Nifanye nini katika hili?

Nifanye nini katika hili?

Yeye mwenyewe mtoto
Wakwe wanaitafuta wamchape eti
Mimi nadhani tunatofautiana mawazo ila uhakika wa maisha ni kuwa makini swala la udogo na ukubwa hapana ndo kama hapo sasa mimi nilichoomba ni ushauri tu ulichocomment wewe ni ipi haya sasa huo ukubwa wako haujawaza hata neno pole alafu ndo ukubwa unaousemea hapana siutaki kaa na ukubwa wako
 
Bila shaka mkeo ni kutoka mikoa ya lindi ,mtwara au pwani ikizid sana tanga
 
Hebu mkae mkue Kwanza maana hata balehe bado
Hata sijui kama mnakojozana
Muache akae kwao akue na wewe ukue Kwanza muda WA kuona ukifika ndo muanze mapema
Watoto wadogo acheni kukurupukia. Ndoa na mapenzi
Ila wewe mungu anakuona shukran
 
Kwema wakuu, naombeni ushauri ili nipite kwa amani.
Mimi ni kijana wa miaka 25, nina familia na mtoto mmoja.

Mwaka huu mwezi wa 6 nilirudi, mzazi mwenzangu akaomba aende kwao, nikakubali. Nilipokuwa nyumbani nikaanza kutembelea marafiki. Rafiki yangu mmoja ambaye tunafanya kazi pamoja tukaamua kwenda kujipongeza. Vitu vilikwenda vizuri na hatimaye tukaenda nyumbani kwangu.

Tulipofika nyumbani tukaanza utani, hata tukampigia simu mzazi mwenzangu tukamdanganya kwamba nimekamatwa na nimepelekwa polisi. Alijibu kuwa kesho atakuja mapema. Baada ya hapo tukaanza story, tukaendelea kucheka mpaka tukalala.

Saa nane usiku nikasikia geti linagongwa. Nilipotoka nikakuta ni jirani yangu pamoja na mama mdogo na mume wake. Wakanuliza kuna shida gani kwa kuwa wamesikia nimekamatwa. Niliwaeleza ilivyokuwa na waliponiambia aliyesema hivyo ni rafiki yangu, nikacheka na kusema ilikuwa ni utani.

Siku kumi baadaye mzazi mwenzangu akarudi nyumbani, na ndipo matatizo yalianza. Alianza kununa kila mara. Nilipomuuliza alinieleza mambo mengi ambayo sikuyajua. Kitu kikubwa alichokisema ni kwamba:
"Nimeambiwa nilienda kunywa pombe kwa sababu nililazimishwa kuwa naye, kwamba simpendi ila najilazimisha."

Nilipomuuliza nani aliyemwambia hivyo, akasema ni yule jirani ambaye alikuja usiku, na jirani huyo kaambiwa na mama mdogo. Nilimwambia aachane na hayo kwa sababu ni kama kufukua makaburi.

Baada ya hapo akaanza kutaka kwenda kwa baba mdogo wake (anayekaa karibu), lakini nilikataa kwa sababu tayari aliwahi kukutana naye alipokuwa kwao. Usiku mzima akanuna, asubuhi nikatoka zangu. Ghafla akanitumia sms kuwa anataka aende kwao, hataki kukaa na mimi na nimwambie sehemu ya kuacha ufunguo. Nikamwambia akienda aache mtoto. Tukabishana, nikafunga mlango na geti nikatoka.

Baadaye mama mdogo akanipigia akisema nirudi tuongee, lakini nilichelewa kurudi. Niliporudi nikawakuta wanacheza. Mzazi mwenzangu akampigia simu baba mdogo wake akimwambia kuwa naogopa labda nitampiga. Baba mdogo akanitaka tuongee kwenye simu. Tuliongea vizuri, akanishauri nitulie. Lakini muda mfupi baadaye akampigia tena na kumwambia kuwa akikugusa tu, nitalipeleka polisi. Nilichukia sana.

Baadaye mzazi mwenzangu akaja kwangu, akalia na kuomba msamaha. Nikamsamehe ili mambo yaishe. Siku chache baadaye akaniomba tena aende kwa baba mdogo, nikampeleka mwenyewe na nikawaacha. Jioni akaniomba nimchukue, nikafanya hivyo.

Lakini siku moja nilichunguza sms zake na nikakuta ujumbe wa shangazi yake ukisema: "Tembea kidogo, kama haji nijulishe nikuitie toyo." Nikashangaa walikuwa wanazungumza nini kuhusu mimi, lakini nikapuuza.

Tangu amerudi kutoka kwao akaanza tabia za kutaka kila kitu akipate, kazi za nyumbani haziendi vizuri, chakula hakieleweki. Nikimwuliza analalamika kuwa namnyanyasa. Nilipuuza.

Kuna siku tulipanga kumwachisha mtoto kunyonya, lakini akasema ni mpaka mtoto awe na mwaka na nusu. Nilijiandaa kwa lishe ya mtoto, nikamnunulia unga na vingine. Lakini alipika uji wa ulezi akaweka mafuta ya alizeti. Nilipomuuliza akasema ni uji wa kawaida. Nikamwambia: "Huo siyo uji mzuri, umeweka mafuta ya alizeti, hamnazo kabisa." Akalia sana, akasema nimemdharau.

Siku nyingine akanitumia sms: "Naomba nauli niondoke, nimechoka haya maisha." Nikamjibu amuombe huyo anayemwendea. Akasisitiza nimpe nauli nimrudishe kwao. Aliposema nikiwa sina hela, akajibu: "Kama hutanipea nauli basi jiandae kwa yatakayoendelea humu ndani mpaka utanipa mwenyewe."

Nikamwambia nadhani na wewe umejiandaa. Akanijibu: "Ya kunywa pombe na kutunyima sehemu ya kulala." Kuna siku nililala kitandani katikati, akadai sitaki walale vizuri. Nilipuuza. Usiku nikawakuta wanacheka na mtoto, nikaingia chumbani. Kesho yake akaniambia ataondoka. Nikamwambia sina mafuta, tukaita toyo na akaondoka saa sita mchana kwenda kwa baba mdogo. Saa nane akanitumia sms: "Nitazoea tu haya maisha. Utaendelea kuharibu maisha ya wengine mpaka lini?"

Akanieleza pia anaenda kuanza maisha upya, na atambadilisha mtoto jina mpaka dini. Nikamwambia afanye hivyo kama anataka.

Kwa sasa muda wangu wa kurudi kazini umewadia. Ameondoka na ufunguo.
Naombeni mnishauri nifanye nini.

Poleni kwa gazeti hili refu, imebidi niandike yote ili mnielewe. Pia naomba msamaha kwa mwandiko wangu.
Wewe ni mzigo kwa nchi hii. Fikiria vipi taifa lingefaidika kama ungetumia muda kuandika kitu Cha maana mfano kilimo, elimu, biashara n.k..
 
Kwishaaaaah enyewee nimezingatia mkuu shukrani
Wewe umeshakuwa kuishi na Mwanamke inahitaji akili 1.bint au Mwanamke ukianza kumkubalia kila jambo ambalo unaona halina maana sana ujuwe hapo utapandwa kichwani mpaka kifo au kuachana 2. Akikwambia nataka kwenda mahal kila mara ujuwe Kuna kitu ananufaika nacho kama vile dudu jipya so kataa ikilazimisha mwambie nenda halafu Fanya mambo Yako kuwa busy 3. Kumbuka Upendo wa muda mrefu haulazimishwi
 
Wewe ni mzigo kwa nchi hii. Fikiria vipi taifa lingefaidika kama ungetumia muda kuandika kitu Cha maana mfano kilimo, elimu, biashara n.k..
Nikupe mtaji mkuu hiyo BIASHARA uifanye wewe
 
Nimejaribu kadri niwezavyo kuelewa lakini kwa kweli imekuwa ngumu.

Ila kwa nilichoambulia kidogo, baba mdogo anakula mzigo wa mkeo.

Pia kumbuka, mwanamke akitishia kuondoka kila mara ujue tayari keshakuwa na plan mbadala wa wewe. Muache aende zake.
Nakazia
 
Mwanaume utaoaje ukiwa na miaka 24? Piga chini huyo mwanamke kula ujana ukifisha kuanzia miaka 30+ ndo uanze kutafuta Bikra uoe, tena tafuta kuanzia Binti wa miaka 18 hadi 23 ndo

Huo umri ulionao sasa utumie kujijenga kiuchumi
 
Ni kosa mkuu mtu mbinafsi pekee anaweza ona sio kosa. Huwezi jua alikua mazingira gani alipopata hizo taarifa,unaweza ua mtu kwa presha. Bado akapoteza muda wa watu waliokufata kujua kulikoni hapo ulimuharibia kwa watu wake wa karibu kiasi cha kupuuzwa na kuonekana mzushi.

Pia kuna vitu umeremba sana unaficha tatizo ili uonekane u msafi. Mkuu hicho unachokificha ni adui yako mkuu
Kwamba hilo ndo kosa? Na imekuwaje kosa nieleweshe
 
Kwema wakuu, naombeni ushauri ili nipite kwa amani.
Mimi ni kijana wa miaka 25, nina familia na mtoto mmoja.

Mwaka huu mwezi wa 6 nilirudi, mzazi mwenzangu akaomba aende kwao, nikakubali. Nilipokuwa nyumbani nikaanza kutembelea marafiki. Rafiki yangu mmoja ambaye tunafanya kazi pamoja tukaamua kwenda kujipongeza. Vitu vilikwenda vizuri na hatimaye tukaenda nyumbani kwangu.

Tulipofika nyumbani tukaanza utani, hata tukampigia simu mzazi mwenzangu tukamdanganya kwamba nimekamatwa na nimepelekwa polisi. Alijibu kuwa kesho atakuja mapema. Baada ya hapo tukaanza story, tukaendelea kucheka mpaka tukalala.

Saa nane usiku nikasikia geti linagongwa. Nilipotoka nikakuta ni jirani yangu pamoja na mama mdogo na mume wake. Wakanuliza kuna shida gani kwa kuwa wamesikia nimekamatwa. Niliwaeleza ilivyokuwa na waliponiambia aliyesema hivyo ni rafiki yangu, nikacheka na kusema ilikuwa ni utani.

Siku kumi baadaye mzazi mwenzangu akarudi nyumbani, na ndipo matatizo yalianza. Alianza kununa kila mara. Nilipomuuliza alinieleza mambo mengi ambayo sikuyajua. Kitu kikubwa alichokisema ni kwamba:
"Nimeambiwa nilienda kunywa pombe kwa sababu nililazimishwa kuwa naye, kwamba simpendi ila najilazimisha."

Nilipomuuliza nani aliyemwambia hivyo, akasema ni yule jirani ambaye alikuja usiku, na jirani huyo kaambiwa na mama mdogo. Nilimwambia aachane na hayo kwa sababu ni kama kufukua makaburi.

Baada ya hapo akaanza kutaka kwenda kwa baba mdogo wake (anayekaa karibu), lakini nilikataa kwa sababu tayari aliwahi kukutana naye alipokuwa kwao. Usiku mzima akanuna, asubuhi nikatoka zangu. Ghafla akanitumia sms kuwa anataka aende kwao, hataki kukaa na mimi na nimwambie sehemu ya kuacha ufunguo. Nikamwambia akienda aache mtoto. Tukabishana, nikafunga mlango na geti nikatoka.

Baadaye mama mdogo akanipigia akisema nirudi tuongee, lakini nilichelewa kurudi. Niliporudi nikawakuta wanacheza. Mzazi mwenzangu akampigia simu baba mdogo wake akimwambia kuwa naogopa labda nitampiga. Baba mdogo akanitaka tuongee kwenye simu. Tuliongea vizuri, akanishauri nitulie. Lakini muda mfupi baadaye akampigia tena na kumwambia kuwa akikugusa tu, nitalipeleka polisi. Nilichukia sana.

Baadaye mzazi mwenzangu akaja kwangu, akalia na kuomba msamaha. Nikamsamehe ili mambo yaishe. Siku chache baadaye akaniomba tena aende kwa baba mdogo, nikampeleka mwenyewe na nikawaacha. Jioni akaniomba nimchukue, nikafanya hivyo.

Lakini siku moja nilichunguza sms zake na nikakuta ujumbe wa shangazi yake ukisema: "Tembea kidogo, kama haji nijulishe nikuitie toyo." Nikashangaa walikuwa wanazungumza nini kuhusu mimi, lakini nikapuuza.

Tangu amerudi kutoka kwao akaanza tabia za kutaka kila kitu akipate, kazi za nyumbani haziendi vizuri, chakula hakieleweki. Nikimwuliza analalamika kuwa namnyanyasa. Nilipuuza.

Kuna siku tulipanga kumwachisha mtoto kunyonya, lakini akasema ni mpaka mtoto awe na mwaka na nusu. Nilijiandaa kwa lishe ya mtoto, nikamnunulia unga na vingine. Lakini alipika uji wa ulezi akaweka mafuta ya alizeti. Nilipomuuliza akasema ni uji wa kawaida. Nikamwambia: "Huo siyo uji mzuri, umeweka mafuta ya alizeti, hamnazo kabisa." Akalia sana, akasema nimemdharau.

Siku nyingine akanitumia sms: "Naomba nauli niondoke, nimechoka haya maisha." Nikamjibu amuombe huyo anayemwendea. Akasisitiza nimpe nauli nimrudishe kwao. Aliposema nikiwa sina hela, akajibu: "Kama hutanipea nauli basi jiandae kwa yatakayoendelea humu ndani mpaka utanipa mwenyewe."

Nikamwambia nadhani na wewe umejiandaa. Akanijibu: "Ya kunywa pombe na kutunyima sehemu ya kulala." Kuna siku nililala kitandani katikati, akadai sitaki walale vizuri. Nilipuuza. Usiku nikawakuta wanacheka na mtoto, nikaingia chumbani. Kesho yake akaniambia ataondoka. Nikamwambia sina mafuta, tukaita toyo na akaondoka saa sita mchana kwenda kwa baba mdogo. Saa nane akanitumia sms: "Nitazoea tu haya maisha. Utaendelea kuharibu maisha ya wengine mpaka lini?"

Akanieleza pia anaenda kuanza maisha upya, na atambadilisha mtoto jina mpaka dini. Nikamwambia afanye hivyo kama anataka.

Kwa sasa muda wangu wa kurudi kazini umewadia. Ameondoka na ufunguo.
Naombeni mnishauri nifanye nini.

Poleni kwa gazeti hili refu, imebidi niandike yote ili mnielewe. Pia naomba msamaha kwa mwandiko wangu.
Wanaomuharibi ni hao ndugu zake baba mdogo na shangazi! Kama maelezo uliyotoa ndio hayo, basi huyo mwanamke ni vilw tu amekuchoka. Fanya muhamie mbali na ndugu zake na umbane kuwapigia simu ndugu zake ndiyo wanampa jeuri, akiharibikiwa atajuta badae!

Pia, uwe unampa mpa vijisenti vya matumizi binafsi, usiwe bahiri sana, wanawake wengine akili zao kama watoto, unakuta kuna muda anakuwa na hamu hata ya kununua pipi!
 
Back
Top Bottom