Ni wizara gani ungependa mawaziri wake wasiwe wanakaa kwa muda mrefu kwenye hiyo wizara?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,333
8,252
Ni dhahiri zipo baadhi ya wizara zipo very delicate kiasi kwamba waziri akiyumba kidogo tu watanzania wote wanapoteana.

Hivi sasa zipo wizara zinalalamikiwa kila siku sio mtaani, wala bungeni, wala mtandaoni, pengine hata kwenye mikutano ya vyama.

Kutokana na kuyumba kwa maamuzi ya wizara basi taifa zima limepoteana.

Sasa basi kwenye wizara kama hizo inapaswa waziri anapoyumba anabadilishwa kwa haraka ili kupunguza makali ya athari zinazoweza kutokea endapo akiendelea kusalia hapo. Muda mwingine anahamishiwa katika wizara nyingine huyu wa wizara nyingine analetwa hapa.

Sio jambo baya kuwabadilishia majukumu mawaziri ambao wizara fulani zimewazidi. Muda mwingine wanaweza wakawa wanajua kuwa hapa wamekosea lakini wakaendelea kujiamini kuwa hizo wizara wanaziweza.

Mara nyingi watanzania huwa hatukubali kushindwa lakini kuna vitu ni bora kukubali, tuwe kama madereva au marubani tukubali kuachia wengine wizara ili tusisababishe ajali kubwa zaidi. Dereva bora au rubani bora anasifa moja, anapoona amechoka na hawezi kuendesha tena huwa anakubali kumwachia dereva au rubani mwingine.

Sasa nije kwenye swali la msingi; Je ni wizara gani ungependa mawaziri wake wasiwe wanakaa kwa muda mrefu kwenye hiyo wizara?
 
Ni dhahiri zipo baadhi ya wizara zipo very delicate kiasi kwamba waziri akiyumba kidogo tu watanzania wote wanapoteana.

Hivi sasa zipo wizara zinalalamikiwa kila siku sio mtaani wala bungeni pengine hata kwenye mikutano ya vyama.

Kutokana na kuyumba kwa maamuzi ya wizara basi taifa zima limepoteana.

Sasa basi kwenye wizara kama hizo inapaswa waziri anapoyumba anabadilishwa kwa haraka ili kupunguza makali ya athari zinazoweza kutokea endapo akiendelea kusalia hapo. Muda mwingine anahamishiwa katika wizara nyingine huyu wa wizara nyingine analetwa hapa.

Sasa nije kwenye swali la msingi; Je ni wizara gani ungependa mawaziri wake wasiwe wanakaa kwa muda mrefu kwenye hiyo wizara?
Wizara ya fedha

USSR
 
Back
Top Bottom