Ni wazi Hakimu Michael Mteite na Thomas Simba walitoa hukumu zenye utata dhidi ya Sugu na akina Mbowe

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
10,228
17,440
Mwezi Februari mwaka 2018 Hakimu Michael Mteite wa Mbeya alimukumu Mbunge Joseph Mbilinyi (CHADEMA) miezi 5 jela kwa kosa la kumkashifu Rais wa Tanzania.

Hukumu hiyo ilitenguliwa mnamo April 2018 na JAJI UTAMWA wa Mahakama Kuu Kanda ya Mneya baada ya Sugu kuwasikisha ombi la rufaa.

Mnamo Machi 2020 Hakimu Thomas Simba wa Mahakama ya Kisutu aliwahukumu kifungo cha miezi 5 au faini ya Tsh 350 Milion Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake kwa makosa ya kufanya maandamano haramu yaliyopelekea kifo cha Akwilina Akwelin aliyekuwa mwanafunzi wa NIT.

Leo 25/ 06/ 21, JAJI wa Mahakama Kuu Irvin Mheta ametengua maamuzi ya Hakimu Simba na kuamuru washitakiwa warudishiwe kiasi hicho cha fedha.

Ni wazi hizo kesi huenda zilikuwa na shinikizo la kisiasa kutoka kwa Mwendazake au Mahakimu walifanya maamuzi hayo kumfurahisha Mwendazake ili awape promotion ya UJAJI.

Nini itakuwa hatima ya Mteite na Simba kwenye maisha yao uraiani baada ya kustaafu?
 
Umesema sugu hukumu yake ilitenguliwa 2018, Kama Magufuli alikuwa anashawihi hukumu ikawaje sugu hukumu yake ikatenguliwa?
Soma tena thread yangu nimesema inawezekana Hakimu alikuwa anafanya vile kujikomba ili apate promotion
 
... watu ambao hadi leo hawaamini jamaa kafa kweli ni kupoteza muda kuwaelimisha ubaya wa mwendazake wakaelewa. Sitashangaa kusikia wanahangaika kwa "wataalamu" kujua kama kafa kweli au "watu wabaya".
Hiyo ndiyo asili yao kukesha kwa vigagura
 
Umesema sugu hukumu yake ilitenguliwa 2018, Kama Magufuli alikuwa anashawihi hukumu ikawaje sugu hukumu yake ikatenguliwa?
Unataka kusema nn sasa? Kama huamini alicholisema kwanini huyo hakimu alikuja kiwa rewarded na u jaji?
Hata hilo unataka kumtetea yule punguani mwendazake?
 
Kumbe hata Michael Mteite ni Jaji? Hiyo ni RUSHWA ya level ya Rais anayoweza kutoa ili kumu CORRUPT Hakimu
 
Turudi hapa tena. Kesi Ugaidi inayomhusu Freeman Mbowe iko mbele ya Thomas Simba kwa mara nyingine.

Je Mawakili wa Mbowe hawana namna ya kumkataa Hakimu Thomas Simba?
 
Mwezi Februari mwaka 2018 Hakimu Michael Mteite wa Mbeya alimukumu Mbunge Joseph Mbilinyi (CHADEMA) miezi 5 jela kwa kosa la kumkashifu Rais wa Tanzania.

Hukumu hiyo ilitenguliwa mnamo April 2018 na JAJI UTAMWA wa Mahakama Kuu Kanda ya Mneya baada ya Sugu kuwasikisha ombi la rufaa.

Mnamo Machi 2020 Hakimu Thomas Simba wa Mahakama ya Kisutu aliwahukumu kifungo cha miezi 5 au faini ya Tsh 350 Milion Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake kwa makosa ya kufanya maandamano haramu yaliyopelekea kifo cha Akwilina Akwelin aliyekuwa mwanafunzi wa NIT.

Leo 25/ 06/ 21, JAJI wa Mahakama Kuu Irvin Mheta ametengua maamuzi ya Hakimu Simba na kuamuru washitakiwa warudishiwe kiasi hicho cha fedha.

Ni wazi hizo kesi huenda zilikuwa na shinikizo la kisiasa kutoka kwa Mwendazake au Mahakimu walifanya maamuzi hayo kumfurahisha Mwendazake ili awape promotion ya UJAJI.

Nini itakuwa hatima ya Mteite na Simba kwenye maisha yao uraiani baada ya kustaafu?
Haya yalikuwa maagizo toka kwa dikteta no 1
 
Turudi hapa tena. Kesi Ugaidi inayomhusu Freeman Mbowe iko mbele ya Thomas Simba kwa mara nyingine.

Je Mawakili wa Mbowe hawana namna ya kumkataa Hakimu Thomas Simba?
Wana uhuru kumkataa, ila hakuna haja ya kufanya hivo ktk hatua hii kwavile mahakama ya simba haina uwezo wa kusikiliza shauri hili. Pale shauri limepita tuu kiutaratibu, hatimaye litapelekwa mahakama kuu.
 
Back
Top Bottom