Niko njia panda, ushauri unahitajika

kalovha

JF-Expert Member
Dec 10, 2017
1,400
2,000
Habari wapendwa natumai wote mko poa kiafya.

Na mnaendelea na majukumu ya ujenzi wa taifa naenda straight to the point mimi ni mwanachuo wa chuo kikuu "X" hapa mkoani Dodoma naingia mwaka wa tatu, nilibahatika kumpata mwenza wa First Year wa chuo fulani cha Mipango. Sasa tumedumu takriban miezi sita majuzi ananiambia amepima na anaujazito wangu.

Aisee nikicheki hata chuo bado sijamaliza kazi sina, nategemea tuhela twa boom (meal and allowance). Nimemwambia asitoe huo ujauzito maana ni dhambi kubwa hata sijui nifanyaje mwenzenu majukumu hayo.

Nikiwaambia wazee ndo nitakosa msaada kabisa yaani najuta kumwagia ndani..niko njia panda mpaka nahisi dunia imefika mwisho kwangu..

Ushauri kwa vijana wenzangu msimwagie ndani.
 

funzadume

JF-Expert Member
Jan 28, 2010
12,242
2,000
I admit ni mistake nimefanya mkuu,ila mkuu hakuna ambaye hajawahi fanya makosa.
Nani aliyekwambia umefanya kosa? Kumpa mimba binti ukiwa chuo wala sio kosa. Kuna faida nyingi sana kama ukija kumuoa huyo binti na mkaendeleza familia yenu. Mimi nilimpa mimba mke wangu nikiwa second year chuo na nilikuwa na wasiwasi ila nikapiga moyo konde akazaa mtoto na baada ya miaka mitatu nikamuoa. Kwa sasa nina miaka 43 mtoto wangu yuko chuo kikuu nje ya nchi mwaka wa pili (umri kama wako). Nasubiri amalize apate kazi. Wenzangu ambao tuko umri sawa vitoto vyao ndio viko la saba kwa sasa. Nakaribia kuitwa babu kama mwanangu nae akitembelea nyota yangu ya ngono zembe

So dogo lea mimba waambie wazazi na uje kumuoa huyo binti faida utaziona baadae. Watu wengi wanaanza kusomesha watoto chuo wakati wanakaribia kustaafu. Wewe utamaliza kusomesha mtoto ukiwa 45 kisha una-concentrate na maendeleo mengine. Na asikwambie mtu kusomesha kazi sana ukilifanya mapema kutokana na kupata watoto mapema utatoboa kimaisha
 

Luv

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
2,023
2,000
Pole kwa kipindi hiki cha ujauzito aanze kuuza viurembo vya kike chuoni like hereni, makeup etc.

Wewe pangilia muda anza kuuza nguo za mtumba za kike hapo chuoni kwako.

Anzieni hapo mengine yatajiweka sawa mbele. Muache utoto nyie ni wazazi watarajiwa.

Siku nyingine mwaga nje.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom