Ni zipi taratibu za kuanzisha chama cha siasa Tanzania?

Wakuu naomba msaada wa hatua za kufata,taratibu na vigezo ili niweze kufungua chama cha siasa
pia njia za kukifanya kifahamike na kukubalika mapema
maisha ni magum naona bora nijaribu na huku
pia nawaza kukipa jina la CHAMA CHA UKOMBOZI
karibuni
Ukisajili kupitia CCM kitasajiliwa Faster
 
Wanajamvi msaada namna ya kusajili chama cha siasa hadi kupata usajili. Nafahamu kuna ofisi ya msajili ila tuanzie kwanza hapa kwa wenye kufahamu utaratibu.
 
Salamu wakuu,

Naomba kufahamu taratibu za kuanzisha chama cha siasa.

Ahsanteni..
SASA NIMEPATA UTARATIBU WA KUSAJILI AU KANZISHA CHA UKO HIVI

Haki ya kusajili na kuwa na chama cha siasa ipo kwa kila mtanzania. Hata wewe unaweza kuwa na chama cha siasa ikiwa utataka kufanya hivyo. Wako wanaofikiri kusajili chama siasa ni jambo kubwa mno. Laa hasha ni jambo la kawaida na utaratibu wa usajili si mgumu kama wengi wanavyodhani.

Tutaona hapa utaratibu wa kusajili chama cha siasa. Sheria namba 5 ya 1992 Sheria ya Vyama vya Siasa na kanuni zake za mwaka 1992 ndizo zinazoeleza utaratibu utakaoelezwa hapa chini.

USAJILI HUPITIA HATUA KUU MBILI.

Kwa mujibu wa kifungu cha8( 1 ) cha sheria ya vyama vya siasa usajili hupitia katika hatua kuu mbili.

Kwanza usajili wa muda na pili usajili wa kudumu. Kwahiyo ili usajili chama cha siasa yakupasa kupitia hatua hizi mbili.

is (1)


  1. USAJILI WA MUDA(PROVISIONAL REGISTRATION).


Usajili wa muda umeelezwa katika kifungu cha 9 cha sheria hiyo. Usajili wa muda maana yake chama kitasajiliwa na kitaruhusiwa kufanya baadhi ya kazi ila usajili huo utakuwa haujakamilika mpaka baada ya kutimiza masharti, sifa na viwango vilivyowekwa na sheria ndani ya muda maalum ulioainishwa na sheria. Usajili wa muda ndio unaoanza na utaratibu wake ni huu ;

( a ) Andaa katiba ya chama na hakikisha unakuwa nayo. Mnajua kila chama cha siasa huwa na katiba yake, basi hiyo ndiyo inayotakiwa hapa.

( b ) Hakikisha mko waanzilishi wasiopungua wawili.

( c ) Andaa kanuni za chama. Kanuni na katiba ni tofauti. Kanuni ndizo zinazotafsiri katiba kwahiyo kanuni hutokana na katiba.

( d ) Mtajaza fomu ya maombi iitwayo PP 1. Inapatikana kwa msajili na pia ipo sehemu ya kwanza ya kanuni za vyama vya siasa za 1992, waweza kutoa kopi.

( e ) Waanzilishi watajaza fomu maalum iitwayo PP 2 ambayo ni kama kiapo(declaration).

( f ) Baada ya hapo hivyo vyote vilivyoandaliwa vitapelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kwa uhakiki. Baada ya uhakiki na kukidhi sifa mtatakiwa kulipa ada kwa maelekezo ya msajili na hapo usajili wa muda utakuwa umekamilika.

( g ) Mtapewa cheti cha usajili wa muda.

  1. USAJILI WA KUDUMU( FULL REGISTRATION).
Kifungu cha 10 cha Sheria ya vyama vya siasa ndicho kinachoeleza hili.

( a ) Usajili hapa unatakiwa ufanyike ndani ya siku 180 tokea kupata cheti cha usajili wa muda.

( b ) Lazima kuwe na cheti cha usajili wa muda.

( c ) Lazima mpate wanachama wasiopungua 200 ambao wana sifa za mpiga kura. Hawa watatakiwa kutoka ndani ya mikoa isiyopungua 10 ya Tanzania , ambapo mikoa isiyopungua 2 kati ya hiyo 10 iwe ya Zanzibar, na katika hiyo 2 ya Zanzibar mkoa mmoja uwe wa Unguja na mwingine Pemba.

( d ) Mtajaza fomu nyingine ya maombi iitwayo PP 3

( e ) Pia wanachama 2 waanzilishi watajaza fomu maalum iitwayo PP 4.

( f ) Taarifa zote hapo juu zitapelekwa kwa msajili, na huko mtalipa ada kwa maelekezo yake ikiwa mmekamilisha mahitaji
 
Back
Top Bottom