Freemason ni shirika au chama cha kindugu kilichojitokeza kwa siri mwishoni mwa karne ya 16 mpaka mwanzoni mwa karne ya 17. Chama hiki cha Freemason kipo katika mitindo mbalimbali karibu sehemu zote duniani, kikiwa na wanachama wanaokadiriwa kufikia milioni sita, pamoja na watu wa karibu laki moja na hamsini elfu.
Ni mradi mkubwa wa kutisha wa ibilisi ulimwenguni, chanzo cha utajiri bandia wa viwanda, mabenki, magari, majumba na mapesa. Ni nguvu binafsi iliyo kubwa, tajiri kuliko na yenye siri za hali ya juu ulimwenguni. Ni udugu usio wa kimungu wa giza la kishetani. Ni jumuiya iliyo kubwa sana ulimwenguni ambayo huendeleza taratibu zake kwa kutumia alama, matamko na viapo ambavyo endapo mtu atavikiuka atakabiliwa na adhabu ya kifo. Wameenea kila sehemu ya sayari yetu katika nyanja zote za maisha ya binadamu yaani wanapatikana katika elimu, taasisi za afya, siasa na uongozi, uongozi wa makanisa, wafanyabiashara, wanamuziki, wanasayansi nakadhalika.
Kati ya wanachama na ndugu hao wa karibu zaidi ya robo milioni wapo nchi za Scotland na Ireland chini ya mamlaka ua utawala wa muungano wa nyumba kubwa ya Uingereza, na wanachama chini ya million mbili wapo Amerika. Hata hivyo, Maana kubwa na inayojulikana sana ya Freemason ambayo wakati mwingine huitwa “The brotherhood” (ukaka au undugu), ni hii kwamba ni undugu wa wanaume wenye heshima, sifa na hadhi kubwa. Daima usomapo kweye vitabu kuhusu Freemason utagundua kwamba “brotherhood” ni jumuiya ya siri na inachukuliwa kama ya zamani zaidi duniani.
Undugu kiutawala ulipangwa katika nyumba au chumba kikubwa huru au muda mwingine Mashariki, kila kimoja kiliongozwa au kilikuwa na mamlaka yake ambayo ilijumlisha nyumba ndogo. Nyumba mbalimbali kubwa zilitambuana au hazikutambuana kwani ilitegemea zaidi uamiinifu kwa alama za mipaka yao. Pia kuna vyombo vidogo ambavyo ni shirikisho lenye uhusiano na tawi kuu la Freemason lakini vyenye utawala wao huru.
Freemason hutumia mifano au mithali za vifaa vya mawe ya kimason katika utekelazaji au utendaji nyuma ya poromoko la jengo la Hekalu la Mfalme Solomoni kujulisha kile kilichoelezwa na wanamason wote na wajuzi kama mfumo wa maadili uliofunuliwa katika fumbo na kudhihirishwa kwa ishara.
Nimesema Freemason ni chama cha siri cha wanaume kumbe kwa upande wa wanawake (kimsingi) hawaruhusiwi kuwa wanachama, kwani tangu kupokelewa kwa katiba ya James Anderson mwaka 1723 imekubaliwa kuwa kawaida wanaume tu wanaweza kuwa wanachama wa Freemason na siyo wanawake.
Hii ni kwa sababu walikuwa wanaamini kuwa kuwaingiza wanawake kutavunja sheria kongwe. Wakati wanawake wachache kama vile Elizabeth Aldworth, walianzisha kubainisha uanachama wa mwanzo huko uingereza hapo mwaka 1723, wanachama rasmi wa freemason ni wanaume tu, wakati kawaida wanawake hawawezi kuwa wanachama lakini ndani ya mipaka ya Marekani zipo taratibu nyingi zinazohusisha wanawake na freemason kama vile utaratibu au mpango wa nyota ya Mashariki, utaratibu au mpango wa Amaranth, pamoja na Madhabahu nyeupe ya Yerusalemu.
Ndugu zangu wauliza swali, kuhusiana na historia ya Freemason, asili na maendeleo yake ni shughuli zilizotokana na mdahalo na maono. Shairi linalojulikana kama “Regius Manuscript” limekuwa likitaja kwa kukadiria mwaka 1390 kuwa vuguvugu ndiyo zilianza na ni maandiko ya zamani ya wamasoni.
Leo hii duniani inasadikika kwamba kuna mamilioni ya wanamason na wapo wanaowatazama au wanowachukulia Freemason kama fumbo. Wapo pia wanaotazama Freemason kama wanaume wanaoendesha mikutano mbalimbali iwe ya kiakili, ya kimwili, kiroho na yenye malengo yote hayo. Lakini hata hivyo, wapo wanaodhani kuwa lengo la Freemason ni kuandaa muundo na mbinu ya siku moja kuja kutawala dunia, kuwaandaa watu wa kupeleka katika moto wa jehanamu, kutumia nguvu zao zote kuzuia watu wasijitoe kwa Yesu ambaye ni adui yao mkubwa.
Kwa mfano hapa kwetu Tanzania, ‘Freemason waliojitokeza waziwazi na kujitambulisha ni kina Chande “Andy Chande” ambao ni matajiri wafanyabiashara maarufu. Katika mahojiano aliyofanya na mwandishi Muhiddin Michuzi wa gazeti la Sunday News la tarehe 3. 4. 2005, ndugu Andy Chande alikiri kuwa anao wanachama zaidi ya 3,000 (yeye mwenyewe ni mkuu wa nyumba ya Wilaya, na kuwa wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa Tanzania na Afrika – hapa sitawataja ingawa yeye aliwataja. Alitamka kuwa mtu yeyote akishajiunga na freemason hawezi kutoka tena, kwa maneno yake “Once a freemason, always a Freemason”.
Mpenzi msikilizaji wa Redio Maria, hata hivyo, inapotokea kuelezea historia ya Freemason, utagundua kwamba vyanzo mbalimbali vinatoa maelezo tofauti tofauti. Vipo vyanzo vinavyosema kuhusu Freemason kwamba umoja huu ulianzia Misri, kibayana zaidi toka kwenye madhehebu ya wanao abudu miungu ya kipagani Osoris, Isis na Horus, ambapo Osiris ni Mungu wa ulimwengu na Isis ni dada yake wakati Horus ni mtoto.
Vyanzo vingine vinasema kwamba Freemason ilizaliwa toka kwenye jumuiya ya Druids. Lakini wataalamu wengi wa Kimason, hata hivyo wanasema kwamba kundi hili la Kimason liliundwa wakati Hekalu la Mfalme Solomon lilipokuwa linajengwa. Wanasema mtu mmoja aitwaye Hiram Abiff, anasemekana kuwa ndiye aliyekuwa mjenzi mkuu wa Hekalu lakini pia kiongozi wa Freemason na aliuwawa kwa kutoa siri za chama hicho cha Freemason.
Inasadikika kuwa wafuasi wa Kimason walikuwa na uhusiano wa kisiri na kundi jingine lijulikanalo la “Knight Templer”, hili ndilo lilikuwa kundi la watawa wa miaka ya 1118 A.D ambalo lilijipa lenyewe madaraka ya kuwalinda mahujaji waliofika kuhiji Yerusalemu.
Kuna hata hadithi zinazosema kuwa hazina zilipatikana kwenye Hekalu la Mfalme Solomon na inasemekana kuwa hawa mashujaa wa Templer ndio walioziona na hivyo wakawa matajiri sana na hatimaye walikamatwa na kufungwa kwani Mfalme wa Ufaransa wa wakati huo naye alizihitaji hazina hizo kwa matumizi yake binafsi. Wakiwa gerezani, wafuasi wa kundi hilo lisemwalo waliendelea kuishi kadiri ya imani ya Kimason na kwa kweli walikuwa tayari kutoboa siri hata kwa watu wengine.
Mtu anaweza kuingizwa au kufanywa mwanamason katika nyumba ambapo anaweza mara kwa mara kubaki mwanachama kwa kuchangia fedha kwa kudumu. Mkuu wa Mason anaweza kutembelea mkutano wowote wa nyumba iliyo chini ya mamlaka yenye urafiki na yake, na pia mkutano maalumu wa nyumba unaweza kumkarimu.
Kwa mtu mgeni kwanza anatakiwa achunguze utaratibu wa hiyo nyumba na anatakiwa awe tayari kukidhi haja kwa utaratibu wake na pia anaweza kukataliwa kama atatuhumiwa ama kudhaniwa kuharibu amani katika nyumba hiyo. Kama anapenda kutembelea nyumba hiyo hiyo kwa mara nyingine anatakiwa kujiunga nayo na kutoa mchango wa fedha.
Freemason kwa kawaida wanakutana kama mkutano na sio kama familia, ingawa katika hali inayoeleweka wanamason hukutana kama nyumba ya kifamilia. Mara nyingine majengo ya Freemason hujulikana kama Mahekalu ya kifalsafa na usanii. Katika nchi nyingi vituo vya wanamason au kumbi zimewekwa mahala pa Hekalu ili kuepuka mkanganyiko na kudhaniwa vibaya.
Nyumba nyingi tofauti za wanamason au za vikundi vingine visivyo vya kimason zimetumia maneno hayo katika nafasi mbalimbali ili kutodhaniwa vibaya. Nyumba kubwa na Makao ya Mashariki ni huru na chombo cha mamlaka ambacho kinaongoza mason katika nchi husika, taifa au eneo fulani la kijiografia. Hakuna chombo kikuu ambacho kipo mbele kuongoza Freemason duniani, kwani muunganiko kati ya mamlaka mbalimbali hutegemea sana tambuzi za pamoja.
Ndugu zangu wanachuo wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOMU), mwalimu kutoka Shule ya Msingi Elerai Jimbo Katoliki la Arusha na TYCS, Yustin na Edha, na Thadei Filipatali wa S. L. P 38 Mafinga Iringa, kwa upande wa Kanuni na kazi wakati inasemekana kuwa Freemason ni chama au ushirika wa siri, wanamason wenyewe wanadai kuwa ni sahihi kusema kikundi cha ndani au kikundi cha faragha na katika mambo fulani kama kikundi cha binafsi. Zaidi ya hapo, kwa ujumla wake katika karne hii ya 21, Freemason kimekuwa siyo chama cha siri bali chama chenye siri.
Freemason ina wajibu zake na Masharti yake ambayo ni yale yanayounda dhehebu, ambamo mteule huapa kufungamana nayo kwa sheria za undugu, kutunza siri za chama (ambazo ni alama, misemo na maneno mbalimbali yanayohusiana na uelewa wa kila kiwango) na kutenda, au kuwatendea wengine kadiri ya utamaduni na sheria za kiuashi au uanachama.
Katika mamlaka rasmi hayo masharti huapwa mbele ya Kitabu Kitakatifu cha sheria kilichotajwa na Katika ushuhuda wa uwepo wa juu wa Kiumbe kikubwa kupita vyote duniani, na mara nyingi kwa uhakika kwamba mtahiniwa anaamua mwenyewe kwa utashi huru kabisa.
Moja kati ya yaliyomo linaloweza kutokea walau mara moja kati ya masharti matatu ambalo linajumuisha, ahadi za mtahiniwa kutenda kama mtu anayefaa kuwa mwana jumuiya iliyostaarabika au iliyoendelea, ahadi ya kutii sheria ya uwepo wa kiumbe kikuu, ahadi ya kutokukosea, kutodanganya wala kulaghai jamii au ndugu na ahadi ya kutoa msaada au wema kwa mwanafamilia, ndugu na familia zao, wakati wa shida kama inaweza kufanyika bila kusababisha uharibifu wa uchumi kwake yeye mwenyewe au kwa wale wanaomtegemea.
Masharti yanajulikana kihistoria kati ya vyanzo kinzani vya uanachama wa chama cha siri cha kusaidiana yaani Freemason, kwa ajili ya kile kinachoitwa adhabu ya damu ama kafara, limetolewa dokezo kwenye adhabu za kimaumbile zilizodhahili, zinazohusiana na kila kiwango. Hili linasababisha masharti mengine kama viapo.
Andiko halitokei katika vyanzo vyenye mamlaka na vilivyoidhinishwa, litafuata uamuzi kwamba marejeo yote kwenye adhabu za kimaumbile zitolewe kwenye masharti yaliyochukuliwa na mtahiniwa katika viwango vitatu na yaliyochukuliwa na mkuu aliyechaguliwa wakati wa kusimikwa kwake, lakini yaliwekwa mahali fulani katika maadhimisho hayo.
Adhabu zinatafsiriwa kimafumbo, na hazitumiwi kiukweli na makao makuu au muhimili wowote wa chama hicho cha Freemason. Hali ya kuelezeka kwa adhabu inadokeza jinsi mtahiniwa anavyotakiwa kujisikia kuhusu yeye mwenyewe kama akikiuka kwa makusudi masharti yake. Adhabu halisi za sasa zinaweza kuwa kuachishwa kwa muda, au kufukuzwa na utoaji wa kafara au kulipia.
Ndugu zangu wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMU), mwalimu wa Shule ya msingi Elerai Arusha pamoja na TYCS, Yustin na Edga kutoka Songea Boys, na Thadei Filipatali wa S. L. P 38 Mafinga Iringa, kuna viwango au digrii katika Freemason ili kuhakikisha kuwa mtu kweli amefuzu kuwa mwanachama.
Hapa unaweza kuona kuwa katika karne ya 19, vyeti vya viwango vilitolewa kwa Wanamason wote kuonesha kuwa wamepitia daraja zote tatu za ufundi au ustadi wa kimason katika nyumba ya kawaida. Na daraja au digrii hizo tatu za ufundi au ustadi ambazo hutolewa na nyumba ya Bluu ya Freemason ni hizi zifuatazo;
Mosi, Kiwangoa au digrii ya kwanza ambayo ni ya kuingizwa mtu kama mwanafunzi wa ufundi au uashi. Hii ni digrii ya kuingizwa ambayo inamfanya mmoja kuwa mwanachama halisi wa Freemasoni.
Pili, Kiwango au digrii ya mshiriki stadi, hii ni digrii ya kiwango cha kati ambayo hujumlishwa pamoja na kujifunza maadili ndani ya chama.
Tatu, Kiwango au digrii ya mwashi mahili (mwajili), hii ni digrii ya kiwango cha tatu ambacho ni cha lazima katika vipengele vilivyovingi vya mwanachama wa Freemason.Digrii au viwango hivyo vinawakilisha hatua za maendeleo ya mtu binafsi.
Hakuna mwanachama wa chama cha siri cha kusaidiana aliyeambiwa kwamba kuna maana moja tu ya istiari hizo. Kama mwanafreemason afanyavyo kupitia vivango na masomo yao hutafsiri kwa ajili yake mwenyewe, tafsiri yake binafsi huwa imefungwa au imezingirishwa tu na Katiba ndani ya kile akifanyacho. Alama ya kawaida ya muundo na vielelezo vya jumla humwezesha kila mwana Freemason kufikia kwenye majibu yake mwenyewe ya maswali muhimu ya kifalsafa kuhusu maisha kwa ujumla. Na hapa hakuna hatua au kiwango cha uanachama stadi wa chama cha siri cha kusaidiana kilicho juu kuliko kile cha mwashi mahili au mwajili.
Mpenzi msikilizaji wa Redio Maria, viwango hivyo vinasimamiwa sanjali na mifumo ya ufundi au nyumba ya kukutanikia iitwayo Nyumba ya Bluu ya wanachama hao. Katika kila chama kuna mfumo wa ofisi mbalimbali unaoleta matabaka ndani ya hicho kiwango au utaratibu huo wa pekee. Katika mamlaka nyingine hasa zile zilizopo katika Bara la Ulaya, wanachama hao wanaofanya kazi zao kupitia viwango hivyo wanaweza kuombwa kutayarisha makala kuhusu mada za kifalsafa zinazoendana na viwango hivyo, na kuwasilisha makala hizo katika nyumba wazi ya kukutanikia.
Kuna mkusanyiko mkubwa sana wa makala za kiuashi, magazeti na chapa zinazozungumzia kutoka kwenye fikira za kubuni zinazounda masomo ya kiroho na kimaadili yenye hadhi tofauti tofauti, kupitia vitabu vidogo vya kiutendaji kuhusu chama, uongozi na uadhimishaji wa madhehebu au ibada zao. Na pia zipo makala makini za kihistoria na kifalsafa zilizoaminishwa kwenye masuala ya kitaaluma.
Baadhi ya wanaushirika wa Freemason wanayo mahitaji ya ziada kama dini kwa mfano wapo wenye imani ya Kikristo wanaotakiwa kukiri Utatu Mtakatifu. Zaidi ya hapo kuna vikundi vingine ambavyo hufikiriwa kuwa na uhusiano na Freemason lakini havina uhusiano wowote ule na Freemason. Navyo vikundi hivyo ni kama utaratibu au mpango wa chungwa, kilichoanzia huko Ireland, na kikundi cha uhuru wa mpango wa marafiki wamoja.
Ndugu zangu wauliza swali, nanyi nyote mnaonisikiliza sasa, zaidi ya viwango hivyo yapo pia mahitaji mengine ya uanachama wa Freemason ambapo uanachama wa Freemason unamhitaji mtahiniwa ambaye atakuwa tayari katika haya yafuatayo;
Kipengere cha kwanza kinahusisha Jitihada zenye fadhila, hapa ni kuonyeha undugu unaohusisha kwa kiasi kikubwa kafara ya watu na uwasilishaji wa shughuli za jumuiya nzima. Kwa wakati wa sasa mara zote, fedha hukusanywa tu kutoka uanachama wa Freemason ulimwengu mzima na hulipa kiasi kikubwa cha fedha kwa kafara za wasio waashi, mahali, kitaifa na kimataifa.
Katika karne zilizopita japokuwa akiba zenye fadhila zilikusanywa zaidi katika misingi ya busara au jamii za kirafiki na kanuni zilikuwa zikinyumbulishwa kuamua ombi la mstahili kwa kuzingatia sadaka, na kulingana na vigezo mahususi. Baadhi ya mifano ya sadaka za kimasonia hujumuisha hizi zifuatazo;
Wanachama ambao hutoa sadaka za kafara. Hawathamini kabisa uhai wa mwanadamu. Kumwaga damu kwao ni kama kumwaga maji. Kuzuia mafanikio ya mtu ili kumshinikiza kupokea uovu wao. Ni wanafiki wanaochangamana na watu ili kuwadhuru au kuwaingiza katika dini yao ya kuabudu shetani.
Wanachama ambao hutoa hifadhi au uangalizi wa kiuguzi.
Elimu na hiba za kielimu au shule kama vile shule ya kifalme ya wamason ya Uingereza ambayo ipo wazi kwa wote si kwa familia za kifreemason tu.
Msaada wa kitabibu/ au utoaji wa madawa kusaidia wagonjwa.
Mipango ya utambulisho wa motto au sera ya kimasonia (CHIP).
Kwa kuongezea, kuna maelfu ya mashirika ya kifadhili duniani ambayo yameanzishwa na Freemason. Kwa mfano, Chama cha huduma cha kimasonia cha uchunguzi wa tiba za maabara, na hospitali ya heshima kwa watoto ni fadhila muhimu zinazotambulika ambazo wamason wameanzisha na zinaendelea kutoa msaada wa kielimu na kifedha. Sanjali na hayo, kipo kipengere kingine kinajumuisha mahitaji ya jumla, kwa kawaida kukubaliwa kwa mwanchama wa Freemason, mwanachama mtarajiwa lazima awe na sifa au vigezo vifuatavyo;
Awe mtu ambaye ni huru na ni ridhaa au hiari yake mwenyewe.
Kuamini katika Mungu, desturi ambayo huachwa wazi ili itafsiriwe na mwanachama mwenyewe.
Kuwa walau na umri mdogo (kuanzia miaka 18-25 hutegemea na mamlaka kwani baadhi ya mamlaka kijana wa kimasonia, anayefahamika kama Lewis huweza kujiunga katika umri wa mwanzo kuliko wengine).
Kuwa na maadili mema na sifa njema.
Kuwa na akili timamu na mwili safi kwani wapagazi walikuwa wakikataa uanachama kwa mtu kwa sababu ya ulemavu kimwili; japokuwa sasa ; kama mwanachama mtarajiwa kama atasema ulemavu hautasababisha matatizo, haitachukuliwa kinyume).
Kuwa amezaliwa huru (yaani sio amezaliwa mtumwa au mdhamini kama ilivyokuwa kabla hili ni tishio zima la kihistoria na huweza kutafsiriwa katika maana sawa kama ilivyo katika mkataba na kuandika ridhaa. Baadhi ya mamlaka yameondoa hitaji hili.
Kuwa na uwezo wa kununua tabia ya kumbukumbu kama vile kumbukumbu mbili toka wamasoni wa sasa hutegemea katika mamlaka. Hata hivyo, baadhi ya nyumba kuu za kukutanikia wanachama katika Amerika kuna ongezeko la mahitaji ya nyumba, ambapo mwanachama mtahiniwa hutarajiwa kuwa ameishi ndani ya mamlaka kwa kiasi fulani cha muda, hasa miezi sita.
Ndugu zangu wauliza swali, kwa ufahamu zaidi zipo alama za uanachama wa Freemason ambazo hupambanuliwa kama miongozo ya zamani na isiyobadilika, vipimo ambavyo kwavyo utaratibu wa makao au vituo na makao makuu hupimwa. Kila makao makuu yana utawala wake na hakuna mamlaka yeyote iliyopo juu ya wanachama wote wa Freemason. Tafsiri ya miongozo hii kwa hiyo inaweza kutofautiana na kukasababisha mabishano na kutoelewana kati yao wenyewe.
Mpenzi msikilizaji wa Redio Maria, wanamason wana ibada zao na alama zao za maadili ambazo hujionyesha wanapofanya mikutano yao kwa kutumia mifumo ya ibada au matambiko. Hakuna ibada ya aina moja kwani kila kundi lenye mamlaka ya kisheria lipo huru kufanya ibada zake za pekee, ingawa kuna ufanano fulani katika ibada zao. Kwa mfano, wanamasoni wote katika ibada hutumia jengo lenye alama ya vifaa vya zamani, kama mawe ya wanamason wa miaka ya kati.
Freemason kama wanaupembuzi au watafiti huwa na majengo ya kifalsafa na siyo ya kawaida tu. Na hutumia hali au alama hiyo kufundisha maadili na tamaduni zao, katika kanuni za upendo wa kindugu, usawa na ukweli. Alama hizo ni kama, Apron;Hii hufuatisha vazi la majani ya mtini ambalo Adamu na Hawa walitengeneza baada ya kula tunda lililokatazwa, dira (Compass), huashiria nguvu za kiume, herufi “G” huwakilisha mungu wa mason, sega la nyuki; huashiria ustawi wa uzazi kama ule wa malkia wa nyuki, nyota ya mashariki, jicho linaloona la Horus.
Na kanuni mbili ambazo ni alama za vifaa vyao, zinazopatikana katika nyumba ya wanamason, ni mraba na duara. Katika alama hizo za mraba na duara ndani yake utaona michoro ya mkasi na mraba mwingine pamoja na herufi G. Baadhi ya nyumba nyingine zina kanuni zinazoeleza alama hizo mbili kama onyo au fundisho la uhusiano ndani ya chama chao. Kwa mfano, mmason anatakiwa afanye mambo yake yakiwa kama mraba wa fadhila, na ajifunze kuzuia matamanio na vionjo na kuvifanya kama duara yaani vizunguke ndani yake tu katika kuwaelekea watu.
Na herufi G inasemekana ndiyo ishara ya Luciferi ambapo wafuasi wake humkiri kuwa siku moja atatawala dunia. Zaidi ya hapo, alama ya mraba ndani yake huwa na michoro ya Panga, Mkono wa kulia na Kichwa. Hapa, Panga huwakilisha utawala wa Luciferi ambaye ndiye mpinga Kristo namba moja, mkono wa kulia huashiria imani na uaminifu wa wafuasi katika viapo vyao, wakati mchoro wa kichwa au fuvu la kichwa cha mtu huashiria utawala mpya wa Shetani.
Ndugu zangu wanachuo wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMU), mwalimu wa Shule ya msingi Elerai, Jimbo Katoliki la Arusha pamoja na TYCS, Yustin na Edga kutoka Songea Boys, na Thadei Filipatali wa S. L. P 38 Mafinga Iringa;
Zipo pia namba nyingi wanazotumia wanamason kwa kutambulishana, mfano wa namba hizo ni, namba moja (1) inamaana kuwa kumheshimu Mungu kunamfanya mtu awe kipofu na mjinga na hivyo wanamason wote hawamtii wala hawamheshimu Mungu; namba mbili (2) humaanisha watu wanaopinga amri za Mungu na hivyo wanajiona kuwa wapo sawa na Mungu; namba tatu (3) humaanisha watu watakaoishi milele na Luciferi na hivyo kuwa sawa na Mungu kwa kujua mema na mabaya. Pia namba tisa na namba kumi na moja, ambapo namba tisa (9) humaanisha maisha ya ukamilifu yaani maisha ya utakatifu milele, na namba kumi na moja (11) humaanisha maisha ya roho tu, yaani utawala wa kishetani wa Luciferi mpinga Kristo.
Kila mwanachama lazima achunguze au apembue alama na malengo ya Freemason, na zaidi wanamason wote wanatakiwa kwa namna fulani wawe wapembuzi wa maana ya ya alama za kimason kama kanuni ya kujiendeleza kupitia daraja zote tatu muhimu. Hata hivyo, hakuna maana iliyotolewa na hakuna msemaji mmoja wa chama cha Freemason yote. Kwani nyumba nyingine hutumia mbao na majukwaa kwa matangazo, mbao hizo na majukwaa yao huchorwa nembo zenye pembe tano na zingine mbalimbali kadiri ya mapendeleo ya Wanamason wenyewe.
Mbao hizo na majukwaa vinaweza kutumiwa pia kama nyenzo za kufundishia wakati wa mhadhara au hutumika kama makaripio yanayofuata daraja tatu, wakati mwanachama mzoefu anapoelezea wazo au fikra au dhana ya chama chao kwa wanachama wapya. Nembo hizo zinaweza kutumika pia na wanachama wazoefu kama kumbukumbu ya fikira walizojifunza wakati au enzi za kipindi cha kuingizwa kwenye Freemason.
Hapa ipo pia alama ya usinisahau kamwe, alama hii huwakilishwa na Ua dogo la bluu, ambalo kwa mara ya kwanza lilitumiwa na nyumba kubwa Zur sonne, mnamo mwaka 1926, kama nembo ya kimason mwishoni mwa ubadilishaji huko Bremen Ujerumani mwaka 1938, nembo au begi ya usinisahau mimi iliyotengenezwa na kiwanda hicho hicho kama begi ya kimason ilichaguliwa mwishoni kama nembo ya chama cha Nazi, chama cha kikarimu na kusaidiana kilichokusanya fedha ili pato la dola zingine ziwe huru na zitumike kwa ajili ya silaha za jeshi. Kushabihiana huku kuliwawezesha Freemason kuvaa nembo yao kama alama au ishara ya siri ya uanachama.
Baada ya vita vya pili, Ua la Usinisahau Mimi, lilitumika tena kama nembo ya kimason kwenye ugeuzwaji wa kwanza wa mwaka wa muunganisho wa nyumba kubwa ya Uingereza mnamo mwaka 1948. Siku hizi nembo hiyo inavaliwa na wanamason ndani ya mkunjo au kifuani pa koti na wanamasoni duniani pote kama kumbukumbu ya wale wote walioteseka kwa jina la Kimason, zaidi sana wale wa kipindi cha Nazi.
Mpenzi msikilizaji wa Redio Maria, sauti ya Kikristo nyumbani mwako, kama ndio unafungua Redio yako sasa kipindi hewani ni ijue Biblia, na hivi naendelea kujibu swali linalohusu ufafanuzi wa chama cha Freemason na kama kuna uhusiano na Kanisa Katoliki, basi kama nilivyosema Freemason haina uhusiano wowote ule wala na Papa au Kanisa Katoliki, na kuhusiana na uanachama na dini, Freemason inaelezwa kikamilifu wazi kuwa, yenyewe si dini wala haipo badala ya dini. Kwa hiyo freemason hupokea watu kutoka dini tofauti kama ubudha, ukristo, uhindu, uislam, uyahudi nakadhalika, na matokeo yake freemason hutumia kiasi kikubwa cha sheria ya dhati ya upana wa sheria takatifu kama sharti yakinifu kwa kitabu cha kidini.
Imani ya Kimason inajumlisha pia imani kwa kiongozi ambaye hutumika kama kiongozi wa chama au kikundi. Tukumbuke kuwa kundi hili la brotherhood halina makazi sehemu moja na badala yake, kuna makao mengi ambayo yanawajibika kutii kwenye makao makuu, yajulikanayo kama makao ya Mashariki. Kila makao yanazo sheria zake ambazo wafuasi wake wanawajibika kuzitii, kama alama za siri, namba za siri na alama za mikononi ni vitu vya kawaida kwa mmason kwa ajili ya mfuasi mmoja kumtambua mwingine. Daima tukumbuka kwamba usiri ni moja ya imani kubwa za wanamason zinazowafanya waonekane wa ajabu au wa kushangaza, yaani watu wasio wa kawaida.
Zaidi tujue kuwa, Imani kwa ukuu wa kiumbe wanachoamini na upana au ukubwa wa utakatifu wake, humtaka mtahiniwa wa Freemason aseme wazi imani yake kwa kiumbe huyo mkuu kuliko viumbe wengine, ingawa halazimishwi au haulizwi aeleze tafsiri yake juu ya kiumbe hicho kikubwa. Na majadiliano ya kisiasa au ya kidini hayaruhusiwi ndani ya nyumba za Wanamason, kwa upande mwingine mmason huwekwa katika hali ya kukiri kuelewa kwa tafsiri binafsi juu ya siasa na dini.
Katika kuamini kiumbe huyo mkubwa kupita viumbe vyote, wao huweza kumaanisha Utatu Mtakatifu kwa mmason Mkristo, Allah kwa mmason Muislamu na Para Brahman kwa mmason Mhindi nakadhalika. Wamason wengi hulinganisha kiumbe huyo mkubwa wanayemwamini na Mungu, wakati wengine hushikilia uelewa mpana wa tafsiri ya kifalsafa. Na katika ibada zao kiumbe huyo mkuu wanayemwamini hulinganishwa na mjenzi wa ulimwengu au aliyeumba ulimwengu ambapo hufanya Wanamason wawe na nembo yake ndani ya majengo yao.
Ukubwa au upana wa sheria ya Utakatifu huonyeshwa katika sehemu zilizowazi za nyumba zile zinazotambuliwa kimamlaka na zenye imani juu ya kiumbe huyo mkubwa kuliko viumbe vyote duniani. Katika nchi zinazotumia lugha ya Kiingereza, hutumia Biblia ya mfalme James au toleo jingine ambalo linajulikana kama Biblia ya Kimason. Zaidi ya hapo, mtahiniwa wa Freemason huachwa huru kuchagua kitabu cha dini anayopendelea. Katika nyumba zinazofuata utamaduni wa kujizuia maandiko mengine yanaweza kutumiwa, yakiwemo maandiko ambayo kwa asili yake siyo ya kidini.
Kwa mtu asiyejua huiona Freemason kama chama kizuri lakini kadri anavyozama katika chama, hujikuta anafanya matambiko ya kipagani, akijihusisha na mizimu na udanganyifu mwingi na akimkufuru Mungu, Mungu wa mbinguni huchukuliwa kama mmoja wa miungu mingi iliyopo duniani Bel(Baal) na kama vile Jah na wengineo. Jina la Yesu halitumiki kabisa katika ibada na sala za Freemason (ni marufuku kulitaja). Hufanya mambo yao kwa siri kubwa sana. Hutafuta wanachama kwa bidii isiyo ya kawaida toka kila kona ya dunia.
Ndugu zangu wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMU), mwalimu wa Shule ya msingi Elerai Arusha na TYCS Yustin na Edga wa Songea Boys, na Thadei Filipatali wa S. L. P 38 Mafinga Iringa, hapa naomba niorodheshe mambo machache yanayohusu hawa Freemasoni.
Mosi, Ni kweli Freemasonry kama ilivyo maana yake ilikuwa ni kundi la kwanza la mafundi waashi (masons) au wajenzi kwa lugha nyingine. Walikuwa ni wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki ya zama hizo zinazoitwa kwa kizungu (medieval times), walikuwa wanajenga mahekalu na mabenki au mahandaki ya kuhifadhia pesa pamoja na kuzikia(catacombs kwa kimombo).
Wamason wanaweza kujenga hayo mahandaki kwa utaalamu mkubwa kiasi kwamba ukiingia ndani ya hayo mahandaki bila ramani unaweza ukashindwa kutoka hata unaweza kupotelea humo humo ndani usiweze kutoka tena kama hakuna msaada wao. Hicho ndicho kilichokuwa ni kiwango cha utaalamu wao.
Pili, Kwa kuwa walikuwa ni waashi ndiyo maana alama zao ni vifaa vya ujenzi kama Pima maji nakadhalika.
Tatu, Inasemekana mji mkuu wa marekani (Washington DC) ulisanifiwa na kujengwa na Freemasons. Na inasemekana ni mji makini ambao umejengwa ukizingatia pembe tatu zenye nyuzi zinazowakilisha u freemason.
Nne, Kuhusu imani yao (freemasons) kwa kifupi huwa wanaamini Yesu na Lucifer ni mtu na ndugu yake. Wanaamini kuwa Lucifer ndiye mwema na mzuri lakini wanaamini kuwa Yesu ndiye mbaya kwani alimfanyia hila Lucifer aonekane mbaya ili Yeye aonekane mwema. Kwao Lusiferihuonekana kama baba, kiongozi na mpaji wa fedha, vyeo, madaraka na mafanikio katika maisha. Hahari za Lusifer utazipata (Isa 14:12-15, Lk 10:18, Uf 12).
Tano, Kinachoendelea ndani ya Freemasoni kuhusiana na ibada zake ni siri kwani kuna daraja tatu kama nilivyosema ambazo mwana freemason anapanda kutokana na kubobea katika imani ikiwa ni pamoja na kutunza siri zao.
Sita, Kwa hiyo ijapokuwa wanatumia Biblia wanapoongelea “Bwana” huwa hawamaanishi Yesu bali huwa wanamaanisha Lucifer ambaye ndiye wanayemwabudu.
Saba, Ni watu wenye nguvu mno na mambo yao ni makubwa mno na siri zao ni nzito mno. Ndiyo maana haziko wazi sana. Kwani hata wafuasi wa kiwango cha chini wala hawajui shirika hili linahusika na nini, kwani hata wao hawaambiwi mambo ya ndani.
Yaani kwa wasiojua kitu kule kwenye nyumba zao ni kama club hivi. Wanachama wengine wasiojua siri wanachukulia kama sehemu za vijiwe vya kushirikishana mambo ya kawaida.
Nane, Freemason inawekwa pamoja na makundi mengine makubwa ya siri, yanayoendesha ulimwengu mzima kwa nguvu za kiuchumi, siasa na mambo ya utawala katika nyanja za siasa.