Nikifanya hivi nitakuwa nimedhulumu?

Nikifanya hivi nitakuwa nimedhulumu?

Katika woooote, wewe ndo umetoa ushauri.
Huwezi kujimilikisha gari, kwa sababu kadi haisomi jina lako; tofauti na hapo wanaweza kusema gari imeibiwa na kadi yake, na wewe ukawekwa ndani.

Cha kufanya, watafute wahusika; kama hawapatikani jisalimishe kituo cha polisi utoe taarifa, ili ikiwezekana wakupe nyaraka yoyote ile ya umiliki wa muda ili chochote kitakachokuja kutokea huko mbele uwe na pointi ya kuanzia.​
 
Wakuu, kwanza poleni kwa mihangaiko ya kutwa nzima ya leo. Ndugu yenu nataka kufanya maamuzi ila sitaki nionekane nimedhulumu haki ya mtu.

Miezi 3 iliyopita kuna jamaa ambao sifahamiani nao; walikuwa wanasafirisha magendo kwa gari binafsi kutoka point "X" kwenda point "Y". Wakakamatwa na polisi njiani wakawekwa ndani. Gari nayo (Spacio) ikazuiliwa kama kielelezo.

Sijui walielewana nini na askari, wakawa wana shida na mill 3. Nikapigiwa simu na mwanangu mmoja ambaye ndio anafahamiana na hao watuhumiwa, akaniomba niwakopeshe hiyo hela kwasababu anawafahamu, ila akakataa kuwadhamini.

Na mimi nikashtuka. Ili kuepuka kugombana na jamaa yangu nikakataa kutoa pesa kwa mali kauli. Mmoja wa watuhumiwa akaomba aagize gari yake itoke mkoani ije iwekwe bond kwangu ili niwape pesa. Gari ikaja.

Nikatoa pesa, jamaa wakatoka mahabusu, tukaandika makubaliano, nikakabidhiwa gari (Toyota crown athlete mpya kabisa) na kadi yake. Mwisho wa wao kunirudishia pesa yangu ilikuwa ni juzi tar 12/08/2023. Makubaliano yanasema wakishindwa kurudisha hiyo pesa kwa wakati bila taarifa yoyote rasmi, basi gari itakuwa mali yangu. Cha ajabu ni kwamba, hadi hiyo tarehe 12 inakaribia hakuna hata mmoja kati ya wale watuhumiwa amenipigia simu! Wote wako kimya na hawapatikani! Ninayewasiliana nae ni huyu jamaa yangu tu ambaye naishi nae huku niliko, na yeye hajui kilichowasibu!

Sasa ningeweza kuwasikilizia ila hela yangu iko kwenye mzunguko, natakiwa niitumbukize mahali niongeze faida. Hapa nafanyaje wakuu? Nikijihamishia umiliki wa hii gari sitaonekana nimedhulumu? Manake wanadamu kwa nongwa hatujambo!

Naombeni ushauri.
Ukiamua kuichukua gari kwa sasa utakuwa umedhulumu

Makubaliano yenu yalikuwa ni kwamba wakishindwa kukurudishia pesa yako kwenye kipindi mlichokubaliana, impliedly huku mkiwa mna mawasilaiano ya kawaida kama mliyokuwa nayo wakati mnaingia makubaliano yenu

Unatakiwa ujiridhishe kabisa kwanza kwamba hao watu wapo katika hali ya kawaida, isipokuwa tu wameamua kutokuwasiliana na wewe kwa makusudi

Vinginenvyo ukiamua kulichukua gari hilo na kulimiliki, kuna siku watakuja kwako wanadai kuwa walikuwa hawapatikanai kwenye simu kwa sababu waliugua na kulazwa hospitalinini ICU na ndiyo maana wakawa hawapatikani kwenye simu.
 
Wakuu, kwanza poleni kwa mihangaiko ya kutwa nzima ya leo. Ndugu yenu nataka kufanya maamuzi ila sitaki nionekane nimedhulumu haki ya mtu.

Miezi 3 iliyopita kuna jamaa ambao sifahamiani nao; walikuwa wanasafirisha magendo kwa gari binafsi kutoka point "X" kwenda point "Y". Wakakamatwa na polisi njiani wakawekwa ndani. Gari nayo (Spacio) ikazuiliwa kama kielelezo.

Sijui walielewana nini na askari, wakawa wana shida na mill 3. Nikapigiwa simu na mwanangu mmoja ambaye ndio anafahamiana na hao watuhumiwa, akaniomba niwakopeshe hiyo hela kwasababu anawafahamu, ila akakataa kuwadhamini.

Na mimi nikashtuka. Ili kuepuka kugombana na jamaa yangu nikakataa kutoa pesa kwa mali kauli. Mmoja wa watuhumiwa akaomba aagize gari yake itoke mkoani ije iwekwe bond kwangu ili niwape pesa. Gari ikaja.

Nikatoa pesa, jamaa wakatoka mahabusu, tukaandika makubaliano, nikakabidhiwa gari (Toyota crown athlete mpya kabisa) na kadi yake. Mwisho wa wao kunirudishia pesa yangu ilikuwa ni juzi tar 12/08/2023. Makubaliano yanasema wakishindwa kurudisha hiyo pesa kwa wakati bila taarifa yoyote rasmi, basi gari itakuwa mali yangu. Cha ajabu ni kwamba, hadi hiyo tarehe 12 inakaribia hakuna hata mmoja kati ya wale watuhumiwa amenipigia simu! Wote wako kimya na hawapatikani! Ninayewasiliana nae ni huyu jamaa yangu tu ambaye naishi nae huku niliko, na yeye hajui kilichowasibu!

Sasa ningeweza kuwasikilizia ila hela yangu iko kwenye mzunguko, natakiwa niitumbukize mahali niongeze faida. Hapa nafanyaje wakuu? Nikijihamishia umiliki wa hii gari sitaonekana nimedhulumu? Manake wanadamu kwa nongwa hatujambo!

Naombeni ushauri.
Usitengeneze vita na watu....wanaweza kukuua umeshaona hao jamaa ni wa magendo. Wakija wape gari yao chukua hela yako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom