Nihurumieni mwenzenu nakufa

Nihurumieni mwenzenu nakufa

Tunakopesha kwa dhamana ya mshahara
ok ka walikupa kwa dhamana ya mshahara waendelee kukata mshahara mpaka wawalize deni na ka hukuwa na mkataba mbona wakakupa mkopo wale wa awali ambao ulidai walitaka kukuingizia 12mil,?
 
Habari zenu wanajf wenzangu nina shida jamani eee Mungu wangu nisaidie niweze kueleweka nahitaji watu wenye moyo wa kujitoa wanisaidie jamani nipo karibu na mauti mimi.

Wapendwa nadaiwa pesa nyingi sana na bank na sijui wapi nitaweka sura yangu maana watu hawa wamechachamaa kweli mfukoni nina elfu 6500 tu jamani mimi nitaenda wapi natamani nijitoe uhai ila nawaza huko niendako itakuwaje nikikutana na moto wa jehanamu milele?

Wanajf nyie ndio tegemeo langu la mwisho naombeni mnisaidie deni linatakiwa kulipwa kabla mwezi kuisha la sivyo mimi nitahukumiwa jamani ohhh

Sina pa kukimbilia yeyote anayeweza kunisaidia kwa masharti yoyote nipo tayari ili mradi mimi niachane na hili deni jamani niishi kwa amani. Nahitaji watu 25 wakujitolea kila mmoja milioni moja nipate milioni 25 nilipe hii bank niishi kama watu wengine. Yeyote atakayenipa nitakua namlipa taratibu au anipe kazi yoyote nimfanyie bure na nitaifanya kwa akili na uwezo wangu wote.

Nisaidien jamani nawaomba Mungu atawaridishia mlipotoa.

I declare my interest ID hii ni mpya kwa sababu zisizozuilika.

Yeyote atakaeweza kunisaidia nipo tayari kuongozana nae hadi bank ili ahakikishe kweli ninadaiwa.

Story ya deni ilivyo
Pesa hizo ziliingizwa kimakosa kwenye akaunti yangu na bank yenyewe na mimi kwa vile nilikua nategemea pesa nikajua ndio zangu nikafanya nazo biashara na biashara yenyewe watu wamenidhulumu nimebaki sina kitu nifanyeje mimi na biashara ilikua haijasajiliwa sina haki hata ya kuwapeleka mbele ya sheria ninaowadai jamani nitakufa mimi dunia itaniua mimi
Chochote ulichonacho naomba mchango wako jamani nitafanyaje mimi sina hela nipo nipo tu natamani nikitembea gari linipitie nife hapohapo dah


Hivi, sheria imekaaje hapo? Anaepaswa kuhoji uwepo wa hela kiasi fulani kwenye akaunti yangu ni benki au serikali? Maana serikali ndiyo wangependa kujua(wakiwa na shaka) kuw animezitoa wapi. Sasa benki wao inakuwaje? Ninaomba ufafanuzi hapo kwa naefahamu sheria hizi za miamala.
 
Mnaonikashifu naheshimu mawazo yenu ila naomba tumieni ubinadamu kidogo hamjui ninacjopitia kwanini mnaniongezea machungu moyoni? Leo kwangu kesho kwako
 
Mdaiwa hafungwi, waambie bank huna uwezo wa kulipa kwa sasa. Wanaweza kushitaki ambapo kesi ikisikilizwa utapangiwa namna ya kulipa kutokana na kipato chako, kwa mfano unaingiza 100 kwa mwezi basi malipo tualipa sh 50 kila mwezi mpaka deni liishe. Nchi zinadaiwa watu wanadaiwa kuwa na madeni ni kawaida.
 
B
Hahahahha si useme tu walikuingizia kimakosa ukajifanya mjanja ukazikomba wajanja kitaa wakakudhulumu pia
malipo
hapa hapa duniani utapata tabu sana
btw I can't buy your story
Bank hawafanyi makosa kama hayo.
Ziingie hadi wewe unaenda kuzitoa zote bado hawajastuk na kuzizuia?

Huyu ni muongo baadhi ya maelezo yake. Hiyo pesa huenda kweli anadaiwa lakini jinsi alivyozichukua hizo pesa na alivyozitumia anasema uongo ulio dhahiri.
 
Asante mkuu ni kweli NEEMA ya Mungu ni kubwa mno naamini atanitoa katika hili janga kama alivyowatoa waisrael Misri

Wewe ni MWIZI,
UNAPASWA KUFUNGWAA!!

Wewe ulivyoona hela imeingia kimakosa ulishidwa nini kuriport bank husika? tena kwa wizi huu usimshirikishe Mungu.Hata leo kuku akiingia ndani kwako ambaye siyo wako utamla ww.
 
Wewe ulivyoona hela imeingia kimakosa ulishidwa nini kuriport bank husika? tena kwa wizi huu usimshirikishe Mungu.Hata leo kuku akiingia ndani kwako ambaye siyo wako utamla ww.
Mbona unanihukumu je umesoma story niliyoandika kuhusu hiyo hela?
 
B

Bank hawafanyi makosa kama hayo.
Ziingie hadi wewe unaenda kuzitoa zote bado hawajastuk na kuzizuia?

Huyu ni muongo baadhi ya maelezo yake. Hiyo pesa huenda kweli anadaiwa lakini jinsi alivyozichukua hizo pesa na alivyozitumia anasema uongo ulio dhahiri.
Mungu anajua kama mimi ni muongo au la
 
Nimeshauriwa kifuatacho na mdau kuhusu tatizo langu nami nalileta kwenu kuomba ushirikiano wenu wana Jf sina kwingine pa kukimbilia ni Mungu na huku Jf

Mdau amenishauri hivi:
Nipate wana Jf 5000 ambao wanweza kunichangia kila mmoja tsh 5000 ili nipate 25m nimalizane na hii bank.

Kila atakaenichangia nitamuandika then kila mwisho wa mwezi nitakua narudishia watu 200 walionichangia hizo elf 5000 hivyo ndani ya miezi 25 nitakua nimemrudishia kila mwana Jf pesa aliyonisaidia. Wana Jf naomba mnisaidie kwa hili bank wanataka pesa kabla mwezi haujaisha
Mnaweza kutafuta mtu wa kupokea hiyo michango na atakaethibitisha kweli ninadaiwa kwenye hiyo bank coz wengine mnaweza kuhisi mimi ni tapeli ila sivyo. Chochote kitakachopatikana hata leo naenda kupeleka bank ili kupunguza deni. Nisaidieni wapendwa sina pa kuanzia nimefiliska vilivyo

Haaaaa! huyu anarusha nyavu atakayeingia halali yake.Chezea msimu huu.
 
Back
Top Bottom