Makaimati
JF-Expert Member
- Apr 4, 2011
- 462
- 87
yeah right hata historia ya Zanzibar mnataka tusahau! Hii Zanzibar ya pepo hiyo iliwahi kuwepo lini? Matatizo ya Kiuchumi, Kisiasa na Maendeleo ni nchi gani ambayo haina? Wengine tuliaminishwa kuwa nchi zote za Kiarabu ni pepo, maskini kina Khalid wametuonesha ile siri kuu. Tunaambiwa Oman ni pepo.. juzi tunaoneshwa kuwa ipo Pepo ya Wachache. Na hivi ndivyo mnavyotaka watu waamini kuwa Zanzibar ilikuwa Pepo kwa kila mtu, kumbe ilikuwa Pepo ya Wachache.
Kweli mnafikiri mkiwa nje ya Muungano ndio matatizo ya Kiuchumi, Kisiasa na Maendeleo yataondolewa? Really? SAudia na mafuta yake yote hayo imeweza vipi kuondoa matatizo yote ya Kijamii? Hata Libya, Iran, na Iraq zote ukiziangalia kwenye kipimo cha maendeleo zinaoneshwa ziko juu ya Tanzania lakini leo tunajua kuwa siyo vyote vinavyomeremeta dhahabu. Jamani msiwaadahe watu kuwa ati Zanzibar ikiwa nje ya Muungano basi pepo itarudi. Msije kujikuta mnabakia kuimbiana taarab za nyimbo za "iliyokuwa Zanzibar" huku watu wanatamani pepo isiyokuwepo.
Ushirikiano wetu unatuhakikishia sote na miye napendekeza zaidi Zanzibar a brighter future kuliko watu wanavyodanganyana.
Mkuu Mwanakijiji sijui wapi hayo ya pepo yameelezwa humu lakini wanachosema Wazanzibari, wanataka self determination na sio jengine. Hayo matatizo ya Zanzibar na Wazanzibari tangu lini kwenu kuwa ni issue?
Lugha hizi zenu ni vile tu mmenogewa na utamu wa kutawala na sio jengine. Kama sisi tuna matatizo na mzigo, si mtuache tu, ya nini kutung'ang'ania? Kwanini msiungane na Congo?
Ya Wazanzibari waachieni wenyewe watajua la kufanya.