Ni ukweli mtupu Mshahara wa kima cha chini TUCTA wanaoutaka hautekelezeki

mimi kuna watu wananiudhi sana, kweli mnadhani taifa hili halina pesa za kulipa mishahara ? kweli ninyi mnanishangaza, Kikwete , Wabunge na Mawaziri wana kula keki zaidi ya asilimia 78, WANAITAFUNA HIVIHIVI, ANGALIA ANALYSIS ZA Sikonge hapo juu, sasa hiyo A na B ni ile Budget ya Kikwete yakuendea nnje ya Tanzania kwenda kutalii na kufanya utumbo huko, leteni budget ya mkewe, leta Budget ya ofisi yake kwa ujumla...aibu ni aibu.
 
MkamaP,

Unafahamu idadi ya Wabunge wanaoongezwa mwakani kutokana na kuongezwa majimbo? Unafahamu WABUNGE wa KUTEULIWA mwakani pia wanaongezwa? Ndiyo maana Mawaziri wanahaha kuwaweka Watoto wao kwenye umoja wa Vijana. Sintashangaa kusikia Ridhwan nayeye kawa Muheshimiwa Mbunge na awe anakunja 10Milioni kwa mwezi. Na hawa wa kuteuliwa hata hawana Majimbo ya kujibu shutuma. Wee unalala tu na mwisho wa mwezi unakunja Milioni zako 10.

Pinda anataka kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa kwao na kuifanya Mpanda kuwa Mkoa. Kikwete anataka kujenga Uwanja wa ndege Bagamoyo na bandari Bagamoyo. Hizo hela zipo ila walau kuvitengeneza viwanja vya ndege vya Mwanza, Kilimanjaro, Tabora, Shinyanga, Kigoma na Mbeya hiyo wao wala hawaioni.
Tunasahau mambo muhimu na kuparamia mambo yasiyo muhimu.

Hizo pesa kama kweli tukibana matumizi na kuongeza uzalishaji, zinalipika. MkamaP, Wahandisi au waliosomea Engineering, MILELE HATUSEMI HAIWEZEKANI. Amini usiamini, angelikuja Joseph Stallin na kusema nawapa miaka miwili uchumi ukue, Dar iwe safi na kima cha chini kiwe dola 300 na bei isipande hata kidogo na sanasana ishuke. Mtu akishindwa kazi RISASI. Ungelishangaa kima cha chini kikawa Dola 400 (hapa siongelei Shamba boi na house girl).

Kwani shamba boy na hause girl sio mfanyakazi? Hiyo kitu ya mshahara kwa tz haiwezekaniki kutokana na hali halisi yenyewe,
Nafikiri watu wanaongelea helo ndogo mno ya wabunge kukidhi haja.
Hata wakisema hakuna Bunge na hakuna waziri kulipwa bado fedha hizo hazitoshi kutosheleza kulipa wafanyakazi ,kwa msingi mmoja tu ya kwamba watanzia asilimia kubwa sio productive.
 
thank You, hapo pia umeiweka vyema kabisa. watu waache kudhani kila asemacho Rais wa Jamuhuri ni kweli ama sahihi, watu wasomi wazima wanakwambia si unasikia Rais kasema hawana pesa za kulipa hao wafanyakazi.....lazima watu wafikiri nnje ya boksi, watu wanamentality za enzi za ujamaa wa Nyerere kua asemacho Nyerere ni kweli na sahihi

Wewe tulia acha kulazimisha watu wawaze kama wewe unavyotaka .Watanzania ni wavivu hiyo mishahara haitekelezeki.
 
MkamaP,
Ebu nambie hiyo mishahara ya Ugiriki ukubwa wake...Mkuu hivi kweli unafuatilia swala hili? Greece inaanguka kiuchumi kutokana na matumizi makubwa na mabaya ya serikali. Nitarudia kusema mgogoro mzima wa greece unatokana na pendekezo la kupunguza ajira (jobcuts) na pia mishahara ya mafanyakazi kulingana na uzalishaji wa ndani ambao unashuka mwaka hadi mwaka. Deficit ya GDP imefikia karibu asilimia 15 hivyo haina maana ya kwamba mishahara ndio mikubwa ila kuna matumizi makubwa ya serikali kinyume cha pato lake la ndani.

