Ni wakati gani wafu hufika kuzimu?


Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
104,335
Likes
124,626
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
104,335 124,626 280
Wakati wa mafunzo yangu huko mbali na baadae kazini nilipata mara si haba wasaa wa kukaa na wagonjwa waliokuwa katika dakika zao za mwisho za kufariki... Wachache nilikuwa nao mpaka roho inaachana na mwili.... Maisha yana vitu vinauma na kuumiza sana... Lakini hakuna maumivu makali kama pale roho inapotaka kujitenga na mwili... Ni tendo moja gumu sana.. Na unayaona wazi mahangaiko ya mfu mtarajiwa....
Nimeshiriki pia mara si haba kuwapokea wafu kwenye chumba cha kuhifadhia maiti(mortuary) na kuwahifadhi wengine hadi wiki na ushee...Nimeshiriki kuwaandaa marehemu kwa ajili ya kuagwa mara ya mwisho na wapendwa wao... Nimeshiriki kuzika kwa udongo.. Na nimeshiriki si mara haba kuwachoma moto marehemu kama utamaduni wao unavyotaka
Kote huko niligundua kitu kimoja kikubwa sana... Kifo sio jambo la maramoja linaloishia hapo hapo... Kifo ni mchakato unaoanzia tangu kutungwa kwa mimba, kuzaliwa, kufa na mwendelezo baada ya kufa..
Mfu anakuwa mfu kwasababu tu roho imetengana na mwili.. Lakini kuna uhai usioonekana unabaki mpaka pale makaburini! Na ndio maana kuna simulizi nyingi za marehemu kabla hawajazikwa na hata baada ya kuzikwa... Rejea mada za vituko vya mochwari na marehemu wengi hurejea sehemu walizofia
Baadhi ya vituko hivyo ni
. maiti kununa ama kutabasamu
. maiti kukunja uso
.maiti kugeuka kidogo
. maiti kukataa kusafirishwa
. maiti kukataa kuvalishwa nguo
. maiti kushindikana kabisa kubebwa nknk

Kuna mkanganyiko mkubwa kwenye imani zetu kuhusiana na swala zima la pepo na kuzimu(akhera) na uhalisia wa mfu kufika kuzimu ama peponi muda gani...
Mchakato wa mtiririko wa kikristo uko hivi
Mateso
Kifo
Kuzikwa
Kushuka kuzimu (kwa tafsiri ya hapa kuzimu kuko chini ya kaburi)
Baada ya hayo yote ndio kupaishwa JUU mbinguni(rejea imani ya kikristo)
Hapa ndio inakuja ile tafsiri ya maneno KILA NAFSI ITAONJA MAUTI.....

Kwahiyo wafu huwa around mpaka wanapozikwa ndio huenda kuzimu... Wale tunaowaona wakirejea duniani kwa vague images, ndoto hisia nk sio wafu tena bali ni mizimu.... Na kwa taarifa yako ni kwamba wafu wote wako kaburini /kuzimu wakisubiri ufufuo siku ya kiama... Hakuna mfu aliye peponi na hakuna mfu anayekwenda kuzimu direct bila kupitia mchakato husika... Hata kama alipotelea baharini, hata kama alioza porini ama aliungua mpaka kubakia jivu... Roho ndio hubeba mchakato wote na kamwe roho haifi...
 
moj6

moj6

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Messages
822
Likes
768
Points
180
moj6

moj6

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2017
822 768 180
Tatizo hakuna mtu aliewah kufa halaf akarud kuleta feedback, ukiachilia mbali misukule ,misukule ni mazingaobwe ni ,mwili wa mtu huchukuliwa na kubadilishwa mnyama mfu ,but mda ukifika hata misukule mwenyew hufa,though am young but nilipata chance yakukaa mortuary sikuona kitu chochote ,kuhus mait kukataa kuvaa au kusafirishwa pia ni mazingaobwe
 
majoto

majoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Messages
1,719
Likes
2,006
Points
280
majoto

majoto

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2013
1,719 2,006 280
. Lakini hakuna maumivu makali kama pale roho inapotaka kujitenga na mwili... Ni tendo moja gumu sana.. Na unayaona wazi mahangaiko ya mfu mtarajiwa....

Wapi hasa panapouma? Unatutish buana.... mtu akifa ni kama amelala usingizi hakuna maumivu. Nini kinakuhakikishia kuna maumivu. Tofa
 
ivunya

ivunya

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Messages
1,487
Likes
882
Points
280
ivunya

ivunya

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2015
1,487 882 280
Huko kuzima Kuna nini rahaa au mateso, Na hizo roho zilizopo kuzima zinakutana na wapendwa wao na kufahamiana Habari za duniani
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
104,335
Likes
124,626
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
104,335 124,626 280
Kufa ni mchakato,ambao kabla roho haijatoka na kwenda Kuzimu kama ulivyosema ndo unakuwa umekamilika!
Haya una uhakika gani na kitu ambacho hujawahi kuki experience hasa kushuka kwa roho kuzimu?
Hapana mchakato wa kufa hauna mwisho... Hivyo hauwezi kuwa kamili I mean kukamilika...
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
104,335
Likes
124,626
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
104,335 124,626 280
Tatizo hakuna mtu aliewah kufa halaf akarud kuleta feedback, ukiachilia mbali misukule ,misukule ni mazingaobwe ni ,mwili wa mtu huchukuliwa na kubadilishwa mnyama mfu ,but mda ukifika hata misukule mwenyew hufa,though am young but nilipata chance yakukaa mortuary sikuona kitu chochote ,kuhus mait kukataa kuvaa au kusafirishwa pia ni mazingaobwe
Hapo kwenye... Though am still young... Panajibu hoja zako... Jipe muda kuna mengi bado huyajui
 

Forum statistics

Threads 1,250,081
Members 481,224
Posts 29,720,333