Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,543
- 113,702
Pole Mzee Mwanakijiji,Kujaribu kuvunja Jamhuri ya Muungano kwa kisingizio chochote kile cha kisiasa ni uhaini. Mnaweza kutafuta kura na support ya wapiga kura lakini ukweli ni kuwa kuna nchi moja ambayo ni Jamhuri ya Muungano ambayo imetokana na kuungana kwa nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar.
Jaribio la upande mmoja kuirejesha kinyemela nchi iliyokwisha ungana na nyingine ni kutangaza secession kutoka kwa Muungano na viongozi wote wanaopanga kufanya hivyo ni wa kutiwa pingu.
Sijawahi kufikiria kusema JWTZ liangalia ulinzi wa Katiba lakini wakati huu endapo mabadiliko yanayopendekezwa Zanzibar yatafanyika ni wakati wa kuwaangalia hawa "maadui wa ndani".
Ati wenyewe wamekaa kupitisha mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ili kipengele kimojawapo kisomeke hivi:
Wenyewe wanashangilia!! Lakini wanasahau kabisa waliapa kulinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema (msisitizo wangu):
na Magenius wetu hawaoni tatizo hapo: Je hii ni chemsha Bongo? Hivi ukisoma katiba hizo mbili utaelewa kuna nchi "ngapi"? Hivi hata hesabu za seti hawazielewi masikini wa Mungu au somo la mantiki linahitaji kufundishwa kuanzia darasa la kwanza?
Kama a. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo "LOTE" la Tanzania bara na eneo "LOTE" la TAnzania Zanzibar, sasa Zanzibar ina ENEO GANI ambalo si sehemuya Eneo la Jamhuri ya Muungano? Kama seti moja inahusisha wanyama wote wa mwituni na seti nyingine inauhusisha simba na chui ambao nao ni wanyama wa mwituni, inakuwaje mtu anaanzisha seti nyingine inayosema "wanyama wa mwituni"?
Wanachezea maneno lakini maneno yana maana. Na miye natumia nasema kinachofanyika ni uhaini... (mnaweza kutafuta namna nyingine ya kulikwepa neno hilo). Lakini wataalamu wetu hawa hawa wanasahau Ibara ya 28:3 ya Katiba (waliyoapa kuilinda) inasema nini:
(
Sasa hawa wahuni wa Zanzibar wamepata wapi ujasiri wa kuridhia kuligawa taifa na kutengeneza nchi nyingine nje ya hii NCHI moja? Kuna njia moja tu ya kuunda Nchi ya Zanzibar- KUJITOA kwenye MUUNGANO. Nje ya hapo ni UHAINI!!!
I couldn't be more blunt than that.
Labda nikumbushie sehemu kidogo tu ya hotuba ya Baba wa Taifa kwenye Bunge lililoridhia Muungano Aprili 25, 1964 (msisitizo wangu):
Ooh how prophetic!!!
I'm standing on guard, by CHOICE!
Rasimu ya mabadiliko hayo, niliyaona kwenye kikao fulani cha nchi wafadhili, nikiamini yangewekwa hadharani ili yajadiliwe na Wanzazibari kabla ya kufikishwa Barazani.
Maana ni kuwa Bara iko very much aware kila kinachoendelea Zanzibar, kwanza waliomba bendera, halafu wakaomba wimbo wa taifa, sasa hawajaomba mipaka, bali wametangaza mipaka ili Zanzibar iwe nchi in terms of defined teritory ila usiwe na shaka, hiyo ni mipaka jina tuu, kama ulivyo wimbo wao wa taifa ni wimbo tuu, na bendera yao nayo ni bendera tuu.
Kama wewe nyumbani kwako unaitwa Baba, mwanao akalipenda sana jina la baba, ukakubali naye aitwe baba, akiitwa baba anafurahi, hivi wewe sasa ndio hautakuwa baba?. Wewe utabaki baba wa ukweli na yeye baba jina.
Hivi ndivyo ilivyo status ya Zanzibar, ni nchi jina tuu ila sio dola kwa sababu bado haina vyombo vya ulinzi, vyombo vya dola, Jeshi, Polisi, TISS etc, unless KMKM ndio polisi wao na JKU ndio jeshi lao, them huu utakuwa uhaini 100%.