NIDA yakanusha kutangaza nafasi za ajira, tuepuke matapeli

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,035
Kufuatia uwepo wa taarifa za baadhi ya wananchi hususani kutoka Zanzibar kupigiwa simu na watu wasiowajua wakiwafahamisha kuwa wanatafutwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili waajiriwe na kuwataka wananchi wanaowapigia simu wawatumie tarifa zao na pesa ili kuwasaidia kupata ajira hizo, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imekanusha kutangaza au uwepo wa ajira zozote katika mamlaka hiyo katika siku za karibuni.

NIDA imeeleza kuwa endapo kutajitokeza haja ya kuajiri watumishi wapya, nafasi hizo zitatangazwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma na hivyo imewaomba wananchi wote watakaopigiwa simu zenye ujumbe huo kutoa vyombo vya usalama ili hatua za kisheria zifuatwe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom