Mtu ameumbwa kwa nafasi tatu. Mwili, pumzi ya MUNGU, na Nafsi.
MUNGU alifinyanga udongo na kuupa umbo,kisha akapuliza puani pumzi yake.
Pumzi ilipopuliwa ndani ya mwili, kikafanyika kitu kingine yaani Nafsi. (Nefesh), kwa Kiebrania.
Roho, na Nafsi, vimeunganishwa na mwili kwa kamba ya rangi ya fedha (Silver cord), ambayo ni kama kioo. Kamba hii ndio waweza iita maisha. Soma Mhubiri 12:6.
Sasa mauti ni nini?. Mauti ni kukatika kwa kamba ya fedha,( Silver cord).Ndio maana watu husema Fulani kakata kamba maana yake Silvercord imekatika.
Hivyo, Mtu anapokufa, huenda mahali pa wafu ,au mahari pa kusubiri ufufuo wa hukumu. (Paradise, au ahera,) kwa aliyeishi kwa kumtii MUNGU, na Kuzimu kwa aliyeishi duniani katika maisha yasiyompendeza MUNGU.
Sehemu zote hizi,ziko katika Mbingu ya tatu, Lakini zimetengwa . Aliyeko paradise, hawezi kwenda kuzimu, wala aliyeko kuzimu hawezi kwenda paradise.
Wengi hufikiri paradise Iko juu na kuzimu ni chini. Lakini huenda si hivyo.
Ikumbukwe kuwa kaburi ni mlango wa kuingia mbingu ya tatu, tena ni katika dimension iliyo tofauti na dunia tunayoishi.
Mfano ni pale pembe tatu ya Bermuda, (Bermuda Triangle). Wengi wamefikiri kuwa shimo lililo wazi ambalo .meli kubwa na ndege huwa zikizama kupitia shimo hilo. Ukweli ni kuwa, hakuna shimo lolote katika Bermuda Triangle, bali kuna mlango ambao hufunguliwa na kufungwa kuelekea katika dimensions zilizo tofauti na maisha tunayoishi. (Star gate).
Wataalmu wa mambo ya miamba wamechunguza na hawajaona shimo lolote pale. Milango hiyo Iko mingi kuelekea katika different dimensions . mfano, Dragons Triangle iliyoko katika pwani ya Japan, kisiwa cha philipino na visiwa vya Wake Bahari ya pacific.
Sent using
Jamii Forums mobile app