Nikifanya hivi nitakuwa nimedhulumu?

Nikifanya hivi nitakuwa nimedhulumu?

Hapo hujakopesha, bali umetoa msaada. Huna sifa za kukopesha, kwa sababu hujakidhi vigezo vya kuwa mkopeshaj...
Hakuna mahali nimesema mimi ni mkopeshaji niliyekidhi vigezo (niliyesajiliwa), sijasema gari ni langu na sijasema nina mkataba wa mauziano, hizo facts ni zako wewe binafsi na sijui umezitoa wapi!

Nilichosema mimi ni kwamba kwa mkataba huu wa kukopesha fedha kwa dhamana ya kitu, naweza kufanya transfer of ownership kwa urahisi tu tena Kisheria. Kule TRA badala ya mkataba wa mauziano unawekwa mkataba huu wa kukopesha fedha ambapo utafanya kazi 'under operation of law'.

Hayo mengine uliyayazungumza ni maoni yako binafsi ambayo yanapaswa yaheshimiwe. Ingawa huo sio uhalisia wangu.

Asante.
 
Kujimilikisha naweza kwasababu nina makubaliano (mkataba) ambao niliandikishiana nao kwa Wakili. Kitaalamu, kule TRA wakati wa transfer of ownership, badala ya mkataba wa mauziano, unawekwa huu mkataba wangu wa kukopeshana fedha kwa dhamana.

Mimi kukamatwa haiwezekani kwani nina mkataba ambao unaonyesha mmiliki halali ndio amenikabidhi gari lake kama dhamana yeye mwenyewe kwa hiari yake.
  • Kubadili umiliki inatakiwa mwenye mali akupe picha zake ndogo, na nakala ya kitambulisho, je vyote unavyo?
  • Je,mkataba unasema baada ya kushindwa kurejesha gari wewe ndiye utakuwa mmiliki halali?
  • Je umeenda TRA kwa ukaguzi na kuthibitisha jina linalosoma kwenye kadi ndio mmiliki i.e wapo wanaofoji hizo document
  • Je hilo gari umepeleka polisi kwa ukaguzi ili kugundua kama lina makosa yoyote i.e uuaji, makosa mengine n.k
 
Wakuu, kwanza poleni kwa mihangaiko ya kutwa nzima ya leo. Ndugu yenu nataka kufanya maamuzi ila sitaki nionekane nimedhulumu haki ya mtu.

Miezi 3 iliyopita kuna jamaa ambao sifahamiani nao; walikuwa wanasafirisha magendo kwa gari binafsi kutoka point "X" kwenda point "Y". Wakakamatwa na polisi njiani wakawekwa ndani. Gari nayo (Spacio) ikazuiliwa kama kielelezo.

Sijui walielewana nini na askari, wakawa wana shida na mill 3. Nikapigiwa simu na mwanangu mmoja ambaye ndio anafahamiana na hao watuhumiwa, akaniomba niwakopeshe hiyo hela kwasababu anawafahamu, ila akakataa kuwadhamini.

Na mimi nikashtuka. Ili kuepuka kugombana na jamaa yangu nikakataa kutoa pesa kwa mali kauli. Mmoja wa watuhumiwa akaomba aagize gari yake itoke mkoani ije iwekwe bond kwangu ili niwape pesa. Gari ikaja.

Nikatoa pesa, jamaa wakatoka mahabusu, tukaandika makubaliano, nikakabidhiwa gari (Toyota crown athlete mpya kabisa) na kadi yake. Mwisho wa wao kunirudishia pesa yangu ilikuwa ni juzi tar 12/08/2023. Makubaliano yanasema wakishindwa kurudisha hiyo pesa kwa wakati bila taarifa yoyote rasmi, basi gari itakuwa mali yangu. Cha ajabu ni kwamba, hadi hiyo tarehe 12 inakaribia hakuna hata mmoja kati ya wale watuhumiwa amenipigia simu! Wote wako kimya na hawapatikani! Ninayewasiliana nae ni huyu jamaa yangu tu ambaye naishi nae huku niliko, na yeye hajui kilichowasibu!

Sasa ningeweza kuwasikilizia ila hela yangu iko kwenye mzunguko, natakiwa niitumbukize mahali niongeze faida. Hapa nafanyaje wakuu? Nikijihamishia umiliki wa hii gari sitaonekana nimedhulumu? Manake wanadamu kwa nongwa hatujambo!

Naombeni ushauri.
Chai hii, tena haina hata maziwa.
 
Kwani gari imekaa ndani kama picha?
Anza kuizungukia na kuifanyia biashara. Bebea hata matofali.
In case wakija hela watakupa, wasipokuja unakua umerudisha hela yako
Kwani giyo gari inatumia maji? Vipi kuhusu service, watakuwa wanafanya hao maharamia?
 
  • Kubadili umiliki inatakiwa mwenye mali akupe picha zake ndogo, na nakala ya kitambulisho, je vyote unavyo?
  • Je,mkataba unasema baada ya kushindwa kurejesha gari wewe ndiye utakuwa mmiliki halali?
  • Je umeenda TRA kwa ukaguzi na kuthibitisha jina linalosoma kwenye kadi ndio mmiliki i.e wapo wanaofoji hizo document
  • Je hilo gari umepeleka polisi kwa ukaguzi ili kugundua kama lina makosa yoyote i.e uuaji, makosa mengine n.k
Polisi sijaenda kwa ukaguzi ila TRA nimeshahakiki taarifa za gari na iko salama. Hili lilifanyika kabla sijatoa pesa.

Kwenye mkataba kuna clause iko wazi inasema kabisa kwamba wakishindwa kulipa pesa kwa wakati bila taarifa rasmi gari itakuwa mali yangu.

Kuhusu picha na kitambulisho naandika KIAPO CHA KUTOKUJUA ALIPO MKOPAJI AU AN AFFIDAVIT REGARDING UNKNOWN WHEREABOUTS OF THE BORROWER. It is that simple.
 
Ndugu za hao jamaa, wakisema wewe ndio umewapoteza ili ujimilikishe gari?
 
Acha uwoga mzee chukua gari hiyo humu wanakutisha kukuonea wivu hao hawawezi kukulipa ni watu wa madili hapo wenzio wanawaza madili mengine washaesabu wamepoteza kama mumeandikishana kwamba wakishindwa uchukue gari unaogopa nini kufa au mbona kufa kawaida kwenye maisha yetu ishi kama manigga wa marekani acha uoga
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom