Ni wazi Hakimu Michael Mteite na Thomas Simba walitoa hukumu zenye utata dhidi ya Sugu na akina Mbowe

Mwezi Februari mwaka 2018 Hakimu Michael Mteite wa Mbeya alimukumu Mbunge Joseph Mbilinyi (CHADEMA) miezi 5 jela kwa kosa la kumkashifu Rais wa Tanzania.

Hukumu hiyo ilitenguliwa mnamo April 2018 na JAJI UTAMWA wa Mahakama Kuu Kanda ya Mneya baada ya Sugu kuwasikisha ombi la rufaa.

Mnamo Machi 2020 Hakimu Thomas Simba wa Mahakama ya Kisutu aliwahukumu kifungo cha miezi 5 au faini ya Tsh 350 Milion Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake kwa makosa ya kufanya maandamano haramu yaliyopelekea kifo cha Akwilina Akwelin aliyekuwa mwanafunzi wa NIT.

Leo 25/ 06/ 21, JAJI wa Mahakama Kuu Irvin Mheta ametengua maamuzi ya Hakimu Simba na kuamuru washitakiwa warudishiwe kiasi hicho cha fedha.

Ni wazi hizo kesi huenda zilikuwa na shinikizo la kisiasa kutoka kwa Mwendazake au Mahakimu walifanya maamuzi hayo kumfurahisha Mwendazake ili awape promotion ya UJAJI.

Nini itakuwa hatima ya Mteite na Simba kwenye maisha yao uraiani baada ya kustaafu?
Mbona unawatisha Mahakimu, kwani kesi hizo ndo za kwanza kutenguliwa na Mahakama za juu? Ni jamii gani hiyo unayosema watakaa nayo vipi? Kwani hizo kesi zilikuwa na uhusiano na jamii au ni uendawazimu wa hao akina Sugu wakishavuta mibangi yao. Chadema hamna maana kabisa
 
Alipewa rushwa ya ujaji baada ya hukumu ile.Ndipo tuliposhuhudia wimbi la mahakimu wakishindana kuwafunga na kuwanyima Dhamana wapinzani Ili wapate teuzi
 
Mbona Hakimu Thomas Simba umri wa kustaafu ulitimia mwaka 2019!! Aliongezewa miaka 2 kama shukrani kwa kuishughulikia CDM.

Halafu aliahidiwa kupata UJAJI na Mwendazake bahati mbaya Magufuli ametema ndowano kabla hajmpa Ujaji aliomuahidi
Wote walipewa ujaji kama shukrani ya kuishughulikia chadema hata baada ya kustaafu.
 
Mwezi Februari mwaka 2018 Hakimu Michael Mteite wa Mbeya alimukumu Mbunge Joseph Mbilinyi (CHADEMA) miezi 5 jela kwa kosa la kumkashifu Rais wa Tanzania.

Hukumu hiyo ilitenguliwa mnamo April 2018 na JAJI UTAMWA wa Mahakama Kuu Kanda ya Mneya baada ya Sugu kuwasikisha ombi la rufaa.

Mnamo Machi 2020 Hakimu Thomas Simba wa Mahakama ya Kisutu aliwahukumu kifungo cha miezi 5 au faini ya Tsh 350 Milion Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake kwa makosa ya kufanya maandamano haramu yaliyopelekea kifo cha Akwilina Akwelin aliyekuwa mwanafunzi wa NIT.

Leo 25/ 06/ 21, JAJI wa Mahakama Kuu Irvin Mheta ametengua maamuzi ya Hakimu Simba na kuamuru washitakiwa warudishiwe kiasi hicho cha fedha.

Ni wazi hizo kesi huenda zilikuwa na shinikizo la kisiasa kutoka kwa Mwendazake au Mahakimu walifanya maamuzi hayo kumfurahisha Mwendazake ili awape promotion ya UJAJI.

Nini itakuwa hatima ya Mteite na Simba kwenye maisha yao uraiani baada ya kustaafu?
Katiba mpya kwa ajili ya mahakama huru.
 
Back
Top Bottom