Ni uhaini - as simple as that! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni uhaini - as simple as that!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 9, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,363
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Kujaribu kuvunja Jamhuri ya Muungano kwa kisingizio chochote kile cha kisiasa ni uhaini. Mnaweza kutafuta kura na support ya wapiga kura lakini ukweli ni kuwa kuna nchi moja ambayo ni Jamhuri ya Muungano ambayo imetokana na kuungana kwa nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar.

  Jaribio la upande mmoja kuirejesha kinyemela nchi iliyokwisha ungana na nyingine ni kutangaza secession kutoka kwa Muungano na viongozi wote wanaopanga kufanya hivyo ni wa kutiwa pingu.

  Sijawahi kufikiria kusema JWTZ liangalia ulinzi wa Katiba lakini wakati huu endapo mabadiliko yanayopendekezwa Zanzibar yatafanyika ni wakati wa kuwaangalia hawa "maadui wa ndani".

  Ati wenyewe wamekaa kupitisha mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ili kipengele kimojawapo kisomeke hivi:

  Wenyewe wanashangilia!! Lakini wanasahau kabisa waliapa kulinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema (msisitizo wangu):
  na Magenius wetu hawaoni tatizo hapo: Je hii ni chemsha Bongo? Hivi ukisoma katiba hizo mbili utaelewa kuna nchi "ngapi"? Hivi hata hesabu za seti hawazielewi masikini wa Mungu au somo la mantiki linahitaji kufundishwa kuanzia darasa la kwanza?

  Kama a. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo "LOTE" la Tanzania bara na eneo "LOTE" la TAnzania Zanzibar, sasa Zanzibar ina ENEO GANI ambalo si sehemuya Eneo la Jamhuri ya Muungano? Kama seti moja inahusisha wanyama wote wa mwituni na seti nyingine inauhusisha simba na chui ambao nao ni wanyama wa mwituni, inakuwaje mtu anaanzisha seti nyingine inayosema "wanyama wa mwituni"?


  Wanachezea maneno lakini maneno yana maana. Na miye natumia nasema kinachofanyika ni uhaini... (mnaweza kutafuta namna nyingine ya kulikwepa neno hilo). Lakini wataalamu wetu hawa hawa wanasahau Ibara ya 28:3 ya Katiba (waliyoapa kuilinda) inasema nini:

  (
  Halafu kama watu wasiojua Katiba wanasahau Katika ya Muungano inasemaje kuhusu wakuu wa mikoa. Katiba inasema hivi:

  sasa magenius wetu wa Zanzibar wameamua kumnyang'anya madaraka Rais wa Muungano ya kushiriki uteuzi wa wakuu wa mikoa ya Zanzibar kama Katiba ya Muungano inavyotaka na kina Werema wamekaa na tai zao wanachekelea!


  Sasa hawa wahuni wa Zanzibar wamepata wapi ujasiri wa kuridhia kuligawa taifa na kutengeneza nchi nyingine nje ya hii NCHI moja? Kuna njia moja tu ya kuunda Nchi ya Zanzibar- KUJITOA kwenye MUUNGANO. Nje ya hapo ni UHAINI!!!  I couldn't be more blunt than that.

  Labda nikumbushie sehemu kidogo tu ya hotuba ya Baba wa Taifa kwenye Bunge lililoridhia Muungano Aprili 25, 1964 (msisitizo wangu):

  Ooh how prophetic!!!

  I'm standing on guard, by CHOICE!
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mkuu nchi zilizo ungana ni Tanganyika na Zanzibar na kuzaliwa Nchi inayojulikana Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, na si Tanzania na Zanzibar.

  Kwa njia moja ama nyingine nadhani Wazanzibar wana haki yua kuujadili muungano kama nchi, kwani kwenye muungano huo Tanganyika ndio ilikufa ila Zanzibar ilibakia na utaifa wake.
   
 3. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mimi naamini kuwa ikiwa itakuwa hivyo basi yule alietiwa kizuizini na wengine ambao wanaona wako huru kutimiza ndoto zao kwa kuwa mwenyewe hayupo tena na wanaweza kumwambia huyu kijana nae akaitikia tu, huo ni uhaini wa "first degree".
   
 4. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  tunahitaji viongozi smart kama wakina Lincolin huko Marekani maana kama Lincolin angekuwa na hulka za Kikwete, i swear today Texas ingekuwa nchi huru! Nashangaa Kiwete yuko kimya!
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,363
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Nimekupata hapo X-Paster.. nilipitiwa
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mkuu tupo pamoja, ni katika kukumbushana tu.
   
 7. JAPUONY

  JAPUONY JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wanaotaka kuvunja muungano wajue kuwa wao hawakuzaliwa ndani ya muungano. Sis tuliozaliwa ndani ya muungano ambao ndiyo wengi kuanzia 1964 tukiulizwa popote pale tunasema sisi ni watanzania. Tuliozaliwa kuanzia 1964 ambao ndiyo watanzania tuko kimya na tunaridhika na muungano. Ambao walizaliwa nje ya muungano ndo wanatupigia kelele, chanzo, wanataka madaraka!ebu mliozaliwa kabla ya 1964 mtupishe tuendeleze tanzania yetu. Subirini muda wenu ufike mkaonane na ahera!!!!!!!!
   
 8. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Waacheni wazanzibar wafanye wanalotaka. Kuwaita wahaini ni kuudhihirisha wanachofikiria juu ya wabara. waacheni wasonge mbele
   
 9. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Haaa... haaa ... heee.. heee.. Kama ni kweli... haya ndio matokeo ya kumchagua msanii na kumpa urais. Mpaka aje aondoke na kwetu Morogoro kutakuwa ni jamhuri ya watu wa Morogoro.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,363
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  of course.. hilo wala siyo hoja; wakitaka watangaze tu kuwa wanataka kutoka nje ya Muungano, wadai kile wanachokiita ni "uhuru". Kikwete awaruhusu kwa sababu sidhani kama ana uwezo wa kuzuia Zanzibar kutoka nje ya Muungano. Na ninaamini guess what will happen:

  Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar watatoa hoja ya kutaka kutoka nje ya muungano na kupendekeza kura ya maoni kwa Wazanzibar wapige kaa wanataka kubakia ndani ya Muungano, hoja hiyo italetwa NEC (musoma au dodoma) CCM hawana watu wa kuutetea Muungano wetu na watasema endeleeni kupiga kura na mkishinda basi tunaachana "salama"..

  Hili LITATOKEA! Kwani baada ya kuiweka Zanzibar kuwa ni nchi na mipaka yake kama ilivyo kwenye mabadiliko haya, kitakachofuata ni kujiuliza "je nchi yaweza kuwa sehemu ya nchi nyingine?". JIbu haliepukiki ni HAPANA.

  OOH HOW I PITY THAT DAY!!
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Kuendelea kuungana nakuto endelea vyote vinawezekana... Si swala la kutishana na kuitana wahaini... Kama tuliweza kuungana na pande zingine zinaona kuwa hazitendewi haki kuna haja ya kuangalia tena huo muungano una faida yoyote kwa Mtanzania wa kawaida kijamii na kiuchumi?
   
 12. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  DAH! huyu MWKJJ ni mtu khatari sana kwa maendeleo ya wa zenj, alijaribu kuwakumbusha wa znj mambo yaliyo pita ili wazenj wasiungane akashindwa, leo wa zenj wamekua wamoja anawaita wahaini, anamawazo yakizamani kwa kweli ana akili mbaya, akili ya kikoloni,anshawishi vitu vya ajabu kweli. kama umri wako unazidi miaka 80 si shangai ikiliyako itakuwa imesha choka, lakini kama chini ya 50 matamanio maovu yasikutawale
   
 13. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  Ndiyo kwani viongozi walifikiri muafaka wa Maalimu na Karume ulikuwa umelenga wapi? ndo hiyo zanzibar iliyo huru, Karume na Seif walielewana kwa sababu tu walikua na common enermy ambaye ndo muungano na mbara. Kwa bahati mbaya baada ya kumuondoa adui yao ambaye ni common watamtafuta mwingine.

  Kikwete anachofanya mimi nafikiri ndo njia sahihi, acha waamue watu mambo yao wanayoyaona yanawafaa, kwanini kulinda kitu kwa mabavu?
   
 14. N

  Ngala Senior Member

  #14
  Aug 9, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kweli leo naamini zanzibar wakipiga chafya bara mafua tayari. hivi ni kwa nini tunaikolia zenji kuna faida gani haswa tuipatayo toka huko au ndo hayo mafuta ya kufikirika wandugu?? kwani wakijitoa tutapata hasara gani wapendwa? enzi ya vita baridi ilishapita nini tena wa bara twasumbuka nao? binafsi sioni faida hata kidogo. kila siku vineno neno hadi lini? waacheni na nchi yao.
   
 15. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Thank you MKJJ kwa kuliweka hili bayana.Watanzania wanaposema hakuna Think Tanks katika uongozi tunafikiri ni utani.
  No doubt JK is in a tight spot.
  Next,Rais wa Muungano has NO JURISDICTION over Zanzibar,another country.
  Muungano is definately dying,but not that we will shed many tears.
  Actually Zanzibar is up to our necks.
   
 16. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nitakuwa wa mwisho kulia kama Zanzibar itajitenga. After all mimi ni shabiki wa nchi tatu. Wakati mnaona Zanzibar inaenda zake, mimi naona Tanganyika inazaliwa upya! Bravo Zanzibar, Keep it up. Mpaka Kieleweke...Mna wimbo wa Taifa na Bendera, go on kudai vyote
   
 17. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,539
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Kwanza jina Tanzania ni nini? Ni jina la kutungwa halikuwepo kabla ya mwaka 1964. Baba yangu alishiriki katika shindano la kutunga jina litakalotokana na Tanganyika+ Zanzibar= Tan+Zan inaongezwa Tan+ Zan+ Nia kuongezea ladha ya matamshi, kuna mtu alijishindia zawadi kwa kutunga Tanzania.

  Jina la nchi hii ya kusadikika Tanzania ingeweza kuitwa Jamhuri Ya Muungano Ya Nchi za Tanganyika na Zanzibar (au Zanzibar na Tanganyika) kama vile nchi ya Bosnia and Herzegovina au kama vile Muungano wa Egypt na Syria ulivyojulikana kama UAR(United Arab Republic) wakati wa Gamal , Muungano huo wa United Arab Republic (UAR) ulimudu kati ya mwaka 1958 -1961.

  Hivyo Muungano haudumishwi kwa sheria, jeshi au Umoja wa Mataifa, Muungano kama ndoa hudumishwa kwa nia, hata kama 1964 Muungano wetu ungeitwa Jamhuri ya Muungano wa Nchi za Tanganyika na Zanzibar au Jamhuri ya Muungano ya Nchi za Zanzibar na Tanganyika, nia ya kuwa pamoja kupitia Muungano ndio itakayowezesha Muungano kudumu kama ilivyoanza 1964 hadi sasa na unaweza kuwepo miaka 200 ijayo.

  Hivyo hakuna sababu ya kuanza kuhisi uhaini, njama au sababu zingine. Suala hapa hata hili jina la kutunga la Tanganyika kuitwa Tanzania Bara isione haya kujiita Tanganyika ili historia ikamilike au isipotee kuwa Tanzania ni jina la kutunga ambalo lilitokana na shindano la kutunga jina kufupisha maneno yenye maana ya Tanganyika + Zanzibar.

  Sijui kuna mwenye data aliyeshinda shindano la kutunga alijinyakulia shilingi ngapi na aliitwa nani?
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,363
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  tatizo wanafikiri kuwa tunazungumza kutoka hewani tu ati tunaitakia Zanzibar mabaya; kama mazungumzo ya watu wawili leo hii (karume na seif) yamechukuliwa kuwa halali na kukumbatiwa yale ya wa Nyerere na Karume nayo yalikuwa na nguvu hiyo. Wazanzibar hawawezi kuwa na keki yao halafu waile huku wabakie nayo. Kama kuna watu Zanzibar wanataka kuwa nchi "nje" ya Muungano, waliseme hilo, kama ni kupigwa kura ipigwe na tuanze mahusiano baina ya nchi mbili.

  But as long as we are a United Republic jaribio lolote la kuivunja ni uhaini - as simple as that.

  Ni jukumu la kila Mtanzania (yes wapo watu wa taifa hilo) kulinda Muungano ulivyo. Hatupaswi na hatuwezi kuachii kikundi cha watu wachache kuivunja ati kwa sababu hawajisikii. Wazanzibari ambao wanajitambua kuwa ni Watanzania na wapo wengi ni lazima wakatae uhuni huu.

  Kama Zanzibar haitaki kuwa ndani ya Muungano kwenye baraza la wawakilishi waseme hivyo mapema, wajitangaze kuwa wanataka kutoka nje ya Muungano na nina UHAKIKA Kikwete na uongozi wa CCM hakuna atakayeweza kujenga hoja za kuzuia kwani mashujaa hao hawapo tena. Basi watoke na kama nilivyosema tuanze uhusiano wa nchi mbili, binafsi wala sina tatizo kabisa. Lakini kama wanataka tuwe wamoja kama nchi ni lazima mpango wao wa kuitangaza Zanzibar kuwa ni nchi sijui madudu gani ukemewe mara moja na KILA MTANZANIA.

  Si kwa sababu hatuwezi kuishi bila Zanzibar au wao bila sisi, bali kwa sababu MUUNGANO UPO na ni lazime utetewe kwa gharama yoyote. Kwanini Zanzibar wasipige kura ya maoni kutaka kujua kama wanataka kubakia ndani ya Muungano?

  PIGENI HII KURA TUMALIZE MZIZI WA FITINA!!!

  viNGINEVYO NI UHALIFU ULIOKUBUHU AMBAO ADHABU YAKE NI KIFO! Uhaini haurembuliwi macho.
   
 19. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #19
  Aug 10, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Waache waende zao mwanakijiji. Mimi sikuwahi kuiona hiyo faida ya muungano hata kidogo. Utaitaje jamhuri ya muungano wa Tanzania ilihali kule kuna bendera yao, kuna ngao yao, kuna rais wao, kuna baraza lao la mawaziri na kila kitu kasoro, jeshi na mahakama. Hii si ni tayari ni nchi inayojitegemea kabisa? Waache tu waendelee na kubadili katiba yao kwa sababu wanazo haki zote za kufanya mambo yao kama nchi kwa kuwa wana maamuzi yao binafsi ambayo wanaweza kuyafanya kupitia baraza lao la mawaziri na bunge lao ambalo ni baraza la wawakilishi. Sasa bara mtaingiliaje maamuzi ya bunge la kule?
   
 20. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #20
  Aug 10, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Hivi katiba ya JMT inasemaje juu ya baraza la wawakilishi na katiba ya Zanzibar, Mimi nimechanganyikiwa Kabisa, itakuwaje katiba ya Zanzibar i-contradict katiba ya Muungano? Itakuwaje Baraza la wawakilishi waende tofauti na maazimio ya Bunge la JMT? nani yupo juu ya mwingine? Katiba ya JMT inasema kuwa Rais wa JMT ndiye mwenye mamlaka ya kugawa mikoa na wilaya ZNZ kwa kushauriana na Rais wa SMZ. Sasa leo kipengere cha kumpa madaraka Rais wa ZNZ kinafuta kingere kile cha JMT? kwani wakuu wa mikoa wa ZNZ wanateuliwa na nani? Siupendi muungano lakini madam upo lazima tukubaliane either kujadili kama hatuutaki na kama tunakubalina hatuutaki basi tuuvunje na kama tutakubaliana kuwa tunautaka basi tuudumishe. Sheria inabaki kuwa halali mpaka pale inapokuwa imebatilishwa na sheria nyingine kupitia kikao halali chenye mamlaka halali ya kikatiba kufanya hivyo. Nadhani tunahitaji kuwajibisha Baraza la wawakilishi ZNZ
   
Loading...