Niijuavyo Freemasonry

Niijuavyo Freemasonry

Bro hicho kitu hakipo na kama kipo sio rahisi sana kama tunavyodhani .

Jinsi vyuma vilivokaza vijana wengi tungechangamkia chapchap Masonic fursa Kwa jins tulivo waroho wa mafanikio (baadhi lakini ila wengi wetu )
Hata mimi nahisi hivyo vitu ni story za kutunga maana havina uhalisia kabisa
 
HABARI ZA KIMATAIFA

BOSI WA FREEMASONS AAGA DUNIA
trra.jpg

Marehemu Sir Jayantilal Keshavji “Andy Chande”. Picha/MAKTABA

Kwa Mukhtasari

Aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Freemasons Tanzania na Afrika Mashariki Sir Jayantilal Keshavji “Andy Chande” ameaga dunia.



ALIYEKUWA kiongozi wa Jumuiya ya Freemasons Tanzania na Afrika Mashariki Sir Jayantilal Keshavji “Andy Chande” ameaga dunia.

Sir Chande amekuwa mwanachama wa Freemasons kwa takriban miongo sita tangu ajiunge na umoja huo mwaka 1954.
Historia yake

Sir Chande alizaliwa Mombasa Kenya Mei 7, 1928 ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania.

Alifika Tanzania mwaka 1950 na alikutana na watu wengi ambao walikuwa wanahudhuria vikao vya Freemasons.

Wakati huo watu hawakuwa huru kuzungumzia Freemasons kama aliyofanya Sir Chande hasa kabla ya vita vikuu ya pili ya dunia.

Wakati huo Freemasons ilikuwa imegawanyika makundi tofauti katika shule, hospitali na mashirika.

Kundi maalumu lilikuwa ni la matajiri na wafanyakazi wakubwa serikalini, wakiwamo Wazungu na Wahindi.

Ilimchukua miaka miwili kukubaliwa kujiunga na Freemasons na aliapishwa rasmi mwaka 1954 akiwa na miaka 28.
Baada ya hapo alipewa nafasi ya kuongoza tawi la Freemasons katika nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.

Sir Chande alistaafu kama kiongozi wa Freemasons Afrika Mashariki mwaka 2005 na aliendelea kushiriki mikutano huko Uingereza kwa sababu alikuwa akiendelea kufanya kazi na mashirika ya huko.



Ahojiwa na Kamati ya Moi Kenya

Katika miaka ya 1990 Freemasons ilipata changamoto kubwa nchini Kenya baada ya Rais Daniel Arap Moi kuunda tume ya kuchunguza watu wanaoabudu shetani ambayo moja ya majukumu ya tume yalikuwa ni kuichunguza Freemasons.

“Nilifika mbele ya tume mara mbili na katika nyakati tofauti kama Mkuu wa Freemasons Afrika Mashariki. Nilitoa ushahidi kuhusu kazi tunazifanya,” alikaririwa Sir Chande.

Ijapokuwa tume hiyo haikutoa majibu ya kazi waliyokabidhiwa na Rais Moi, inasemekana kuwa ilisafisha tuhuma zilizoelekezwa kwa Freemason.
“Nafurahi kusema kuwa tuhuma zile zilisafishwa zaidi na Rais aliyefuata baadaye Rais Mwai Kibaki ambaye katika moja ya hotuba zake alisema Freemasons imetoa mchango mkubwa sana nchini Kenya,” alisema Sir Chande.



Kazi zinazofanywa na Freemasons

Kazi zinazofanywa sasa hivi ni kuwafundisha wanachama wake kuhusu majukumu yao kwa Mwenyezi Mungu, kwa nchi zao, familia zao na nchi wanazofanyia kazi hata kama ni ugenini.



Jinsi ya kujiunga
Ili kujiunga na Freemasons ni lazima uwe na umri wa miaka 21. Ni hiari pia uwe unamwamini Mungu haijalishi ni Mungu gani na watu ambao hawamwamini Mungu hawaruhusiwi kuwa wanachama wa Freemasons na ni lazima uwe mkweli.

Pia ni lazima familia yako ikubali wewe kujiunga na Freemasons.

Ni lazima upeleke maombi yako kwa mtu unayemfahamu ambaye yuko Freemasons au kama humjui mtu unapawa kuandika barua na kamati itakupeleleza wewe na familia yako na pia watakutembelea nyumbani na kuongea na familia yako.

Inawezekana ikachukua mwaka mmoja hadi mwaka na nusu kuruhusiwa kujiunga.



Baada ya kujiunga

Unatakiwa kujifunza vitu vingi na kuvihifadhi kichwani kama vile maneno ya kusema wakati unafanya ibada za Freemasons kwa sababu unavyozungumzia sifa za kuwa binadamu kamili unaweza ukafananisha na ibada ya kanisani.



Faida

Hakuna faida za kupata fedha kama wengi wanavyoambiwa kwamba ukijiunga na Freemasons unapewa fedha nyingi.

Faida ni kuongeza idadi ya marafiki na kuongeza ufahamu.

Hakuna utoaji wa kafara kama inavyosemekana na pia hakuna uhusiano kati ya Freemasons na Agano la Kale.
 
Aliyekuwa analeta taharuki za free Manson ni mwandishi mmoja ktk gazeti la Tazama Tanzania alikuwa kila wiki lazima ashtushe watu Mara kafala Mara kifo akuhusisha na FM...other than that hao Masons jana tuu wametoa tangazo kuwa wananyanyapaliwa huko ktk dunia ya kwanza
 
Weka mbali na MAGUFURI, mpk sasa idadi ya vichaa imepungua ni mwendo wa PANGA
 
Sasa wale wanaoshangaa Mungu kuwa na nafsi Tatu, yaani Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ndio wajifunze kitu. Mwanadamu ambaye si lololte si chochote kiuwezo ukilinganisha na Mungu anaweza kuwa na nafsi kwa maana ya Ids za jF zaidi ya moja vipi Mungu muweza wa yote. Hapa jF una kuta mtu mmoja huyo huyo ana nafsi ya kupinga tu, kupongeza tu, kujifanya ujuaji tu nk.


Na washawasha!
Mungu sio athuman
 
Mkuu nimeshangaa tu kwasababu nimeshangaa kweli kweli kwenye mada hii....

Nilitaka kuandika mambokadhaa lakini nimeamua kuacha maana naona kama utakuwa ni mvurugano tu...

Nimeamua nimuache mkuu na mada yake na nitasoma tu....
Kwanini usiandike ili lengo la kuwa jamii forum litimie. Naamini neno lako litakuwa na thamani kwa wenye uhitaji wa kujifunza
 
Hii maada ya mleta Uzi ilikuwa nzuri sana isingekuwa watu wanajibu kulingana na dini zao sasa wanakatisha tamaa tu badala ya kutaka kujua zaidi Mimi naamini mleta Uzi alikuwa anajua mengi zaidi
 
Habar za leo wanabodi,
Rejeeni kichwa cha habar chajieleza
Naandika habar hii nikiwa na ufaham na utashi wa kutosha kama mtu mzima,pia naandika habar hii nikiwa sijatumia au kula au kunywa kitu chochote ambacho kinaweza kuathiri ufahama wangu

Najua humu wamo watu mbalimbali kutoka kada mbalimbali na wenye uzoefu tofauti tofauti kuhusiana na masuala mbalimbali ya kiulimwengu
Kwa yeyote anayefahamu namna ya kujiunga na Freemason naomba anipe msaada wa kujiunga na jamii hii ya siri,nataka kujiunga na jamii lkn so kwa lengo la kutafuta utajir bali nahtaji kuwa mwanachama au mwanafamilia
I need to be a part and parcel of it
Vilevile kama kuna mtu anafahamu zilipo Grand logdes au majumba yao ya kuabuadia hasa kwa jijini Mwanza basi naomba tuwasiliane (majumba yao ya DSM na Moshi nayafahamu mahali yalipo)
TANBIHI;kama hufahamu chochote naomba usichangie katika Uzi huu!
 
Hi ni ID ni ya monde Arabi kweli? Au iko hacked
 
monde arabe, Freemasons ni kama Usalama wa Taifa (TISS) "Watu wasiojulikana"
Yaani huwezi kuapply, huwezi kuomba kujiunga, wala hawatangazi nafasi za kujiunga.
Unaowaona wanajitangaza kuwa wakala wa Freemasonry ni matapeli na hawajui lolote kuhusu Freemasons.!
Kuwa makini sana utaishia kukutana na matapeli.
 
Back
Top Bottom