Ni Zanzibar ipi wanaitaka?

Ni Zanzibar ipi wanaitaka?

Huku mitaani naishi na wznz, hawa ni watu wa kawaida na wanaendesha maisha yao bila wasi wasi, wao muungano ni sehemu ya neema kwani wakienda bahari wanaleta pweza, wakirudi znz wamebeba viazi, watoto wanakwenda shule wanatibiwa n.k. kundi hili hawaoni Znz ya pepo yenye mito ya maziwa na asali bali Znz ya juhudi zao na fursa ya muungano.

Kuna kundi la wale waliosoma vitabu na kuamini kuwa Znz ya enzi hizo ilikuwa ni bora sana, znz ya sultani kwani tende, halua na mchele vilipatikana bure kutoka uarabuni. Kundi hili linaungwa mkono na wafanyabiashara kutoka uarabuni wanaotaka kurejesha usultan kwani nao wanatamani zama za usulatan wao a.k.a znz yao.

Wapeleke mswaada wa kura ya maoni ili warudishe nchi ya neema, nchi ya kusadikika, yenye mito ya asali, na mabwawa ya maziwa.

Mkuu.
Haya mambo ya muungano yanakugonga sana inaonekana. Maana yake lugha unayoiteremsha katika michango yako.... utafikiri Nyerere kafufuka!

Mkuu nguruvi3.
Tutalinda mapinduzi mpaka lini?

Bora jamaa warudishiwe sovereignty yao halafu wataamua wenyewe kama watachinjana au watatoana macho, au watakwenda baharini kutafuta pweza au kutafuta ng'ombe kukamua maziwa au kufuga nyuki ili wapate asali.

Mwanamapinduzi Gaddaffi si unamuona anavyolinda mapinduzi yake?
Sasa unataka ya Libya yaje TZ pia? Kuna kauli zinatolewa wajaribu wakione...kuna crime against humanity siku hizi ukiteleza wenye maliasili zao wanakuja na manoari za kivita na drones kukuletea demokrasi.

Mimi nafikiri wale wazee wa umri kama wako,nafikiri tu,kwa sababu unazungumza kama mwanamapinduzi.., au Jumbe, Ali hassan mwinyi, Nassor Moyo, Edwin mtei, Bomani, warioba, salim Ahmed salim, Seif sharif wakati wao umepita...sasa kuna vijana wa utandawazi, wa internet na twitter, wametembea ,wanaona mambo, wanasoma...kizazi kipya kina madai yake na si vyema kupuuzwa....wimbi la mageuzi limeshika kasi hata kama tutajaribu kulizuia litakuwa ni suala la muda tu.

Sisi tulipigana vita ya Kagera kuhakikisha Amin hachukui Ardhi yetu, sehemu ndogo tu...sasa kama wazanzibari wanaufananisha muungano na uvamizi au kutawaliwa basi hakuna lugha itakayowapoza mpaka watakapopata wanachokitaka.

Ni wazi wao wanataka ama shirikisho na sio unitary union au wanataka Zanzibar ya asali na maziwa kama unavyoiita.

Nafikiri mpira wameturushia sisi kaka viranja!

Mimi sifahamu kwa nini serikali inakataa mjadala wa wazi juu ya muungano na muundo wake? Muungano huu haujawahi kufanyiwa review, sisi tunauimarisha tu bila ya kujua wananchi wetu wanauonaje, faida na hasara zake.

muungano gani ambao hauna annual report? muungano ambao haujulikani mapato wala matumizi yake?kasoro au kero zipo zinajulikana sasa kwa nini iwe ni kosa kwa watu kutaka mjadala wa wazi wa muungano?

Mimi nazungumzia mjadala wa kitaifa sio kama hivi, mapinduzi, nywele za kimanga, visa za oman...Tanganyika haihitaji maoni.. serikali tatu mzigo...bajeti ya millioni 500.

Watu walio na Muungano fuctional, ambao wanaona faida yake hawalalamiki wala kupiga mayowe bana?

Nimesoma makala aliyoiweka Makaimati,kaimati....
Kama hata Mwanamapinduzi Moyo analalamika basi ameona kuwa mapinduzi yamepinduliwa!! Muungano unachakachuliwa!!!
 
=Nonda;1889565]!
Bora jamaa warudishiwe sovereignty yao
Mkuu ndipo hoja ilipo, wanaweza kufanya bila matusi, kashfa na dharau wakifahamu kuwa muungano umekuwa na faida, kama hakuna haja ni vema kuachana kwa amani. Na suala la kura ya maoni lipo ndani ya uwezo wao na si internet,
kinachowashinda nini?
sasa kuna vijana wa utandawazi, wa internet na twitter, wametembea ,wanaona mambo, wanasoma...kizazi kipya kina madai yake na si vyema kupuuzwa....wimbi la mageuzi limeshika kasi hata kama tutajaribu kulizuia litakuwa ni suala la muda tu.
Hakika kati ya wau waliohoji sana muungano nipo.Hoja yangu ilikuwa ni muungano uangaliwe upya kwani malalamiko yalikuwa pande zote,kama haiwezekani basi uvunjwe kwa amani. Unakumbuka G55 ya jenerali na Njelu kasaka?
sasa kama wazanzibari wanaufananisha muungano na uvamizi au kutawaliwa basi hakuna lugha itakayowapoza mpaka watakapopata wanachokitaka
.
Ndiyo maana tunawashauri wapeleke mswada BLW ili kuanzisha mchakato wa kuvunja muungano, hilo hawataki wanataka serikali ya Tanganyika ili iwepo serikali ya shirikisho. Wanajua kuna faida lakini element za unafiki ndizo zinawachanganya.
Ni wazi wao wanataka ama shirikisho na sio unitary union au wanataka Zanzibar ya asali na maziwa kama unavyoiita.
Shirikisho lishughulikie mambo gani? mbona hakuna anayetuambia yapi yawe ya shirikisho? na watachangia nini?
Nafikiri mpira wameturushia sisi kaka viranja
!
Mpira wanao wao,kwasababu Tanganyika hawahitaji kura ya maoni, wapo tayari kwa lolote, na kura ya maoni labda iwe Ilala dhidi ya Znz kuleta usawa.
Mimi sifahamu kwa nini serikali inakataa mjadala wa wazi juu ya muungano na muundo wake? Muungano huu haujawahi kufanyiwa review, sisi tunauimarisha tu bila ya kujua wananchi wetu wanauonaje, faida na hasara zake.
Ndiyo maana watu wamekataa mswada ulioletwa bila muungano kujadiliwa
Mimi nazungumzia mjadala wa kitaifa,Watu walio na Muungano fuctional, ambao wanaona faida yake hawalalamiki wala kupiga mayowe bana?
Haswaa ilipaswa iwe hivyo, lakini wazanzibar wameshatoa hukumu hata kabla ya mjadala, sasa mjadala utasaidia nini, wao wanasema wameonewa bila kutaja hata chembe ya jema. Hili ndilo linatia hasira tukijua kuwa rasimali za bara na hata upendeleo maalumu umefanyika lakini fadhila zake ni matusi.

Hii mada inanigusa kama mwananchi,namshukuru mungu, nimeishi sehemu nyingi sana duniani. Nimeishi na wznz kwao na hapa bara, ninajua malalamiko ya pande zote na faida zitokanazo.

Tatizo kwa wznz, wengi wanaimba nyimbo, hawajui tungo zake zina maana gani, Hawawezi kujibu maswali rahisi kwasababu wamekaririshwa ujio wa nchi ya ahadi, yenye matunda ya dhahabu, visima vya maziwa, mito ya asali,hewa ya jasmini na sinia za biriani barabarani.
Wamekariri toka kwenye hekaya na ngano za watunzi tofauti na leo hawajui mapinduzi ni halali au haramu.

Znz wafikishe mswada wa kujitenga baada ya pasaka ikiwezekana ili warejea kwao tayari kula matunda ya misaada na visa ya Oman.!!!(ref. mzalendo.)
 
Hapo Zamani kulikuwa kuna Chama kinaitwa ZANZIBAR AND PEMBA PEOPLE'S PARTY (ZPPP). hivi kwani Pemba siyo sehemu ya Zanzibar?, kwa nini hicho chama hakikuitwa ZANZIBAR PEOPLE'S PARTY?.
 
Mkuu ndipo hoja ilipo, wanaweza kufanya bila matusi, kashfa na dharau wakifahamu kuwa muungano umekuwa na faida, kama hakuna haja ni vema kuachana kwa amani. Na suala la kura ya maoni lipo ndani ya uwezo wao na si internet,
kinachowashinda nini?
Hakika kati ya wau waliohoji sana muungano nipo.Hoja yangu ilikuwa ni muungano uangaliwe upya kwani malalamiko yalikuwa pande zote,kama haiwezekani basi uvunjwe kwa amani. Unakumbuka G55 ya jenerali na Njelu kasaka?
.
Ndiyo maana tunawashauri wapeleke mswada BLW ili kuanzisha mchakato wa kuvunja muungano, hilo hawataki wanataka serikali ya Tanganyika ili iwepo serikali ya shirikisho. Wanajua kuna faida lakini element za unafiki ndizo zinawachanganya.

Shirikisho lishughulikie mambo gani? mbona hakuna anayetuambia yapi yawe ya shirikisho? na watachangia nini?
!
Mpira wanao wao,kwasababu Tanganyika hawahitaji kura ya maoni, wapo tayari kwa lolote, na kura ya maoni labda iwe Ilala dhidi ya Znz kuleta usawa.

Ndiyo maana watu wamekataa mswada ulioletwa bila muungano kujadiliwa
Haswaa ilipaswa iwe hivyo, lakini wazanzibar wameshatoa hukumu hata kabla ya mjadala, sasa mjadala utasaidia nini, wao wanasema wameonewa bila kutaja hata chembe ya jema. Hili ndilo linatia hasira tukijua kuwa rasimali za bara na hata upendeleo maalumu umefanyika lakini fadhila zake ni matusi.

Hii mada inanigusa kama mwananchi,namshukuru mungu, nimeishi sehemu nyingi sana duniani. Nimeishi na wznz kwao na hapa bara, ninajua malalamiko ya pande zote na faida zitokanazo.

Tatizo kwa wznz, wengi wanaimba nyimbo, hawajui tungo zake zina maana gani, Hawawezi kujibu maswali rahisi kwasababu wamekaririshwa ujio wa nchi ya ahadi, yenye matunda ya dhahabu, visima vya maziwa, mito ya asali,hewa ya jasmini na sinia za biriani barabarani.
Wamekariri toka kwenye hekaya na ngano za watunzi tofauti na leo hawajui mapinduzi ni halali au haramu.

Znz wafikishe mswada wa kujitenga baada ya pasaka ikiwezekana ili warejea kwao tayari kula matunda ya misaada na visa ya Oman.!!!(ref. mzalendo.)

Mkuu Nguruvi inaonekana unajua mengi kuhusu Zanzibar kuliko Wazanzibari wenyewe.

Iwe faida au hasara Zanzibar hawaukubali mfumo huu wa Muungano uliopo.

Kama kwenu mnaona Zanzibar ni mzigo basi tayari mngeshaachana nayo lakini kwenu una faida kubwa na ndio maana mnaung'ang'ania kwa matumizi ya nguvu za dola.

Kuhusu BLW kupitisha mswada/azimio la kujitoa katika "muungano" huu feki, angalia Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ambayo imewashtua sana. Tukijua kuwa mmetuvamia, tunakwenda polepole na karibu mtajikuta hamna Tanzania wala Tanganyika.

Mtachonga sana mwaka huu lakini Zanzibar hio inawatoka wakoloni wetu.

Zanzibar for Zanzibaris.
 
Mzizimkavu nje ya muungano kuna "Sisi Wapemba wao waungunja" hakuna Zanzibar...Muungano ndo unafanya kuwepo na Zanzibar...
 
Kuna watu wanadai Tanganyika imehodhi jina la Tanzania, lakini watu hao hao hawajiulizi Zanzibar ambalo ni jina jingine la Unguja kuhodhi jina la nchi nzima ya "zanzibar and Pemba".
Labda Wazanzibari watueleze kwa nini nchi yao inaitwa "THE REPUBLIC OF ZANZIBAR AND PEMBA"
 
Mzizimkavu nje ya muungano kuna "Sisi Wapemba wao waungunja" hakuna Zanzibar...Muungano ndo unafanya kuwepo na Zanzibar...

Kwani kilichokuja mwanzo nini Horseshoe? Ni Zanzibar au Tanzania?

Zanzibar ilikuwapo kabla ya Tanganyika na mkaleta fitna zenu mkatufisidi.

Wewe na wenzako wenye mawazo kama yako, mmeijua Tanzania tu, hamkuijua Tanganyika wala Zanzzbar kabla ya kutuvamia.

Wewe ulie tu, Zanzibar bila ya Tanzania inawezekana, jee Tanzania bila Zanzibar?

Keep watching this page mdau, Zanzibar for Zanzibaris.
 
Hapo Zamani kulikuwa kuna Chama kinaitwa ZANZIBAR AND PEMBA PEOPLE'S PARTY (ZPPP). hivi kwani Pemba siyo sehemu ya Zanzibar?, kwa nini hicho chama hakikuitwa ZANZIBAR PEOPLE'S PARTY?.

Si kazi yako na hayakuhusu hayo.

Zanzibar for Zanzibaris.
 
Makaimati, dhambi ya ubaguzi haitaishia hapo...baada ya kujitenga hamtaishia hapo,mtakuja na sisi wapemba na wao waunguja! Then Mimi wa kusini Unguja,mimi wa mji mkongwe na mwishoni utakua umesimama mwenyewe!...sijasema muungano uendelee kuwepo na sijasema pia uvunjike!...
 
Dah, napata taabu kidogo kujadili, nahisi kama nimeingia mzalendo.net.
Anyway, hivi jina lina uhusiano gani kiuchumi,kisiasa au kiutamaduni. Kwamfano Tanganyika ikibadili jina na kuwa Tanga then so what.
Burma wanajiita jina jipya inawasaidiaje. Hata sasa hivi Tanzania ni Tanganyika kwasababu Zanzibar haijiiti Tanzania ikiwa ni pamoja na ninyi wachangiaji.

Tafadhali kama huna hoja za kufikirisha, rejea mzalendo.net kwasababu JF inakuwa level ya juu kidogo. Usishushe hadhi ya mjadala kwa hoja rojo rojo. Please

Serikali tatu zishughulikie nini? ni mambo gani unadhani seriakali ya shirikisho inapaswa kuyashughulikia, fafanua kwasababu neno tatu halijatusaidia kukuelewa.

My take: Post zilizopita nimewahi kusema wazanzibar wanataka Tanganyika irudi ili wajenge hoja kuwa tuwe na shirikisho tofauti na unafiki wa kusema eti wanataka Tangnayika kwani ndiyo inawashikilia. Sasa wanakuja na siri tuliyoijua mapema.
Tanganyika haihitaji maoni, mzigo wa muungano upo kwa Wznz, kuamua kunyoa au kusuka.
Serikali tatu hapana hadi watakaposema mambo gani yawe ya seriakali tatu kwanza.
Serikali tatu ni kubebesha mzigo bara kwasababu wao watachangia nini kwa bajeti ya bilioni 500.
Serikali tatu maana yake kuwasaidia kwa yale wanayonufaika ndani ya muungano.

Kura ya maoni ndiyo itaamua hatma ya nchi ya matunda, asali na maziwa Zanzibar.

Kitaba ya Muungano iliyopa sasa inazuwia chama chochote cha siasa kuupinga Muungano...Chama kinapokua na sera ya kujitoa katika Muungano, inabidi hicho chama kitafungiwa au hakitasajiliwa kuwa chama cha siasa. Kwahiyo, vyama vinalazimishwa kukubali Muungano hata kama raia hawautaki.

Madai ya kuwa na serikali tatu ni kurudishia kila upande wa Muungano mamlaka yake. Mambo ya muungano yalikua 11 tu, sasa yanakaribia 40...Haya mambo ya Muungano yanatakiwa yapunguzwe ili kuondoa huu mzigo ambao nyinyi wa Tanganyika mnasema mnabebeshwa. Mambo haya yanaweza yakawa katika vyomba vya ulinzi na usalama tu...

Raia wa Zanzibar,wako tayari kuwa bila ya Muungano lakini mfumo uliyopo sasa wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano haitoi "option" yeyote ya kuzungumza uvunjaji wa Muungano...Kwa maana hiyo, kama huu Muungano lazima uwepo!!! basi uwe wa serikali tatu. Lakini kuendelea kama hali ilivyo sasa hicho hakita vumilika tena.

Muungano hivi sasa unalazimishwa na CCM Tanganyika ,kwasababu hapa ndio sera na agenda na mikakati inapotokea, vile vlie wana kauli zao za kuenzi sera za yule mzee wenu (dikteta) Nyerere. Kumbuka kama rasimu ya katiba mpya inakataza kujadili Muungano. Kwanini? Sababu hazijulikani, na hii ndio uliozusha vurugu Zanzibar wakati wa mjadala.

Kila siku tunasema Kuna kero za Muungano, lakini mnazuwia zisijadiliwe...Sasa tuwaelewe vipi? Kama huu si ukoloni ni kitu gani? Au unataka kunambia kami hii ndio Demokrasia ambayo wewe unaikubali? Siasa za ukandamizaji zimeshapitwa na wakati dunia ya leo siyo ile ya Nyerere.
HIZI SIO ZAMA ZA NYERERE... MPAKA KIELEWEKE....
 
Mtoto akililia wembe mpatie acheze nao halafu umkate,gari kama engine inasumbua dawa ni kuishusha chini na ku overhaul pia unaweza
kununua engine mpya ukaweka mambo yakasonga mbele vizuri zaidi nasi Muungano wetu napendekeza uvunjwe halafu tuzungumze upya kila nchi ikiwa huru zaidi naamini baada ya hapo tutahashimiana.
 
Makaimati, dhambi ya ubaguzi haitaishia hapo...baada ya kujitenga hamtaishia hapo,mtakuja na sisi wapemba na wao waunguja! Then Mimi wa kusini Unguja,mimi wa mji mkongwe na mwishoni utakua umesimama mwenyewe!...sijasema muungano uendelee kuwepo na sijasema pia uvunjike!...

Horseshoe hizo zilikuwa ni fitna za Nyerere alipomlaghai Karume na hali imebadilika sana,

*"Ule wakati wetu na Nyerere tulikuwa tunakubali lakini hawa vijana wa leo hawakubali, Bw. Sitta, ITS OVER*". - Hassan Nassor Moyo, former SMZ/SMT Minister and ASP/CCM Veteran

Na hata Nyerere ulifika wakati na kumwambia Dr. Omar (late SMT VP),

"Viongozi wetu hawana la maana kuwaeleza wananchi wao, isipokuwa Hizbu,imefanya hili na Sultani alikuwa akifanya lile na lile.Jee, jamani vijana wetu tuliokuwa nao, hivi sasa ni nani anaeijuwa Hizbu ni nani anaemjuwa Sultani? Hivi kweli hamna zaidi ya haya kuwaeleza wananchi?"

Hivyo msijidanganye sana, kwani kwenye masuala ya UTAIFA hakuna Upemba na Uunguja wala U CCM au U CUF

ZANZIBAR FOR ZANZIBARIS

Mtoto akililia wembe mpatie acheze nao halafu umkate,gari kama engine inasumbua dawa ni kuishusha chini na ku overhaul pia unaweza
kununua engine mpya ukaweka mambo yakasonga mbele vizuri zaidi nasi Muungano wetu napendekeza uvunjwe halafu tuzungumze upya kila nchi ikiwa huru zaidi naamini baada ya hapo tutahashimiana.

Hatulilii kitu bali tunadai haki yetu ilioporwa Mkuu BENTA
 
Mi naona wanataka zanzibar ile ya ki-al shabaab zaidi
 
Yaani zanzibar ya ki-oic na ile ya kimahakama ya kadhi.......................
 
Yaani zanzibar ya ki-oic na ile ya kimahakama ya kadhi.......................

Hayo mtajua wenyewe wala haituhusu, sisi tunataka Zanzibar yetu ambayo tutaweza kujiamulia mambo yetu.

Mahkama za Kadhi zipo Zanzibar toka dahari na imo ndani ya Katiba yetu.

OIC ni fitna zenu maana hata Msumbiji ni member.

Huo uhasidi na uchoyo wenu kwa Zanzibar ndio iliotufikisha hapa tulipo.

"If I could tow that island out into the middle of Indian Ocean, Id' do it." - JK Nyerere.
 
Wanaitaka nchi "yao" ya Zanzibar; Wanataka kurudia "utukufu wa Zanzibar" kwa kuwa hapa walipo sasa hawaoni manufaa "yoyote" kwa Zanzibar. Wanasema wanaitaka nchi yao waliyonyang'anywa na Wadanganyika (ati Watanganyika). Wanataka warudishiwe nchi yao waliyonyang'anywa na Nyerere na watu wa bara.

Ni Zanzibar ipi hiyo wanayoitaka?

  • Zanzibar ya historia ya kale (Zenj - nchi ya weusi?) ambayo ni zaidi ya visiwa vya Unguja na Pemba bali na mwambao wa Afrika ya Mashariki
  • Zanzibar ya Sultani(ambaye naye utawala wake ulizidi mipaka ya Unguja na Pemba)
  • Zanzibar ya Sultani chini ya Mwingereza
  • Zanzibar ya baada ya Uhuru na Sultani akiwa bado ni Mkuu wa Nchi na serikali ya Mseto
  • Zanzibar ya Mapinduzi kabla ya Muungano
  • Zanzibar "mpya" ambayo haijawahi kuwepo yaani ya baada ya muungano

Ni ipi hasa wanayoitaka? Ni ipi hasa Zanzibar "proper". Isije kuwa ni kama nchi ya ahadi ambayo iko katika fikra za watu tu lakini haijawahi kuwepo; yaani ile nchi imiminikayo maziwa na asali na kwamba watu wa bara na dunia nzima wanataka kuwanyang'anya Wazanzibari. Na labda hapa itabidi tulijibu swali pia kuwa Mzanzibari ni nani hasa?

Haya masuali ya ki-kejeli na majibu yake hufuata mkondo huo huo. Maana mtu anakupora nyumba yako halafu anakuuliza kwanini unadai nyumba yako...Baadae mnalaumu , oh...mbona unajibu kwa hasira, oh mbona matusi, oh punguzeni jazba.

Heshima kitu cha bure mkuu...jeheshimu kabla huja heshimiwa....Zanzibar mliyo ikuta kabla Muungano ndio hiyo inatakiwa irudishwe...period
 
Mie nadhani Zanzibar inafahamika kweli kweli. Majibu yako hata TRA. Wao wanatoza ushuru wa Zanzibar kizanzibar na bidhaa hiyo ikitokea kule Zanzibar kuja Dar es Salaam hutozwa tena ushuru mwingine. Ukiwauliza mbona mnatoza ushuru mara mbili mbili husema hizi ni nchi mbili tofauti kijiografia. TRA wanaijua Zanzibar hiyo ingawa inaweza kuwa tofauti na ile iliyotajwa katika katiba ya Zanzibar na ile ya muungano
 
Hayo mtajua wenyewe wala haituhusu, sisi tunataka Zanzibar yetu ambayo tutaweza kujiamulia mambo yetu.

Mahkama za Kadhi zipo Zanzibar toka dahari na imo ndani ya Katiba yetu.

OIC ni fitna zenu maana hata Msumbiji ni member.

Huo uhasidi na uchoyo wenu kwa Zanzibar ndio iliotufikisha hapa tulipo.

"If I could tow that island out into the middle of Indian Ocean, Id' do it." - JK Nyerere.
Kwa hiyo? kwa nini msifanye maandamano mbaki na nchi yenu mfe njaa
 
wazenj wanataka nchi yenye uhuru zaidi, wanataka mipaka yao itambulike rasmi, wanataka maendeleo yao bila kupitia upande wa pili
Wasiongee ongee tu wafanye kwa vitendo tangu wameanza kulalamika ni lini tulisikia kundi fulani limeanzisha hoja hii ili kushinikiza viongozi wao waombe huo uhuru?
 
Back
Top Bottom