Kuna Visiwa vingapi kandokando ya Afrika? Jee, hivi Visiwa vinategemea kuwepo kwa Tanganyika? Jee, hivi Visiwa vinapata ruzuku yeyote kutoka Tanganyika ? Je, viwango vya maisha ni sawa kama Tanganyika? Unajua GDP ya kisiwa kama Mauritius? Tanganyika iko nafasi ya ngapi kiuchumi katika Afrika?
Mafuta yakiwepo yasiwepo,Zanzibar itaendelea na harakati za kujikomboa...MPAKA KIELEWEKE... HIZI SIO ZAMA ZA NYERERE ...
Unapokuwa na jazba unapoteza thamani ya mjadala na hata hoja zako zinavurugika na kupandana.
Niliposema uchumi utategemea kwa kiwango kikubwa uhusiano na Tanganyika, halikuwa na maana ya kudhalilisha bali upo ukweli ambao werevu wanautambua.Kwa bahati nzuri huko Mauritius na Zanzibar nimekaa kwahiyo nafahamu vema kile ninachoongelea.
Nitakufafanulia kidogo. Visiwa havitegemei uwepo wa Tanzania kwani vingine havikaribiani kabisa. Mauritius nimeishi sehemu inaitwa (Katrebon kwa kifaransa) nimeona maisha ya mtu wa kawaida na maisha ya matajiri. GDP unayoiongelea ni nzuri sana lakini si kama unavyoona kwenye internet.Nimeona utamaduni wao, uchumi na mahusiano yao na wafaransa.
Comoro ambayo ina ukaribu sana na ZNZ si kama Mauritius na ni mshiriki mzuri wa biashara na Bara, ungejiuliza kwanini si msumbiji.
Kampuni ya Maersk iliwahi kukataa mizigo ya kwenda Znz, na walitoa sababu kuwa ni bora konteina 14 za Znz zikashushwe Dar iwe sehemu ya konteina 400. Na hivi tunapoandika wafanyabiashara wengi kutoka Znz wantumia bandari ya Dar pamoja na ubovu na uzembe uliopo. Hapa ndipo unapaswa kujiuliza kwanini! ili hali kuna bandari huru nchi ya neema Znz.
Kampuni ya Zantel iliyojinasibu kuwa mkombozi wa cellphone visiwani kwa tech ya satellite kutoka uarabuni, ilifikia mahali serikali ya ZNZ kuzusha zogo kwanini isisajiliwe Bara. Hii ni kufuatia hofu ya Zantel kutaka kufunga virago kutokana na volume ya biashara. Sasa na makao makuu wanahamisha kabisa. Ni bora kuwa na soko la watu laki moja wa Ilala wenye nguvu katika biashara na si vinginevyo.
Si Znz, hata Tanganyika inawashirika wake inawategemea kiuchumi. Kufutwa kwa ubaguzi South Africa kumeifanya Zambia isitumie Tanganyika na matokeo yake ni kuangaka kwa biashara ya Tanganyika. Kenya nayo pia inaitegemea Tanganyika kama soko lake, Uganda inategemea Kenya. Kama ilivyo US inategemea Canada na Mexico ndivyo Japan inategemea US na China inalenga Africa.Ni mahusiano ya kibiashara yanayonifanya niseme Znz itaathirika kwa kiasi fulani.
Rwanda na Burundi ambazo hatukuwa na mahusiano kwa misingi ya mipaka na tamaduni za kikoloni, zimepigana sana kuwa ndani ya EA. Si kwasababu nyingine bali kwa fursa zilizopo. Huu ni mfano tu wa kuonyesha ni jinsi gani size na population vinavyohusika kiuchumi.
Kwa mwekazaji yoyote atakayetaka kuwekeza Zanzibar, kwanza hata angalia Znz bali nchi jirani. Kwa jinsi ilivyo Tanganyika itapewa jicho la kwanza kwa kuzingatia vigezo vyote vya kiutamaduni, kisiasa na kiuchumi vinavyoshabihiana sana na Znz.
Hata kufikiri kwa kiwango cha kawaida, wznz wenye biashara bara haina maana hawawezi kufanya kenya au kwao, lakini kuna sababu za msingi wao kufanya hivyo, na labda kawaulize ili wakupe jibu wao wenyewe.
Yote hapo juu ni mifano ya kuweka sawa mjadala na neno 'tegemezi'. Ni lazima ukweli uitwe ukweli hata kama unauma.
Pamoja na yote haya ni muhimu sana mkaomba mswada wa kura ya maoni ili muamue hatima ya nchi yenu yenye mito na asali.