Nombeni ushauri niko njia panda. Huu ni uchawi au kiini macho?

Anonymous77

JF-Expert Member
May 29, 2022
299
847
Kwanza kabisa nianze na salamu kwenu wote wana JF asalam alaykum warahmatullah wabarakatuh, ndugu zangu kaka zangu dada zangu naombeni ushauri wenu, kuna tukio ambalo limekuwa linanisumbua sijui ni uchawi ama kiini macho sijui niseme lipi ndugu zanguni.

Ila hivi sasa miezi zaidi ya 5 nimekuwa nikitokewa na hili tukio kila siku ninapokuwa nikipata chakula kiwe cha mchana ama usiku unakuta nakula vizuri na chakula kinaenda tumboni ila shida iliyonifanya nije niombe ushauri kwenu ndugu zangu wana JF, Kuna mtoto mmoja ambae nakaa kwa makadilio ya umri wake ni miaka 7+ shida yangu huwa kila ninapomaliza kula au nikiwa naendelea kula akitokea huyu akakaa karibu na mimi basi nitashindwa nitashindwa kula na kutapika chakula chote hata kama nikiwa nikiwa nimemaliza kula chakula hicho muda mfupi yani dakika kadhaa zilizopita na chakula kiwe kimeshafika tumboni.

Ila anapotokea huyu mtoto ikitokea kasogea karibu na mimi hata kama hajanigusa hali I abadilika kisha natapika chakula chote hakitabaki hata tonge moja tumboni kwangu, kitu cha kushangaza ni kuwa sio mchafu wala hana uchafu wowote nimekaa nae muda mwingi ila hali kama hii haikuwa ikitokea ila hii hali imeanza kutokea hivi karibu ni miezi sasa kinachoniaminisha kuwa yeye ni Chanzo ni kwamba sijawai kutapika ikiwa yeye hayupo nikiwa nimekaa na watu wengine chakula kinaenda vizuri tu na sijawai kutapika.

Nimefanya utafiti wangu kwa kina zaidi ya miezi 3 nimejirizisha kuwa chanzo ni yeye sasa kila anapokuwa na mimi lazima nitapike cha kushangaza nikiwa nakula nikamaliza alafu yeye hayupo mambo yanaenda vizuri tu ila ikitokea amekuja wakati huo hapo hapo mambo yanabadilika natapikia chakula chote ndugu zangu, Je hili linawezakuwa na maana gani ndugu zanguni niko njia panda.
 
Pole.

Kama wewe ni jinsia KE basi ujue umepata ujauzito hujafahamu ama kuna inakuja...

Kama wewe ni jinsia ME, ujue umeacha kiumbe mahala na kinataka ukawajibike na matunzo 🙂.

Hata hivyo, waswahili husema, ni hisia tuu mtuwangu.

Waweza zipotezea.
 
Kubali kataa, umetiwa mimba tayari, haijalishi wewe ni mwanamke au mwanaume, utake usitake umetiwa mimba tayari
 
Pole.

Kama wewe ni jinsia KE basi ujue umepata ujauzito hujafahamu ama kuna inakuja...

Kama wewe ni jinsia ME, ujue umeacha kiumbe mahala na kinataka ukawajibike na matunzo 🙂.

Hata hivyo, waswahili husema, ni hisia tuu mtuwangu.

Waweza zipotezea.
Jinsi ni "ME" lakini sina mtoto. Pia shukran kwa ushauri wako
 
Back
Top Bottom