Niko Njia Panda.... Ushauri wenu ni muhimu

Niko Njia Panda.... Ushauri wenu ni muhimu

Huyu hafai kabisa. Kwanza ana mke, na hata hajakuambia umri wake (umri aliokuambia ni uongo) na usikute he is jobless! Una watoto jamani huitaji stress kutoka kwa outsider na hauna hata undugu naye. Jamani kuna hata njia simple za kumchunguza m2. Mi hata hugoogle kwenye FB na Linkedin.

Na witholding the truth is not lying - meaning never tell nobody about your property, money, assets unless its your hubby or lawyer in a will...:tape:
kwani watu wote wapo kwenye mitandao?
 
Smile, kilichonisaidia mimi mpaka niko hapa nilipo sirudi nyuma. watoto wangu na watu wa karibu wanalijua hili. nikisema NO i mean it, sibadiliki. Niamini....

nashukuru kwa kujitambua usije kugeuka lakini
 
Umemuamini mapema xana kiasi cha kumruhusu awe free kuingia mpaka chumbani kwako....anyway we Learn through mistakes


#ryt ur wrongz moM
 
Smile, kilichonisaidia mimi mpaka niko hapa nilipo sirudi nyuma. watoto wangu na watu wa karibu wanalijua hili. nikisema NO i mean it, sibadiliki. Niamini....
aya mama yangu nashukuru
 
Kinyau nimekupata sana mdogo wangu. Usiwe na wasiwasi, hana ubavu wa kunipeleka kwenye 4 walls, labda huko nimepeleke mimi.
Jinsi ninavyosoma nasaha zenu hapa nina mawili, kum delete kabisa mpaka kwenye recyle bin au kum delete ana maybe ku restore later, depending na nitakavyojisikia. lakini kila nikipima yakum delete hadi kwenye recyle bin ndio ina nguvu zaidi.
Leo mpaka ninapoandika hii msg sijapokekea simu yake na sijajibu msg yake hata moja. Natamani kama ningeweze kuziweka msg zake hapa muone anavyobembeleza na kujuta, lakini huwezi amini hata mshipa haunichezi, naona kama anapoteza muda wake badala ya kuwajibika ofisini kwake. usishangae nitakapokuambia kwamba sikuonana nae na kili kitu ni over.
Message yako uliyoni pm imenipa changamoto sana, usiwe na wasiwasi mdogo wangu, at least mwanga unazidi kuongezeka.
mchana mwema

Sikiliza dada asia, mimi dada yangu ameolewa akiwa above 40 na tayari akiwa na watoto, na huyo mume alikuwa tayari na watoto kwa mkewe wa kwanza.. hajui cha matumizi wala nini, na kilichotokea huyo shemeji yangu alikuwa anamlazimisha dadangu aweke mortgage nyumba yake wachukue mkopo bank, dadangu akakataa basi huyo mume alikasirikaje??? akaacha kabisa kwenda home kwa dadangu( dadangu amemzidi kipato as well) kumbe yeye shida yake ilikuwa apate mkopo wa biashara kupitia nyumba ya dadangu na si kwamba alimpenda dadangu, mana baada ya kukosa mkopo na penzi nalo likayeyuka..sasa huyo wa kwako kama yuko dizaini hii utamjua tu, hajifichi

Ila sasa wewe msikilize hiyo historia yake, na uhakikishe ufanye uchunguzi ujue ukweli wa atakachokuambia, halafu ukae nae kwa makini usimtrust sana.. hakikisha humuweki kokote katika mali zako km nyumba n.k..

Lakini pia kama kweli anakupenda kama anavyodai basi usimkatae, endelea nae na umpe masharti ambayo akiyatimiza yote basi kubali ndoa..sidhani kama wewe una shida ya hela kiivyo, kama unaona atakupa faraja basi we ishi nae tu.. ni bora kuwa na huyo msumbufu kuliko kukaa maisha ya upweke... cha muhimu ni amani dada asia, pesa kitu gani..mbona sisi wengine tuna waume ndani lakn mtu anaweza kukaa hata miezi 2 hujaona senti yake..watoto ada hatoi, unajikuta unahangaika mwenyewe tu wakati una mume....
chakula cha mtu mmoja si kitu hasa kama unampenda, ukizingatia umemzidi kipato, ila tu awe muwazi ujue pesa zake zinaenda wapi na pia achangie japo kidogo, ambapo naamini atakuelewa tu..
halafu wewe kwa sasa huna mtoto wa kusomesha una nafasi nzuri tu ya kuishi naye kwani naamini yale matumizi makubwa ya kusomesha yamepungua.., cha muhimu mkalishe chini umueleze kinaga ubaga na kero zake zooote uziorodheshe..
Mwisho kabisa iangalie nafsi yako, ikiwa anakupa furaha japo kwa (60%) basi mchukue tu, muishi/akuoe..

hakuna mwanaume mzuuri duniani, kila mmoja na makasoro yake..kama ambavyo sisi wanawake tuna makasoro yetu..cha muhimu kuvumiliana..naamini wewe umeshapitia maisha ya ndoa na unajua uhalisia wake...kiukweli hakuna mzuri isipokuwa kuna wenye afadhali..sasa kama huyo ana afadhali basi forget his bad side and move on..
naamini kuwa unahitaji furaha katika maisha yako hata kama umebakiza miaka 5 tu kuishi duniani..ikiwa hiyo ndio furaha yako basi usiiache, endelea nayo..mapungufu hayakosekani...
 
Pole ndugu yangu. Wanaume wengi siku hizi wanapenda mtelemko. Huyo ana familia ndiyo maana hataki ujue anaishi wapi wala mazingira yake. Mtu wa namna hiyo baadaye atakuwa mzigo wa misumari ambao hutakuwa na pakuuegesha ukishakubaliana kuishi naye. Timua mbio uanze upya.

Jipange upya utapata mwenye sifa za kuwa mwenzi wa mzuri.
 
Huyo mwanaume ni muongo dada yangu tena ana mke ndo maana hataki kwenda hata hotelini.sasa mtaishi vp kama hataku uijue familia yake?na anang'ang'ania kwako coz he gets everything fr free
 
yaani natamani tungekuwa na uwezo tumfungie mahali kwa muda! maana sisi wanawake bana sijui tuna nini utashangaa anatuletea kadi za mwaliko hapa sijui tutaweka wapi sura zetu
hahahaha mwenzangu hmm ntavaa mask
 
Kuwa makini asije akakutambulisha kwa wazazi feki na watoto wasiokua wake mjini hapa dada yangu chochote kinawezekana
Wana MMU hata cha kuwalipa sina ila mwenyezi mungu ndio atakayewalipa kwa nasaha zenu zilizokwenda shule. Hakuna hata mmoja ambaye amenishauri jambo likanikwaza, kwa kweli wote mmeongea kuonyesha wote ni wanafamilia ya MMU.
Nashukuru sana kwa hilo na muendelee hivyo.
Sasa basi kwa ufahamisho tu wapenzi, baada ya kumkalia kooni huyo shemeji yenu bandia kua uhusiano kwishnei na yeye hili neno hataki kulisikia, leo nina kikao nae joini, amekiomba yeye, eti atafunguka kunieleza background yake ambayo aliogopa kunieleza siku za nyuma kwa kudhani hatonipata.
Week end pia ameahidi kunitambulisha kwa wazazi wake ambao wote wako Dar.
Mtoto wake mmoja wa kiume ndio kasema ni simple atanitambulisha kwake kwanza kabla ya wale wakubwa wakike ambao anasema kitabia hawajakaa sawa, hivyo inabidi awaweke sawa kwanza kabla hajanikutanisha nao.
Lakini wapenzi naomba tu niwaambie, baada ya kusoma nasaha zenu wote zilizojaa busara, kuolewa na huyu mtu haipo tena, kwani nimeishi miaka yote hii bila mume, nimeharibikiwa na nini. Kama nitaridhika na maelezo yake tutaishi kama bf na gf that's all. Sitaki kesho nife halafu watoto wangu wapate tabu kwa sababu ya mtu ambaye mimi mwenyewe nimemleta kwenye familia ambaye kumekutana wakati umri umeshaenda awape tabu watoto wangu.
Kuna wengine wamesema labda hana kazi. Naomba niwahakikishie kua yuko kazini, na ofisi yake nimeshaenda mpaka boss wake na wafanyakazi wenzie baadhi nawafahamu kwani aliwahi kunialida kwenye function ya ofisini kwao. Hilo halina mjadala ila tatizo tu ni hizo jazba zake na kulazimisha ndoa ya kuishi kwangu, hapo ndio kuna utata.
Sijawahi kumpa msaada mkubwa sana wa kutisha zaidi ya mambo madogo madogo sana kwani nilishamuonyesha toka mwanzo kua mimi ni mwanamke na yeye ni mwanamme no matter what, hivyo a play roll zake kama baba anavyotakiwa.
hiyo kidogo ilimrudisha nyuma, hivyo kama alikua anategemea kupata chochote kwangu, alijua hakipo kwa sasa.
Naomba niwashukuru sana sana kwa ushauri wenu na sitasita kurudi tena kuwapa updates za kikao maana hili litakua fundisho si kwangu tu bali ni kwa wengine pia.
Asanteni na muwe na asubuhi njema....
 
Kinyau natamani niwasiliane nawe kwa ushauri zaidi na makolo-kolo nilonayo dah! Smile umevunja mbavu zangu una maneno hatareee
 
Last edited by a moderator:
Mimi ni mdada above 40 niliolewa nikaachana na mwenzangu some years ago. Kwa vile nilikua busy kusomesha watoto zangu watatu ambao sasa wameweza kujitegemea, sikutaka kua na uhusiano wa kimapenzi na mtu yoyote maana elimu ya watoto wangu na kuwasimamia was my priority.

The time has now come that I need a companion wa kumalizia nae hii n’ngwe ya maisha niliyobakiza kuliko kua mwenyewe. Watoto pia wameshasambaratika kuhangaika na maisha. Wawili wako nje ya nchi wanafanya masters na mmoja ambaye ndio mkubwa ameshaolewa ana degree ya BSc electronics aliyopata UDSM.

Nimekutana na kaka mmoja above 40 nae japo nimemzidi 3 years, hii hainipi tatizo kwani umri kwangu sio shida, most important kwangu is how we feel for each other. Nae aliwahi kuoa akazaa watoto wanne lakini pia akaachana na mkewe. Mtoto mmoja katika hao wanne alizaa wakati wa ujana na mwanamke mwingine ambaye hawakubahatika kuoana. Aliyemuoa ndio walizaa watoto watatu.
Ni miezi kama 5 – 6 hivi tangu nifahimiane na huyu kaka. Sote ni waajiriwa japo mimi kipato changu kinamzidi mwenzangu. Hili pia si tatizo kwangu, kama nilivyosema mwanzo najali tunavyojisikia tukiwa pamoja.

Tatizo kubwa ni kwamba, huyu bwana amekua kama limbukeni wa mapenzi tangu tufahamiane. Kama ni kupendwa kwa style hii mwenzenu nahisi nashindwa. Amekua king’ang’anizi kupita maelezo na wakati mwingine kulazimisha yasioyowezekana.

Analazimisha anataka kuhamia kwangu na atanioa. Sio tatizo kwangu lakini kwa maisha niliyoishi for years nikiwa mwenyewe sio kitu naweza kuamua in a night. Hataki kuelewa kwa namna yoyote ile. Juzi juzi hapa tulikwaruzana, actually niliamua kuachana nae kabisa! Lakini alinipa vitisho sana, kwamba siwezi kumuacha na hayuko tayari kuniacha hata iweje. Mpaka alitaka kuja kuleta fujo nyumbani baada ya kumwambia sitafungua gate akija.

Naomba mfahamu kwamba huyu anayejifanya ananipenda kupita kiasi, hana msaada hata mmoja katika maisha yangu. Nahangaika na maisha yangu mwenyewe kama nilivyozoea, ninachokula au ninachovaa nakijua mimi. Yeye kutwa ni kujitetea kua kipato chake ni kidogo kuliko cha kwangu japo sioni kama ni kigezo cha kutotoa msaada kama baba mtarajiwa. Sihitaji msaada 100%, hata 20% kwangu nitashukuru maana sijashindwa kuendesha maisha yangu. Ila msaada wake kidogo kwangu will mean so much ili kudumisha uhusiano wetu. Sasa hivi nina wasiwasi maana ananisumbua kupita kiasi kua lazima tuishi pamoja. Siwezi kuamua hili mara moja hasa kutokana na maisha niliyoishi ya muda mrefu nikiwa mwenyewe na pia nina watoto, I have to make them understand, na siwezi kuwafanya waelewe kwa mara moja. Watoto ni wakubwa na wana akili hivyo ni lazima niwapeleke polepole waelewe kua nili sacrifice my love life kwa sababu yao na sasa nahitaji mwenza. Sijui watalielewaje hili maana ni process. Hapa napo mkinishauri jinsi ya kulileta kwa watoto nitashukuru, maana naamini hapa jamvini wapo waliopitia mtihani kama huu.

Kikubwa ambacho ndio mtachoka, mtu huyu mwenye mapenzi mazito kwangu, sijui anaishi wapi..... japo yeye anajua kwangu na watoto wangu wawili anawafahamu. Huyo mmoja anayeishi nje ya nchi alikuja likizo wakaonana alipokuja nyumbani. Wanamjua as Mama’s friend, japo nahisi vile ni wakubwa they might have smelt something, japo hainipi shida maana mwisho wa siku its my happiness. Simfahamu mtoto wake hata mmoja maana anasema watoto wake hawawezi ku support yeye kua kwenye mahusiano, sina hakika na hili, sasa sijui akiamua kutelekeza watoto watatu ambao anaishi nao itakuaje, maana mmoja huyo mdogo anaishi na mama yao, nashindwa kupata hesabu inayojumlishika kwa hili. Niko katika harakati za kumalizia nyumba yangu nje ya mji ambayo nahamia soon, ana insist kua tuhamie pamoja, nisiende kuishi mwenyewe maana ni sehemu ya ugenini na nyumba ni kubwa. He’s got a point in a way, lakini haiwezi kua rahisi kiasi hiki anavyofikiria yeye. Kwangu mimi bado niko njia panda. Pia hatujawahi kujadili kua anakuja kuishi na mimi kwa namtiki gani na watoto wake atawaacha wapi. Vile ni kitu ambacho sijakiunga mkono 100% hata nguvu ya kuuliza haya sijawa nayo.

Naomba ushauri wenu wapendwa, hivi unaweza kweli kumpenda mtu kwa moyo wako wote, lakini mwenzio asijue unakoishi zaidi ya kazini kwako na usitoe msaada hata mmoja kwake, ilhali ukienda kwake unataka ukarimiwe kwa chakula na mapenzi? Hii mimi hainiingii akilini.

Tulipokwaruzana juzi niligundua nilifanya makosa kumfanya awe free nyumbani kwangu, as he used to come any time. Japo alikua anaingia chumbani kwangu only kama tuko wawili tu ndani ya nyumba, maana nina msichana wa kazi ambaye weekends mara nyingi anaenda kwao kusalimia na binti wa mdogo wangu ambaye namsomesha. Naye pia weekends anaenda kwa mama yake. Baada ya kugundua hilo kosa na mkwaruzano uliokuwepo, nilimwambia kuanzia sasa hatakuja tena nyumbani kwangu. Tutaonana nje ya nyumbani kwangu, in a hotel, for drinks, dinner etc... lakini kwangu sio sasa mpaka niweke mambo sawa na watoto. Hili tunalumbana nalo kwa karibu wiki mbili sasa hataki kunielewa. Anadai yuko more comfortable kama tutaonana nyumbani kwangu. Mimi nahisi anapenda kuja kwangu kwa vile he gets everything for free. Samahani kama nitawakwaza wanaume lakini ndivyo nidhaniavyo, maybe am wrong, mtaniambia. Tangu kumetokea kutoelewana hajaja tena nyumbani maana nimekataa kata kata ila tunaongea kwenye simu na kubishana ndio kwingi zaidi maana hataki kunielewa. Naomba mnijuze kama nina kosa hapa.

Niliamua kumueleza kua, kama yeye ameona haiwezekani mimi kujua kwake na kufahamu watoto wake vile anawaheshimu, kwanini mimi pia hataki ku consider hili? Kama ni makosa nilishayafanya, na nimegundua, sitaki kurudia tena! Hataki kuelewa, maana ameshikilia kwa vile mimi nina kipato namnyanyasa vile hana uwezo wa kulipia hotels, drinks and maybe meals if we decide to sit somewhere kuongea.

Kwa kweli sijui nielezeje maana mimi sio mwandishi mzuri but niko njia panda! Nawagetemea nyinyi mnipe ushauri maana huyu baba si muelewa. Kutwa anajitetea kua mimi namnyanyasa kwa vile hana kipato kizuri kama mimi. Ni mtu wa kulalamika kutwa hana pesa! Kwa kweli nachoka maana hata mimi nina shida zangu na majukumu ya ndugu lakini silalamiki kwa mtu yoyote kuhusu matatizo yangu, sana sana natafuta ufumbuzi mwenyewe. Mwanamme mzima kutwa kulalamika hana pesa kwa mwanamke, mimi sioni kama ni sawa.

Naomba msinihukumu kwa lolote, ninachotaka ni msaada wa ushauri maana nimekamatwa na huyu baba ambaye nashindwa kujua ananitafuta nini kusema kweli na nitamtoka vipi maana hataki kusikia kitu kinaitwa kuachana.

Samahani pia kwa kuwachosha, mimi sio mwandishi mzuri hivyo uandishi wangu ni wa kuzunguka zunguka ila naamini mtanielewa.


Kwanza napenda nikupongeze dada yangu ni wanawake wachache sana wenye ujasiri na uthubutu kama wa kwako kwa kuweza kuwasimamia wanao despite of da rough road!Big up indeed!

Kuhusu huyo mwanaume achana nae ucje ukajutia muda wako mwingi ulio spent mwenyewe na wanao!Wengine huwa ni waharibifu in nature!Keep distance na atambue msimamo wako!
Ukiona vitusho vyake vinazidi mreport polisi mapema!
M
Allah akufanyie wepec In shaa Allah!
 
Da Asia
Another thing I smell here is Incompatibility kati ya yeye na background yake na wewe. Imagine wanao umewakuza kwa maadili, have gone to some good school waje wamingle na rough kids of his? they may resent each other so much that you wont be at peace(umesema yeye kasema wanae hawana maadili) na samaki hakunjiki ukubwani.

In this meeting ya leo , please don' t show a sign of needing him but present yourself with highest mature mind, without forgeting to let you close people know where you are meeting. Please msimeet in a room --women are very weak kubembelezwa in closed doors. And this fellow has al signs of a conman isije hata hao parents are ghost ones , watch all the signs kuwa hao ni wazazi kweli au kawalipa wazee hapa mjini. Question them politely and judge .

Jinsi ulivyohangaika na maisha ulivyokuwa single ni wazi u need a patner to soothe your life, to console , to at least be able to buy some classy cologne and take you out ocassionally -- let it not be this specie please , umri huu ufokewe ? You deserve something better and I pray you get that.

Above all seek divine guidance from God

Well spoken!
 
life is short, "right selection" huwa hawaandikwi usoni. na mimi sio wa kwanza kupata wrong selection. hata wewe unaweza kujiona you are right but wrong selection kwa mtu mwingine. mimi sio wa kwanza kukutana na wrong selection. wako waliokutana na wrong wa ma wrong mpaka watolewa uhai sababu hiyo, laiti mtu ungeweza kumsoma mwenzie anawaza nini kichwani basi kila mtu angekwenda kwa right selection.
hata wewe kama mwanaume pia nina amini ushakutana na ma fox wakike. vile wengine hapa mnajivika ngozi ya kua watakatifu wakati hamko hivyo. wako wanaume wangapi wanatendwa na wanawake wanalia kutwa kucha na bado wanang'ang'ania. Life is never perfect under the sun.... leo ni mimi kesho utakua wewe and we learn through mistakes. Weakness kubwa niliyonayo ni kusimamia watoto wangu wakasoma vizuri kukuzidi hata wewe unayebwabwaja hapa. Umefanya nini hapa duniani kama kweli wewe mwananume. Utumbo wako huu peleka FB kama hukua na kuniambia.

Da Asia mbona unakuwa mkali? Pole sana, tunajua what u are going thru but don't be bitter!
Responds zako ziko politely, sweet and wisely!
But this one noooo! ma siss! Chill out! You are better than this!
Kusema za ukweli nilianza kufall for u! Gudluck
 
Yahaya unaishi wapi? Jina lako halisi ni nani Yahaya eeeeh! Yahaya yahayaa. Naimba tu jamani. Ushauri wangu alifika muwekee huo wimbo

Ha ha ha ha haa my ribs!..... Kuna vituko humu jamvini haki ya nani
 
hahahaha mwenzangu hmm ntavaa mask
ahaaaa mask zenyewe sokoni za kichina zitasaidia nini ..cheki michambo ya jamaa from page one? mi nitajitoa jf kwa kweli
 
kwanza napenda kukupongeza kwa kufunguka macho mapema!..ila nimecheka sana jamani ..duniani hakuna mtu anapenda shida etiii!!!
nani anapenda kuishi kwa shida! hapo kwako full kiyoyozi soseji na maaple na k juu kwanini asiombe kuhamia?...
da asia achana nae huyo kwanza ana mke ndo maana hataki kukupeleka kwake piga chini.tena shtaki polisi
raha ya mwanaume ni akujali ..kama mwanaume akujali ..hajui unakula au unalala wapi hana mchango wowote kwako ni wa nini huyo?

hahahaha! Hatar sana, ila jamaa kazingua kweli kung'ang'ania kwa bi mkubwa sio mpango she want a real love and not playing,,, you 40yrs is so huge atleast get someone can bring hope and happiness ila huyo jamaa mmmmmh!
 
hahahaha! Hatar sana, ila jamaa kazingua kweli kung'ang'ania kwa bi mkubwa sio mpango she want a real love and not playing,,, you 40yrs is so huge atleast get someone can bring hope and happiness ila huyo jamaa mmmmmh!
jamaa keshapigwa chini ...chezeiya nguvu ya wapambe jf ?
 
Back
Top Bottom