Ni ukweli mtupu Mshahara wa kima cha chini TUCTA wanaoutaka hautekelezeki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni ukweli mtupu Mshahara wa kima cha chini TUCTA wanaoutaka hautekelezeki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MkamaP, May 6, 2010.

 1. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Wananchi na wana jamii wenzagu

  Kiu -halisia mshahara wa kima cha chini cha zaidi ya US dola 300 kwa wafanyakazi wa Tanzania hautekelezeki.
  Haiwezekani na haiwezekani, mfanyakazi anayedai huo mshahara itambidi adai zaidi ya hapo mara mbili ili atekeleze. Mfano wewe ni mwalimu wa kike una mtoto na umeajiri dada wa kumlea nyumbani itakubidi umlipe dada huyo zaidi ya us dola 300. Na utaishi je? itabidi udai tena zaidi us dola 300 kutoka serikalini ili upate kuishi.

  Ugiriki lwo wamefirisika kwa sababu nao wafanya kazi wali dai ongezeko kama hilo. Ugiriki wanahaha kutafuta sehemu ya kukopa, EURO imeanguka sababu ya ugiriki.

  Naungana na JK mshahara huo hautekelezeki.
   
 2. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ebu TUCTA na JK wekeni pembeni tutadiscuss kuanzia tarehe 8, wana forum. Maana tumeongea sana kwenye forum hii.
   
 3. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,743
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hautekelezeki kwa nani? serikali au mwajiri binafsi? be precise!
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tusubiri tarehe 8 ikishindikana ni msituni
   
 5. l

  leon Member

  #5
  May 6, 2010
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mbona kwa Wabunge na wafanyakazi wengine wa serikali kama BOT, TRA, n.k. unawezakana, iweje usiwezekane kwa wengine? Mbunge anapata posho ya kikao kwa siku ambao ni almost sawa na mshahara wa KCC na ananalamika hautoshi. Wa-Tz tusiwe wavivu wa kufikiri. Tanzania yenye neema kwa wote inawezekana. Simuungi mkono JK kwa hili...
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mitanzania bwana ninakereka sana siku zote tunazungumzia kugawana kidogo sana tulichonacho badala ya kusema tunaweza kujilipa hata $1000 kama kima cha chini lakini hilo lawezekana kama tukifanya kazi tu na kuzalisha sana.

  Sasa kwa nini nimekereka sio Rais wala TUCTA waliobainisha kwamba tatizo ni uzalishaji tu!!!
   
 7. MANI

  MANI Platinum Member

  #7
  May 6, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  MkamaP kima kinachodaiwa ni Tsh 315,000.00 na siyo USD 300.00 Sidhani kama kiwango hicho kinashindikana.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  May 6, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  MkamaP,
  Mkuu hata sikuelewi unachozungumza. Hili swala la kufilisika kwa Ugiriki halitokani na mishahara hata kidogo. Ni kushuka kwa uchumi wa nchi hiyo ambako kumetokana na matumizi makubwa ya serikali kinyume cha pato na uzalishaji wa ndani hasa ktk kipindi hiki kilichoitetemesha dunia kiuchumi. Machafuko yanayotokea huko ni pamoja na pendekezo la kupunguza mishahara na kupotea kwa thamani ya akiba za wananchi. Kifupi pigo kubwa la uchumi wa Ugiriki watalibeba wananchi hali makosa yalifanyika kiutawala wa fedha na uchumi wa nchi.

  Turudi hapa kwetu, wewe nambie sababu ambayo inathibitisha maneno yako kwani unaposema mwalimu anayepokea dollar 300 kumlipa mlezi wake dollar 300, hizi habari umezipata wapi?..Je, umeelewa vizuri madai ya TUCTA au?..Je, unajua kwamba kila sekta ya uzalishaji nchini ina viwango vyake kwa wafanyakazi wake na kila daraja la kazi na vyeo lina mishahara tofauti?
   
 9. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  Mkuu igiriki imefilisika kwa kuripa wafanyakazi mishahara mikubwa kupindukia, hii ni baada ya wapinzani kuchukua nchi na kutekeleza ahadi yao kwa maisha bora kwa wafanyakazi. Habari ndo hiyo.

  Mkuu kima cha chini cha mfanyakazi ni pamoja na house girl, ama muuza kiosk ulio mwajiri ktk kiosk chako. Hayo madai mengine ya tucta sijayaonelea lakini kiwango cha chini cha mshahara wanachodai hakiwezekaniki na hakitekelezeki. Hapo nipo pamoja na JK
   
 10. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Hakuna nchi yoyote duniani ambayo inawezekana kuripa wafanyakazi kwa kiwango sawa. Karibu nchi zote hao uliowataja wanalipwa mishahara minono kuliko wengine
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  May 6, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  unajua upuuzi wa Watu wetu wengi hapa Tanzania ndio unaoinufaishaga CCM na Rais Kikwete.
  Kikwete alikua anaparamia hoja hovyohovyo bila mtiririko wa kisomi na wala uchambuzi makini.
  TUCTA ni shirikisho huru la vyama vya wafanyakazi hapa Tanzania, linaunganisha vyama kama CHAMA CHA WALIMU , RAAWU,TUGHE, TALGWU ,TUICO nk.
  kwahiyo katika mtiririko wa vyama hivyo hakuna vyama vya mahausigeli na mashamba boy, TUCTA wanasimamia hoja ya kutetea wafanyakazi hasa katika sekta rasmi za UMMA na ZISIZO ZA UMMA.
  Alikua anaunganisha mishahara ya wauza duka katika swala hili ili apate compromise ya UMMA....., alipotoka ,alijipotosha ama alipotoshwa.
  TUCTA wanamadai mengi sana, kama Rais wa Jamuhuri alipaswa kujikita katika hoja moja baada ya nyingine, badala ya kujikita katika hoja moja, nakuimba taarabu na kuchombeza na vimipasho.
  mshahara wa 315,000 Unawezekana katika sekta rasmi zooote hapa nyumbani, waache kuchezea hela katika mambo yasiyo na maana, waache kulipana posho za safari za kwenda kubembea Jamaica, apunguze makundi ya wapambe akiwa safarini, wadhibiti kodi, wajiepushe na misamaha hewa....vilevile upandaji wa mishahara usizingatie hoja ya asilimia sawa, maana ailimia kumi ya mshahara wa muhudumu ni Tsh 10000 wakati kwa mishahara ya mawaziri, makatibu wakuu ni TSh 300,000.
  Tanzania Amka achana na mawazo kuwa Rais adanganyi , Rais huwa anadanganya kama mtu mwingine yoyote.
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  MkamaP,

  Unafahamu idadi ya Wabunge wanaoongezwa mwakani kutokana na kuongezwa majimbo? Unafahamu WABUNGE wa KUTEULIWA mwakani pia wanaongezwa? Ndiyo maana Mawaziri wanahaha kuwaweka Watoto wao kwenye umoja wa Vijana. Sintashangaa kusikia Ridhwan nayeye kawa Muheshimiwa Mbunge na awe anakunja 10Milioni kwa mwezi. Na hawa wa kuteuliwa hata hawana Majimbo ya kujibu shutuma. Wee unalala tu na mwisho wa mwezi unakunja Milioni zako 10.

  Pinda anataka kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa kwao na kuifanya Mpanda kuwa Mkoa. Kikwete anataka kujenga Uwanja wa ndege Bagamoyo na bandari Bagamoyo. Hizo hela zipo ila walau kuvitengeneza viwanja vya ndege vya Mwanza, Kilimanjaro, Tabora, Shinyanga, Kigoma na Mbeya hiyo wao wala hawaioni.
  Tunasahau mambo muhimu na kuparamia mambo yasiyo muhimu.

