Nifanyaje ili mbwa wangu awe mkali!? Naomba ushauri

Nifanyaje ili mbwa wangu awe mkali!? Naomba ushauri

Usimzoeshe kumfungua mchana labda kama unamuogesha...mpe chakula mara moja tu usiku ukimfungulia..mpe chakula ila at least mara moja nyama na mifupa kutest meno yasilemae na softfood....halaf ujaribu kuwa una msemesha matendo kama kukamata au kuacha kufanya kitu....zingatia itasaidia...ila inategemea na aina ya mbwa ulikomtoa...kama ile jamii flan inayoshinda sebulen kwa Wema Sepetu hawezi kuwa mkali hata ukimvutisha bange ndo atazidisha usingizi

Salute
 
Kuna groups kama nne za mbwa (hapa sizungumzii breeds maana ziko nyingi sana)
1. Pet dogs hawa ni mbwa wa ndani ambao ni kwa ajili ya kuchangamsha nyumba mf Chihuahua.
2. Security dogs hawa ni mbwa kwa ajili ya ulinzi wa familia na mali zake mfano German Shepherd dogs, Doberman Pinscher,Rottweiler, Great dane, Boxer and Boerbull
3. Show dogs hawa ni kwa ajili ya kuonyesha kwenye mashindano au hata kwenye matembezi yako. Ni kwa ajili ya show off.
4. War dogs. Hawa ni special dogs from security group especially trained to be used in the warfare. Wanatumika vitani kama kunusa mabomu kufanya raking nk.

Swali langu mbwa wako ni aina gani? Naomna unitajie breed yake. Kwa sababu hiyo ni muhimu sana.

Pili ukali wa mbwa kinyume na wadau wengi walivyo shauri. Ni mafunzo. Wapo watu ambao wana taaluma ya kufundisha mbwa kuwa mlinzi wa familia na mali za familia. Hawezi ku attack bila kupewa amri na handler wake.

Kwa kuwa unampenda sana mbwa wako nakushauri nenda kituo cha Polisi Kilwa Rd. Kikosi cha Mbwa na Farasi utapata askari atakayemfundisha mbwa wako ili aweze kutii amri na pis kushambulia au kukamata pale inapobidi.
Kamilisha haya. Then lete mrejesho.
 
Kuna sehemu Mwenge niliona bango la mwalimu wa mbwa (dog trainer) inawezekana wao wanajua sababu za kitaalam zinazomfanya mbwa awe mkali au mpole kesho nikipita nitasoma namba yake nitaileta hapa. Ila moja ya basics ni kumtenga,asiwe ana mazoea na watu awe anafungiwa mapema alfajiri na kufunguliwa usiku si chini ya saa nne,niliwahi kuwa na mbwa nikiwa mdogo mbinu hii ilinisaidia japo matokeo hayakuwa mazuri kama nilivyotaka. Wengine waliniambia mbwa hatakiwi kula vyakula vilivyoungwa na vyenye chumvi, wengine ndo kama mkuu dabo wakadai niwape bange ila zote hizi hazina uhakika na ni kama imani tu (myth). Mbwa umpe bange akiwa kichaa akakudhuru wewe mwenyewe utasemaje?

Hii kitu kufunga mbwa asione watu naipinga sana. Ulaya au Amerika na hata Asia watu wanaishi na mbwa ndani ya nyumba. Wanakula pamoja wancheza na watoto wadogo mle ndani na wanashare hata mabafu na vitanda lakini ni mbwa wakali hasa. Huwezi shika kitu mle ndani. So hiyo si kweli ni imani tu.
Angalia channel ya Annimal Planet kwenye DStv ndo utaelewa nachosema.

Wenzetu kama Marekani mbwa wa Police anaishi naye nyumbani kwa yule askari aliyekabidhiwa maana saa yoyote inaweza tokea dharua akaitwa kwenye tukio. Na hao mbwa ni balaa kwa ukali na wanaishi na familia tena kwenye flats.
 
Last edited by a moderator:
Hawa mixed breeds aka mbwa koko wa kawaida ni kupoteza muda. Tafuta breed anayefahamika kama pitbull. Sijui kama wapo Bongo. Huyu ni hatari. Anaweza kukurarua hata wewe mwenyewe ukapoteza viungo na kuumbuka mtaani kwenu.

Nakubaliana na wewe ukali wa mbwa pamoja na breed anahitaji TLC (Tender Love and Care) lazima atakuwa mkali.

Nimekuwa nafuga mbwa maisha yangu yote tangia mtoto mpaka sasa watoto wangu nao wanafuga. Kuna breed ambazo naturally ni wakali sana mojawapo ni Pitbull ingawa hawa wanahitaji uangalizi wa karibu vinginevyo jiandae kwa majanga.
 
Mimi Nina mbwa ni anapata msosi Wa kueleweka sana na analala sehemu nzuri sana. Sasa ni kwamba mbwa wangu sio mkali hata kidogo!

Sasa naombemi msaada Wa ushauri wenu ni mlishe nini ili awe mkali!! Naombeni ushauri wenu wadau maana ninampenda sana mbwa wangu!

Karibuni washika dau na poleni na majukumu ya kila Siku!!! Karibuni kwa jukwaaaa
hapo red
punduza kulishalisha vyakula sana, hakikisha anakula mara moja kwa siku!
blue
mfungie kenye banda na uwe unamtoa jion tu!
 
Kwny chakula chake mjengee mazoea ya kumchanganyia na bange mbichi halafu kwny maji ya kunywa angalau kisikosekane angalau kiroba kimoja kila cku , hapo nakuhakikishia hata simba watakuwa wanamuogopa[/QUOTE
walah hatakua mkali bali atazd atadata
 
Huu ndo ukweli sio kila mbwa ni mbwa wa kuwa mlinzi kuna mbwa wa mapambo, kuna mbwa ilimradi uwe na mfugo na kuna mbwa mlinzi tafuta species ya mbwa mlinzi kama german shepherd huyo mbwa ni mkalii tuu haiitaji umfundishe au eti asione watu cjui umfungue saa 7 usiku yaan huyo ni mkali tuu ndo asili yake
 
Mimi Nina mbwa ni anapata msosi Wa kueleweka sana na analala sehemu nzuri sana. Sasa ni kwamba mbwa wangu sio mkali hata kidogo!

Sasa naombemi msaada Wa ushauri wenu ni mlishe nini ili awe mkali!! Naombeni ushauri wenu wadau maana ninampenda sana mbwa wangu!

Karibuni washika dau na poleni na majukumu ya kila Siku!!! Karibuni kwa jukwaaaa

Wewe ndiyo umemwalibu mbwa kama una mlaza kwenye godoro unategemea nini! Hapa mpe bhange mkuu ila ukuwe care ful maana anaweza ata kukuswaga Master wake!
 
mpe bangi dozi tatu kwa siku kwa siku kumi.....baada ya hapo kiumbe che uhai kamwe asikione isipokua mlisha bangi
 
Mi nilishawahi kuwanywesha viloba haikusaidia maana siku walipokuwa wakinywa viloba walikuwa wakipiga usingizi sana na usiku unaisha bila kubweka


Ungewapa viloba vya Malawi ungeona wanavyo kuwa wakali jaribu kiloba cha Malawi
 
Weka Bange kwenye chakula & mletee Siafu wamuume na pia yale nyumba ya manyigu mchanganyie kwenye msosi wake.

Ukifanya hivyo utakuja nipa majibu yake baada ya week moja tu asogei mtu maskani . Chakula ni mara moja tu masaa ya

usiku kwenye saa tatu unapomfungulia, hakikisha pia asionane na watu wengi tofauti na yule ampaye menu.
 
Back
Top Bottom