Ni Zanzibar ipi wanaitaka?

Ni Zanzibar ipi wanaitaka?

Wasiongee ongee tu wafanye kwa vitendo tangu wameanza kulalamika ni lini tulisikia kundi fulani limeanzisha hoja hii ili kushinikiza viongozi wao waombe huo uhuru?

Sio muda mrefu...Madanguro yote tutapiga moto...sijui kibarua utafanya wapi?
 
Nadhani watanzania tulio wengi hatujawaelewa wazanzibari wanachotaka.
Ni hivi, wanataka haki yao kama nchi itambuliwe nadani ya muungano ikishindikana wanataka nchi yao ijitenge.
Wanataka watambue wao kama wazenj wameungana na nchi gani? maana wanachosikia ni Muungano wa Tanzania hawamsikii mshirika wao Tanganyika ndo wanataka wamsikie wakae wajadiliane nae namna ya kusongesha mbele muungano uliopo,
Wanataka rasirimali za nchi yao zisiingiliwe na nchi nyingine, wao kama nchi wanataka kuwe na nchi ya Tanganyika inayotambua mipaka yake ndo waunganishe na yao ( kumbuka wao mipaka ya nchi yao inatambulika kwenye katiba yao)
Wanataka kuwe na serikali tatu, ya TANGANYIKA, YA ZANZIBAR NA YA MUUNGANO.
Sasa hivi utasikia wabara na wazanzibar, kuna nchi ya bara? ipi? wengine wanaona hata aibu kutamka kuwa ni watanganyika wanasema wabara
Mimi nawaelewa na nina waunga mkono ila nawapongeza sana kutusaidia wabara kudai nchi yetu tanganyika
 
Muulize yule mzee wenu ( dikteta) Nyerere kakopa hela mara ngapi kwa Karume ?

avatar14880_1.gif
badilisha avator
 
Hawajui walitakalo, wao ni kupiga makelele tu kwamba wanaonewa............ wanadhurumiwa............ wananyanyaswa................. WAKIACHWA PEKE YAO HAO WATAKUFA KWA KUKOSA UMEME............


Mkuu Ngalikihinja,

Nadhani sasa unatukosea adabu maana Zanzibar ipi Wazanzibari wanaitaka, imeshaelezwa sana humu na wachangiaji kibao, hususan, mwenzenu Takashi ambae amekuwa akijibu kila hoja zenu potofu na za uchokozi.

Mara mnakuja na paspoti, mara mnakuja na ya kuudai sijui ukanda gani almuradi kuivuruga hoja mliokuja nayo wenyewe mkidhani Wazanzibari mtawababaisha.

Mnauliza Zanzibar ipi Wazanzibari wanaitaka? Kwani nyinyi mliikuta ipi mkaichakachua? Hio ndio Wazanzibari wanayoitaka.

Mnasema tutakufa kwa kukosa umeme, mnajua Zanzibar imekuwa na umeme tangu lini?

Mmekosa hoja za maana na sasa mnakuja na pumba.

Sichoki kuwakumbusha kuwa iko siku mtakuja kuamka hamna Tanganyika mlioiua wenyewe wala Tanzania mlioilleta ili kuifuta Zanzibar.

Madhal Zanzibar mliikuta basi mjue mtaiwacha.

Zanzibar itakuwepo bila ya Tanzania, Tanzania jee?
 
Baada ya mjadala kuvurugwa kwa hoja za madanguro kutoka kwa wenzetu waliokosa uvumilivu au ustaarabu, leo nimepita katika gazeti moja na kukuta habari ifuatayo ambayo inaunga mkono hoja niliyowahi kutoa. Inaunga mkono kwasababu imetolewa na mwana mapinduzi ambyae indirectly amikiri faida ya muungano. Soma.

Elias Msuya
MUASISI wa Mapinduzi ya Zanzibar, Hassan Nassoro Moyo, ameitaka serikali kuruhusu wananchi kujadili muundo wa muungano, ili waamue mustakabali wake.
Akizungumza kwenye mahojiano maalum nyumbani kwake jana, Fuoni Zanzibar, Moyo alionyesha kushangazwa na Muswada wa Marejeo ya Katiba ulioondolewa Bungeni hivi karibuni, akisema serikali inawabana wananchi kujadili mambo muhimu ya nchi yao.
Moyo anasema hayo wakati muungano huo ukiwa unatimiza miaka 47, huku kukiwa na malalamiko mengi yanayodhihirisha watu kutoridhishwa na muundo wake.
"Naunga mkono vijana wanaohoji muungano, muungano ni wao, sisi muda wetu umekwisha, wananchi wana haki ya kuhoji uhalali wa muungano," alisema Moyo.
Alionyesha kuguswa na ibara ya 9(2) ya muswada wa marejeo ya Katiba, inayokataza wananchi kuondoa mambo muhimu kama muungano, urais, uwapo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na mengineyo na kwamba, wananchi wasizuiwe kujadili mambo hayo.
Moyo, alikuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano katika Serikali ya Abeid Amani Karume mwaka 1964 na baadaye Waziri wa Sheria SMZ.
"Kwa sasa serikali inafanya jitihada za kurekebisha Katiba, pia muungano utaangaliwa. Lakini sasa wamezuia mambo muhimu kuzungumziwa," alisema Moyo na kuhoji:
"Kwanini uazuie watu kujadili muungano, kwanini wanasiasa wasishiriki kwenye mchakato wa Katiba? Nyerere hakuwa Askofu wala Karume hakuwa Mufti, wote walikuwa wanasiasa na ndio waliounda muungano, kwanini wanasiasa wa leo wasiruhusiwe?"
Alisema huu ni wakati wa wananchi kujadili muungano, kutoa mawazo yao na kwamba, muungano wa wakati ule ulikuwa ni wao na marehemu Karume, kizazi cha sasa kinataka kujua na kiachwe kiseme kinachokitaka.
Kuhusu mkataba wa Muungano, Moyo alisema awali ulikuwa na mambo 11, lakini yakaongezwa hadi kufikia 22, huku yote yakiwa yameingizwa na upande wa bara.
Akigusia kuondolewa madarakani aliyekuwa Rais wa SMZ, Aboud Jumbe mwaka 1983, alisema kilichomponza ni kutaka serikali tatu bila kushirikisha wenzake kwenyea Baraza la Mapinduzi.
"Mambo ya muungano yalikuwa 11, lakini yakaongezeka kufikia 22, juzi kwenye kongamano nimeambia kuwa yamefika 32 sasa na yote mmeyaleta ninyi wabara. Moja tu lililetwa na Mzanzibari na akafukuzwa kazi. Alikuwa Jumbe alipofasili mojawapo ya kifungu cha muungano," alisema na kuongeza:
"He was not wrong (Hakukosea), tatizo lake hakulishirikisha Baraza la Mapinduzi ili limtetee kwenye vikao."
Kuhusu mgawanyo rasilimali, Moyo alisema mkataba wa awali haukuzungumzia ushirikiano wa rasilimali, kama vile mafuta kuwa chini ya muungano, bali yaliwekwa na Bunge.
Pia, Moyo alisikitishwa na kitendo cha Serikali ya Muungano kulipisha kodi bidhaa zitokazo Zanzibar, akisema kimeua biashara visiwani humo

My Take
Suala la kujadili muungano kama lilivyowasilishwa katika muswada limepingwa na pande zote na wananchi wametaka kila kitu kijadiliwe bila masharti, hili si la Znz bali wote, tofauti ni kuwa huku bara limepingwa kwa hoja na Visiwani oops! Znz limehusisha tafrani na jazba.

Kilichomuondoa jumbe ni hicho cha serikali tatu, lakini Moyo ni mnafiki akisema baraza la mapinduzi halikushirikishwa! Si kweli, Jumbe nje ya madaraka amekaririwa akisema alisalitiwa na wenzake ndani ya baraza. Yeye kama kiongozi alikuwa anaongoza move, wenzake akiwemo Moyo wakamsaliti alipoitwa kuhojiwa. Kwa hasira za usaliti hajashiriki shughuli za baraza la mapinduzi na amesema hataki heshima siku mwenyezi akiamua vinginevyo.
Aliyevujisha habari za move ya Jumbe ni Mroho mmoja ambaye leo yupo madarakani.
Cha kushangaza ni huyu huyu msaliti ndiye amekuwa anapita duniani kusema muungano unawaonea Wznz. Nia yake ni kuwa rais na kukidhi haja yake na si muungano au serikali tatu kama alivyotaka Mzee Jumbe.
N.Moyo na msaliti mwenzie wote walimsaliti mzee Jumbe, asitake kusingizia kitu kingine.
Nassoro Moyo na Mzee Thabiiti Kombo Jecha wote walikuwa maswahiba wa Nyerere leo ushujaa wa kuongelea ubovu wa muungano anautoa wapi, aache kizazi kiamue bila kuingiza fitna akijua fika kilichotokea akiwa kiongozi.

Kuhusu rasilimali sijui kama mzee anajua maana yake halisi au anataka kujenga hoja kwa kutufanya mazuzu. Ujumbe anaotaka kuusema hapa ni kuwa mafuta kama yapo si ya muungano, lakini hajasema resource nyingine kwa kujua huenda zikaigusa Znz. Kama mafuta ni ya wznz ni haki yao lakini wawe wakweli na kwa rasilimali zingine pia.
Mkondo wa umeme kwenda ZNZ umegharamiwa kwa msaada na mkopo ambao Mtanganyika ameulipia bila manufaa,znz inapopata umeme rahisi na bila mgao ukilinganisha na mkazi wa kidatu wapi iliandikwa katika mambo 11 au 22 au 32. Angesema kama hayo mafuta yapo ni ya znz, period! asilete hoja kwa unafiki.

Mwisho, amekubali kuwa kuweka kodi tu kumeua biashara znz. Nimeeleza huko nyuma kuwa kwa vyovyote iwavyo Tanganyika ina impact kubwa sana katika uchumi wa ZNZ nikashambuliwa kwa kejeli na kashfa, sasa nauliza kama Tanganyika inaweka kodi kwanini wasifanye biashara na mauritius, Kenya, Uganda ili kukwepa kodi za bara kama wachangiaji wengi walivyosema huko nyuma.

Kama Nassoro Moyo amekubali hili basi namshukuru sana kwa kunitetea kuwa uchumi wa Znz based on the geo- position, social and cultural interaction una uhusiano mkubwa sana na Tanganyika na kwamba hata ikijitenga leo hilo halita epukika, ambaye anakataa ukweli huu asinijibu mimi amjibu Mzee Moyo, mwanampainduzi, waziri, na kiongozi.
 
Nguruvi3

Mkuu bado hajukua tayari kuwa mkweli , bado ile dhana ya kiutawala bado unayo. Kama nimekuelewa vizuri wewe hujali kiasi gani Muungano umeibana Zanzibar. Na bado unashangaa kwanini kelele nyingi zanatoka Zanzibar na sio Tanganyika? Mimi sio mwana sheria wala mwana siasa kwahiyo nitashindwa kukupa hivyo vipengele . mimi nitakua brief tu, WAZANZIBARI WAMESHACHOKA NA HUU MUUNGANO JINSI ULIVYO, SASA WAZO LAO UWE WA SERIKALI TATU AU TUUVUNJE KABISA...JEE WEWE KAMA MTANGANYIKA UNATAKA MUUNGANO GANI ,AU IWE VIPI ? nadhani uliangalia hapo nyuma niliandika ugumu wa kuvunja Muungano kisiasa, kwahiyo watu wanajitayarisha kutafuta njia nyengine. Kuhusu ,umeme,mji nitarudi tena. Ila wakati umefika sio tena ujanja ujanja .
 
Nyie mnaojifanya wazanzibari bure kabisa, kama mnataka zanzibar yenu do sumting bout that, cyo kukaa mnalalamika..binafsi mi natamani huu muungano ufe mrudi kwenu tuu, afu ndo mjue umuhimu wa muungano. kwanza mmejaa ubaguzi tuu hamna lolote...mngejua ni kiasi gani zanzibar inafaidika na muungano msingeongea pumba. ZINDUKENI
 
Nyie mnaojifanya wazanzibari bure kabisa, kama mnataka zanzibar yenu do sumting bout that, cyo kukaa mnalalamika..binafsi mi natamani huu muungano ufe mrudi kwenu tuu, afu ndo mjue umuhimu wa muungano. kwanza mmejaa ubaguzi tuu hamna lolote...mngejua ni kiasi gani zanzibar inafaidika na muungano msingeongea pumba. ZINDUKENI

Bora kuwa masikini kuliko kupoteza mamlaka yako...
 
Nyie mnaojifanya wazanzibari bure kabisa, kama mnataka zanzibar yenu do sumting bout that, cyo kukaa mnalalamika..binafsi mi natamani huu muungano ufe mrudi kwenu tuu, afu ndo mjue umuhimu wa muungano. kwanza mmejaa ubaguzi tuu hamna lolote...mngejua ni kiasi gani zanzibar inafaidika na muungano msingeongea pumba. ZINDUKENI

Mnaofaidika ni nyinyi mnaoung'ang'ania na kudai mtaulinda kwa hali yoyote.

Zanzibar ilikuja mwanzo kabla ya Tanzania, na ni nyinyi iko siku hamtakuwa na Tanganyika wala Tanzania
 
Dunia inashangaza tena sana Mzee Mwanakijiji, tunaomba waje hao wahafidhina wa Zanzibar waje hapa jamvini watwambie Zanzibar ipi wanaitaka?
 
Waje wazanzibar hapa jamvini watwambie Zanzibar ipi wanaitaka? wahafidhina wa zanzibar karibuni jamvini jibuni hoja ya Mzee Mwanakijiji
 
Hawajui walitakalo, wao ni kupiga makelele tu kwamba wanaonewa............ wanadhurumiwa............ wananyanyaswa................. WAKIACHWA PEKE YAO HAO WATAKUFA KWA KUKOSA UMEME............


Zanzibar imekuwa na umeme wakati London wanawasha gas lamps.
 
wanaitaka iwe kama nchi huru isiwe na mchanganyiko na wabara na hata serikali yao wanataka ijitegemee labda hapa mie niongezee kisub question hivi mfano muungano ukavunjika na zanzibar ikawa taifa linalojitegemea wanaweza kua na maendeleo kuipita bara?
 
Back
Top Bottom