Leo hii Tanzania tupo ktk jarida hilo hilo... tuna matumizi makubwa ya serikali na mishahara ya civil servants sii moja ya matumizi yetu makubwa ila viongozi na posho zao. Hivyo deni la taifa letu linazidi kupanda kila siku na kusema kweli tupo ktk kufilisika ndani ya umaskini sema mikopo ndio unatusaidia sana. Sasa itakuja siku tunafilisika watu wa kwanza kuumia itakuwa hawa hawa wafanyakazi na sii viongozi. Ni sawa na mtu anayeishi kwa creditline akitumia mikopo kuendesha shughuli zake. Ukweli wa mambo ni kwamba uzalishaji umepungua sana na pnengine tupo chini ya asilimia 50 ya uzalishaji na mzunguko wa fedha yetu unategemea zaidi fedha zilizoibiwa au zinazoibiwa ktk mabenki na mashirika, pengine hata uchapishaji wa fedha zaidi umetumika kutuwezesha mzunguko kuwepo.. Kifupi tunajidanganya wenyewe.

Watanzania ni wavivu kwa asili. Sii wafanyakazi kutokana na mfumo mzima wa ajira. Watu wanatakiwa kulipwa kwa masaa ya uzalishaji na sii mfumo wa ajira wa kijamaa ktk uchunkazi naKuna sababu nyingi za kimsingi zinazoweza kutumika kutoongeza mishahara kwa sababu kila siku uzalishaji unapungua. Huwezi kuongeza mishahara wakami unaoendeshwa na soko huria.. wafanyakazi wengi wanavuna ambacho hawakupanda na hii ni hatari kubwa kiuchumi kwani hakuna sababu ya kuboresha uzalishaji ikiwa paycheck haina kiwango cha masaa ya uzalishaji..Na sababu kubwa ya uvivu wetu umetokana na ukosekanaji wa MIUNDOMBINU.
Uzalishaji unazidi kupungua kutokana na miundombinu mibovu. watu wanafanya kazi masaa chini ya sita kutokana na usafiri mbovu, ukosekanaji wa mara kwa mara wa umeme na upungudu wa maji. Kuna kila dalili mbaya ya sisi kuanguka kiuchumi

Mkuu
Ugiriki tatizo ni kwamba wapinzani waliahidi mishahara minono na wakafanikiwa kuiangusha serikali, na wakatekeleza kulipa mishahara minono kwa wafanyakazi, ugiriki mishahara yao ipo juu kuliko UK hata na ujerumani. Sasa wameishiwa fedha maana walikuwa wanalipana mishahara minono bila kufanya kazi za uzalishaji kuiwezesha hiyo mishahara minono.

Sasa wameenda kukopa european union fedha na wamepewa hiyo condition ili wapewe mkopo lazima walipe wafanya kazi EURO zisizosidi 400 na kukata wafanyakazi kodi kwa 33% . Hawana jinsi inabidi watekeleze ili wapewe mkopo , ndio maana unaona wafanyakazi wanagoma na huo mgogoro. Chazo cha mgogoro ni mishahara minono na uvivu wa kuiwezesha mishahara minono.

Tukirudi kwetu wagiriki ni angalau wanachapa kazi kuliko sisi watanzania, huo ndo ukweli .kuiwezesha hiyo mishahara kwa watanzania hakika ni kuchimba bonge la kaburi. Wataweza kulipa ndani ya miezi sita tu harafu baada ya hapo ndo vile tena .Huko ulikoelekea maelezo mengine nafikiri unaelekea sasa kwenye pointi yangu ya kwamba kuiwezesha mishahara hiyo kwa watanzia sisi ni kuchimba bonge la kaburi.
 
MkamaP, naona wewe huna tofauti yoyote na wale wanaoitwa "Wazee wa DSM" waliokuwa pale Diamond Jubilee. Kwa hiyo siwezi kubishana/kushindana na wewe, period

Tatizo mnaongea tu blaah blaah blaah weye vipi?
Chukua bajeti yote ya mwaka 2009/2010 gawa kwa wafanya kazi wote wa umma na hilo jibu gawa kwa 12.
 
MkapaP ni sampuli halisi ya watu wanaomzunguka Mhe. Rais wetu unategemea atashauriwa nini na watu kama hawa. Hoja yake na madai yanayosupport hoja hiyo yanaonyesha uwezo wake. Tunayokazi kubwa kwasababu waliomzunguka Rais 'wanakaribiana nae' hawezi kupata mawazo mbadala wala mawazo yakinifu. Sorry Mkama leo ndo nimekupata vizuri.
 
MkapaP ni sampuli halisi ya watu wanaomzunguka Mhe. Rais wetu unategemea atashauriwa nini na watu kama hawa. Hoja yake na madai yanayosupport hoja hiyo yanaonyesha uwezo wake. Tunayokazi kubwa kwasababu waliomzunguka Rais 'wanakaribiana nae' hawezi kupata mawazo mbadala wala mawazo yakinifu. Sorry Mkama leo ndo nimekupata vizuri.

Mkuu,

MkamaP yuko mbali sana na Kikwete. Msome katikati ya mistari. Nafahamu macho yake (tabiya yake) ina makengeza, ukimuona kaangalia kushoto, basi unaweza kuta macho yanaangalia kulia.

Mkama, hilo linawezekana ndugu yangu. Si unaona hata Ugiriki sasa hawawezi kusema waongeze Bunge? Sisi viongozi wetu wamelala sana. Kama angelikuja kiongozi na kuhakikisha watu wanafanya kazi, kima cha chini kingelifika hapo. Ukisema HAKIWEZEKANI basi unakubaliana na Wazungu wanaodai WAAFRIKA IQ zetu ziko chini sana. Inakuwaje Wajapan ambao hawana kitu chochote hata ardhi, wanakuwa matajiri duniani na sisi tuna kila kitu, tunakuwa mafukara na tunasema waziwazi kabisa hatuwezi?

Kama na wewe unaamini hivyo ki kweli basi hamia Sikonge/Tabora tuje tumpongeze Kikwete kwa hotuba nzuri. CCM Tabora OYEEEE!!!!!
 
MkapaP ni sampuli halisi ya watu wanaomzunguka Mhe. Rais wetu unategemea atashauriwa nini na watu kama hawa. Hoja yake na madai yanayosupport hoja hiyo yanaonyesha uwezo wake. Tunayokazi kubwa kwasababu waliomzunguka Rais 'wanakaribiana nae' hawezi kupata mawazo mbadala wala mawazo yakinifu. Sorry Mkama leo ndo nimekupata vizuri.

KWeli kazi kubwa ipo, maana watu kulilia kuvuna wasichopanda ni ajabu na kubwa. Mafisadi ni kweli wanavuna wasichopanda lakini haina maana na wewe uvune usichopanda ili mdrooo. Mentality za namna hii ni mfu. Sisi wenyewe tukijituma kufanya kazi.Kwa hali iliyopo na uwezo wetu mishahara haitekelezeki

Na kama itekelezwe
Mkandara
ametoa option saafi sana kulipwa kwa masaa na kusimamiwa kama mkoloni ukimiss saaa unakatwa hilo lisaa .Mbona hiyo hamuongelei??
 
Mkuu,

MkamaP yuko mbali sana na Kikwete. Msome katikati ya mistari. Nafahamu macho yake (tabiya yake) ina makengeza, ukimuona kaangalia kushoto, basi unaweza kuta macho yanaangalia kulia.

Mkama, hilo linawezekana ndugu yangu. Si unaona hata Ugiriki sasa hawawezi kusema waongeze Bunge? Sisi viongozi wetu wamelala sana. Kama angelikuja kiongozi na kuhakikisha watu wanafanya kazi, kima cha chini kingelifika hapo. Ukisema HAKIWEZEKANI basi unakubaliana na Wazungu wanaodai WAAFRIKA IQ zetu ziko chini sana. Inakuwaje Wajapan ambao hawana kitu chochote hata ardhi, wanakuwa matajiri duniani na sisi tuna kila kitu, tunakuwa mafukara na tunasema waziwazi kabisa hatuwezi?

Kama na wewe unaamini hivyo ki kweli basi hamia Sikonge/Tabora tuje tumpongeze Kikwete kwa hotuba nzuri. CCM Tabora OYEEEE!!!!!

He he he exactly
hapo ndo ninakuja lakini watu wanakurupuka.
TUCTA wangehakikisha wafanya kazi wao wanafanya kazi kwa kujituma na ndio yaambatane na malipo. JK anajuwa kwa sasa system ilivyo ni ngumu kuwabana wafanya kazi wachape mzigo sahihi.
Ndio maana kuwezesha huo mshahara lazima na system ibadirike watu wafanye kazi kwa masaa ni si kwa mwezi?
 
MKAMAP sidhani kama wafanyakazi wanaozungumziwa ni house boy/bar maid, hao wanakatwa kodi kwenye mishahara yao?
 
Profesa Shivji ashauri walimu walipwe zaidi ya mawaziri




Na Joseph Mwendapole



6th May 2010


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa



comment_bubble.png

Maoni




Shivji%283%29.jpg

Mwanazuoni maarufu nchini, Profesa Issa Shivji.



Mwanazuoni maarufu nchini, Profesa Issa Shivji, ameishauri serikali iwalipe walimu mishahara mizuri zaidi ya mawaziri kwa kuwa kazi wanayofanya ni ngumu.
Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati wa Jukwaa la Wazi la Uchumi wa Afrika lililofanyika katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).
Jukwaa hilo liliandaliwa kwa pamoja na mashirika ya ActionAid Tanzania, Oxfam, Forum CC, FemAct, Yuna na Kepa.
Profesa Shivji alisema elimu inazidi kuporomoka kwa kuwa hakuna jitihada zinazochukuliwa na serikali kuondoa hali hiyo.
Alisema serikali inaangalia zaidi ongezeko la majengo na idadi ya wanafunzi mashuleni jambo ambalo alisema haliwezi kuinua kiwango cha elimu.
"Mwalimu akiwa bora na akiwa katika mazingira mazuri ya kufundisha hata akifundishia chini ya mti, wanafunzi watafanya vizuri sana, lakini ukiwa na majengo mazuri mwalimu akawa mbovu ina maana elimu itakayopatikana hapo ni ya kiwango cha chini," alisema.
Alisema walimu wengi kutokana na hali ngumu wameamua kuachana na hali hiyo na sasa wanafanya shughuli zao za kuwaingizia vipato.
"Mimi sioni sababu kwanini mwalimu ambaye ni muhimu zaidi ya waziri kwenye jamii, alipwe mshahara kidogo na waziri alipwe mshahara mnono na marupurupu mengi kumzidi mwalimu," alisema.
Vile vile, Profesa Shivji alisema ingawa Tanzania ni ya pili kwa kuwa na mifugo mingi Afrika, wafugaji wamekuwa hawanufaiki na mifugo yao.
Alisema wafugaji wamekuwa wakihangaishwa kama vile si raia wa Tanzania kwa maeneo yao kuchukuliwa kiholela akitolea mfano wa Ngorongoro.
Awali, akifungua mkutano wa jukwaa hilo, Mkurugenzi wa ActionAid Tanzania, Aida Kiangi, alisema inaonekana mkazo mkubwa wa ustawi na ukuaji wa uchumi katika jukwaa hilo la kiuchumi umeelekezwa zaidi kulenga maslahi ya makampuni makubwa dhidi ya Waafrika walio wengi hususani wanawake, wakulima wadogo na wafupaji pamoja na maskini wanaozidi kuongezeka hasa maeneo ya mijini.
Kiangi alisema kumekuwa na ukuaji wa uchumi kwa nchi za Afrika lakini wanaonufaika na ukuaji wa uchumi huo ni wachache.
"Tunaweza kujiuliza ni nani anayenufaika zaidi na ukuaji wa uchumi huu," alihoji.



CHANZO: NIPASHE

Haya ndo mawazo ya kimapinduzi
 
MKAMAP sidhani kama wafanyakazi wanaozungumziwa ni house boy/bar maid, hao wanakatwa kodi kwenye mishahara yao?

Mkuu
Hawa tucta ni kweli wafanya kazi wa ndani hawamo. Lakini nenda kasome kwenye ile aliyoisoma kapuya kwa sekta binafsi.
Hause girl wamo, mashamba boy wamo, wauza viosk wamo. Na ndiyo maana ukiangalia kwa makini hata serikali ikiwalipa hiyo mishahara na ikaamuwa kutekeleza na kusimamia hasa.Bado watarudi kudai tena mara tatu zaidi ya hapo maana huo mshahara utakuwa unalipa ma hause girl.

Ndiyo na kwambieni ya kwamba kuna vitu tunavikurupukia bila kuwa na mikakati thabiti. Wafanyakazi wangependekeza njia sahihi na mwisho kudai mishahara hiyo. Leo wakiamuwa kutoa hiyo mishahara baadae ndo hata elfu hamsini itakuwa bonge la mshahara. Kama Ugiriki vile.
 
Mitanzania bwana ninakereka sana siku zote tunazungumzia kugawana kidogo sana tulichonacho badala ya kusema tunaweza kujilipa hata $1000 kama kima cha chini lakini hilo lawezekana kama tukifanya kazi tu na kuzalisha sana.

Sasa kwa nini nimekereka sio Rais wala TUCTA waliobainisha kwamba tatizo ni uzalishaji tu!!!


Kasheshe. Nakubaliana kwamba kuna watu wasiofanya kazi. Ni kweli kabisa. Lakini nataka nikwambie kuna watanzania wengi sana wanafanya kazi sana lakini kwa kipato kidogo sana.

Sikubaliana na porojo hizi za wanasiasa wa Tanzania kwamba watanzania hawalipwi vizuri kwa sababu they are not hard workers. Hapana watanzania wasiofanya kazi ni wachache sana lakini wengi wanafanya kazi sana. Tena watanzania ni wafanyakazi sana kama wanajua kazi itawalipa. Lakini nakwambia hawalipwi vizuri kiasi kwamba wengi wanakata tamaa sana.

Leo hii wanasiasa ambao kwa kweli hawazalishi lolote zaidi ya porojo majukwaani ndio wanaolipwa pesa nyingi sana pamoja na kundi la marafiki na relatives wao. Hawa jamaa na marafiki ndio wanaotumika kufisadi kwa ofisi za mfukoni kwa mfano wa Richmond. Hawa ndio tunaona wametoka kirahisi na wakiishi maisha ya anasa sana. Wakati wale tufanyao kazi sana hatulipwi itakiwavyo. Hawa ndio wanatukoga sisi tunaofanya kazi kwa bidii.

Kuna mifano mingi iliyo wazi ambayo imezungumzwa hapa jf na kwenye media zingine jinsi wanasiasa wetu wanavyotumbua kodi zetu kana kwamba wana viwanda vya kufyatua pesa huku wakitoa takwimu za uongo kuwa mambo nchini yanakwenda vizuri.

Kwa sababu nyingi naweza kuwatetea wadanganyika kuwa ni wachapa kazi lakini kama utachapa kazi ulipwe pesa ambayo haiwezi hata kununua robo kilo ya sukari au chumvi nani yuko tayari kufanya kazi hivyo kwa nguvu? Nguvu hizo zitatoka wapi?

Ili mambo katika nchi hii yaende vizuri ni lazima kila mmoja kuanzia rais wetu hadi mtu wa chini awe na nidhamu katika kazi. Tufanya kazi, tulipwe inavyostahili, tuwe na matumizi yaliyo na nidhamu, na hapo kila jambo litakwenda vizuri. Mkulima alipwe stahili zake na vyama vya ushirika ili akidhi mahitaji yake. Na mfanya kazi alipwe kwa kazi aliyofanya pia.

Haiwezekani wote tushinde ofisini tukichapa kazi hadi saa 11 jioni maana tumejiweka katika nafasi ya kufanya kazi kwa bidii, na mwisho wa mwezi napata 100,000.= na mwingine anayefanya ofisi hiyo hiyo anapata 1,000,000= exclusive marupurupu kisha huyo huyo aniambie tufanya kazi kwa bidii ili tutoke. This is a joke. Ni vigumu kuelewa reality katika jambo hili.

 
He he he exactly
hapo ndo ninakuja lakini watu wanakurupuka.
TUCTA wangehakikisha wafanya kazi wao wanafanya kazi kwa kujituma na ndio yaambatane na malipo. JK anajuwa kwa sasa system ilivyo ni ngumu kuwabana wafanya kazi wachape mzigo sahihi.
Ndio maana kuwezesha huo mshahara lazima na system ibadirike watu wafanye kazi kwa masaa ni si kwa mwezi?
Mkama Pendekeza basi mshahara wa mtumishi wa serikali kwa siku basi iwe shilingi ngapi? ili wadanganyika wafanye kazi na kulipwa kwa saa basi.
Kwani nani alikataa hiyo system? Watumishi au mwajiri wao?
Pendekezo lako la kulipwa kwa kila saa mtu afanyayo kazi nakubaliana nayo kabisa! lakini kwa hesabu zako unaona alipwe shillingi ngapi rafiki we! Hili pendekezo tuwape Tucta.
 
thank You, hapo pia umeiweka vyema kabisa. watu waache kudhani kila asemacho Rais wa Jamuhuri ni kweli ama sahihi, watu wasomi wazima wanakwambia si unasikia Rais kasema hawana pesa za kulipa hao wafanyakazi.....lazima watu wafikiri nnje ya boksi, watu wanamentality za enzi za ujamaa wa Nyerere kua asemacho Nyerere ni kweli na sahihi

Yeye mwenyewe kawambia waongeze na akili yao kama mbayuwayu kwa wanayoambiwa. Amewambia nao waongeze na yao. hahahahahahahah!
 
MkamaP.. kwa maoni yako ni kima gani cha chini cha mshahara wa mfanyakazi wa Tanzania serikali inaweza kumudu na kikamfanya mfanyakazi amudu maisha?
 
Tu na mismanage resources halafu tunajilinganisha na wagiriki? Mafisadi wanabwia vijisent kwa kwenda mbele halafu tunajilinganisha na wwagiriki? tunajua hela inakokimbili, kamavile kwenye ziara zisizo na tija za JK, kila Dar panapopata mota, halafu tunajilinganisha na Wagiriki? Ah ah, Bw mkama, acha bwana, kima cha chini cha 315k kinawezekana kabisa tena pamoja na kupunguza kodi kama tutamanage resources za taifa vizuri!
 
MkamaP.. kwa maoni yako ni kima gani cha chini cha mshahara wa mfanyakazi wa Tanzania serikali inaweza kumudu na kikamfanya mfanyakazi amudu maisha?

Kima cha chini kinachomfaa mtu ni kutokana na uzarishaji wake na uvumlivu kazini. Upo marekani mtu anayebeba maboksi masaa 18 kima chake cha chini kipo juu kuliko anayebeba maboksi masaa 8.
 
Back
Top Bottom