Kadi ya chama cha siasa haiwezi kutumika nje ya mipaka ya chama hicho

JamiiCheck

Member
Nov 3, 2023
54
41
Kadi ya chama.jpg

Kadi ya chama cha siasa, ni nyaraka anayopewa mtu aliyejiunga na chama fulani cha siasa kuthibisha kuwa yeye ni mwanachama halali au hai wa chama hicho.

Wapo watu wengi wamekuwa hawatambui kazi ya kadi ya vyama vya kiasa na hudhani au huaminishwa na aidha wanaowashawishi kujiunga na vyama au wao wenyewe hudhani kadi zao zina nguvu ya kutumika nje ya mipaka ya kichama. Wapo wanaowashiwishi watu wajiunge na vyama vyao ili wapate kadi zitakazo wawezesha kupata huduma nyingine mbali ile ya utambulisho wa uanachama wa chama hicho,.

Mfano, wapo ambao huamaini au huamishwa kadi za vyama vya siasa watakavyojiunga zitakuwa na nguvu ya kutumika kama kadi za kutolea fedha benki, au kuwapa upendeleo wa aiana aia fulani nje ya mipaka ya kichama.

Kadi ya chama cha siasa haina sifa za kumuwezesha mwananchi kupata nafasi ya upendelea kwenye huduma za kijamii au kupata haki ya kupata ajira serikalini au kwenye sekta binafsi.

Kadi ya chama cha siasa haimpi mwanachama wa chama chochote upendeleo wa kusamehewa kodi, au kuwa juu ya sheria. Kadi ya chama cha siasa huwa na thamani ndani ya chama husika, na haiwezi kuvuka mipaka ndani ya chama husika.

Kumekuwa na uzushi unaozushwa kwa wananchi kuwa wakiwa na kazi za vyama vya siasa wataweza kupata huduma za kijamii kwa upendeleo, au kuweza kupata upendelea kwenye baadhi ya mambo, taarifa za namna hiyo huwa za uladhai na hazina ukweli wowote.

Kadi ya chama cha siasa mipaka yake huishia ndani ya chama, itakuwezesha kufanya shughuli zinazohusika na chama hicho tu, kama kuchaguliwa na kuchagua.

Kama utahitaji kuwa na kadi ya chama chochote cha siasa uwe nayo kwa sababu umeona chama hicho kitakupa manufaa kwaajili ya kukukuza kisiasa au kukupa haki ya kuchaguliwa au kumchagua mgombea ndani ya chama husika na si vinginevyo.

Hivyo ni muhimu wananchi na wanachama wa vyama vya kisiasa kutambua kuwa kadi ya chama cha siasa ni utambulisho tu uanachama na si zaidi ya hapo a itatumika ndani ya chama pekee.

Zaidi, tembelea Jukwaa la JamiiCheck kwa kubofya HAPA.
 
Back
Top Bottom