiki kwa mtu yoyote kuhusu matatizo yangu, sana sana natafuta ufumbuzi mwenyewe. Mwanamme mzima kutwa kulalamika hana pesa kwa mwanamke, mimi sioni kama ni sawa.

Naomba msinihukumu kwa lolote, ninachotaka ni msaada wa ushauri maana nimekamatwa na huyu baba ambaye nashindwa kujua ananitafuta nini kusema kweli na nitamtoka vipi maana hataki kusikia kitu kinaitwa kuachana.

Samahani pia kwa kuwachosha, mimi sio mwandishi mzuri hivyo uandishi wangu ni wa kuzunguka zunguka ila naamini mtanielewa.
 
Da Asia naamini wengi wamekushauri vema tu hapo juu! Mwanaume gani anayedai anataka kukuoa at the same time anataka kuhamia kwako! Mi nachojua mwanamke huwa anamfata mwanaume na siyo mwanaume kumfuata mwanamke at-least kwa culture zetu. Kingine huyo mwanaume anaonekana hana busara wala ustahimilivu. Haiwezekani mwanaume hata hamjaoana anaanza vitisho nk. Je mtakapo declare legally kuwa nyie ni wana ndoa itakuwaje! Jaribu kutafakari kwa undani sana. Na kama leo yeye anaona kipato chake hakitoshi kukusupport wewe hata kidgo je ni lini kitatosha? Wanasema kutoa ni moyo na wala siyo utajiri! Kwa ufupi huyo bwana hakufai he will just end up ruining your happiness kama hutafanya mahamuz mapema kadri iwezekanavyo. Mwambie wazi kabisa kuwa unaona this relationship can't work between two of you na unaomba muachane peacefully! Kama hataki utachukua hatua zakisheria kwa vitisho anavyokupa! All the best my sister!
 
Pole dada ni heri ukamchunguza kujua ukweli wake ili iwe rahisi kumuacha mana kama ulivyosema unapata vitisho sasa tumia uongo wake kumuacha....

Pili kwenye hiyo nyumba mpya anapajua..? Kama hapajui unahama kimyakimya unaachana nae...

La mwisho siku nyingine jitahidi usijiachie sana kwa mwanaume akajua mambo yako mengi kabla haujamfaham vzur...
 

huyo hakufai,kuna anachovizia
hapo kwako na c kwamba anakupenda
achana nae muongo huyo
 
Hello mamii,miss you too....hawa wanaume wengine wanapenda mteremko.....mi mwanaume akijilizaliza namuweka kwenye negative list haraka sana.....

Akiwa hana hela lakini ana ule utajiri adimu si utakuwa unampa hela hata kama hajakuomba etiiieehh!
 
Some times we are doing crazy things 4 love, umri ulio nao najua how desprate you are.. Ok kama anakupenda na unampenda fight for it, mwambie tell me the truth.. Hata hivyo jamaa ameshkueleza past yake nafkiri he real mean something to you
 
Himidini wala silazimishi ndoa, soma uzi wangu vizuri. Ndoa nilishaipata. Nilikaa 8 years kwenye ndoa. Raha na karaha za ndoa nazijua hivyo sina cha kulazimisha mpendwa wangu. All I need is a company lakini si dizaini ya Mariooo (kula kulala) kama wewe...

^^
Nafahamu ulichokiandika hali kadhalika nilichoandika.. Ni kweli kuwa
1. Unahitaji mtu wa kushirikiana nae katika hisia,upendo na mental security,,hilo ni hitaji lililo ndani ya kila mwanadamu mkamilifu
2. Ni sahihi kiasi kuwa ulichukua uamuzi wa kulea watoto mwenyewe kwa sababu ambazo wakati huo zilikuwa muafaka.
..
KWA NINI NASEMA UNALAZIMISHA NDOA?
Ni hivi;
1. ULIEMPATA SI MWANANDOA hajui anataka nini na kama anajua basi ana ajenda ya siri. Zaidi hajui wapi pengo lako lipo ili alizibe. Hivyo ktk umri wako na wake ndoa ni kulazimisha
2. UNAHITAJI KAMPANI YA MUDA AU KUDUMU
Kama ni ya kudumu ulipaswa ukae nae umweleze mipaka na matarajio yako kwako. Ama sivyo wote mna mahali hampo wazi/mnaogopana. Yeye aliko anajua amepata nawe uliko umeweka wazi humhitaji,lakini mwanzoni hamkuambiana ya ndani. Mlitamaniana tu sasa mnajenga kutupiana lawama
3. MATATIZO MENGI YA SINGLE MOTHERS NI HAYA
-Kukimbilia kutafuta ndoa kwa hofu ya macho ya jamii
-Kuwa na mpango wa siri yaani mume wa kumtimizia haja za kimwili kwa kuficha watoto,mpango huo unapoingia dosari hutaka ndoa au kuhalalisha mahusiano pasipo kuchunguza mtu kama ufanyavyo sasa
..
U-MTU MZIMA SASA umeona mengi,unajua mengi,umekutana na mengi,,siku zote unapojua kuchimba shimo la kuingilia ujue kuchimba na la kutokea.
Kama hitaji ni zito na haraka, legeza mwendo
cc: Smile
^^
 
Last edited by a moderator:
Kama kweli anakupenda kwanini asikwambie ukweli juu ya watoto wake? Kuna vitu anaficha huyo!! Be patient jipe muda huku ukiwaandaa watoto wako psychologically ,mbona wanaume above wewe wapo tena wazuri wenye nia kama yako! Achana naye huyo anakumalizia sofa zako tu na rungu pia aoshe loh! Mwambie ukweli wake.
 
how? hebu fafanua ! kwani ni vibaya mwanamke kutaka kuolewa kaka?

^^
Hapana,umefikiri mbali sana kuliko nilivokusudia. Ni vizuri mwanamke kuolewa nilichokusudia ni kwa huyu ambaye alimkubali pasipo kuwekana wazi matarajio yao.
^^
 
Uzuri the inner you ameshamstukia kuwa huyo si mwema kwako,simply msikilize the inner you.
 
haya madege, hili nalo dege? Everything for free!? Nayangana, hambohambo kupela sengi!! Watu wa hivyo hawanaga mshipa wa aibuuuu lohh!
 
Himidini angalau umeongea vya maana. japo no. 3 sikubaliani nayo. Macho ya jamii mimi hayanipi homa maana mimi mwenyewe nimesimama kama mwanamme pamoja na kwamba am a woman. Niliyoyafanya hata walio katika ndoa na vipato vyao vikubwa hawajafanya zaidi ya kutupiana lawama. Kusomesha watoto watatu mpaka kufikia hatua ya degree na kuozesha sio kitu kila mzazi anaweza. Am proud of myself for that.
Kuwa na kampani ni muhimu japo sio priority kwangu, ndio maana nimekuja hapa mnishauri baada ya kuona mambo hayaendi sawa, vinginevyo ningeingia kichwa kichwa.
Nashukuru kwa ushauri wako.

^^
Nafahamu ulichokiandika hali kadhalika nilichoandika.. Ni kweli kuwa
1. Unahitaji mtu wa kushirikiana nae katika hisia,upendo na mental security,,hilo ni hitaji lililo ndani ya kila mwanadamu mkamilifu
2. Ni sahihi kiasi kuwa ulichukua uamuzi wa kulea watoto mwenyewe kwa sababu ambazo wakati huo zilikuwa muafaka.
..
KWA NINI NASEMA UNALAZIMISHA NDOA?
Ni hivi;
1. ULIEMPATA SI MWANANDOA hajui anataka nini na kama anajua basi ana ajenda ya siri. Zaidi hajui wapi pengo lako lipo ili alizibe. Hivyo ktk umri wako na wake ndoa ni kulazimisha
2. UNAHITAJI KAMPANI YA MUDA AU KUDUMU
Kama ni ya kudumu ulipaswa ukae nae umweleze mipaka na matarajio yako kwako. Ama sivyo wote mna mahali hampo wazi/mnaogopana. Yeye aliko anajua amepata nawe uliko umeweka wazi humhitaji,lakini mwanzoni hamkuambiana ya ndani. Mlitamaniana tu sasa mnajenga kutupiana lawama
3. MATATIZO MENGI YA SINGLE MOTHERS NI HAYA
-Kukimbilia kutafuta ndoa kwa hofu ya macho ya jamii
-Kuwa na mpango wa siri yaani mume wa kumtimizia haja za kimwili kwa kuficha watoto,mpango huo unapoingia dosari hutaka ndoa au kuhalalisha mahusiano pasipo kuchunguza mtu kama ufanyavyo sasa
..
U-MTU MZIMA SASA umeona mengi,unajua mengi,umekutana na mengi,,siku zote unapojua kuchimba shimo la kuingilia ujue kuchimba na la kutokea.
Kama hitaji ni zito na haraka, legeza mwendo
cc: Smile
^^
 
Waliyosema wachangiaji wote ni sahihi, ili kuthibitisha we mwambie uko tayari kuishi nae ila kwanza akutambulishe kwa watoto wake na ndugu na jamaa zake ikiwemo kukupeleka kwao asilia. Kama wapo wazazi wake akupeleke huko. Mpe hayo kama condition kuwa akishindwa hayo basi asikusumbue na hata sim asikupigie. Nina hakika atajitoa mwenyewe maana hataweza kwani ni tapeli wa mapenzi huyo.
 
Himidini angalau umeongea vya maana. japo no. 3 sikubaliani nayo. Macho ya jamii mimi hayanipi homa maana mimi mwenyewe nimesimama kama mwanamme pamoja na kwamba am a woman. Niliyoyafanya hata walio katika ndoa na vipato vyao vikubwa hawajafanya zaidi ya kutupiana lawama. Kusomesha watoto watatu mpaka kufikia hatua ya degree na kuozesha sio kitu kila mzazi anaweza. Am proud of myself for that.
Kuwa na kampani ni muhimu japo sio priority kwangu, ndio maana nimekuja hapa mnishauri baada ya kuona mambo hayaendi sawa, vinginevyo ningeingia kichwa kichwa.
Nashukuru kwa ushauri wako.

^^
Asante kwa kunielewa Da Asia basi kama ni hivyo,,nakukumbusha tu wapo wanaume wengi wenye hitaji kama lako,la msingi usiwakubali upesi upesi na ikibidi wawekee vizingiti mwanzoni ili uwapime.
Take my note:
Mwanamke anaeweza kufikia kiwango hicho cha mafanikio yanayoshinda wanaume wengi.. ANATAFUTWA KAMA DHAHABU.
Usimuweke Mungu wako pembeni
^^
 
Last edited by a moderator:
Mh dada Asia pole saana. hii ni ngumu kumeza. kwa dume hilo nakushauri ufikirie mara nyingi zaidi ya mbili.
Nnaona maono ya mbaali ya ma-Mushi/Munisi yatatokea muda si mrefu.

Jamaa linalalamika kipato chake kidogo sasa anataka umleee? Mwanaume gani huyu. Sisi wanaume hata kama una EPA zako si hatujali tunatoa vijasho vyetu kuonesha kuwa usinidharau hata kama una EPA zako ila niheshimu tu kwa moyo wangu wa kutoa kwa nimpendae.

Halafu linalazimisha kuhamia kwako kwanini asilazimishe wewe uhamie kwake? Looooh dume gani hili.

Natamani usubiri hata japo kidogo uyaone anayowaza maana hataweza yaficha muda si mrefu. miezi michache tu kaona unamchelewesha kuhamia kwako analeta vitisho. Akihamia kumtoa akikukosea/ukimshindwa si ndio mambo ya sisi kuona Risasi zinamfanyaje mtu?!!!!!

Fikiria dada Mara nyingi zaidi ya mbili
 
Da Asia, mimi nakupa lawama wewe moja kwa moja!
Umekuwa na uhusiano na mwanaume kwa miezi mitano;
...Huwajui watoto wake?
...Hujui hata anapokaa?
Mko katika uhusiano wa aina gani;
...Anakuja kwako tu siku zote na wewe huulizi wapi anaishi, ama anaishi na nani?
...Kwa nini asikutambulishe angalau kwa ndugu yake mmoja?

Je, akifia kwako usiku(siombi/sisemi hivo) utampeleka kwa nani?
 
Last edited by a moderator:
Ulichukua uamuzi mzuri kusomesha watoto mpaka hapo walipofika,hongera.
Ni jambo jema nawe kuwa na mwenza wa kuwa naye ila sidhani kama huyo baba ni mtu sahihi. Umevumilia muda wote huo sasa ni wakati wako wa kupumzika na kufurahia maisha ila kwa huyo uliyenaye sidhani kama utapata kile unachohitaji.
Think twice.
 
Back
Top Bottom