Ni wakati sasa Jeshi la Wananchi lifanyiwe Maboresho makubwa upande wa Kamandi ya Wanamaji

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Kipindi cha Majanga ndicho kipindi sahihi zaidi cha kupima uwezo wa jeshi husika katika ubora na vifaa

Zimetokea ajali nyingi za maji hapa Tanzania kuanzia Mv Bukoba, Vivuko Kigamboni, Zanzibar , Mwanza na sasa imetokea ajali ya ndege ziwani Bukoba

Napenda tu kusema tuna jeshi la maji lisilo la uwezo wa vifaa na teknolojia ya kisasa kabisa. Bila juhudi za wananchi kwenye mazingira haya ni ukweli usiopingika kuwa hata kwenye ndege ya Precision leo wananchi wengi wangekufa

Ingawa mambo ya Ulinzi na Usalama ni masuala nyeti sana ila napendekeza sasa kuwe na complete reforms kwenye jeshi letu la wananchi kamandi ya wanamaji

Mambo yafuatayo yafanywe
1. Tuingie makubaliano na moja ya Taifa kubwa kati ya haya( Marekani, China, Uingereza au Ujerumani) na tuwape mkataba wa kuliwezesha Jeshi letu kivifaa na kiteknolojia bila kusahau ujuzi. Tununue meli za kutosha na both za kutosha za kisasa bila kusahau manowali na nyambizi ziwekwe kufanya kazi kwenye maziwa yote kuanzia Nyasa, Tanganyika, Victoria na Bahari ya Hindi

2. Tanzania kutengeneza karakana yetu ya kutengeneza meli za kivita na za kijeshi kama ilivyo kwa Kenya

Tusipofanya haya sasa yajayo yanasikitisha sana
 
UZOEFU WA MAZOEZI YA UTAYARI KUKABILIANA NA MAJANGA UTUMIKE
Kazi sasa ya vikosi vya uokozi na usalama kuja na ule mpango kazi walionao wa utayari kukitokea majanga kama haya.

Idara jeshi la Zimamoto, Mamlaka za Viwanja vya Ndege, Mamlaka ya Bandari Tanzania, Polisi na serikali ya mkoa, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na serikali kuu taifa pia bila kusahau Ma -Engineer wanatakiwa kuingia kazini kwa pamoja kufanya uokozi kwa kutumia vifaa vyao na utaalamu wao.
 
Bandari ya Bukoba haina hata tug-boat wala boti ya zimamoto.

Idara ya Zimamoto inatakiwa iwe na zana zote nyepesi na nzito za uokozi wa ardhini na majini.

Tujiulize je Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania linawezeshwa sawa sawa kwa kupatiwa rasilimali watu wenye mafunzo tosha, rasilimali vifaa vya uokozi n.k

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
http://www.frf.go.tz
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji – Kuokoa Maisha na Mali

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lina jukumu ya kuzima moto na kufanya maokozi. Maokozi yanayofanywa na Jeshi hili ni pamoja na mtu ......... Source : boti mpya ,2022 – Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

boti mpya ,2022

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni akikabidhi boti mpya la kufanyia maokozi kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John W. Masunga
Source : boti mpya ,2022 – Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

UGENI TO HAMBURG UJERUMANI WATOA VIFAA KWA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini limepokea Ugeni toka Jiji la Hamburg ikiwa ni maadhimisho ya miaka 12 kati ya Jiji la Dar es Salaam na Jiji la Hamburg. Kwa kipindi cha miaka 12 ya ushirikiano baina ya Jiji la Dar es Salaam na Hamburg nchini Ujerumani, Jeshi hilo limefanikiwa kupata mafunzo ya uzimaji moto, maokozi na vifaa vya uokoaji nchini.

Akisoma taarifa yake kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kaimu Kamishna wa Operesheni DCF Charo Mangare alipokuwa akipokea ugeni huo. Alisema ndani ya miaka hiyo 12 tumeweza kupata mafunzo mbalimbali pamoja na kubadilishana programu kati ya majiji haya mawili. Zaidi ya Maafisa na Askari 48 wamenufaika na programu za maafunzo kutoka jijini Hamburg.

Shukrani za pekee ziende kwa Mratibu wa Uhusiano huu, Bi. Inken Bruns na Mratibu wa Zimamoto, Bw. Reinhard Paulsen.

Upande wake Katibu wa mazingira Jimbo la Hamburg, Michael Pollmann alisema amefurahi kuona mafunzo waliyoyatoa yanafanyiwa kazi iliyokusudiwa kwa vitendo.

Nimeona kupitia mafunzo hayo wameweza kujisimamia na kuyaendeleza kupitia uzoefu walioupata kwa sababu Zimamoto ni eneo nyeti linalookoa Maisha na Mali za watu mijini na vijijini

PIX-5-1024x683.jpg

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Nyanda, akitoa maelezo mbele ya ujumbe toka Jiji la Hamburg, vifaa vya msaada walivyopatiwa na Jiji hilo vinavyolisaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika kutekeleza majukumu yake, wakati ugeni huu ulipowasili katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam
PIX-3-1024x683.jpg

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kitengo cha Maokozi wakionesha umahiri wao mbele ya ugeni toka Jiji la Hamburg jinsi ya kufanya uokoaji kwenye majengo marefu pindi madhara yanapotokea wakati ugeni huu ulipowasili katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam.

