naomba nitumie sms yeyote kwa pm yangu..!! usitumie ile previous chat... nimeifuta sasa nashindwa kuku pm...Ooh I mean karibu PM
Jr[emoji769]
sijui utanielewa😐😐😐
naomba nitumie sms yeyote kwa pm yangu..!! usitumie ile previous chat... nimeifuta sasa nashindwa kuku pm...Ooh I mean karibu PM
Jr[emoji769]
Mbona unaamua kupotosha watu na stori zako za kufikirika. Hayo unayoongea unayajua au nawe wasoma hadithi tuKaribu tena... Uliadimika kidogo.....!!!
Subiri ndoto za usiku huu uone zinasemaje kwakuwa zinaweza kukupa ujumbe fulani... Tofauti na hapo hizo ni ndoto za kawaida ambazo sometimes tafsiri yake huja kinyumeMkuu samahan leo nimmeota rafik yangu amekufa
Pia nmeota mama mmoja wa hapa mtaani napoish amekufa pia
Mkuu samahan leo nimmeota rafik yangu amekufa
Pia nmeota mama mmoja wa hapa mtaani napoish amekufa pia
Rafiki maandiko yapi? Au kisa cha Lazaro na tajiri waliokufa na tajiri akaenda kuzimu?Kwahiyo hata maandiko yamedanganya? Kama kuzimu hakupo kuna nini basi
Yako mengi tu. Ila wengi hutumia sana fungi hilo. Unless wewe una version nyingine ilete babaHayo pekee ndio reference yako?
lete fungu!Mimi si mmojawapo kati ya hao wengi
naona huna mafungu acha nuikupe ili na wengine wanafaike.Mimi si mmojawapo kati ya hao wengi
Mtu akifa hajui lolote. Ijara yake kwishnei! Anaoza! Ukisikia kuzimu = ni ushetani huo no uongo mkubwa huo. Hakuna kitu kama hicho
Ufunuo wa Yohana 20:13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.naona huna mafungu acha nuikupe ili na wengine wanafaike.
ukisoma vema utaona kuwa habari ya kuzimu kunashabihiana sana na ibilisi! / shetani/ giza. hakuna matumaini, hakuna uzima hapo. hakuna heri hapo bakli uangamivu. washukao kuzimu hawana nuru ya Mungu. swali lini hiyo? tunachoamini sio pale mtu anapokufa hapana bali Yesu atakapokuja kuuuhukumu ulimwengu kuna miaka 1000 amabapo wateule watapaa mbinguni kabla ya kurudi na yerusalem mpya! watakaobakia hapa na ilisi watakuwa kuzimu maisha magumu, shida mateso n.k na yerusalem itakpokuwa ianshuka ndipo shetani atawaongoza walio huku kuushambulia na hapo yesu akiwa mfalme atawasha moto na kuteketekeza dhambi na ibilisi. na hawatakuwepo milele. kwa hiyo sio kuwa mtu anakufa hapo hapo anakuwa kuzimu!! hapana
mafungu haya hapa chini yapo 73! katika biblia
Mwanzo 37:35 Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia.
Kumbukumbu la Torati 32:22 Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu, Unateketea hata chini ya kuzimu, Unakula dunia pamoja na mazao yake, Unaunguza misingi ya milima.
1 Samweli 2:6 Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.
2 Samweli 22:6 Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego ya mauti ikanikabili.
Ayubu 7:9 Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa.
Ayubu 11:8 Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe?
Ayubu 14:13 Laiti ungenificha kuzimuni, Ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita, Na kuniandikia muda ulioamriwa, na kunikumbuka!
Ayubu 17:13 Nikitazamia kuzimu kuwa nyumba yangu; Nikitandika malazi yangu gizani;
Ayubu 17:16 Litashuka kwenye makomeo ya kuzimu, Itakapokuwapo raha mavumbini.
Ayubu 21:13 Siku zao hutumia katika kufanikiwa, Kisha hushuka kuzimuni ghafula.
Ayubu 24:19 Chaka na hari hukausha maji ya theluji; Kuzimu nako hao ambao wamefanya dhambi.
Ayubu 38:17 Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu?
Zaburi 6:5 Maana mautini hapana kumbukumbu lako; Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?
Zaburi 9:17 Wadhalimu watarejea kuzimu, Naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.
Zaburi 16:10 Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.
Zaburi 18:5 Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti ikanikabili.
Zaburi 30:3 Umeniinua nafsi yangu, Ee Bwana, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao shimoni.
Zaburi 31:17 Ee Bwana, nisiaibishwe, maana nimekuita; Waaibishwe wasio haki, wanyamaze kuzimuni.
Zaburi 49:14 Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na mauti itawachunga; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Umbo lao litachakaa, kao lao ni kuzimu.
Zaburi 49:15 Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanikaribisha.
Zaburi 55:15 Mauti na iwapate kwa ghafula, Na washuke kuzimu wangali hai, Maana uovu u makaoni mwao na katikati yao.
Zaburi 86:13 Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.
Zaburi 88:3 Maana nafsi yangu imeshiba taabu, Na uhai wangu umekaribia kuzimu.
Zaburi 89:48 Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti, Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?
Zaburi 116:3 Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni;
Zaburi 139:8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
Zaburi 141:7 Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi, Ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu.
Mithali 1:12 Tuwameze hai kama kuzimu, Na wazima, kama wao washukao shimoni.
Mithali 5:5 Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu;
Mithali 7:27 Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.
Mithali 9:18 Lakini huyo hajui ya kuwa wafu wamo humo; Ya kuwa wageni wake wamo chini kuzimuni.
Mithali 15:11 Kuzimu na Uharibifu vi wazi mbele za Bwana; Si zaidi basi, mioyo ya wanadamu?
Mithali 15:24 Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu; Ili atoke katika kuzimu chini.
Mithali 23:14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.
Mithali 27:20 Kuzimu na Uharibifu havishibi; Wala macho ya wanadamu hayashibi.
Mithali 30:16 Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi!
Mhubiri 9:10 Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
Isaya 5:14 Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo.
Isaya 14:9 Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi.
Isaya 14:11 Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika.
Isaya 14:15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.
Isaya 28:15 Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli;
Isaya 28:18 Na agano lenu mliloagana na mauti litabatilika, tena mapatano yenu mliyopatana na kuzimu hayatasimama; pigo lifurikalo litakapopita, ndipo ninyi mtakapokanyagwa nalo.
Isaya 38:10 Nalisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.
Isaya 38:18 Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako.
Isaya 57:9 Ulimwendea mfalme na mafuta ya marhamu, ukaongeza manukato yako, ukawatuma wajumbe wako waende mbali, ukajidhili sana hata kuzimu.
Ezekieli 31:15 Bwana MUNGU asema hivi, Katika siku ile alipotelemka mpaka kuzimu naliamuru matanga, nalikifunika kilindi kwa ajili yake, nikiizuia mito yake, nayo maji makuu yalizuiwa; naliamuru Lebanoni kumwombolezea, na miti yote ya kondeni ilizimia kwa ajili yake.
Ezekieli 31:16 Niliwatetemesha mataifa kwa mshindo wa kuanguka kwake, hapo nilipomtupa chini mpaka kuzimu, pamoja nao washukao shimoni; na miti yote ya Adeni, miti iliyo miteule na iliyo mizuri ya Lebanoni, yote inywayo maji, ilifarijika pande za chini za nchi.
Ezekieli 31:17 Hao nao walitelemka kuzimuni pamoja naye kwa watu waliouawa kwa upanga; naam, wale waliokuwa mkono wake, waliokaa chini ya uvuli wake kati ya mataifa.
Ezekieli 32:21 Walio hodari watasema naye, toka kati ya kuzimu pamoja nao wamsaidiao; wameshuka wamelala kimya, hata wasiotahiriwa, hali wameuawa kwa upanga.
Ezekieli 32:27 Je! Wasilale pamoja na mashujaa wao wasiotahiriwa, walioanguka, walioshuka kuzimu pamoja na silaha zao za vita, ambao wameweka panga zao chini ya vichwa vyao, na maovu yao mifupani mwao? Maana waliwatisha mashujaa katika nchi ya walio hai.
Amosi 9:2 Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawatelemsha toka huko.
Yona 2:2 Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe ukasikia sauti yangu.
Habakuki 2:5 Naam, pamoja na hayo, divai ni mchumi mdanganyifu, mtu wa kiburi asiyekaa nyumbani mwake; huongeza tamaa yake kama kuzimu, naye huwa kama mauti, hawezi kushibishwa; bali hujikusanyia mataifa yote; hujiwekea kabila zote chungu chungu.
Mathayo 11:23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.
Mathayo 16:18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Luka 10:15 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu.
Luka 16:23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.
Matendo ya Mitume 2:27 Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.
Matendo ya Mitume 2:31 yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu.
Warumi 10:7 au, Ni nani atakayeshuka kwenda kuzimuni? (Yaani, ni kumleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.)
Waebrania 11:19 akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano.
Ufunuo wa Yohana 1:18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
Ufunuo wa Yohana 6:8 Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi.
Ufunuo wa Yohana 9:1 Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu.
Ufunuo wa Yohana 9:2 Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.
Ufunuo wa Yohana 9:11 Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.
Ufunuo wa Yohana 11:7 Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua.
Ufunuo wa Yohana 17:8 Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako.
Ufunuo wa Yohana 20:1 Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
Ufunuo wa Yohana 20:3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.
Ufunuo wa Yohana 20:13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Ufunuo wa Yohana 20:14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
ahsante, ni vema kusema kile unaamini ili mradi huzodoi, hubezi, hudharau wengine lakini kutoa mafundisho muhimu halafu kwa vile Mungu katuumba na utashi wa uchaguzi basi kila mtu anachagua ili mradi unapochagua ujue matoke ya mbeleni hapo ndio mtihani! Hata Adam alijua matoke aliishaambiwa lakini yet akala!Ufunuo wa Yohana 20:13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Ufunuo wa Yohana 20:14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Asante kwa bandiko refu lililibeba vifungu vya Bible... Kwa muktadha wa kidini (ukristo) na Biblia takatifu uko sahihi kabisa.... Lakini kumbuka hapa si jukwaa la dini bali ni intelligence... Ambako kuna waamini wa imani mbalimbali na wasio waamini pia.... Hivyo tunapochangia lazima tuangalie na hilo pia