  Hizo pesa kama kweli tukibana matumizi na kuongeza uzalishaji, zinalipika. MkamaP, Wahandisi au waliosomea Engineering, MILELE HATUSEMI HAIWEZEKANI. Amini usiamini, angelikuja Joseph Stallin na kusema nawapa miaka miwili uchumi ukue, Dar iwe safi na kima cha chini kiwe dola 300 na bei isipande hata kidogo na sanasana ishuke. Mtu akishindwa kazi RISASI. Ungelishangaa kima cha chini kikawa Dola 400 (hapa siongelei Shamba boi na house girl).
   
 13. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kasheshe, tatizo si uzalishaji tu bali ni mentality ya viongozi wetu. Viongozi wa ngazi za juu wakiwemo Rais, Mawaziri na Wabunge wangeacha kuwaza uchumia tumbo wakapekeka akili zao kwenye mbinu za kuwahamasisha wananchi wafanye kazi kwa bidii wakiwemo na wao wenyewe viongozi, wapige vita rushwa na madudu mengine yanayorudisha nyuma maendeleo tungeliweza kupiga hatua. Lakini, aah wao wanawaza kuiga maisha ya kifahari na kulipwa mishahara wanayolipwa viongozi na watendaji wa nchi zingine zenye uwezo kifedha.
   
 14. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,793
  Likes Received: 20,734
  Trophy Points: 280
  mkuu,huu ndio mshara wa mbunge wetu kwa mwezi??
   
 15. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #15
  May 6, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  thank You, hapo pia umeiweka vyema kabisa. watu waache kudhani kila asemacho Rais wa Jamuhuri ni kweli ama sahihi, watu wasomi wazima wanakwambia si unasikia Rais kasema hawana pesa za kulipa hao wafanyakazi.....lazima watu wafikiri nnje ya boksi, watu wanamentality za enzi za ujamaa wa Nyerere kua asemacho Nyerere ni kweli na sahihi
   
 16. l

  leon Member

  #16
  May 6, 2010
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  MkamaP, naona wewe huna tofauti yoyote na wale wanaoitwa "Wazee wa DSM" waliokuwa pale Diamond Jubilee. Kwa hiyo siwezi kubishana/kushindana na wewe, period
   
 17. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #17
  May 6, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  haswaaa !
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Date: 2/20/2010

  Kila mbunge kuvuna Sh46 milioni za kiinua mgongo

  *Ni asilimia 40 ya mishara yate ya miaka mitano

  Exuper Kachenje
  Mwananchi  KILA Mbunge ataondoka na zaidi ya Sh46milioni kama kiinua mgongo baada ya Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge Julai mwaka huu.

  Bunge hilo litavunjwa baada ya mkutano wa bajeti unaotarajiwa kumalizika mwishoni mwa Agosti mwaka huu kwa ajili ya kujiandaa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.

  Fedha hizo ni sawa na asilimia 40 ya mishahara ya miaka yote mitano ya utumishi bungeni ambapo mshahara wa kila mbunge kwa sasa anafikia jumla ya Sh1,921,000 kwa mwezi.

  Kwa mujibu wa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah, wabunge watalipwa fedha zao mara baada ya Bunge kuvunjwa.

  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina wabunge 325, kati yao 49 ni mawaziri na manaibu waziri. Ukiondoa mawaziri na manaibu wao ambao kinua mgongo chao hulipwa na serikali, hivyo watakao lipwa na Bunge ni 276. Kwa mantiki hiyo jumla ya Sh12,724,704,000 zitalipwa kama kiinua mgongo kwa wabunge hao ukiondoa mawaziri.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa malipo ya wabunge hao, yatatolewa kwa mujibu wa sheria ya mafao ya viongozi wa kisiasa ya mwaka 1999 ambayo ilianza kutumika 2000.

  Kwa mujibu wa sheria hiyo, iliyotokana na marekebisho ya sheria ya awali ya mafao ya viongozi maalum wa kitaifa ya mwaka 1986, kila mbunge atalipwa asilimia 40 ya mshahara wake alioupokea kwa kipindi chote cha miaka mitano.

  Marekebisho ya mishahara ya viongozi wakuu wa nchi na viongozi wa kisiasa yaliyofanywa Julai mwaka jana, yameonyesha kuwa, mbunge anapokea Sh1,921,000milioni kwa mwezi.

  Hata hivyo sheria imeeleza kuwa sio wabunge wote watakaovuna kiasi hicho cha fedha, kwa kuwa muda wao wa kuwa bungeni unatofautiana.

  Afisa mmoja mwandamizi katika ofisi ya Bunge ambaye hakutaka kutajwa gazetini alilidokeza gazeti hili jana kuwa wabunge watapata mafao hayo baada ya Rais Kikwete kulivunja Bunge.

  "Mimi si msemaji wa Bunge lakini, kwa kukusaidia tu fedha hizo zitalipwa baada tu ya rais kutangaza rasmi kulivunja Bunge.

  Wabunge watazikuta fedha hizo kwenye akaunti zao kati ya Julai na Agosti," alisema na kuongeza:

  "Malipo hayo yatafanywa kwa kuzingatia Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Kisiasa ya mwaka 1999 iliyopo sasa, iliyoanza kutumika mwaka 2000. Sheria hiyo ilitokana na marekebisho yaliyofanywa kwa sheria ya awali, ambayo ni Sheria ya mafao ya viongozi maalum wa kitaifa ya mwaka 1986".

  Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilillah alilithibitishia Mwananchi kuwa malipo hayo ya kiinua mgongo yatafanyika kwa kutumia sheria hiyo baada ya bunge kuvunjwa.

  "Sheria iliyopo ndiyo itakayotumika na ndiyo itayoongoza kufanya malipo hayo. Sheria hiyo ni ya Mafao ya Viongozi wa Kisiasa ya mwaka 1999 iliyoanza kutumika mwaka 2000," alisema Dk Kashilillah.

  Alifafanua zaidi akiasema: "Malipo yanaweza kufanyika 'at either' (wakati wowote), kabla au baada ya kuvunjwa Bunge".

  Kuhusu kiinua mgongo kwa mawaziri na manaibu wao Kashilillah alisema sheria ipo wazi kuhusu viongozi hao na kueleza kuwa hawalipwi mishahara na Bunge bali serikali kupitia wizara husika.

  "Kuna mafao ya Bunge na serikali, sisi hatulipi mishahara ya mawaziri, bali ya wabunge. Mawaziri wanalipwa mishahara na serikali, sheria ipo wazi, ukiisoma imeweka wazi hilo," alisema Dk Kashilillah.

  Sheria hiyo imeainisha pia viwango vya malipo vya viongozi wa juu serikalini ikiwamo rais, makamu wake na waziri mkuu.

  Aidha, imewajumuisha mawaziri na manaibu wao, wakuu wa mikoa, wilaya, Spika wa Bunge na Naibu wake.

  Spika wa Bunge na naibu wake watapata kiinua mgongo cha kiwango sawa na rais mstaafu, lakini, watatofautiana kwenye baadhi ya mafao.

  Kwa mahesabu ya viwango vya mishahara yao, mawaziri na manaibu wao watuchukua jumla ya Sh2,658,768,000 kama kiinua mgongo chao.

  Mwaka uliopita serikali iliwaongezea mishahara viongozi wakuu wa nchi na viongozi wa kisiasa ambapo mishahara ya wabunge ilipanda kutoka Sh1,840,000 hadi 1,921,000 na naibu Spika kutoka Sh Sh2,080,000 hadi Sh2,172,000.

  "Viwango vya mishahara kwa viongozi wa serikali vinawekwa na serikali, mimi hainihusu hivyo siwezi kuthibitisha hilo. Nimesikia tu kama mlivyosikia ninyi," Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilillah aliliambia gazeti hili alipotakiwa kuthibitisha ongezeko hilo la mishahara mwaka jana.

  Hata hivyo, viwango hivyo vya mishahara, havijumuishi posho za vikao, mafuta ya gari na fedha za kujikimu ambapo sasa Mbunge mmoja anapata Sh135,000 kama posho kwa kikao kimoja cha Bunge ambayo pia mawaziri na manaibu hunufaika nayo.
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  May 6, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  MkamaP,
  Ebu nambie hiyo mishahara ya Ugiriki ukubwa wake...Mkuu hivi kweli unafuatilia swala hili? Greece inaanguka kiuchumi kutokana na matumizi makubwa na mabaya ya serikali. Nitarudia kusema mgogoro mzima wa greece unatokana na pendekezo la kupunguza ajira (jobcuts) na pia mishahara ya mafanyakazi kulingana na uzalishaji wa ndani ambao unashuka mwaka hadi mwaka. Deficit ya GDP imefikia karibu asilimia 15 hivyo haina maana ya kwamba mishahara ndio mikubwa ila kuna matumizi makubwa ya serikali kinyume cha pato lake la ndani.

  Leo hii Tanzania tupo ktk jarida hilo hilo... tuna matumizi makubwa ya serikali na mishahara ya civil servants sii moja ya matumizi yetu makubwa ila viongozi na posho zao. Hivyo deni la taifa letu linazidi kupanda kila siku na kusema kweli tupo ktk kufilisika ndani ya umaskini sema mikopo ndio unatusaidia sana. Sasa itakuja siku tunafilisika watu wa kwanza kuumia itakuwa hawa hawa wafanyakazi na sii viongozi. Ni sawa na mtu anayeishi kwa creditline akitumia mikopo kuendesha shughuli zake. Ukweli wa mambo ni kwamba uzalishaji umepungua sana na pnengine tupo chini ya asilimia 50 ya uzalishaji na mzunguko wa fedha yetu unategemea zaidi fedha zilizoibiwa au zinazoibiwa ktk mabenki na mashirika, pengine hata uchapishaji wa fedha zaidi umetumika kutuwezesha mzunguko kuwepo.. Kifupi tunajidanganya wenyewe.

  Watanzania ni wavivu kwa asili. Sii wafanyakazi kutokana na mfumo mzima wa ajira. Watu wanatakiwa kulipwa kwa masaa ya uzalishaji na sii mfumo wa ajira wa kijamaa ktk uchunkazi naKuna sababu nyingi za kimsingi zinazoweza kutumika kutoongeza mishahara kwa sababu kila siku uzalishaji unapungua. Huwezi kuongeza mishahara wakami unaoendeshwa na soko huria.. wafanyakazi wengi wanavuna ambacho hawakupanda na hii ni hatari kubwa kiuchumi kwani hakuna sababu ya kuboresha uzalishaji ikiwa paycheck haina kiwango cha masaa ya uzalishaji..Na sababu kubwa ya uvivu wetu umetokana na ukosekanaji wa MIUNDOMBINU.
  Uzalishaji unazidi kupungua kutokana na miundombinu mibovu. watu wanafanya kazi masaa chini ya sita kutokana na usafiri mbovu, ukosekanaji wa mara kwa mara wa umeme na upungudu wa maji. Kuna kila dalili mbaya ya sisi kuanguka kiuchumi
   
 20. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #20
  May 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280

  MBUNGE wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa, hivi karibuni aliweka wazi kiwango cha mshahara anaopata mbunge kwa mwezi, kwa kuutaja mshahara wake, wakati akihutubia wananchi wa mji mdogo wa Hedaru, mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni mfululizo wa mikutano ya hadhara ya chama hicho, almaarufu, Operesheni Sangara. Dk. Slaa alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akisema kuwa mshahara wake kwa mwezi ni sh 7,000,000 (milioni 7), na wakati huo huo bado anapokea posho ya sh 135,000 kwa siku awapo kwenye shughuli za Bunge.
  (From: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=3498 )

  Mkuu, sasa hapo ukiweka na za POSHO ya kikao kama ilivyoandikwa hapo juu, jamaa wanapata bila wasiwasi wowote 10 Milioni. Mengine soma hapo juu ULIE.
   
Loading...