Nihurumieni mwenzenu nakufa

Nihurumieni mwenzenu nakufa

Habari zenu wanajf wenzangu nina shida jamani eee Mungu wangu nisaidie niweze kueleweka nahitaji watu wenye moyo wa kujitoa wanisaidie jamani nipo karibu na mauti mimi.

Wapendwa nadaiwa pesa nyingi sana na bank na sijui wapi nitaweka sura yangu maana watu hawa wamechachamaa kweli mfukoni nina elfu 6500 tu jamani mimi nitaenda wapi natamani nijitoe uhai ila nawaza huko niendako itakuwaje nikikutana na moto wa jehanamu milele?

Wanajf nyie ndio tegemeo langu la mwisho naombeni mnisaidie deni linatakiwa kulipwa kabla mwezi kuisha la sivyo mimi nitahukumiwa jamani ohhh

Sina pa kukimbilia yeyote anayeweza kunisaidia kwa masharti yoyote nipo tayari ili mradi mimi niachane na hili deni jamani niishi kwa amani. Nahitaji watu 25 wakujitolea kila mmoja milioni moja nipate milioni 25 nilipe hii bank niishi kama watu wengine. Yeyote atakayenipa nitakua namlipa taratibu au anipe kazi yoyote nimfanyie bure na nitaifanya kwa akili na uwezo wangu wote.

Nisaidien jamani nawaomba Mungu atawaridishia mlipotoa.

I declare my interest ID hii ni mpya kwa sababu zisizozuilika.

Yeyote atakaeweza kunisaidia nipo tayari kuongozana nae hadi bank ili ahakikishe kweli ninadaiwa.

Story ya deni ilivyo
Pesa hizo ziliingizwa kimakosa kwenye akaunti yangu na bank yenyewe na mimi kwa vile nilikua nategemea pesa nikajua ndio zangu nikafanya nazo biashara na biashara yenyewe watu wamenidhulumu nimebaki sina kitu nifanyeje mimi na biashara ilikua haijasajiliwa sina haki hata ya kuwapeleka mbele ya sheria ninaowadai jamani nitakufa mimi dunia itaniua mimi
Chochote ulichonacho naomba mchango wako jamani nitafanyaje mimi sina hela nipo nipo tu natamani nikitembea gari linipitie nife hapohapo dah
Bado upo?
 
Nilikua nachukua top up bank fulani pesa zikaingia kama ule mkopo wa mwanzo almost 12m. Nikakumbuka mkataba niliosaini kabla ya hizo pesa kuingia ulikua unasoma the same amount ambayo iliingia kwenye akaunti yangu. So nikajiridhisha that was my top up loan. Nikawa nadraw kidogo kidogo kama kawaida tu bila shida. After a month the bank called me and asked why I took the money I was not supposed to. By that time I had already put the money into a business ya kukopeshana. Watu wamenidhulumu hela nikajikuta sina nilichokifanya zaidi ya kupoteza hela. Today is almost four months toka wanitafute hiyo bank na huwa nadepost at least kila mwezi laki tatu kutoka kwa wateja baadhi kuwa waaminifu. Sasa wateja waaminifu wamemaliza madeni yao na mimi sina pa kupata hela zaidi ya mshahra wangu wa laki2 sina mali yoyote wala biashara tena benk wananizalilisha kila sehemu nashindwa hata kutoka nje..watu wananicheka kila wakiniona natamani tu Mungu anichukue hata SAA hii..nadhalilika mno nisaidieni jaman
Watu mnaojidai kuongea vingereza bwana,matapeli sanaaa
 
Ww jiuwe tu ptu...ptu unazan kwenye shida ni peke yako hzo ela umekula na nan alafu uje kuomba msaada huku JF

Kama ww ni ke uza kipochi manyoya ukalipe deni
Kama me uza 0713......
 
Nimeshauriwa kifuatacho na mdau kuhusu tatizo langu nami nalileta kwenu kuomba ushirikiano wenu wana Jf sina kwingine pa kukimbilia ni Mungu na huku Jf

Mdau amenishauri hivi:
Nipate wana Jf 5000 ambao wanweza kunichangia kila mmoja tsh 5000 ili nipate 25m nimalizane na hii bank.

Kila atakaenichangia nitamuandika then kila mwisho wa mwezi nitakua narudishia watu 200 walionichangia hizo elf 5000 hivyo ndani ya miezi 25 nitakua nimemrudishia kila mwana Jf pesa aliyonisaidia. Wana Jf naomba mnisaidie kwa hili bank wanataka pesa kabla mwezi haujaisha
Mnaweza kutafuta mtu wa kupokea hiyo michango na atakaethibitisha kweli ninadaiwa kwenye hiyo bank coz wengine mnaweza kuhisi mimi ni tapeli ila sivyo. Chochote kitakachopatikana hata leo naenda kupeleka bank ili kupunguza deni. Nisaidieni wapendwa sina pa kuanzia nimefiliska vilivyo
Upo daslamu au mkoani?
 
Hizi story za kitoto!
Uingiziwe 25m, then ujue ni zako how comes!
Then 25m umedhurumiwa kwenye biashara tena!!
Wewe kufa tu, au acha wakufunge!
 
Wakati unakopa ulitushirikisha?ulitugawia?iweje kulipa tusaidiane?mbaya zaidi eti una elfu sita,bora hats ungekuwa umetoa kiasi kikubwa tayari bado kias kidogo usaidiwe kumalizia
 
Back
Top Bottom