Habari na picha kwa hisani kubwa : ZIMAMOTO YAPOKEA UGENI TOKA JIJI LA HAMBURG - Mzalendo
 
Kipindi cha Majanga ndicho kipindi sahihi zaidi cha kupima uwezo wa jeshi husika katika ubora na vifaa

Zimetokea ajali nyingi za maji hapa Tanzania kuanzia Mv Bukoba, Vivuko Kigamboni, Zanzibar , Mwanza na sasa imetokea ajali ya ndege ziwani Bukoba

Napenda tu kusema tuna jeshi la maji lisilo la uwezo wa vifaa na teknolojia ya kisasa kabisa. Bila juhudi za wananchi kwenye mazingira haya ni ukweli usiopingika kuwa hata kwenye ndege ya Precision leo wananchi wengi wangekufa

Ingawa mambo ya Ulinzi na Usalama ni masuala nyeti sana ila napendekeza sasa kuwe na complete reforms kwenye jeshi letu la wananchi kamandi ya wanamaji

Mambo yafuatayo yafanywe
1. Tuingie makubaliano na moja ya Taifa kubwa kati ya haya( Marekani, China, Uingereza au Ujerumani) na tuwape mkataba wa kuliwezesha Jeshi letu kivifaa na kiteknolojia bila kusahau ujuzi. Tununue meli za kutosha na both za kutosha za kisasa bila kusahau manowali ziweke kufanya kazi kwenye maziwa yote kuanzia Nyasa, Tanganyika, Victoria na Bahari ya Hindi

2. Tanzania kutengeneza karakana yetu ya kutengeneza meli za kivita na za kijeshi kama ilivyo kwa Kenya

Tusipofanya haya sasa yajayo yanasikitisha sana

Kwa wizi unaoendelea serikalini hakuna haja ya kupoteza hizo pesa ! Tuendelee tu kuomba Mungu majanga yasitufike

Serikali yenyewe hii ni janga tosha !
 
Kipindi cha Majanga ndicho kipindi sahihi zaidi cha kupima uwezo wa jeshi husika katika ubora na vifaa

Zimetokea ajali nyingi za maji hapa Tanzania kuanzia Mv Bukoba, Vivuko Kigamboni, Zanzibar , Mwanza na sasa imetokea ajali ya ndege ziwani Bukoba

Napenda tu kusema tuna jeshi la maji lisilo la uwezo wa vifaa na teknolojia ya kisasa kabisa. Bila juhudi za wananchi kwenye mazingira haya ni ukweli usiopingika kuwa hata kwenye ndege ya Precision leo wananchi wengi wangekufa

Ingawa mambo ya Ulinzi na Usalama ni masuala nyeti sana ila napendekeza sasa kuwe na complete reforms kwenye jeshi letu la wananchi kamandi ya wanamaji

Mambo yafuatayo yafanywe
1. Tuingie makubaliano na moja ya Taifa kubwa kati ya haya( Marekani, China, Uingereza au Ujerumani) na tuwape mkataba wa kuliwezesha Jeshi letu kivifaa na kiteknolojia bila kusahau ujuzi. Tununue meli za kutosha na both za kutosha za kisasa bila kusahau manowali na nyambizi ziwekwe kufanya kazi kwenye maziwa yote kuanzia Nyasa, Tanganyika, Victoria na Bahari ya Hindi

2. Tanzania kutengeneza karakana yetu ya kutengeneza meli za kivita na za kijeshi kama ilivyo kwa Kenya

Tusipofanya haya sasa yajayo yanasikitisha sana
pesazl zinapigwa na wachache nani atatoa hivyo vifaa
 
Watanzania tumeshalemazwa akili na wanasiasa.

Kila jambo tunataka tufanyiwe na watu wengine.

Mleta mada ni mfano mzuri.
 
Leo bila ya wanaoitwa WAVUVI HARAMU sijui angekuja Nani kuokoa maana jamaa ndiyo wamefanya kazi kubwa ya uokozi Kwa masaa kadhaa mpaka wanausalama kutokea inashangaza mitumbwi Leo ndiyo imekuwa vifaa vya uokozi
Bila hawa wavuvi leo ilikuwa balaa kubwa sana na kama tungekuwa na jeshi lenye utaalam na vifaa vya kisasa inawezekana abiria wote wangekuwa wameshapona leo
 
Watanzania tumeshalemazwa akili na wanasiasa.

Kila jambo tunataka tufanyiwe na watu wengine.

Mleta mada ni mfano mzuri.
 
Novemba 6, 2022
Bukoba, Kagera
Tanzania

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LIKITEKELEZA MAJUKUMU ENEO LA AJALI YA NDEGE ZIWA VICTORIA

Jumapili Novemba 6, 2022 ni juu ya kuanguka kwa Ndege ya Shirika la Precision Air mjini Bukoba Mkoa wa Kagera. Ndege hiyo inaonekana ikielea kwenye maji katika Ziwa Victoria ambapo watu wanaokolewa hivi sasa.......
Source : Global TV Online
 
Back
Top Bottom