Nikifanya hivi nitakuwa nimedhulumu?

Nikifanya hivi nitakuwa nimedhulumu?

Kwann mnakabidhiana vitu kienyeji hivyo?? Hao wanaweza hata kukugeuka gari lao limeibiwa ukawa matatizoni!! Kifupi hao ndo wake ninaowasema WAABESHI umekutana nao
Hakuna uenyeji wowote mkuu. Unless kama hujasoma uzi wangu between lines. Nimesema kuna makubaliano (mkataba) ulioandikwa, tena kwa Wakili.
 
Acha uwoga mzee chukua gari hiyo humu wanakutisha kukuonea wivu hao hawawezi kukulipa ni watu wa madili hapo wenzio wanawaza madili mengine washaesabu wamepoteza kama mumeandikishana kwamba wakishindwa uchukue gari unaogopa nini kufa au mbona kufa kawaida kwenye maisha yetu ishi kama manigga wa marekani acha uoga
Dah mkuu umezungumza kiungwana sana.

Unajua, kuna baadhi ya watu wamezoea michezo ya kupata na kupoteza. Pengine wao hata hawaiwazi hii gari

Sema wakuu wanavyonitisha sasa humu!
 
huo msala kwa 70% na salama kwako kwa 30% …mwanzo kabisa ungekataa kujihusisha na hayo makubaliano kama rafiki yao alivyowaruka maana alifahamu mabalah yao . Ila pia watu wa madeal wanamambo mengi inawezekana kabisa hiyo gari wamechukulia kuwa imeshapotea so hawana mpango nayo tena, lakini kwa usalama wako fanya namna nyingine ya kupata hiyo 3M irudishe kwenye biashara zako ziendelee na gari iache kama ilivyo kwa muda flani wanaweza kuifata tena na wengine(Ma-mafia)uwaga wanaroho safi wanaeza kuja wakakulipa na fidia juu hadi haitoamini, ila usijekubali tena biashara kama hiyo
 
huo msala kwa 70% na salama kwako kwa 30% …mwanzo kabisa ungekataa kujihusisha na hayo makubaliano kama rafiki yao alivyowaruka maana alifahamu mabalah yao . Ila pia watu wa madeal wanamambo mengi inawezekana kabisa hiyo gari wamechukulia kuwa imeshapotea so hawana mpango nayo tena, lakini kwa usalama wako fanya namna nyingine ya kupata hiyo 3M irudishe kwenye biashara zako ziendelee na gari iache kama ilivyo kwa muda flani wanaweza kuifata tena na wengine(Ma-mafia)uwaga wanaroho safi wanaeza kuja wakakulipa na fidia juu hadi haitoamini, ila usijekubali tena biashara kama hiyo
Asante sana mkuu.

Umetoa ushauri mzuri sana ambao haujaelemea upande mmoja. Nashukuru
 
Wakuu, kwanza poleni kwa mihangaiko ya kutwa nzima ya leo. Ndugu yenu nataka kufanya maamuzi ila sitaki nionekane nimedhulumu haki ya mtu.

Miezi 3 iliyopita kuna jamaa ambao sifahamiani nao; walikuwa wanasafirisha magendo kwa gari binafsi kutoka point "X" kwenda point "Y". Wakakamatwa na polisi njiani wakawekwa ndani. Gari nayo (Spacio) ikazuiliwa kama kielelezo.

Sijui walielewana nini na askari, wakawa wana shida na mill 3. Nikapigiwa simu na mwanangu mmoja ambaye ndio anafahamiana na hao watuhumiwa, akaniomba niwakopeshe hiyo hela kwasababu anawafahamu, ila akakataa kuwadhamini.

Na mimi nikashtuka. Ili kuepuka kugombana na jamaa yangu nikakataa kutoa pesa kwa mali kauli. Mmoja wa watuhumiwa akaomba aagize gari yake itoke mkoani ije iwekwe bond kwangu ili niwape pesa. Gari ikaja.

Nikatoa pesa, jamaa wakatoka mahabusu, tukaandika makubaliano, nikakabidhiwa gari (Toyota crown athlete mpya kabisa) na kadi yake. Mwisho wa wao kunirudishia pesa yangu ilikuwa ni juzi tar 12/08/2023. Makubaliano yanasema wakishindwa kurudisha hiyo pesa kwa wakati bila taarifa yoyote rasmi, basi gari itakuwa mali yangu. Cha ajabu ni kwamba, hadi hiyo tarehe 12 inakaribia hakuna hata mmoja kati ya wale watuhumiwa amenipigia simu! Wote wako kimya na hawapatikani! Ninayewasiliana nae ni huyu jamaa yangu tu ambaye naishi nae huku niliko, na yeye hajui kilichowasibu!

Sasa ningeweza kuwasikilizia ila hela yangu iko kwenye mzunguko, natakiwa niitumbukize mahali niongeze faida. Hapa nafanyaje wakuu? Nikijihamishia umiliki wa hii gari sitaonekana nimedhulumu? Manake wanadamu kwa nongwa hatujambo!

Naombeni ushauri.
Usihamishe umiliki kwa njia za mkato itakusumbua sana.. Watu wa namna hiyo hawana huruma na wamejawa na ukatili wa ajabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah mkuu umezungumza kiungwana sana.

Unajua, kuna baadhi ya watu wamezoea michezo ya kupata na kupoteza. Pengine wao hata hawaiwazi hii gari

Sema wakuu wanavyonitisha sasa humu!
Kuna watu bongo wanaishi kama manigga wa marekani wao ni madili makubwa tena hapo wenzio washaipotezea wewe unawaza Kwa uoga na kutishwa humu jamii forum chukua ndinga hiyo mkataba wao na wewe inamaana wao wamevunja mkataba Sasa ukiendelea na roho ya uoga utaendelea kuitazama tu mpaka unakufa
 
Acha uwoga mzee chukua gari hiyo humu wanakutisha kukuonea wivu hao hawawezi kukulipa ni watu wa madili hapo wenzio wanawaza madili mengine washaesabu wamepoteza kama mumeandikishana kwamba wakishindwa uchukue gari unaogopa nini kufa au mbona kufa kawaida kwenye maisha yetu ishi kama manigga wa marekani acha uoga
Haya we mdanganye mwenzako hivyo hivyo!ukute jamaa wamezoea deal mbovu wa-deal nae nje ya sheria wamuumize.

Mimi nadhani hao jamaa baada ya kuwa nje kwa bond huko mkoani kwa mleta mada walienda kupiga show mahali pengine ikasanuka wakang'ang'aniwa tena so case mpya ikawakausha hela pamoja na kupigwa beat na polisi wasishiriki uhalifu wao so wamekosa namna ya kurudi kugomboa mali yao ukichukulia wamezoea kuishi kiujanja ujanja,but kupitia hawa jamaa tunaweza kuona jinsi watu tunavyo-fake life hapa bongo.

Kwa mtu anaemiliki Crown Athlete inayo-cost zaidi ya 17mill ungetegemea awe na cash imekaa tu zaidi ya 10mill,ni kusema siku ana shida na hiyo hela (3mill) alikosa tu namna ya ku-access anakoweka hela zake ila alipotoka tu faster angeenda ku-draw aende kuchukua mali yake but kwa sababu ni mtu unga unga mwana anaweka mafuta siku akikosa anaiacha home ndiyo kama hivi kumtia mtu roho juu na mali yake,milion tatu kwa mtu anaemiliki gari siyo hela ya kusumbuana miezi.
 
Ngojea Nikwambie Kitu Mkuu,ishu hiyo nyepesi sana.

Wewe shida yako si Hela 3m tu, sasa wala usisumbuane na mtu uzuri mlisha andikishana.

Chukua gari na uzuri una..mpaka KADI ya gari Tafuta Microfinance yoyote wanaokopesha kawakope 3M hiyo hiyo (ACHA TAMAA)

Kopa 3m kisha tulia zako, Usirejeshe hata shilingi wakikupgia wambie Mtu ulotegemea akupe hela zako Hapokei simu ( unawataja hao wahusika)

Basi wao kwakua wana vibali na ruhusa Zote Watauza Gari watajilipa Chao.

Huko mbeleni majamaa wakikinukisha Unasema ukikwama ukaenda Kukopa Hela sehemu flani na ndio gari wameliuza Hao.

Muhimu : Kopa 3m tu hela uliyowapa ndio utaonekana kweli ulikua na shida na hela yako. ila ukikopa ZAIDI utatwangwa swali kwann ukope zaidi na gari si lako? utakosa majibu.

Kakope 3M Tia hela yako mfukoni, tulia hao majamaa wakija wambie kama mnataka kuuza GARI uzeni hilo hapo.
 
Ila wabongo kwa ujuaji 🙌
Humu ndani wote tumegeuka washauri wa kisheria kabisa 😂😂😂

Mkuu, mimi ushauri wangu ni watafute wataalamu, nenda kwa huyo mwanasheria uone anasemaje kisheria,

Kibusara, wasubiri jamaa wape japo mwezi au miezi miwili ya ziada, kumbuka tupo Africa na muda huwa hauzingatiwi kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom