Nikifanya hivi nitakuwa nimedhulumu?

Nikifanya hivi nitakuwa nimedhulumu?

Kuna watu bongo wanaishi kama manigga wa marekani wao ni madili makubwa tena hapo wenzio washaipotezea wewe unawaza Kwa uoga na kutishwa humu jamii forum chukua ndinga hiyo mkataba wao na wewe inamaana wao wamevunja mkataba Sasa ukiendelea na roho ya uoga utaendelea kuitazama tu mpaka unakufa
Nashukuru kwa mawasilisho haya mkuu, nitayafanyia kazi.
 
Ila wabongo kwa ujuaji
Humu ndani wote tumegeuka washauri wa kisheria kabisa

Mkuu, mimi ushauri wangu ni watafute wataalamu, nenda kwa huyo mwanasheria uone anasemaje kisheria,

Kibusara, wasubiri jamaa wape japo mwezi au miezi miwili ya ziada, kumbuka tupo Africa na muda huwa hauzingatiwi kabisa
Hiyo paragraph ya kwanza imenitoa kwenye reli nilitaka kushauri
 
Kujimilikisha naweza kwasababu nina makubaliano (mkataba) ambao niliandikishiana nao kwa Wakili. Kitaalamu, kule TRA wakati wa transfer of ownership, badala ya mkataba wa mauziano, unawekwa huu mkataba wangu wa kukopeshana fedha kwa dhamana.

Mimi kukamatwa haiwezekani kwani nina mkataba ambao unaonyesha mmiliki halali ndio amenikabidhi gari lake kama dhamana yeye mwenyewe kwa hiari yake.
Wanayejua mmilki halali wa gari TRA maana ndo anaweza kutofautisha kadi feki dhidi ya kadi halali
Siku nyingine kataa kushirikiana na mhalifu kwa namna yoyote ile
 
Nakushauri urudi kwa mwanasheria huyo huyo, akupe ushauri namna ya kujinasua kwenye huo mtego
Mimi mwenyewe ni Wakili mkuu. Sijauandaa mkataba wala kuufanyia attestation kwasababu ya kuogopa conflict of interest. So nilimpigia my colleague akafanikisha jambo, kwasababu ukiwa Wakili huwezi kujiapisha.
 
Wanayejua mmilki halali wa gari TRA maana ndo anaweza kutofautisha kadi feki dhidi ya kadi halali
Siku nyingine kataa kushirikiana na mhalifu kwa namna yoyote ile
Ukisoma kwenye replies zangu kwa baadha ya commentors utaona nimesema nilihakiki uhalali wa kadi TRA kabla ya kutoa pesa na kusaini mkataba. So everything is under control.
 
Ila wabongo kwa ujuaji
Humu ndani wote tumegeuka washauri wa kisheria kabisa

Mkuu, mimi ushauri wangu ni watafute wataalamu, nenda kwa huyo mwanasheria uone anasemaje kisheria,

Kibusara, wasubiri jamaa wape japo mwezi au miezi miwili ya ziada, kumbuka tupo Africa na muda huwa hauzingatiwi kabisa
Asante sana mkuu. Nitauzingatia ushauri wako kwenye aya ya mwisho.

Mimi pia ni Wakili. Sijauandaa mkataba wala kuufanyia attestation kwasababu ya kuogopa kitu tunaita conflict of interest.

Ukiwa Wakili/Kamishna wa Viapo huwezi kujiapisha mwenyewe.

So nilimpigia my colleague akamaliza jambo. Ndio maana nasema Kisheria hakuna mahali sijajiweka salama. Nilitaka tu kusikia busara za waja. Kwasababu Sheria huenda sambamba na busara.
 
Ngojea Nikwambie Kitu Mkuu,ishu hiyo nyepesi sana.

Wewe shida yako si Hela 3m tu, sasa wala usisumbuane na mtu uzuri mlisha andikishana.

Chukua gari na uzuri una..mpaka KADI ya gari Tafuta Microfinance yoyote wanaokopesha kawakope 3M hiyo hiyo (ACHA TAMAA)

Kopa 3m kisha tulia zako, Usirejeshe hata shilingi wakikupgia wambie Mtu ulotegemea akupe hela zako Hapokei simu ( unawataja hao wahusika)

Basi wao kwakua wana vibali na ruhusa Zote Watauza Gari watajilipa Chao.

Huko mbeleni majamaa wakikinukisha Unasema ukikwama ukaenda Kukopa Hela sehemu flani na ndio gari wameliuza Hao.

Muhimu : Kopa 3m tu hela uliyowapa ndio utaonekana kweli ulikua na shida na hela yako. ila ukikopa ZAIDI utatwangwa swali kwann ukope zaidi na gari si lako? utakosa majibu.

Kakope 3M Tia hela yako mfukoni, tulia hao majamaa wakija wambie kama mnataka kuuza GARI uzeni hilo hapo.
Asante sana mkuu kwa mnyumbulisho huu. Once again, nashukuru sana.
 
Haya we mdanganye mwenzako hivyo hivyo!ukute jamaa wamezoea deal mbovu wa-deal nae nje ya sheria wamuumize.

Mimi nadhani hao jamaa baada ya kuwa nje kwa bond huko mkoani kwa jamaa walienda kupiga show mahali pengine ikasanuka wakang'ang'aniwa tena so case mpya ikawakausha hela pamoja na kupigwa beat na polisi wasishiriki uhalifu wao so wamekosa namna ya kurudi kugomboa mali yao ukichukulia wamezoea kuishi kwa ujanja ujanja,but kupitia hawa jamaa tunaweza kuona jinsi watu tunavyo-fake life hapa bongo.

Kwa mtu anaemiliki Crown Athlete inayo-cost zaidi ya 17mill ungetegemea awe na cash imekaa tu zaidi ya 10mill,ni kusema siku ana shida na hiyo hela (3mill) alikosa tu namna ya ku-access anakoweka hela zake ila alipotoka tu faster angeenda ku-draw aende kuchukua mali yake but kwa sababu ni mtu unga unga mwana anaweka mafuta siku akikosa anaiacha home ndiyo kama hivi kumtia mtu roho juu na mali yake,milion tatu kwa mtu anaemiliki gari siyo hela ya kusumbuana miezi.
Mkuu, hata mimi wakati naiona ile gari sikuamini kama mmiliki anakosa milioni 3! Gari ni mpya kabisa, kwa sisi wazoefu wa magari, hata ukiiendesha unajua ni gari ambayo iko na hali nzuri, kama ni kutumika imetumika kwa muda mfupi sana.

Kweli sio wote wenye magari mazuri wanajiweza. Wengine kuna vitu wanaficha.
 
kama unamganga wako we chukua tu hilo gari, ila kama huna.
Polee gari ya watu utarudisha tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom