Nifanyaje ili mbwa wangu awe mkali!? Naomba ushauri

Nifanyaje ili mbwa wangu awe mkali!? Naomba ushauri

Hii kitu kufunga mbwa asione watu naipinga sana. Ulaya au Amerika na hata Asia watu wanaishi na mbwa ndani ya nyumba. Wanakula pamoja wancheza na watoto wadogo mle ndani na wanashare hata mabafu na vitanda lakini ni mbwa wakali hasa. Huwezi shika kitu mle ndani. So hiyo si kweli ni imani tu.
Angalia channel ya Annimal Planet kwenye DStv ndo utaelewa nachosema.

Wenzetu kama Marekani mbwa wa Police anaishi naye nyumbani kwa yule askari aliyekabidhiwa maana saa yoyote inaweza tokea dharua akaitwa kwenye tukio. Na hao mbwa ni balaa kwa ukali na wanaishi na familia tena kwenye flats.

Nadhani kwa mtindo huu unaoutaka wewe dog trainer haiepukiki au siyo? tulikuwa tunajaribu kepeana mawazo/ushauri kulingana na experience zetu.Wenzetu huko Ulaya na Marekani mbwa huhesabiwa katika possessions za familia,hapa kwetu ipoje? Mbwa wana sehemu maalum za kupata msosi "special" hapa kwetu je? Nina imani hata mbwa wa polisi wa hapa na huko Marekani unakosema hawatakuwa wanaangaliwa kwa usawa au siyo? Kitu kingine mkuu,kwa waafrika kuishi na mbwa kama wazungu waishivyo nao si kitu kilichozoeleka,kwa hiyo si kila kitu kiigwe kutoka huko maana hata sisi tuna watumia mbwa kwa namna tunavyoona inafaa kwa mazingira yetu na wao wana namna zao.
 
Mbwa wako ana meno au hana??

Anazo kucha au hana??

Kama hana basi mtoe sadaka kwa wachina...
 
MPE Chamkongo!!!!aka bangi ufurahie matunda!!nendapalesinza mapambano opp kunajaa wanauza matofali uliziahapo watakuuzia
 
Huyooo atakuwa mmbwa wakibisaaa tuuu habadilikiii hata kwa dawaa. Ukali wa mbwa unatokana na asili na mazingiraaa anapofugiwaa. Mbwa anaishi mtaaa ambao vigodoro ni 24 hrs unataka awe mkali kwa lip?
 
Mimi Nina mbwa ni anapata msosi Wa kueleweka sana na analala sehemu nzuri sana. Sasa ni kwamba mbwa wangu sio mkali hata kidogo!

Sasa naombemi msaada Wa ushauri wenu ni mlishe nini ili awe mkali!! Naombeni ushauri wenu wadau maana ninampenda sana mbwa wangu!

Karibuni washika dau na poleni na majukumu ya kila Siku!!! Karibuni kwa jukwaaaa
Weka picha ya mbwa wako tuweze kukupa ushauri kiduchu, angalia usije kuwa na wale mbwa haina ya wanaoshinda uani na bata na kuku.
 
kwanza asiwe exposed muda mwingi usimpe uhuru ya.pia jitahid wawe wawil akiwa mmoja confidens inapungua ila kuwa na mwenzake huwa wanaonesheazna utem nan zaid
 
nimecheka hadi machozi haijanitokea siku nyingi! watanzania tuna mawazo sijui kwa nini maendeleo hakuna
 
Hivi umbwa inavutaje tena........?......niliona siku nyingi nimesahau..........

Mbona rahisi...unamfungia kwenye chumba kidogo, halafu unamwekea bangi kwenye kifuu pamoja na kaa la moto ili bangi ifuke moshi, na unamwacha humo hadi bangi imeungua yote. Ila utakapomfungulia hakikisha umehamisha ndugu zako wote hapo nyumbani, na wewe umevaa suti ya chuma.
 
Mbona rahisi...unamfungia kwenye chumba kidogo, halafu unamwekea bangi kwenye kifuu pamoja na kaa la moto ili bangi ifuke moshi, na unamwacha humo hadi bangi imeungua yote. Ila utakapomfungulia hakikisha umehamisha ndugu zako wote hapo nyumbani, na wewe umevaa suti ya chuma.

Umenishaaaaa mzeeee VP unatania??
 
Mimi Nina mbwa ni anapata msosi Wa kueleweka sana na analala sehemu nzuri sana. Sasa ni kwamba mbwa wangu sio mkali hata kidogo!

Sasa naombemi msaada Wa ushauri wenu ni mlishe nini ili awe mkali!! Naombeni ushauri wenu wadau maana ninampenda sana mbwa wangu!

Karibuni washika dau na poleni na majukumu ya kila Siku!!! Karibuni kwa jukwaaaa

Wengi wa wafuga mbwa wanaieleza kanuni moja kwa kuirudia rudia, yaani niliyowahi zungumza nao siku za nyuma:

Ili kumfanya mbwa awe mkali asiwe na mazoea na binadamu au kiumbe kingine chochote, kama ni nyumbani kwako basi amzoee yule mwenye kumhudumia tu...
 
Kuna groups kama nne za mbwa (hapa sizungumzii breeds maana ziko nyingi sana)
1. Pet dogs hawa ni mbwa wa ndani ambao ni kwa ajili ya kuchangamsha nyumba mf Chihuahua.
2. Security dogs hawa ni mbwa kwa ajili ya ulinzi wa familia na mali zake mfano German Shepherd dogs, Doberman Pinscher,Rottweiler, Great dane, Boxer and Boerbull
3. Show dogs hawa ni kwa ajili ya kuonyesha kwenye mashindano au hata kwenye matembezi yako. Ni kwa ajili ya show off.
4. War dogs. Hawa ni special dogs from security group especially trained to be used in the warfare. Wanatumika vitani kama kunusa mabomu kufanya raking nk.

Swali langu mbwa wako ni aina gani? Naomna unitajie breed yake. Kwa sababu hiyo ni muhimu sana.

Pili ukali wa mbwa kinyume na wadau wengi walivyo shauri. Ni mafunzo. Wapo watu ambao wana taaluma ya kufundisha mbwa kuwa mlinzi wa familia na mali za familia. Hawezi ku attack bila kupewa amri na handler wake.

Kwa kuwa unampenda sana mbwa wako nakushauri nenda kituo cha Polisi Kilwa Rd. Kikosi cha Mbwa na Farasi utapata askari atakayemfundisha mbwa wako ili aweze kutii amri na pis kushambulia au kukamata pale inapobidi.
Kamilisha haya. Then lete mrejesho.

umesahau pia wapo mbwa wa nyama
 
Tafuta mbwa wa ulinzi mkuu...kuna wadau wameshauri breed za mbwa tafuta hutakuja kulalamika humu!! tafuta germany shepherd au rottweiler hutojuta!!pitbull sio wazuri kwa familia
 
Back
Top Bottom