Nihurumieni mwenzenu nakufa

Nihurumieni mwenzenu nakufa

Poleee, ID/Account umefungua usiku saa tatu, Huu uzi umeuandika usiku huu saa tisa kamili, ngoja tukusubr mpk asubu ukanushe au laaa.... pengne unaota au n haya masimu ya tecno umelilalia limeshafungua ID lenyewe likacopy mavitu kutoka FB au kweny Msg za kawaida likaingia Jf likapest lika post, maana inaonesha umepost tu n kama lijisaa limepita hukurud tena hewan, Au ndo umepata usingz? M mwenyewe sidaiwi wala sina stress zozote lakn nimekosa ka usingz sembuse mtu anaefikiria kufaaa?

Kama n kweli, Pole sanaaa kwan huna assets zozote zinazofka hio 25M Au kukaribia? Mda wa kulipa deni kwa hiari walikupa na umeshapita? umejarb kuongea nao kwa busara ukawaeleza nia yako ya kulipa? huwez huko huko bank ukafanya kaz bure kwa mda utakaofidia hilo deni?
M25 si haba kama huna hata mia na huna mzunguko wa kuipata, ila huwez ilinganisha na uhai wako dada, una uhakika wapo serious wanataka wakufunge?

Mana Hakuna watu wenye mikwara kwenye kudai kama bank, hata wakikukopesha au wakikuomba ukope wanakuletea vijidada vizurii vinawaka waka, sauti nyororo, ngozi chocolate,
Wakija kudai sasaaa.... Unaletewa njemba imefumuka usoo. Nyeusi tiii huku imevaa miwani inafunika mpk matundu ya pua, suruali kama pajama, chini bonge ya buti au raba kama za kangi, ikiingia inakua na mbwembwe mnasalimiana huku anazima switch huku anachomoa cable za tv, fridge n.k

Unasema atakae kusaidia utampa chochote atakachotaka,
My dear sister hicho chochote baadae inaweza iwe mthan zaid ya huu utaman ukakope tena bank hata mara mbili ya hio ulipe kuondokana na chochote,
Binafsi mimi na hvyo sina familia bd, ningetoroka kwanza nikaanze kuzisaka, Kama kuna watakachofanya huko nyuma poa tu, LAWAMA HAPEWI MBUZI, siku nazipata nawaletea kwa suprise uone kama watakusumbua,

Wazee tujifunze kitu hapa, usikubar kutoka kapa
Tecno imefungua ID yenyewe
 
pole sana tena sana, ila mkuu kusema ukweli ka hautudanganyi benk kama benk kuingiza hela kimakosa kwenye akaunt ya mtu mpaka unazitumia zote hawajashtuka hio benk hawako makini na hauna haja ya kuangaika nao,
kingine hapa jf watu wana hamasika kumsaidia mtu aliekwama eidha afya au kimaisha na msaada wake ukihita laki 5 kushuka chini, huyu akitoa elfu 10 huyu 50 mwingine laki zaidi ya hapo kwa kweli sidhani kama hapa jf wanaweza kuhamasika kwa hilo la kwako kwa kweli. labda sana ingekua ni matibabu na hapo bado hela ni nyingi mno.
lakini uziogope maana Neema ya Mungu ni kubwa mnoo USIOGOPE.
 
Habari zenu wanajf wenzangu

Nina shida jamani eee Mungu wangu nisaidie niweze kueleweka.

Nahitaji watu wenye moyo wa kujitoa wanisaidie jamani nipo karibu na mauti mimi.

Wapendwa nadaiwa pesa nyingi sana na bank na sijui wapi nitaweka sura yangu maana watu hawa wamechachamaa kweli mfukoni nina elfu 6500 tu jamani mimi nitaenda wapi.
Natamani nijitoe uhai ila nawaza huko niendako itakuwaje nikikutana na moto wa jehanamu milele?

Wanajf nyie ndio tegemeo langu LA mwisho naombeni mnisaidie deni linatakiwa kulipwa kabla mwezi kuisha la sivyo mimi nitahukumiwa jamani ohhh

Sina pa kukimbilia yeyote anayeweza kunisaidia kwa masharti yoyote nipo tayari ili mradi mimi niachane na hili deni jamani niishi kwa amani. Nahitaji watu 25 wakujitolea kila mmoja milioni moja nipate milioni 25 nilipe hii bank niishi kama watu wengine. Yeyote atakayenipa nitakua namlipa taratibu au anipe kazi yoyote nimfanyie bure na nitaifanya kwa akili na uwezo wangu wote.

Nisaidien jamani nawaomba Mungu atawaridishia mlipotoa.

I declare my interest ID hii ni mpya kwa sababu zisizozuilika.

Yeyote atakaeweza kunisaidia nipo tayari kuongozana nae hadi bank ili ahakikishe kweli ninadaiwa.

Story ya deni ilivyo
Pesa hizo ziliingizwa kimakosa kwenye akaunti yangu na bank yenyewe na mimi kwa vile nilikua nategemea pesa nikajua ndio zangu nikafanya nazo biashara na biashara yenyewe watu wamenidhulumu nimebaki sina kitu nifanyeje mimi na biashara ilikua haijasajiliwa sina haki hata ya kuwapeleka mbele ya sheria ninaowadai jamani nitakufa mimi dunia itaniua mimi
Chochote ulichonacho naomba mchango wako jamani nitafanyaje mimi sina hela nipo nipo tu natamani nikitembea gari linipitie nife hapohapo dah
Acha hadithi za kitoto.
Maelezo yako haya shawishi kukusaidia.
RUDIATENA KUTUNGA HIYO HADITHI
 
Hiyo pesa uliyonayonayo anzisha biashara ya wanzuki na gongo mara moja mpaka mwezi unaisha utakuwa umerejesha laki moja-tano kwa kuwa wewe ni wakike unaweza ukautoa mwili wako kwa muda maalumu wakati huohuo unaofanya biashara ya gongo unakuwa "Multipurpose worker" 😂😂😂
 
Mmmmh chai hii...

Anyway muone Dr shika anaweza kukusaidia billionaire yule
 
Hizo ambazo ulitegemea ziingizwe na zo umeoeleka wapi?si ungelipa bank?aunuliwaona wajinga ukala na hizo nyingine,umekula milioni 50 halafu sisi tukulipie,wafuate wale makahaba ulikokaanao pale BAR YA TABATA.
 
Yaani unawapangia kabisa kila mmoja atoe miliooo... Yaani milioooo kwa mtu tu. Usione hivi, humu kila mtu anashida zake.

Ungesema mtu kama anachochote achangie ungeshangaa mpaka mchana unazaidi ya milioo ya kuwapooza.
 
Swali: Kama hizo 25 ml.ziliingia kimakosa nawewe ukadhani ndo zile ulizokuwa ukizitazamia, je, zile ulizozitazamia mbona hautuletei mrejesho wake?
Ziko wapi, ulitarajia zitoke wapi ?
Jibu kwanza haya maswali ili wengine tuanze kuchambua. Tatizo mjini kila mtu tapeli, pesa kuitoa sasa mpaka ujiridhishe.
 
Mimi sio tapeli jamani ila kila mtu ana maoni yake na ninayaheshimu hii story ni ndefu sijui nianzie wapi na niishie wapi hiyo milioni 25 haikuingizwa yote iliingizwa 12m na mimi nilikua na deni na hiyo bank so wamepiga mahesabu natakiwa kurudisha 25m mimi naipata wapi mwenzenu sina hata pa kuanzia jamani sina mali zozote zaidi ya fridge na godoro langu uwiii mimi
 
Back
Top Bottom